Christiano Ronaldo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 258
- 41
TENA 10 SI 5:-Mkuu acha Porojo.
Nitajie mambo matano tu yaliyopiganiwa na mbunge Eugene Mwaiposa kuhusu Ukonga.
Pili nielezee kuhusu barabara za Ukonga kipindi cha mvua.
1. Barabara ya mombasa - kivule pale Mombasa mwanzoni ukonga palikuwa si barabara bali korongo lakini pamejengwa kwa lami na mradi unaendelea kila mwaka.
2. Barabara ya banana kitunda ilifikishwa na Mahanga mbele kidogo ya reli ya tazara lakini mwaiposa ameendeleza kidogo na bado kidogo itafika kitunda stendi
3. Barabara kivule na kipunguni b imeboreshwa hata kama si kwa lami
4. Barabara ya mvuti Msongola inaendelea kujengwa kwa lami na sasa karibu inaungana na mpaka wa Msongola na chamazi
5. Barabara ya kiltex kuelekea Pugu mnadani imeboreshwa sana.
6. Barabara ya nzasa imeboreshwa
7. Hili ndilo jimbo lililojenga shule nyingi za wananchi za sekondari kuliko jimbo lolote Dar miaka ya hivi karibuni - shule 22
8. Mwaiposa amehamasisha sana akina mama na kuwasaidia kuanzisha vicoba na saccos ili kuondokana na umasikini wao na akina mama wengi wanampenda kwa hilo.
9. Juzi ameahidiwa visima virefu vitano vya maji kwenye jimbo lake baada ya kumbana waziri wa maji ili kuongezea visima vilivyopo.
10. Kwa ufuatiliaji wake zahanati za jimbo la ukonga zimeboreshwa sana - nenda kazitembelee
Kuhusu barabara wakati wa mvua, lazima tujue kwamba miaka michache iliyopita maeneo mengi yalikuwa mapori yenye mabonde na mito kadhaa hivyo itachukua muda kidogo kuboresha jimbo hilo lifikie majimbo mengine ya wilaya ya Ilala yaani segerea na Ilala. Hivyo haishangazi hali ya barabara wakati wa mvua kuwa mbaya, lakini zinaendelea kuboreshwa na mwaiposa na serikali ya CCM. Aidha kwa sasa ndipo watu wengi wanahamia ukonga hivyo na maendeleo yatakwenda kwa kasi zaidi sasa.