CCM Yakalia kuti kavu Ukonga

CCM Yakalia kuti kavu Ukonga

N ukonga ipi unayoiongelea ww,acha kuropoka vtu usivovijua ww,,,,,,ukonga ipo shwari kabsa na sisi ndo wakaz wa ukonga na ndo wapiga kura sasa ww fanya ziara njaa yako uwaongopee vichaa mbuz wenzako,,,mAma bdo anaushawish mkubwa jimbon kwake,kupiga kelele jukwaan sio utendaji kaz huo,hatuchagui mtu anaelezea mapungufu,tunataka mtu anaelezea strategz atakazozitumia kuleta chachu ya maendeleo jimboni.

Unaishi ukonga kata gani ndugu! Ukonga ndilo jimbo la mwisho kabisa kimaendeleo kaw jiji la Dar, ndilo jimbo ambalo barabara zake kwa 90% hazina ubora, si lami si kifusi, tazama wakazi wa kitunda wataabikavyo kurudi majumbani mara mvua zinyeshapo, wakazi wa Moshi bar vilevile wanavyovunjika viuno wakiwa ndani ya magari, ishu maji sizungumzii kabisa maana kwa kijana wa miaka 18 sasa hivi nadhani hajawahi kukutana na maji ya Dawasco jimbo hili tangu azaliwe!
Kifupi Eugene amepoteza jimbo na ndio maana anaona haya hata kukutana na wapiga kura wake!

Ndo maana nakwambia waongea vitu usivovijua ww,njoo kitunda mwanagati kama hutokuta bomba la dawasco,na kwa taarifa yako miongon mwa majimbo bora dsm kwa upatkanaj wa maji safi ukonga lipo,n wapi unaskia kuna shida ya maji ukonga,npo kitunda n barabara ipi isiyokuwa na ubora?leta za Kawe,ubungo kuelekea kibangu,maziwa,leta jimbo ya segerea,,,,,acha kuongea vtu kwa msukumo wa itkadi yako so far wanaukonga ndo wapigao kura sion 7bu yako ww kukata mauno ngoma ya jirani.

Samahani sana bwana Kiboko, nimeshindwa kukuvumilia kwa hiki ulichochangia. Mimi ni Mwanaukonga, niko Kivule Muembeni, na ni mkazi wa Kivule toka mwaka 2001, kwa kifupi katika majimbo mabovu kabisa, mabovu kabisa kwa miundo mbinu ya Barabara na Maji ni Ukonga hususan barabara tatu (Banana Kivule hadi Msongola, Banana Mwanagati na Mombasa Kwa diwani au kwa Mkuremba. Haisaidii kuja kusema uongo humu JF wakati ni kweli, sisi wa Kivule tunashindwa hata kuendesha gari aina ya Saloon, ni lazima uwe na Prado, RAV4 au SUZUKI (Punda), hali ni mbaya sana. Kuhusu maji, uyasemayo si kweli kwamba kuna Dawasa, isipokuwa kwa kuwa nyumba nyingi zimejengwa na waliohamia ambao kidogo wanajiweza, hivyo kila mmoja amechimba kisima, na maji yake ukibahatika ni mazuri hayana chumvi. Acha Propaganda bwana, hii CCM tumeanza nayo tangia TANU, si yako peke yako na wala usilete ushabiki wa Kichama katika hili. We from Kivule are very serious on this matter. We no longer entertain with the so called CCM or the current MP, she is completely impotent. Tafadhali tuombe radhi wana Ukonga na wala si masuala ya kivyama hapa ila Jimbo letu lina barabra mbovu sana.
 
Maendeleo jimbo la ukonga kwa sasa yako wazi na yanaweza kupingwa tu na watu wasiotaka kufanya tathmini ya ukweli. Ni chuki tu dhidi ya CCM kwa wengi wenu humu.

Labda unazungumzia maendeleo ya kisangoma ambayo yanaonwa na wachawi peke yao!
Ukonga kuna maendeleo gani ambayo hata wewe mwenyewe mfuasi wa mwaiposa unaweza kuyataja?
Barabara ni utata mtupu. Shule/Elimu utata mtupu. Vituo vya Afya mgogoro mtupu. Masoko mgogoro mtupu. Na maji ndiyo kabisaaa huwezi kuthubutu kuyataja! Sasa wewe tuambie ni kipi kina afadhali katika hayo makuu niliyoyataja!
 
