CCM yadaiwa kuwapa kichapo walimu Tarime

Acha wapigwe tuu labda akili zitawaingia, chama cha mboga mboga kimekua kinawatumia kama toilet paper kila mara wakiambiwa wanaona wana tukanwa sasa ndio malipo yao hayo, wapigwe tuu
 
Wapi Mpwayungu Village [emoji2369][emoji3]

Ukuje huku utupe kisa na mkasa wa jamaa zako.

Kuliko hasa?! [emoji3]
 
Kama ni kweli basi hao Green Guard kuwajibishwa na kulaaniwa. Vijana wa aina hiyo hufanya chama kuchukiwa. Chama cha PF Zambia kiling'olewa madarakani kwa kuendekeza vijana kama hao. CCM tusiige huo ujinga.
 
Wanawatumia kwenye uchaguzi na mapokezi ya misafara ya wageni [emoji14][emoji14]
 
Kuna tuhuma kuwa kule Tarime Kamati ya siasa wilaya Tarime ikiongozwa na mwenyekiti wake anaefahamika kama Ngicho, mkuu wa wilaya, wabunge pamoja na viongozi wengine wa chama waliwaamuru vijana wa CCM (Green guard) kuwashambulia walimu wa shule ya msingi Nkende baada kutokea kutokuelewana baina yao na walimu, vile vile kaimu afsa elimu aliyekuwa anapinga walimu hao kushambuliwa na green guard nae alipokea kichapo toka kwa vijana hao.

Kwa mujibu wa chanzo changu cha habari waandishi waliokuwepo katika msafara huo walipigwa stop kuripoti tukio huku walimu hao wakinyimwa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu, chanzo changu kinaendelea kutabainisha kuwa walimu hao wamepewa vitisho wasiongee na chombo chochote cha habari, na mkuu wa mkoa wa Mara, Mtanda amefika leo kusawazisha mambo.
CCM Hoyeee

CM 1774858 naona ilani inatekelezwa vyema huko Tarime.
 
Safiii sanaaa wapigwe saaana!! maana wanaibiaga ichochama kura wanaficha kwenye mapichu. Nlikuwa wakala wachama 2020 unashangaa mnapohesabu karatasi zinakaarufu kapapu...!!
 
Ni kweli haya mambo yametokea nkende primary TARIME MJI.
 
Kuna tuhuma kuwa kule Tarime Kamati ya siasa wilaya Tarime ikiongozwa na mwenyekiti wake anaefahamika kama Ngicho, mkuu wa wilaya, wabunge pamoja na viongozi wengine wa chama waliwaamuru vijana wa CCM (Green guard) kuwashambulia walimu wa shule ya msingi Nkende baada kutokea kutokuelewana baina yao na walimu, vile vile kaimu afsa elimu aliyekuwa anapinga walimu hao kushambuliwa na green guard nae alipokea kichapo toka kwa vijana hao.

Kwa mujibu wa chanzo changu cha habari waandishi waliokuwepo katika msafara huo walipigwa stop kuripoti tukio huku walimu hao wakinyimwa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu, chanzo changu kinaendelea kutabainisha kuwa walimu hao wamepewa vitisho wasiongee na chombo chochote cha habari, na mkuu wa mkoa wa Mara, Mtanda amefika leo kusawazisha mambo.
Chama Cha Majambazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom