CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

Kufukuza madiwani ndiyo sahihi kabisa kuliko kushinda umeya ukiwa na viroboto kama wale.kwa sasa chama kiko safe pamoja na kupoteza.Tunataka viongozi wanaochukua maamuzi kama kagame, tunahitaji uongozi kama wa cdm.Mbona hata ccm walipoteza arumeru yote sawa tu kinachohitajika ni uongozi imara ndani ya chama siyo sifa ya kushinda, maana kushinda unaweza kushinda hata kwa kuiba kura hapo utasema una uongozi bora????? tafakarini nawapa hongera cdm kwa kufukuza madiwani na pole kwa kushindwa ndiyo matokeo ya kushindana songeni mbele.
 
Nchi hii sasa ni ya matapeli na wezi kila kona! Namwonaga kwenye Tv yule Mayor wa JIji la London anavyowajibika hadi naona wivu. KATIBA MPYA ijayo ma-Mayor wachaguliwe moja kwa moja na WANANCHI. Tabia ya sasa ya Mayor wa JIji kubwa kama la Mwanza kuchaguliwa na watu 11 tu ni AIBU.

tena it is a total loss
 
Katika kuonyesha jinsi Nape anavyowapeleka puta CDM kwasasa nchini kaingia Mwanza siku tatu baada ya Dr. Slaa,kaongoza kikosi kazi cha ccm mpaka wamechukua jiji la Mwanza baada ya kuwagaragaza cdm kwa kura 11 kwa 8 za cdm!

Nimefuatilia. Vikao vya mikakati hapa jiji Mza vikiongozwa na Nape na DR. Slaa kila moja kwa style yake! Jana usiku saa mbili nikashuhudia DR. Slaa aliyekuwa kaambatana na Mpendazoe wakiondoka Mwanza kwa ndege ya precion kurudi Dar, nikajua Nape kawazidi akili nao wamejua!
Hongera Nape, pole sana Dr. Slaa!
 
Niko mjini katikati na hamna shangwe yoyote, hiyo yako iko wapi?.Dr. Salaa hayuko Mwanza toka jana, huyo aliyekuwepo jiji umemtoa wapi?, au ulikuja nae kutoka nyumbani?
 
Nadhani CHAGULANI na wenzie sasa roho zao zimefurahi na kutulia sasa?! is it not what you wanted Chagulani?!
 
Niko mjini katikati na hamna shangwe yoyote, hiyo yako iko wapi?.Dr. Salaa hayuko Mwanza toka jana, huyo aliyekuwepo jiji umemtoa wapi?, au ulikuja nae kutoka nyumbani?

Weye hayupo!! hebu ongea ukweli kaondoka lini saa ngapi au unabuni.
 
Yasemekana dokta hayupo tena mwanza, baada aya matokeo kutangazwa alitoka nje fasta na kutokomea kusiko julikana, ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa dokta
Bora kukosa umeya kuliko kubaki na wale wanafiki!! Huyu Meyor asifike Mitaa yetu ya Bugarika
 
Yasemekana dokta hayupo tena mwanza, baada aya matokeo kutangazwa alitoka nje fasta na kutokomea kusiko julikana, ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa dokta
Aibu gani? Unamfahamu vizuri aliyeshinda? Hivi kuwanunua watu 11 ni kazi kubwa kwa tapeli kama Mabula?
 
Umeya umeenda CCM kwa sababu viongozi wa CHADEMA ni madikteta. CCM ahufukuzwi unajitoa mwenyewe.
Jifunze ku argue kwa fact kama wengine,mbona wewe upo kama shoga ake na anty kessy? Wewe ni blaablaa mchana kutwa hakuna hata hoja unayoibua inayoweza kujisimamia!!unakera mno!!muige mwenzio ritz,ni msema kweli japo yupo ccm.
 
Umekasirika? Mambo ya ushoga yametoka wapi? Acha matusi mimi sijui kutukana.
 
Hongera meya mpya. Maslahi ya wananchi mbele, achana na taarab za kisiasa
 
MODS ; Hii thread msije kuichakachua na kuiunganisha na zingine kwani zile ni za matokeo na hii ni hali halisi ilivyo mwanza hizi sasa

Ndugu wana JFKama mlivyo kwisha sikia katika mitandao ya kijamii na vyombo mbali mbali vya habari, cdm wamebwagwa kwa ushindi wa sunami na ccm kwenye kiti cha meya wa jiji la mwanza ambacho ndio muhimu kuliko hata kile cha ilemele ambacho kitatoa mwenyekiti wa manispaa. Kwa hali ilivyo hivi sasa haya ndio yaliyotoke na yanayo endelea kutokea:

1. baada tu yakutangazwa matokeo ndani ya ukumbi wa uchaguzi, dr Slaa ambae alikuwapo wakati wa uchaguzi alionekana ni mwnye huzuni na simanzi kubwa , na hakukaa tena bali aliondoka haraka. Hata waandishi wa habari walikuwa wanamtafuta wamuhoji hakuonekana tena, sasa sijui ni aibu yakushindwa ama lipi.

2. baada ya matokeo kutangazwa vifijo na nderemo vilikuwa vingi kiasi cha kwamba watu walikuwa hawasikilizani kabisa. Na hapo basi , sherehe za ushindi zilihamia mpaka nje na kusambaa katikati ya jiji la mwanza na kufanya shughuli nyingine kusimama, mpaka sasa shughuli zimesimama na sherehe zimetapakaa mji mzima huku foleni za magari zikiwa ndefu.

3. meya mteule wa jiji la mwanza anategemewa kuongea na wananchi wa jiji kutoa shukrani zake na imani yake yakulitumikia jiji hili kwa weledi mkubwa na uliotukuka

Kwa sasa ni hayo tu, ntawaletea kitakacho jiri zaidi.

Asante kwa Taarifa!! CCM ni Baba lao na kitaendelea kuwa hivyo MILELE!!!
 
Katika kuonyesha jinsi Nape anavyowapeleka puta CDM kwasasa nchini kaingia Mwanza siku tatu baada ya Dr. Slaa,kaongoza kikosi kazi cha ccm mpaka wamechukua jiji la Mwanza baada ya kuwagaragaza cdm kwa kura 11 kwa 8 za cdm!

Nimefuatilia. Vikao vya mikakati hapa jiji Mza vikiongozwa na Nape na DR. Slaa kila moja kwa style yake! Jana usiku saa mbili nikashuhudia DR. Slaa aliyekuwa kaambatana na Mpendazoe wakiondoka Mwanza kwa ndege ya precion kurudi Dar, nikajua Nape kawazidi akili nao wamejua!
Hongera Nape, pole sana Dr. Slaa!

ficha upumbavu wako.dr. Slaa leo alikuepo kwenye uchaguzi wewe unasema aliondoka jana saa 2 usiku.!
 
Back
Top Bottom