Ameniboa sana huyu jamaa, tena ameniharibia siku. Jimbo la Ukonga lina Maendeleo? kwanza binafsi hata huyo Mbunge simjui japo ni mkazi wa Kivule toka 2001-huwa naonyeshwa alama zake tu, Jamaa wa ajabu sana na inaonyesha hajwahi fika huko tunakosema. Ukipita Banana pale unatamani utoe lift kwa watu wote jinsi wamama wanavyoteseka kwa usafiri. Barabara mbovu, magari mabovu, hakuna maji, shule zero tupu, Afadhali watu umeme tu kidoogo.
 
Nawashauri jengeni hoja hapo Lumumba muweze kuandaliwa safari ya kuzunguka kila kata au mtaa wa Jiji hili la Dar, vinginevyo mtaonekana wendawazimu mnapochangia baadhi ya mada maana inaonyesha baadhi yenu mmetoka mikoani na hamuelewi sehemu yoyote ya Dar zaidi ya Lumumba. Mtakapotembelea kata au mitaa hiyo, mtaweza kujua namna ya kuongopa na kutetea upuuzi wenu ili angalau kwa wanaojua waweze kuwa kimya. Lakini mkileta uchangiaji na utetezi kama huu, hata wale waliokuwa na uvumilivu dhaifu nao utaondoka maana wataona kumbe nyie watu ni hatari sana na mna dharau sana. Haiwezekani ukasema maendeleo ya Jimbo la Ukonga yako waziwazi-ulipelekwa Posta wewe ukaambiwa hili ndio Jimbo la Ukonga, sio bure.
 
Ni Ukweli mchungu sana kwa sisi wanaCCM hapa Dar.
Iwe isiwe 2015 majimbo ya Ukonga na Segerea tutayapoteza kwa aibu kubwa sana. Mpaka sasa sioni wapi pakutokea kwa CCM.
Kama wewe ni CCM basi chuki yako ni Mahanga kukushinda au ndugu yako kwenye kura za maoni 2010. Kwa upande wa CDM tunajua wanamchukia Mahanga kwa mambo mawili: 1. Kuwashinda mahakamani, 2. Eti kakaa ubunge muda mrefu kuliko mbunge yeyote Dar - miaka 15. Lakini kwa maendeleo huyu ni mtaalamu wa ufuatiliaji na lobbying, na mwaka 2015 atapendwa kuliko mbunge yeyote Dar kwa MAENDELEO, siyo mengine! Juzi nimefuatilia alivyakagua barabara na madaraja yanayojengwa jimboni kwake Segerea, kwa kweli nimemkubali. Barabara zilizojengwa au zinaendelea kujengwa kwa lami: kinyerezi hadi kwa afisa mtendaji, daraja la kinyerezi/Segerea, barabara ya Segerea -barracuda-liwiti-bima, barabara ya barracuda- vingunguti, barabara ya st. Mary, barabara ya kimanga-Mazda, barabara za kata ya vingunguti na daraja la vingunguti. Ikumbukwe ile stendi ya Segerea mwisho alijenga kwa akili na lobbying yake binafsi kwani haikuwa kwenye mpango wowote wa manispaa wala tanroads. Na sasa tayari amesha lobby barabara zifuatazo zinaanza kujengwa kwa lami karibuni: kinyerezi-kifuru, kinyerezi-ulongoni-kiltex gongolamboto, tabata dampo-kigogo, barracuda-chang'ombe-Mazda- maji chumvi- Makoka-kilungule kimara, Segerea oil com-Segerea seminari-majumba Sita relini, Segerea-bonyokwa-kimara mavurunza, na kubwa yake kuboresha kata nzima ya kiwalani kwa barabara za lami, mifereji, maji, taa za barabarani n.k. Na hiyo juzi kasema kwa upande wa maji kwa sasa mgao umeboreshwa maeneo mengi ya jimbo lake, pia wanaongeza visima, lakini mwanzoni mwa mwaka 2015, tatizo la maji Segerea litakwisha kabisa kwa mipango ya mradi wa Ruvu Juu. Kwa kuwa Mahanga anachukiwa tu kama Mahanga si kwa kushindwa kuleta MAENDELEO, nadhani kwa kuwa amekuwa mbunge toka mwaka 2000 wakati wana JF wengi walikuwa darasa la 3-7, ashauriwe tu mwaka 2015 aache kugombea Segerea, lakini kwa maendeleo haya mwana CCM yeyote atakayemwachia atapeta bila shaka yoyote. Sasa nyie mnaomchukia Mahanga ni maendeleo gani hayo mnataka? Aje kuwaletea pesa na chakula majumbani kwenu? MKUBALI CHUKI NI KUSHINDA ILE KESI AMBAYO HAIKUWA NA KICHWA WALA MIGUU. HATA WANASHERIA WALIOBOBEA WA CHADEMA WALIMSHAURI MPENDAZOE AACHANE NAYO LAKINI KWA UBISHI WAKE WA TOKA UTOTONI ALING'ANG'ANIA AKISAIDIWA NA KIBATALA. HIVI MWANASHERIA GANI WA MAANA WA CHADEMA MLIMWONA ANAFUATILIA ILE KESI? MNABAKI OOH ALIBEBA MASANDUKU! KWANI YEYE AFISA TUME? VINGINEVYO MNAMCHUKIA MAHANGA KWA UMRI WAKE, SURA YAKE MBAYA, AU KUKAA MIAKA 15 BUNGENI - LAKINI KWA HAKIKA SI MAENDELEO.
 
Samahani sana bwana Kiboko, nimeshindwa kukuvumilia kwa hiki ulichochangia. Mimi ni Mwanaukonga, niko Kivule Muembeni, na ni mkazi wa Kivule toka mwaka 2001, kwa kifupi katika majimbo mabovu kabisa, mabovu kabisa kwa miundo mbinu ya Barabara na Maji ni Ukonga hususan barabara tatu (Banana Kivule hadi Msongola, Banana Mwanagati na Mombasa Kwa diwani au kwa Mkuremba. Haisaidii kuja kusema uongo humu JF wakati ni kweli, sisi wa Kivule tunashindwa hata kuendesha gari aina ya Saloon, ni lazima uwe na Prado, RAV4 au SUZUKI (Punda), hali ni mbaya sana. Kuhusu maji, uyasemayo si kweli kwamba kuna Dawasa, isipokuwa kwa kuwa nyumba nyingi zimejengwa na waliohamia ambao kidogo wanajiweza, hivyo kila mmoja amechimba kisima, na maji yake ukibahatika ni mazuri hayana chumvi. Acha Propaganda bwana, hii CCM tumeanza nayo tangia TANU, si yako peke yako na wala usilete ushabiki wa Kichama katika hili. We from Kivule are very serious on this matter. We no longer entertain with the so called CCM or the current MP, she is completely impotent. Tafadhali tuombe radhi wana Ukonga na wala si masuala ya kivyama hapa ila Jimbo letu lina barabra mbovu sana.

Ndugu yangu Mipangomingi hakika ni mwendawazimu tu anayeweza kusimama na kusema jimbo la Ukonga lina maendeleo.

Umaarufu mkubwa wa Chadema sasa Jimboni Ukonga kwa kiasi kikubwa unachangiwa na Mateso ya wananchi.

Nilisema awali niliwahi kutoka Mombasa mpaka Bombambili kwa nauli ya 6000/- kwenda na kurudi.Je ni watu wangapi wana uwezo huo?

Hata hivyo nimefurahi kitu kitu kimoja kwamba wananchi sasa wamejitambua na kwa kiasi kikubwa Chadema wamefanikiwa kuwaaminisha wananchi kwamba mateso yao yametokana na kuchagua CCM.
 
Last edited by a moderator:
Labda unazungumzia maendeleo ya kisangoma ambayo yanaonwa na wachawi peke yao!
Ukonga kuna maendeleo gani ambayo hata wewe mwenyewe mfuasi wa mwaiposa unaweza kuyataja?
Barabara ni utata mtupu. Shule/Elimu utata mtupu. Vituo vya Afya mgogoro mtupu. Masoko mgogoro mtupu. Na maji ndiyo kabisaaa huwezi kuthubutu kuyataja! Sasa wewe tuambie ni kipi kina afadhali katika hayo makuu niliyoyataja!

Mkuu si ajabu huyu mtu ni mlinzi wa shule za Mwaiposa ndiyo maana ni yeye pekee anayeona maendeleo ya Ukonga.
 
Ameniboa sana huyu jamaa, tena ameniharibia siku. Jimbo la Ukonga lina Maendeleo? kwanza binafsi hata huyo Mbunge simjui japo ni mkazi wa Kivule toka 2001-huwa naonyeshwa alama zake tu, Jamaa wa ajabu sana na inaonyesha hajwahi fika huko tunakosema. Ukipita Banana pale unatamani utoe lift kwa watu wote jinsi wamama wanavyoteseka kwa usafiri. Barabara mbovu, magari mabovu, hakuna maji, shule zero tupu, Afadhali watu umeme tu kidoogo.

