GE2025 Shingo: Ukonga nichagueni niondee michango batili na kusimamia haki

GE2025 Shingo: Ukonga nichagueni niondee michango batili na kusimamia haki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bakari Shingo, amesema uteuzi wake si wa bahati mbaya bali ni dhamira ya chama chake kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi wa Ukonga zinapatiwa ufumbuzi.

Akizungumza Septemba 15, 2025 katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mombasa, Kata ya Ukonga, Shingo amesema wananchi wa jimbo hilo wamesumbuliwa kwa muda mrefu na ukosefu wa maendeleo licha ya kuwa na viongozi waliopata nafasi kubwa serikalini.

“Hatugombei kwa bahati mbaya, tumegombea kwa sababu tumevurugwa. Kijana tuliyemuamini ameshindwa kutulipa hisani. Hatujapata mwakilishi anayeishi na kushirikiana na wananchi wake. Ndiyo maana tumeamua kusimama kudai haki ya watu wa Ukonga,” amesema Shingo.

Amezitaja changamoto zinazolikabili jimbo hilo kuwa ni pamoja na ukosefu wa stendi ya mabasi, soko, miundombinu duni, msongamano wa wanafunzi mashuleni, michango isiyo halali katika shule na mfumo mpya wa ulipaji vibali vya marekebisho ya nyumba bila elimu kwa wananchi.

Aidha, amesema wananchi wa Ukonga wanapaswa kutambua kuwa huu ndio wakati sahihi wa kuchagua mabadiliko yatakayokomesha ufisadi na kuleta maendeleo halisi katika jimbo hilo.

Kwa upande wake, uongozi wa ACT Wazalendo umewashukuru wananchi na wanachama waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni, wakisisitiza kuwa ni wakati wa kuchagua viongozi bora watakaosimamia masilahi ya jamii.

Chanzo: Jambo Tv​
 
Back
Top Bottom