CCM yampongeza Richard

Mzee, Mimi binafsi ninakubali kukosolewa kwa CCM. Na penye raha huwa pia nasherehekea!

Kumbukeni ninatazama pande zote za shilingi!


FD sijasema kukosolewa... nimesema kama wanafurahia ushindi wa Richard kuwa ni ushindi wa "malezi bora ya CCM" naamini wakati umefika tukubali makosa na mapungufu ya watu wetu kuwa ni makosa ya CCM! Kumkosoa mtu ambaye hakubali makosa ni kupoteza muda na ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa...
 
Unajua ndio maana naona sitakuwa mwana CCM mzuri kwani sifuati falsafa ya "chama changu, right or wrong". Tatizo la CCM na watetezi wake ni kuwa mazuri wanataka yaimbwe na kutungiwa tenzi mabaya tunaambiwa ni "hoja za wapinzani"...
 
ama kweli tanzania tumeishiwa na maadili! ikiwa chama kinachoshika madaraka kinasema kuwa aliyoyafanya richard ni malezi bora kweli maana ya malezi yasiyokuwa bora siyajui!!

richard amejishindia mwenyewe, na nakataa kuwa ushindi wake utuhusu watanzania wote........sina tabia mbaya kama zile na sizifagilii vile vile
 
Mimi naomba kuuliza hivi, huyu Bwana Richard ni nani na amefanya nini mpaka chama tawala CCM kimeamua kumpa hongera na hiyo $100,000, alikuwa upinzani akahamia CCM au? Sijawafahamu vizuri hapo...
 
Rais Kikwete, amepokea salaam nzito toka kwa marais wa karibu nchi zote za Afrika Mashariki na ya kati kwa kutokana na ushindi wa m-Tanzania, Richie, kwenye maisha kuna wakati wa kila kitu,

Wakati wakulia na kucheka, wakati wa mvua na summer, kupanda na kuvuna, sasa hivi ni wakati wakusherehekea ushindi wa m-Tanzania mwenzetu aliyekwenda na kuiwakilisha bendera yetu kijasiri na kulitangaza taifa zima letu la Tanzania,

Respect kwa Richie!
 
hongera kijana kwa kutumia shortcut kupata mtaji,
cha muhimu ni mikakati mizuri ya kupunguza umaskini kama si kuondoa, inawezekana ndoa yake na mkanada ilikuwa ni moja wapo ya strategy ya mkukuta,
sidhani kama aliliwakilisha taifa, nfikiri alistruggle kivyake hadi akafika huko, kwa kuwa ni utamaduni wa serikali yetu ya kuwapongeza wananchi wake pale wanaposhinda na kuwalet constant pale wanaposhindwa, hongera sisiem kwa kukumbuka hilo.
 
FD sijasema kukosolewa... nimesema kama wanafurahia ushindi wa Richard kuwa ni ushindi wa "malezi bora ya CCM" naamini wakati umefika tukubali makosa na mapungufu ya watu wetu kuwa ni makosa ya CCM! Kumkosoa mtu ambaye hakubali makosa ni kupoteza muda na ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa...

Mzee, ninakubali kabisa kukosolewa CCM. Hata mimi nadhani umeshaona ninaikosoa CCM kwenye baadhi ya mambo, ninaamini utakubaliana nami ktk hili.

Lakini sijawahi wana kuona Chadema wala KHAF wakikubali kuna sehemu wameharibu... Chaunguza utaniambia!
 
Rais Kikwete, amepokea salaam nzito toka kwa marais wa karibu nchi zote za Afrika Mashariki na ya kati kwa kutokana na ushindi wa m-Tanzania, Richie, kwenye maisha kuna wakati wa kila kitu,

Wakati wakulia na kucheka, wakati wa mvua na summer, kupanda na kuvuna, sasa hivi ni wakati wakusherehekea ushindi wa m-Tanzania mwenzetu aliyekwenda na kuiwakilisha bendera yetu kijasiri na kulitangaza taifa zima letu la Tanzania,
Respect kwa Richie!

Yote nakubali , ila kwenye bold hapo utani mzee. ujasiri alotumia ni upi kutangaza taifa. Tuweni serious bwana, hii habari ya kudandia tu kusingizia taifa zima hata kwa mambo ya kijinga mi sipendi,cha msingi wangeacha tu clouds na multchoice ndo wakampokee mshkaji ila hili la ccm mi sijalikubali kabisa na hasa wanavyosisitiza malezi bora waliyompa, oh what a shame. inaonyesha hawana kitu cha msingi cha kufanya na wakati vijana kibao hawana ajira wa hukohuko ccm.
 
Haya sasa,ina maana hta wale waliokua wanamponda Rich kwa uzinzi pia hili nalo walitupie macho kwani kama Rich alipata huo ushindi kwa Uzinzi it means CCM ndio zaidi kwa kujifunga kibwebwe kumshangilia.Wabongo tuacheni unafiki na unazi.

Mbona hawa watu wanajua kudandia kila kitu? Kwa hiyo hata mamiss wote waliofail miss world ni sera mbovu za CCM,taifa stars sina hakika kama bado wanbatambulika kama JK boys au la,na njaa inayowakabili wahadzabe pia ni matokeo ya sera za CCM au sio?

Umaskini wetu uliokithiri unatokana sera za wapinzani au? Chama kilichoongoza kwa miaka 45 huku tukipigwa bao kiuchumi hata na nchi zilizokua kwenye vita kama Rwanda,Burund na Uganda iliyoporomoshwa kiuchumi na utawala wa Dikteta asiyekua na elimu Idd Amini leo hii wanatupita kiuchumi si aibu tupu na kinyaa ?

Kama tunaweza kukubaliana kwenye hayo mambo hapo juu basi dhamira ya CCM kumpongeza Rich ni ya kweli

Rich hongera kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania bora uinvest hizo hela utoe ajira kwa vijana wetu umaskini huu upungue.Hao vilaza waaache kujigamba sasa wajafdili mambo ya msingi.Sasa wasiache kuijadili Richmond leo,waanze kufikiria kukupokea na kukuita bungeni.

Itakua tusi kwetu sisi wananchi
duh!
 
Back
Top Bottom