Mkuu nikuhakikishie hata wanachama wengi wa CCM hawamfahamu huyu mbunge.Sijui walipatwa na shetani gani mwaka 2010 wakamchagua huyu mbunge.

Niliwahi kumsikia mara moja tu bungeni akizungumzia tatizo la soko la Karafuu za Zanzibar.Huyu mbunge ni Janga kubwa.
 
Kama wewe ni CCM basi chuki yako ni Mahanga kukushinda au ndugu yako kwenye kura za maoni 2010. Kwa upande wa CDM tunajua wanamchukia Mahanga kwa mambo mawili: 1. Kuwashinda mahakamani, 2. Eti kakaa ubunge muda mrefu kuliko mbunge yeyote Dar - miaka 15. Lakini kwa maendeleo huyu ni mtaalamu wa ufuatiliaji na lobbying, na mwaka 2015 atapendwa kuliko mbunge yeyote Dar kwa MAENDELEO, siyo mengine! Juzi nimefuatilia alivyakagua barabara na madaraja yanayojengwa jimboni kwake Segerea, kwa kweli nimemkubali. Barabara zilizojengwa au zinaendelea kujengwa kwa lami: kinyerezi hadi kwa afisa mtendaji, daraja la kinyerezi/Segerea, barabara ya Segerea -barracuda-liwiti-bima, barabara ya barracuda- vingunguti, barabara ya st. Mary, barabara ya kimanga-Mazda, barabara za kata ya vingunguti na daraja la vingunguti. Ikumbukwe ile stendi ya Segerea mwisho alijenga kwa akili na lobbying yake binafsi kwani haikuwa kwenye mpango wowote wa manispaa wala tanroads. Na sasa tayari amesha lobby barabara zifuatazo zinaanza kujengwa kwa lami karibuni: kinyerezi-kifuru, kinyerezi-ulongoni-kiltex gongolamboto, tabata dampo-kigogo, barracuda-chang'ombe-Mazda- maji chumvi- Makoka-kilungule kimara, Segerea oil com-Segerea seminari-majumba Sita relini, Segerea-bonyokwa-kimara mavurunza, na kubwa yake kuboresha kata nzima ya kiwalani kwa barabara za lami, mifereji, maji, taa za barabarani n.k. Na hiyo juzi kasema kwa upande wa maji kwa sasa mgao umeboreshwa maeneo mengi ya jimbo lake, pia wanaongeza visima, lakini mwanzoni mwa mwaka 2015, tatizo la maji Segerea litakwisha kabisa kwa mipango ya mradi wa Ruvu Juu. Kwa kuwa Mahanga anachukiwa tu kama Mahanga si kwa kushindwa kuleta MAENDELEO, nadhani kwa kuwa amekuwa mbunge toka mwaka 2000 wakati wana JF wengi walikuwa darasa la 3-7, ashauriwe tu mwaka 2015 aache kugombea Segerea, lakini kwa maendeleo haya mwana CCM yeyote atakayemwachia atapeta bila shaka yoyote. Sasa nyie mnaomchukia Mahanga ni maendeleo gani hayo mnataka? Aje kuwaletea pesa na chakula majumbani kwenu? MKUBALI CHUKI NI KUSHINDA ILE KESI AMBAYO HAIKUWA NA KICHWA WALA MIGUU. HATA WANASHERIA WALIOBOBEA WA CHADEMA WALIMSHAURI MPENDAZOE AACHANE NAYO LAKINI KWA UBISHI WAKE WA TOKA UTOTONI ALING'ANG'ANIA AKISAIDIWA NA KIBATALA. HIVI MWANASHERIA GANI WA MAANA WA CHADEMA MLIMWONA ANAFUATILIA ILE KESI? MNABAKI OOH ALIBEBA MASANDUKU! KWANI YEYE AFISA TUME? VINGINEVYO MNAMCHUKIA MAHANGA KWA UMRI WAKE, SURA YAKE MBAYA, AU KUKAA MIAKA 15 BUNGENI - LAKINI KWA HAKIKA SI MAENDELEO.

Rudi kwenye mada---Maendeleo ya Jimbo la Ukonga.
 
Jimbo la Ukonga ni kati ya majimbo ambayo CCM ina hali ngumu sana na hii ni kutokana na maendeleo duni katika jimbo hilo. Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa ni kati ya wabunge ambao hawaongei chochote cha kupigania Jimbo lake. Ni mbunge ambaye ameshindwa kufanya mkutano wowote wa hadhara Jimboni kwake kwa aibu ya kuzomewa na kushindwa kujibu kero za wananchi.

Jimbo la Ukonga barabara zake asilimia 90% ni mbovu na hazipitiki kabisa kipindi cha mvua.Kutokana na ubovu wa barabara hizo kipindi cha mvua wananchi wanatozwa mpaka shilingi 1000/- kutoka kituo kimoja hadi kingine. Hali hiyo imekuwa ni kicheko na mbeleko kubwa kwa chama cha CHADEMA. Kwa sasa CHADEMA ndio inashikilia siasa za Ukonga na wamekuwa wakifanya mikutano mfululizo kwenye matawi na Kata. Kunawiri kwa CHADEMA Jimboni Ukonga kunachangiwa pia na viongozi wa chama hicho ngazi ya Jimbo kushirikiana kwa pamoja kuimarisha chama kwa kufanya kazi bila kuchoka.

CHADEMA wamekuwa wakiwaeleza wazi wananchi kwamba mateso yao yanatokana na kuichagua CCM kwenye uchaguzi uliopita. CHADEMA imekuwa ikiwapa mfano wa majimbo ya Ubungo na Kawe yanayoshikiliwa na CHADEMA jinsi wabunge wake wanavyopiga kelele na jinsi kulivyo na maendeleo makubwa katika majimbo yao. Ni ukweli ulio wazi kwa hali ya CCM jimboni Ukonga ni ya kusikitisha sana.Matawi mengi yanafungwa na kugeuzwa kuwa ngome za CHADEMA.

Na endapo hali ikiendelea hivi hivi ni wazi CHADEMA itapata ushindi mkubwa kwenye jimbo hili uchaguzi ujao na idadi kubwa ya madiwani. Wanachpaswa CHADEMA tu ni kuteua wanachama wanaokubalika kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.

Hii ni Tathmini yangu binafsi baada ya kuzunguka kata zote za Ukonga kwa ziara binafsi kwa kipindi cha wiki mbili.

Huyu mama ni janga la kitaifa
 
Kwani jamvi hii ni ya wana CDM pekee? Na mbona michango ya wachangiaji na yenyewe imepata counter arguments mara nyingi tu humu wala si mimi wa kwanza?

Mkuu acha Porojo.

Nitajie mambo matano tu yaliyopiganiwa na mbunge Eugene Mwaiposa kuhusu Ukonga.

Pili nielezee kuhusu barabara za Ukonga kipindi cha mvua.
 
Ninatoka katika kijiji kilichopo Mbozi Magharibi.

nimefika mbozi... sasa sijui ni kijiji gani maana tunapolinganisha basi tuwe wakweli au realistic; jimbo la ukonga ni kubwa na kuna sehemu zina barabrara nzuri zaidi kuliko mbozi mbagharibi and vice versa

tofauti labda ni ule utelezi wakati wa mvua na wale ngombe na nguruwe wanaofugiwa chini ya mti kwa kufungwa kamba kwenye miguu badala ya shingoni
 
Kama huku kusini, jimbo la mbinga mashariki na magharibi hatuna wabunge, mfano barabara ya kutoka nyoni kuelekea tingi hali ni mbaya sana, wakandarasi feki wameharibu barabara kuliko ilivyokuwa zamani!
 
nimefika mbozi... sasa sijui ni kijiji gani maana tunapolinganisha basi tuwe wakweli au realistic; jimbo la ukonga ni kubwa na kuna sehemu zina barabrara nzuri zaidi kuliko mbozi mbagharibi and vice versa

tofauti labda ni ule utelezi wakati wa mvua na wale ngombe na nguruwe wanaofugiwa chini ya mti kwa kufungwa kamba kwenye miguu badala ya shingoni

Hakuna njia unayoweza kutumia kumsafisha huyu mbunge wa Ukonga.

Tena utaonekana ni kituko hapa Jamvini kujaribu kufananisha maendeleo ya barabara za Ukonga iliyoko katika Jiji kuu la DSM kilomita chache kutoka Ikulu ya Tanzania na barabara za Mbozi iliyoko maelfu ya Kilometa kutoka DSM.

Mwambie Eugene Mwaiposa amechokwa na hana thamani yoyote hapa Ukonga.Kilio cha kinamama kutoa nauli 1000/- ndiyo laana kwa mbunge huyu.
 
Back
Top Bottom