CCM wamekosea kutumia M4C kumnadi Magufuli

Hivi CCM mmeishiwa kiasi hicho? hamuoni aibu kutumia slogan ya mwenzanko tena mshindani wako mkuu? Hii si ni kuconcede defeat? CCM hapa wanaonekana wameshakubali wamezidiwa!

Nyie hamuoni aibu kumtumia mgombea URAIS kutoka CCM
 
Kwa hiyo hawana ubunifu,lazima wanye kilaghai kwa mambo yafananayo na ukawa ili wakubalike
AIBU
K"ma mae
mkuu ccm wameshajuwa hawawezi kupona kwa njia yoyote ndiyo maana wamekosa mwelekeo kama ndege ikiwa angani!
 
Meaning of Logo:
Grouped into twos
1.logotype.
A graphic representation or symbol of a company name, trademark, abbreviation, etc., often uniquely designed for ready recognition.

2.Logogram;
A written symbol representing an entire spoken word without expressing its pronunciation; for example, for 4 read "four" in English, "quattro" in Italian. Also called ideogram, logograph

As the above clarification regarding "Logo" then how many officially logo for Chama Cha Demokrasia na Maendeleo? and if possible,kindly assist to put forward the Authorized copyright for those logo, then from there we can prove it to CCM as a fraud criminal act.otherwise it's better we keep it in dark
 
Kwani anaitumia hyo Logo??Ushamba tu wa watu,ni sawa baadhi yetu wanavyoita Chadema kuwa nı Chaga Development Manifesto au wao wanavyokııta CCM Chama cha majambazi.
 
Mtoa uzi huu ametulia sana. kwa maneno hayo tu unaweza simama mahakamani na tukapata haki yetu.

Kwa vyovyote vile CCM wamechoka na wameishafika mwisho wa kufikiria.

Ikitokea CCM wakashinda Urais Basi Chadema/UKAWA wanahaki ya kudai wamehujumiwa ushindi wao kwa CCM kuwachanganya wanachama wao na Mashabiki wao kwa wao (CCM) kutumia identity yao kichama.

Hii inakubalika kabisa.

Waacheni waendelee na wala msiwashitue kwa maana mwaka huu ni ushindi kwa UKAWA moja kwa moja bila shaka yeyote.
 
chadema kusema watamshitaki mahakamani eti anatumia logo yao kivipi.wao ni MOVEMANT FOR CHANGE.
MAGUFURI FOR CHANGE.
ni tofauti na kusema jamii forum na mwanahalisi forum au cocacola na pepsi cola au azam cola au mo cola.
muwe makini msije mkaingia kichwa kichwa
Kitengo cha propaganda Ukawa kitawachezea mchezo ccm hamtapata pa kutokea kuhusu hilo logo.

swissme
 
Mtoa uzi huu ametulia sana. kwa maneno hayo tu unaweza simama mahakamani na tukapata haki yetu.

Kwa vyovyote vile CCM wamechoka na wameishafika mwisho wa kufikiria.

Ikitokea CCM wakashinda Urais Basi Chadema/UKAWA wanahaki ya kudai wamehujumiwa ushindi wao kwa CCM kuwachanganya wanachama wao na Mashabiki wao kwa wao (CCM) kutumia identity yao kichama.

Hii inakubalika kabisa.

Waacheni waendelee na wala msiwashitue kwa maana mwaka huu ni ushindi kwa UKAWA moja kwa moja bila shaka yeyote.

Dah kwa mawazo yako basi CCM itatawala milele.

Hivi hujui matokeo ya Urais yakishatoka ndio basi tena hayapingwi popote.
 
Na Malisa GJ,

Tangu jana kumekuwepo na mijadala sehemu mbalimbali kuhusiana na matumizi ya logo ya M4C kwa chama cha Mzpinduzi (CCM). Wengine wakisema ni sawa lakini wengine wakisema si sawa.

Sikutaka kulizungumzia hili lakini naona kuna upotoshaji (wa makusudi) unaoendelea, hivyo nimeona nitumie uzoefu wangu ktk taaluma ya Mahusiano (Public Relations) na uelewa mdogo wa Sheria nilionao kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili.

Lakini kabla sijaendelea nimpongeze sana mwanasheria wa CHADEMA John Mallya kwa kutoa msimamo wa Chama kuwa wataifikisha CCM mahakamani kwa kitendo cha kurudufu nembo yao.

Kwa uelewa wangu kinacholalamikiwa si logo tu, kinacholalamikiwa ni kitendo cha CCM kutumia nembo ya utambulisho ya chama kingine (Corporate Identity) ya CHADEMA, while are two oponent parties.

