Kilimanjaro: Wananchi wafikia hatua kulinda ugali wezi wasipite nao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Ukweli ni kwamba hali hairidhishi kijijini Msaranga wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kutokana na upungufu wa chakula

Anayelalamika hali iliyotawala, Pulceria Marandu, mkazi wa Kitongoji cha Kwasuva kijijini Msaranga, anatumia kauli: "Ukipika ugali, ukienda chooni au kutafuta sahani chumbani au kuhemea maji, ukirudi wezi wameiba sufuria yenye ugali. Chakula chenyewe tunakwenda kuhemea huko ukanda wa juu kwa kufanya vibarua.

Shida ni nini na kipi kilichotawala? Ni swali kuu ambalo Nipashe inalazimika kutembea nalo kupata ufafanuzi kijijini huko.

Pulceria, mjane na mama wa watato wanane, analalamika maisha yao yamezidi kuwa magumu kutokana na wezi hao ambao kwa sasa wameachana na wizi wa kuku na mbuzi, wamegeukia kwenye wizi wa chakula kilichopikwa.

Mama huyo anasema tatizo hilo jipya kijijini huko limechangiwa na uhaba wa chakula unaowakabili wakazi wa vijiji vingi vilivyoko wilayani humo, hasa kwa ukanda wa chini kutokana na kutokuvuna chakula.

Pulceria anasema kwa sasa hali imekuwa ngumu kwa kuwa hakuna chakula wala biashara wanazoweza kufanya katika kijiji hicho.

"Wengi wetu hujishughulisha na vibarua vya mashambani pamoja na ukataji wa majani kwa ajili ya kuuza lakini kwa sasa hakuna kazi, hatupati vitu kama hivyo, hivyo inatuwia vigumu kupata riziki ya kila siku.

"Kwa sasa mimi siwezi kufanya kazi kutokana na kuumwa, watoto wangu huwa wanakwenda kuhangaika huku na huko, wakipata tunakula, wakikosa tunalala, hatuna uhakika wa maisha. Vibarua wanavyotafuta ni vya kuchimba mashimo na shughuli zozote, hakuna mwenye kazi ya uhakika," anasema.

Anasema tangu mumewe afariki dunia miaka 16 iliyopita, amepambana kuwalea watoto wake, akiwasomesha na kumaliza elimu ya msingi na mmoja kuendelea na masomo ya sekondari, sasa akiwa kidato cha pili, kukiwa na ugumu katika kufanikisha mahitaji ya shuleni.

Suzan Grigori, mjane na mama wa watoto saba kijijini Msaranga, anaungana na mtangulizi wake, Pulceria, kupaza sauti dhidi ya uhaba wa chakula unaowakabili, akibainisha wanakula mlo mmoja kwa siku, huku akiutaja ukame kuwa mzizi wa madhila hayo.

Anasema kuwa wakati mwingine hulazimika kutembea Km 20 hadi 25 kwenda ukanda wa juu kutafuta chakula kutokana, akikiri watoto wake watatu kati ya saba wamelazima kuondoka nyumbani na kwenda kujitafutia vibarua ili wasaidie upatikanaji wa chakula kwa familia yake.

"Licha ya kukipata chakula kwa shida, kuna tatizo la wizi wa chakula, ukipika chakula ni lazima uhakikishe unakilinda na unakula hadi kiishe bila kunyanyuka, hapa hatuna umeme katika kitongoji chetu na wezi wa vyakula ni wengi.

"Kwa kweli hadi sasa hatuwezi kujua ni nani anaiba chakula maana tupo mpakani mwa Kenya na Tanzania na vijana wa kifugaji hutembea tembea huku kwa lengo la kutafuta malisho. Tunashindwa kuelezea nani anayefanya kitendo hicho," anawasilisha kilio chao.
ucia Corineli (55), mama wa watoto wanne na mkazi wa eneo hilo, anaendelea mazungumzo ya Suzan na Nipashe katika kudadisi kinachojiri kijijini huko, akitamka:

"Ninamshangaa Mungu ninavyoamka salama, maana kulala njaa kwa siku mbili tatu kwangu ni kawaida, na nimelazimika kuwatoa mabinti zangu waliomaliza kidato cha nne wameenda huko kwa ndugu zangu wakawasaidie ili wapate chakula, sitaki niwaone wanavyokufa kwa njaa hapa.

"Kama hali itaendelea kuwa hivi, mimi siwezi kufika mwaka 2023, hakuna maji, hakuna umeme, hakuna chakula. Akipatikana mfadhili, ninaomba anisomeshee watoto wangu ili wakue na wamudu kujitegemea kimaisha.

"Mimi nipo karibuni kufa japo sijakata tamaa, ninalima na kupanda labda mvua itanyesha na nitapata chakula. Tunaomba serikali kuchukua hatua za haraka, kwa sasa kuna wizi mkubwa wa chakula hasa kilichopikwa."

Anasema hatambui watoto wake wako katika mazingira gani ila anachokijua wako katika maeneo mbalimbali wanapata chakula ili asiwashuhudie wakipata tabu nyumbani kwake, hata kupoteza maisha kwa njaa.

Bathalameo Kilau, mkazi wa Kijiji cha Msaranga, anasema kwa sasa njaa haiepukiki, akiiomba serikali kupeleka haraka chakula cha msaada ili kusaidia wanafunzi, watu wenye ulemavu, wajane na wananchi wote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za chakula.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwasuva, Fransic Shirima anasema tatizo uhaba wa chakula linaathiri kwa kiwango kikubwa wanafunzi, akibainisha baadhi yao sasa wanalazimika kukacha vipindi vya masomo na hawana uwezo wa kushiriki masomo ya ziada na michezo kutokana na kutopata chakula.

"Tunaomba msaada wa chukala hasa kwa wanafunzi ili wasome kwa bidii na kufanya mabadiliko katika mitihani yao ya kitaifa. Pia kuna wizi wa vyakula ingawa tayari tumeshatoa taarifa katika vijiji na tumeahidiwa kuundwa sungusungu kwa ajili ya kutokomeza hilo," anasema.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Msaranga, Fratern Arsen anakiri eneo lake la kazi kukabiliana na shida katika upatikanaji wa huduma ya maji, pia kuibuka wizi wa chakula nyumbani.

"Kuna baadhi ya shule zilizoko katika kijiji changu watoto hawali ugali, bali uji, tena kwa siku moja moja. Walimu wanalalamika watoto wanapofundishwa hasa nyakati za mchana wanalala sana na walimu wanapowahoji, hulalamika njaa, unakuta nyumbani alilala bila kula na anakuja huku shuleni nako hakuna chakula, hali ni mbaya, hatujui matokeo ya mitihani hasa ya taifa itakuwaje.

"Kuna utaratibu wa sungusungu unakuwapo, lakini hali kiuchumi ni mbaya, mifugo inakufa. Kwa kweli wananchi wanahangaika," anasema Arsen.

Mathias Assenga, Diwani wa Kisale Msaranga, anabainisha kata hiyo ina kaya 2,201. Kati yake, kaya 1,137 ziko katika hali mbaya kutokana na kukabiliana na uhaba wa chakula, akiwa na mrejesho kwa Nipashe kwamba tayari wameshatoa taarifa kwa mamlaka husika ili kuzisaidia kaya hizo.

"Hali ya wananchi wetu ni mbaya na tayari timu ya wataalamu imefanya tathmini na kubaini hali halisi. Kwa sasa tunangoja mamlaka zichukue hatua ili kuwasaidia wananchi kujinusuru. Watoto wetu hawawezi kusoma vyema, serikali itunusuru kwa njaa hii," Diwani Assenga anasema.

Kuhusu wizi wa chakula, kiongozi huyo wa kisiasa anasema tayari wameshapatiwa askari polisi katika utaratibu mpya wa Jeshi la Polisi kupeleka huduma hadi ngazi ya kata. Anasema askari huyo ameanza kuunda sungusungu katika vitongoji 20 vya kata yao vitakavyosaidia kutokomeza uhalifu, ukiwamo wizi wa chakula.

Mararie Lyimo, Diwani wa Mwengwe wilayani Rombo anasema kinachoshuhudiwa Kata ya Kisale Msaranga, kinavikabili pia vijiji vitatu ndani ya kata yake, kimoja kikiwa katika hali mbaya zaidi na hatua walizochukuliwa ni kuliwasilisha suala hilo kwa uongozi wa halmashauri.

"Tuna vitongoji 12 katika kata yangu, ila hali ya njaa ni kubwa sana katika Kijiji cha Mfuriashi, tulishaongea na mkurugenzi wa halmashauri ili kuandika andiko la kuona namna ya kupata chakula cha bei nafuu kwa ajili ya wananchi," anasema.

Godwin Chacha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, anasema timu ya wataalamu imeshafanya tathmini ya hali halisi, ikibaini baadhi ya kaya zinakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na ukame uliolikumba eneo hilo katika misimu minne mfululizo iliyopita.

"Halmashauri imechukua hatua za kutuma wataalamu kama tulivyoelekezwa na mkoa na tayari tumeshapeleka maombi katika ghala la taifa ili tupewe chakula kwa bei nafuu," anasema Chacha.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, akiwa katika kikao na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ofisini kwake mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, aliwataka kufanya tathmini ya kina na kuona kama kuna uhaba wa chakula ili kuomba chakula cha bei nafuu serikalini.

Kiongozi huyo pia alitoa angalizo kwa viongozi hao, akiwataka kusimamia utolewaji wa chakula hicho ili kisinunuliwe na wafanyabiashara na baadaye kuuzwa kwa wananchi kwa bei ya juu.

"Tunatambua kulikuwapo uhaba wa mvua kwa misimu zaidi ya mnne mkoani kwetu. Kwa vyoyote kutakuwa na uhaba wa chakula kama watu hawakuhifadhi vyema chakula.

"Wakurugenzi kwa kushirikiana na wataalamu hakikisheni mnafanya tathmini ya kina katika kila halmashauri, ili kuona namna ya kuandika dokezo la kuomba chakula cha bei nafuu. Hatutawavumilia wafanyabiashara watakaonunua vyakula hivyo na kuja kuuza kwa dei ya juu.

"Na ninyi wananchi, wakati serikali yenu inaangalia suala la chakula cha bei nafuu, msiuze vyakula kwa sasa na acheni tabia ya kuwakaribisha wageni nyumbani kwenu ili kunusuru hali ya chakula," Babu aliagiza.

Chanzo: Nipashe
 
Mfalme wao Mbowe alisema Magufuli aliuchukia Mkoa wa Kilimanjaro lkn wakati wa Magufuli Wachaga hawakugombania Ugali kama leo hii, ikumbukwe chanzo cha Habari ni Gazeti la Nipashe wamiliki ni Wachaga wenyewe, hivyo ni kweli Mkoa wa KLM umeshuka kiasi hicho zamani KLM ilikuwa ni Jewel of Tanzania leo hii wanagombea Ugali kwa njaa sijui adui yao ni nani sasa kwa maana Magu hayupo tena isitoshe Magu alishaanza kujenga reli ya kuunganisha KLM na Dar, amejenga daraja la Wami kuwasaidia usafiri alifungua Kiwanda cha viatu Moshi, lkn leo mnagombania ugali?
 
Lile zee lenye kengeza na baga fresh wamejaza funza tu kichwani
Mfalme wao Mbowe alisema Magufuli aliuchukia Mkoa wa Kilimanjaro lkn wakati wa Magufuli Wachaga hawakugombania Ugali kama leo hii, ikumbukwe chanzo cha Habari ni Gazeti la Nipashe wamiliki ni Wachaga wenyewe, hivyo ni kweli Mkoa wa KLM umeshuka kiasi hicho zamani KLM ilikuwa ni Jewel of Tanzania leo hii wanagombea Ugali kwa njaa sijui adui yao ni nani sasa kwa maana Magu hayupo tena isitoshe Magu alishaanza kujenga reli ya kuunganisha KLM na Dar, amejenga daraja la Wami kuwasaidia usafiri alifungua Kiwanda cha viatu Moshi, lkn leo mnagombania ugali?
 
Mfalme wao Mbowe alisema Magufuli aliuchukia Mkoa wa Kilimanjaro lkn wakati wa Magufuli Wachaga hawakugombania Ugali kama leo hii, ikumbukwe chanzo cha Habari ni Gazeti la Nipashe wamiliki ni Wachaga wenyewe, hivyo ni kweli Mkoa wa KLM umeshuka kiasi hicho zamani KLM ilikuwa ni Jewel of Tanzania leo hii wanagombea Ugali kwa njaa sijui adui yao ni nani sasa kwa maana Magu hayupo tena isitoshe Magu alishaanza kujenga reli ya kuunganisha KLM na Dar, amejenga daraja la Wami kuwasaidia usafiri alifungua Kiwanda cha viatu Moshi, lkn leo mnagombania ugali?

Adui ni yule yule hajabadilika toka 1961

Ujinga + usimamizi mbovu wa rasilimani.

Bado watu wetu wengi ni wajinga pia hao wanaojiita serikali maweshindwa kabisa kutoa hata basic needs maji, umeme kama huyo mama amesema.
 
Mfalme wao Mbowe alisema Magufuli aliuchukia Mkoa wa Kilimanjaro lkn wakati wa Magufuli Wachaga hawakugombania Ugali kama leo hii, ikumbukwe chanzo cha Habari ni Gazeti la Nipashe wamiliki ni Wachaga wenyewe, hivyo ni kweli Mkoa wa KLM umeshuka kiasi hicho zamani KLM ilikuwa ni Jewel of Tanzania leo hii wanagombea Ugali kwa njaa sijui adui yao ni nani sasa kwa maana Magu hayupo tena isitoshe Magu alishaanza kujenga reli ya kuunganisha KLM na Dar, amejenga daraja la Wami kuwasaidia usafiri alifungua Kiwanda cha viatu Moshi, lkn leo mnagombania ugali?
Kama Magufuli asingeiba matrillion yetu, mabilion ya rambirambi, kujenga useless international airport na kukomba Hazina na kutapanya hovyo hovyo kwa kuwagawia mahawara zake hali isingekuwa hivi.

Kaondoka na hatarudi. Mfuate huko umsaidie kukusanya kuni.

Nyauww!

Kammoon!
 
Back
Top Bottom