Muaasisi wa Taaluma ya Public Relations, Arthur Page alisema ili kutengeneza utambulisho wako kwa jamii (Corporate Identity) unahitaji kuwa alama zitakazokutambulisha.

Alama hizo ni pamoja na Nembo (Logo), Jina (brand name), Rangi (corporate colour), Mundo wa maandishi (designing) kama ilivyo Cocacola, etc.

Vyote hivi ndio vinatengeneza kinachoitwa utambulisho wa kampuni/shirika/asasi/chama etc.

Nembo ya M4C ni Corporate Identity ya Chama cha Demokrasia na maendeleo na imesajiliwa hivyo. Kwa hiyo CCM au chama kingine kutumia nembo hiyo bila ridhaa au makubaliano maalumu na CHADEMA ni kosa kisheria (Criminal Fraud).

KWANINI CCM WAMEKOSEA.

Sheria zinazolinda haki miliki Tanzania (The copyright and neighbouring Act, ya mwaka 1999 na The Trade and Service marks Act, ya mwaka 1986) pamoja na Sheria za kimataifa zinazolinda haki miliki zinataka kuwe na utouti wa utambulisho kati ya asasi moja na nyingine, bidhaa moja na nyingine, shirika moja na jingine etc.

Utofauti huo unakuwa kwenye maeneo mengi lakini kwa uchache ni kama ifuatavyo;

1. Jina/Brand name.
Jina moja haliwezi kutumiwa na asasi mbili tofauti zinazofanya kazi za kufanana. Kwa mfano Kampuni ya bia ya TBL ikizindua kinywaji kiitwacho "Burudani" kampuni ya Serengeti haipaswi kuanzisha kinywaji chenye jina kama hilo. Sheria inazuia ili kutowachanganya wateja na kulinda haki ya mwanzilishi wa hiyo "brand name".

Kwa hiyo kitendo cha CHADEMA kusajili nembo ya M4C kama "operation brand name" yake kinazuia chama kingine cha siasa kutumia jina hilo. Kwa hiyo CCM kutumia M4C ni kosa kisheria.

2. Muundo/Designing.
Muundo wa maandishi una hati miliki kisheria. Kwa mfano muundo wa neno Cocacola ulivyo ni tofauti na muundo wa neno Pepsi. Cocacola wanaandika kwa kucharaza. Hiyo ni designing yao. Pepsi hawaruhusiwi kuiga muundo huo unless kuwe na makubaliano maalumu na Cocacola.

Sasa CCM kwa ujinga wa kiwango cha "PhD" wameiga muundo wa neno M4C. Bora hata wangeandika kwa muundo mwingine, kwa mfano M-FOR-C, au m4c au namna nyingine itakayotofautisha brand name yao na ya CHADEMA. Lakini wamecopy na kupaste. Hapa haihitaji degree ya sheria kujua kuwa CCM wamekosea.

3. Rangi/Corporate colour.
Unaposajili bidhaa yako au kampuni yako ni vizuri kusajili na rangi yako ya utambulisho.

Kwa mfano hati ya usajili ya Chama cha mapinduzi inatambua rangi za kijani na njano kama rangi zao za utambulisho (corporate colour). Chadema rangi zao ni Blue, nyekundu, nyeupe na nyeusi.

Ukisajili rangi yako ya utambulisho ni kosa kisheria kutumia rangi ya mshindani wako hasa kwenye ulimwengu wa leo wa ushindani wa kimasoko wa "Oligopoly Marketing"

Simba hawaruhusiwi kuvaa jezi za Njano kwa sababu sio rangi yao ya utambulisho, vivyo hivyo Yanga kuvaa nyekundu.

Japo Sheria inatoa ruhusa kubadili rangi ikiwa unaona kuna haja ya kufanya hivyo. Yani ukiona "clients" wako au "audience" wako hawaridhiki na rangi yako unaweza kubadili kwa kufuata taratibu za kisheria. Na si rangi tu bali hata logo au muundo (design).

Ndio maana Vodacom ilianza na rangi ya Blue na nyeupe, lakini wakachange na sasa wanatumia nyekundu na nyeupe. Sheria inaruhusu kubadilisha.

Lakini CCM hawakufanya hivyo. Bado hati yao ya usajili inaonesha rangi zao za utambulisho ni Kijani na Njano, lakini leo wamekurupuka kutengeneza logo ya M4C kwa rangi ambazo si zao. CCM hawana utambulisho wa rangi nyekundu, blue, nyeupe wala nyeusi. Wamezitoa wapi?

Haihitaji elimu ya sheria kujua hawa watu wamekurupuka. Yani baba Njano, mama Kijani halafu mnazaa mtoto mwekundu au mweupe.. haya ni maajabu ya 8 ya dunia.

Haiwezekani baba awe Punda, mama awe Nyumbu halafu mnazaa mtoto Twiga?? Hakuna "cross genetics" ya aina hiyo. CCM u have proved failure.

Nisiwachoshe sana lakini kwa kifupi CCM wamekurupuka mno. Ni kukosa umakini kwa kiwango kikubwa. CCM ina wataalamu wa Sheria, ina wataalamu wa PR and Marketing, ina wataalamu wa Communication, kwanini wanafanya "Technical Mistake" ya kitoto namna hii? Hizi ndio akili za kushauriwa na kina Lusinde (standard seven) na kupuuza wataalamu. Poor u.!

Source:Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!
 
Mtaeza kuishinda serikali ya ccm mahakamani? Endeleeni kuweweseka mwaka huu lazma tuwanyooshe tuu
 
yaani, kampeni manager wao ni January, hapo ndo uwezo wake wa ubuinifi umefikai
 
Mtaeza kuishinda serikali ya ccm mahakamani? Endeleeni kuweweseka mwaka huu lazma tuwanyooshe tuu
Kuna kesi ambayo Serikali ya CCM iliwahi Kushinda? yaani kuanzia kwenye Halmashauri za Wilaya na Taifa.
1. Sakata la EPA imeshindwa na watuhumiwa kuachiwa
2. Madawa ya kulevya kesi zote kubwa imeshindwa na watuhumiwa kuachiwa
3. Samaki wa Magufuli taifa limeshindwa na tunalipa Billion zisizopungua 3.6
4. Ugaidi wa Lwakatare imeshindwa
5. Wakandarasi wa Barabara wameshinda na wanatakiwa kulipwa mabillion ya fedha kama riba kwa kutolipwa kwa muda stahili fedha zao.
6. Prof. mahalu na kesi ya jengo la ubalozi kule Italy Mahalu aliishinda Serikali
Na zingine nyingi tu, hivyo Serikali ya CCM haina ubavu wa kushinda kesi yeyote labda Mahakama zitoe hukumu za huruma.
 
Unaona jinsi akili kubwa inavyo ongoza akili ndogo? Sisi wa tanzania tunajua kabisa kuwa m4c ni mali ya chadema hivyo John Pombe Magufuli alitakiwa atengeneze yakwake. Angeweza kuiita J4C au P4C au JPM4C au 4CJPM, labda tungemuelewa ila anaposema yeye ni M4C manayake anatuambia watanzania tuichague chadema. Namimi nashauri watanzania tufanye kama anavyotaka magafuli i.e tuichague chadema ili kumufikishia ujumbe kuwa somo lake alilotufundisha wakati wa kampeni tumelielewa.

Mimi najiuliza kitu kimoja yeye anaposema Magufuli for change anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama siyo kutoka ccm kwenda chadema? unajua wazee hawa mara nyingi huwa wanafundisha kwa mifano na mafumbo kama alivyokuwa akifanya Yesu. Amejaribu kutumia njia ya kawaida akaona hatuelewi sasa ameamua kutumia mfano wa M4C kama Yesu alivyotumia mfano wa shamba la mizabibu. Yesu alikuwa akiongea mfano wa shamba la mizabibu akimaanisha watu na magufuli anatumia M4C akimaanisha tuichague chadema.

Magufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama sera anazo hubiri ndio hizohizo ambazo chama chake kimehubiri tangu mwaka 1961 hadi leo na wameshindwa kabisa kuleta matumaini ya maisha bora kwa watanzania.

Mgufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama baba wa taifa alisema ccm siyo baba yangu wala mama yangu hivyo unadhani yeye ndio atapenda ccm awe babayake au mama yake? inamaana magufuli ananguvu kuliko nyerere?

Mgufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama barabara alizotengeneza kwa kiwango kikubwa zinaharibika ndani ya miaka mitatu.

Mgufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama serikali imejaa madeni kila kona ya dunia, inawakopa hadi bibi zetu wanaolima korosho na mahindi

Mimi naona magufuli anamapenzi mema na tanzania ndiyo maana anatuambia watanzania kuwa tutumie nembo ya chadema kuitoa ccm madarakani. Kwamimi ambaye ni mtaaramu wa kuhubiri kanisani ujumbe huu wa magufuli nimeupata na kuuelewa vizuri na nitautumia kanisani kuwaeleza waumini wangu juu ya nia hii njema aliyonayo magufuli.

This might be the biggest liked ever before.👆👆👆✌✌✌✌
 
Wao mbona wanatumia Mgombea Urais wa kuazima kutoka CCM.

Wewe utakuwa ndio uliyeshika hili bango

12011285_983983074999020_4346160185616375206_n.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom