CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu?

Taifa la Tanzania lina maadui wanne
1. umasikini
2. Maradhi
3. Ujinga
4. CCM

Inaonekana mwenzangu una maradhi makubwa zaidi. Umasikini, Maradhi na Ujinga, havina usajili wa makaratasi. CCM imesajiliwa kama vilivyosajiliwa vyama vingine. Maradhi hayo yakikuzidia nenda kwa babu Samunge, anaweza kukusaidia kama una imani ya kutosha. Ukikosa nauli, tutakuchangia kama tulivyofanya kwa wengine.
 
Ngoma ikilia sana hupasuka.
Huyu kijana NAPE atakuja kuwadhalilisha ccm hadi wataingia dodoma tena kumvua gamba..
Mwendo wa huyu kijana si mzuri, kasi yake itaishia ukingoni, wenye akili zao wananielewa..
Matusi na kejeli zake kwa watu wasio wa chama chama chake yanaonyesha ukosefu wa SUBIRA, na hicho kitakachomponza na kumpa majuto ya kudumu.
 
Na Waandishi wetu



PAMOJA na uamuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya vigogo, baadhi ya makada maarufu wa chama hicho wameibuka na kusema bado chama hicho kina wakati ngumu.

Makada hao wameeleza kuwa uamuzi uliofikiwa na chama hicho hautakisaidia chochote na kusema kuwa ni sawa na kuoga mwili bila kubadili nguo safi.

Hivi karibuni aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, na sekretarieti yake waling'olewa kama hatua ya chama hicho kuzaliwa upya kwa lengo la kurejesha imani na umaarufu wake kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, makada hao: Stephen Galinoma na David Butinini walisema uamuzi huo hautasaidia chochote ndani ya CCM zaidi ya kuongeza mpasuko na kuendelea kuvipa umaarufu vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Galinoma alisema hatua ya CCM kujivua gamba ni moja ya mchakato mzuri katika wakati huu, ingawa uamuzi huo umekuja kwa kuchelewa mno, hivyo hautakuwa msaada kwa chama.

Galimona ambaye amepata kuwa mbunge wa Kalenga kwa tiketi ya CCM, alisema dalili za aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba kukivuruga chama ilianza kujionyesha mapema, lakini uongozi wa juu haukuchukua hatua wala kusikiliza maoni ya wana CCM hadi chama kimefika mahala pabaya. "Tunashukuru chama sasa kimechukua hatua ya kumuengua katika nafasi hiyo pamoja na makada wengine ambao walikuwa wakikivuruga chama chetu..ila ukweli bado CCM ina wakati mgumu kujisafisha na kufanya Watanzania kurudisha imani yao kama mwanzo," alisema Galimona.

Alisema makundi ndani ya CCM hayatamazilika kutokana na mizizi ya makundi hayo kuenea hadi ngazi za chini na kuwa baada ya kufanya mabadiliko hayo ngazi ya juu ni vizuri kuanza jitihada za kusafisha chama hicho ngazi ya mikoa, wilaya hadi vitongoji.

Aidha, alisema mabadiliko hayo yafanyike katika ngazi ya serikali kwa kuwapumzisha wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wazembe na ikiwezekana hata baraza la mawaziri kuvunjwa na kuundwa upya.
"Ukweli sasa CCM imechafuka sana tena uchafu huo umeshuka hadi huku chini sasa kusafisha juu pekee haitoshi ni sawa na kuchafua, kwani kuoga mwili huku nguo ni chafu ni sawa na kutooga kabisa. Hapa CCM imeanza kupunguza matawi kwa lengo la kuangamiza magugu bila kuchimbua mizizi yake ardhini," alisema Galimona.

Kuhusu moto ambao viongozi wapya wameanza nao zikiwemo kauli za Nape Nnauye kuwa mafisadi ndani na CCM wakae chonjo, Galinoma alisema anawatakia mafanikio viongozi hao kutimiza mipango hiyo, japo matunda yake ni madogo.

Kwa upande wake, kada maarufu wa chama hicho Mkoa wa Iringa, Butinini alisema moto wa vyama vya upinzani hasa ule wa CHADEMA ni mkali zaidi na kuwa bila CCM kujitathmini upya na kujipanga vema moto huo unaweza kuiteketeza CCM.

Alitaka CCM kuwa makini na wapinzani wanaokimbia vyama vyao na kujiunga na CCM kuwa ni vizuri hao kuogopwa na kutoaminiwa haraka na kupewa nafasi za uongozi ndani ya chama, ili kuwachunguza taratibu.

Wakati huohuo, viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyoosheana vidole kutaka wajivue magamba kwa kutokuwa waadilifu.

Tafrani hiyo ilitokea juzi baada ya CCM wilaya kuitisha kikao cha Halmashauri Kuu maalumu kwa lengo la kupongeza hatua iliyochukuliwa na chama hicho ngazi ya taifa ya kujivua gamba kwa kuwatosa baadhi ya viongozi.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa kuzuka kwa mvurugano huo kunatokana na baadhi ya wajumbe kushinikiza viongozi wa chama ngazi ya wilaya wajivue magamba kwa kujiuzulu kutokana na kuchangia chama kutofanya vema katika baadhi ya maeneo kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Habari hizo zilieleza kuwa wajumbe katika kikao hicho waliwapasha viongozi wao kuwa mahiri kupongeza maamuzi ya kitaifa yaliyofanyika huku miongoni mwao wakiwa hawana uadilifu.

Katika malumbano hayo, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kahama Mjini, Mathias Misungwi, aliwaeleza viongozi hao kama wanaunga mkono hatua zilizochukuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nao wajivue magamba kwa kujiuzulu nyadhifa zao. Misungwi alisema viongozi wote wa CCM ngazi ya wilaya kuanzia Mwenyekiti wa CCM wilaya pamoja na watendaji wake wote wanastahili wapime uadilifu wao kwa kutambua kuwa utekelezaji wao kuanzia kipindi cha mchakato wa kura za maoni, uchaguzi mkuu hadi sasa hauna maslahi na chama hivyo kuwapasa kujivua magamba yao kwa kuachia ngazi.


Hapa naona Galinoma amekata tamaa tu. Anasema kuwa hatua ya kujivua gamba ni nzuri lakini imechelewa, sasa alitaka CCM ifanye nini, na imechelwa kupata kitu gani hata aone kuwa mageuzi hayo hayana tija? Unajua nanyi waandishi wa habari wakati mwingine munajiharibia kwa kwenda kuwahoji makada wa Chama waliochoka akili, na hayo ndio matokeo yake sasa.
 
watanzania wakati mwingine tuache unafiki...tulipewa nafasi ya kumuondoa Kikwete kwa njia ya kura, tukamrudisha madarakani....kama walichakachua matokeo kwa nini hatukuwa tayari kufa kwa kuandamana...kuwa hatukumchagua iwe vipi atangazwe mshindi....haya yote tuliyataka wenyewe..next time tuwe tayari kwa lolote endapo tutakuwa na uhakika kuwa aliyetangazwa mshindi si chaguo letu....inwezekana tukiamua....!

Hapa umenena. Tukiwa na ushahidi kuwa matokeo ya uchaguzi yamechakachuliwa tudai haki yetu kwa maandamano. Sio kama anavyodai Mzee Slaa.
 
Wakuu ukisoma vizuri hiyo habari hapo juu, utaona Dr. Slaa katamka wazi kuwa kikwete ajivue gamba ndani ya ccm sababu kashirikiana na wenzake kufanya ufisadi. Hapo mwishoni amemtega kuwa awachukulie hatua za kisheria watuhumiwa wote au kama anashindwa aondoke. Huo ni mtego kwa sababu kikwete hataweza kuwachukulia hatua watu alioshirikiana nao kuiba.

Huo ni mtego kwa wajinga wake, na sio kwa watu wenye upeo wa kuelewa. Angekuwa na uhakika kuwa Jakaya Kikwete ni fisadi, asingemtaja ktk orodha ile pale Mwembe Yanga, angemuacha kwanza, asubiri hatua za kisheria zichukuliwe halafu baadae JK angeunganishwe ktk kesi. Alijua kuwa akimtaja Rais wa nchi, hakuna mtu wa kuchukua hatua za kisheria. Alifanya hivyo makusudi kuwazuga wajinga wenzake. Huyu mzee ni muongo sana, na haya ni madhara ya kumdanganya Mungu kuwa utamtumikia halafu baadae unamsaliti. Wote tunaelewa waliomsaliti Mungu wanaitwaje. Dr. Slaa haya yote yasingekukuta kama unemtii Mungu kwa kumtumikia kule madhabahuni. Lakini kama kweli ana ushahidi kuwa JK ni fisadi kwanini asimshitaki? Maana kwa njia hii anaweza, kwanini asifanye hivyo? Kama ana hela za kumnunulia kimada nyumba na gari, atashindwa za kushughulikia jambo kubwa la nchi kama hili?
 
Slogan yenyewe imekosa mashiko. Haina mantiki yoyote. Aliyebuni slogani hii si mbunifu kabisa, hii inatokana na ukungu uliowajaa. Hawaoni tena. Ila kwa muvi hii nina hakika chama cha magamba kitakufa bila wasi wasi.
Mungu ibariki Tanzania.

Ni mapema mno kujifanya Sheikh Yahya Hussein. Tusubiri, tuone mambo. Kila mtu unayemuona anakimbia leo hii, alikuwa mtoto, akajifunza kutambaa, kutembea na sasa anakimbia. Musiwabeze akina Nape, wapeni muda. Kama kweli hamjatumwa na mafisadi, basi toeni mikakati ya kuwasaidia akina Nape wawashughulikie vizuri mafisadi, maana wao wanadai kuwa wanawajua na tayari wameishawaandikia barua
 
Matukio mengie yametokea siku za hivi karibuni kwenye siasa za nchi yetu. Nadhani tukio kubwa ninalokumbuka ni lile la CCM kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani akina Yusufu MAKAMBA na kuweka damu mpya ya akina January MAKAMBA.

Je ni kweli sasa CCM siyo nyoka tena bali sasa amekuwa ni mjusi tu asiyekuwa na madhara kwa watanzania tena? Swali hilo ndio sijaweza kulijibu; na ndiyo maana naanzisha thread hii ili baada ya wiki moja niweza kufahamu kama kweli magezui yaliyofanyika ndani ya CCM ni ya kweli au ni danganya toto tu. jambo moja linalokera zaidi ni kuwa gamba lililovuliwa na CCM ni lile la ufisadi, ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi ni kosa la jinai. Je ni kweli mafisadi waliovuliwa CCM watafikishwa kwenye vyombo vya sheria; yaani kuna anayeweza kuniaminisha kuwa Januari atamfikisha Yusufu kwenye vyombo vya sheria ili hali Januari huyo amefika hapo kupitia mgongo wa Yusufu?

Kujivua gamba kwa nyoka hakumaananishi kuwa ameacha tabia zake, bali kunampa nguvu na sura mpya ya kufanya mambo yake. CCM kujivua Gamba ni mfano tu alioutumia Rais Kikwete, angeweza kutumia mifano mingine pia, kama angekuwa nayo karibu. Sio kweli kuwa CCM yote ni mafisadi, ila kuna baadhi ya vibaka waliopenyeza ndani ya CCM ndio wanatakiwa kushughulikiwa sasa. Tujitahidi kufanya tahthimini ya akili, tusitake kuwapotosha wananchi kwa kulinganisha tabia za nyoka na tabia za CCM.
 
CCM kujivua gamba maana yake ni nini hasa? Kimsingi sababu ya kuvua gamba ni kutaka kubaki na ngozi mpya. Connotatively hii ina maana kuwa CCM inazaliwa upya. Denotatively kuvua gamba haina maana ya kuzaliwa upya bali ni kubadili sura tu. Kwani kuvua gamba hakuondoi internal characteristics za yule anayevua gamba. Kwa mfano kama mnyama ana ugonjwa fulani ndani ya mwili wake kama vile kansa ugonjwa huo hautaweza kuondoka bali utaendeleakubaki pale pale. Hii ndo kusema kuwa ikiwa CCM ilikuwa na ugonjwa fulani basi bado hawezi kundoka kwa kitendo cha kuvua gamba pekee.
Gamba likichakaa mara nyingi sababu huwa ni za ndani ya mwili. Kwa hivo kulivua hakumalizi tatizo lililofanya gamba kuchakaa. Ufisadi uko ndani ya CCM na jamii kwa jumla na hivo hauwezi kuvuliwa kama gamba. Kelele za kina Nape kuwataka mafisadi ndani ya chama hicho waachie ngazi ndani ya miezi mitatu sio tafsiri halisi ya kuvua gamba. Kuwaondoa kina Y. Makamba na kuwaweka kina Nape si kuvua Gamba bali ni kubadili sura tu. Basi ingefaa kutafuta falsafa nyingine hii haijatulia kwa kweli.
Harakati za kina Nape kuwapa mafisadi siku tisini waachie ngazi zina maana gani? Nape na wanzake wachache ndani ya CC ni nani na wana mamlaka gani? Sisi hatutaki kuwasikia kina Nape na porojo zao. Wao sio dola. Kama kweli CCM imebaini Mafisadi ndani yake basi ingefaa iwasilishe majina yao kwenye dola na ushahidi au mashaka waliyonayo ili washughulikiwe. Haiingii akilini kuwapa waovu siku 90 za kujiuzulu badala ya kuwafukuza mara moja huku hatua nyingine za kisheria zikifuata. Kwa nini chama tawala kinajigeuza kuwa kama chama cha upinzani kwa kulalamika wakati kimeshika dola? Au ndo maana ya falsafa ya kuvua gamba?
 
Nyoka akiwa anajivua gamba huwa mkali zaidi akisogelewa,na inaaminika kuwa akikung'ata kupona huwa bahati sana!Nadhani kuliko kujivua gamba tu,ilitakiwa kung'oa mihogo michache iliyoshambuliwa na ugojnwa wa BATOBATO ili kunusuru mingi iliyo na afya shambani!
 
Nami naunga hoja hasa kuhusu IGP amekuwa kada zaidi ya mtendaji mkuu wa jeshi kulinda mali za watu na amani....yeye amekuwa anafuata amri za wanasiasa kuliko wananchi suala la watu waliouaawa kule kwembe linatia uchungu sana maana yeye ndie aliepigiwa simu kwanza akakataa akasukuma kwa kova na yeye akakkataa.....hadi mauaji yakatokea..........
 
Ngoma ikilia sana hupasuka.
Huyu kijana NAPE atakuja kuwadhalilisha ccm hadi wataingia dodoma tena kumvua gamba..
Mwendo wa huyu kijana si mzuri, kasi yake itaishia ukingoni, wenye akili zao wananielewa..
Matusi na kejeli zake kwa watu wasio wa chama chama chake yanaonyesha ukosefu wa SUBIRA, na hicho kitakachomponza na kumpa majuto ya kudumu.

Mkuu uko sahihi. Nnape ni mpiganaji lakini kwa cheo chake hiki kipya kinahitaji busara kubwa na siyo kuongea kwa hisia manake yeye sasa ni msemaji wa chama na siyo mwanachama wa kawaida, kauli yake ni kauli ya Chama na wala siyo kauli ya Nnape. Kama hatafungwa speed governor basi nadhani si muda mrefu atavuliwa gamba.
 
Na John Daniel

SEKRETARIET mpya ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimebaini mbinu chafu za mafisadi waliopewa siku 90 kujiondoa ndani ya Halmashauri Kuu
(NEC), kuanza kujihami kwa kukihujumu chama hicho na kumhujumu Rais Jakaya Kikwete.

Wamesema wamebaini mbinu hiyo inayolenga kuvuruga hoja ya kuwaondoa ili waonekane kuwa hawana hatia kwa kuwapakazia watu wengine akiwemo Rais Kikwete na familia yake vitendo vya kifisadi kwa lengo la kuondoka na kundi kubwa au kufuta hoja ya kuwaondoa.

Akihutubia mkutano wa hadhara ya kuwatambulisha kwa wana CCM katika uwanja wa Manzeshe maarufu kama Bakhresa jana, Katibu wa NEC Ikitikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, alisema wamebaini watuhumiwa hao kuwatumia baadhi ya vyama vya siasa na viongozi wa dini kufanikisha azma yao.

"Tumebaini kuwa baada ya kuchukua uamuzi wa kuwaondoa mafisadi kwenye NEC kule Dodoma, wameanza kutumia baadhi ya vyama vya siasa kuhujumu chama, kibaya zaidi wanaelekeza hujuma zao kwa mwenyekiti wetu na familia yake.

"Licha ya kutumia viongozi wa baadhi ya vyama pia wanatumia hata baadhi ya viongozi wa dini kutaka kuhalalisha hoja yao, kudanganya Watanzaia na kutaka kufuta dhambi zao mbele ya jamii ili ionekane chama chote hakifai na si wao,"alisema Bw. Nape na kuongeza.

"Nataka niwaonye kuwa wasianzishe vita vya mawe wakati wanaishi kwenye nyumba ya vioo, tulipoanzisha vita vya ufisadi hatutanii, sababu tunayo, nia tunayo na uwezo tunao,"alisisitiza Bw. Nnauye.

Alisema uamuzi wa kuwapa nafasi ya kutumia busara zao kujiondoa wenyewe ilikuwa ya makusudi hivyo wasithubutu kukihujumu chama hicho na Mwenyekiti wake Rais Kikwete kama walivyoanza.

Alisema CCM haina ugomvi na vyama vya siasa kwa kuwa inapenda kukuza demokrasia nchini ndio maana hata wakisema maneno ya kashfa na uchochezi haiwachukulii hatua japo ina uweo wa kufanya hivyo.

"Sisi tunasema hatutaki malumbano na vyama vingine kutokana na hujuma za mafisadi tunaotaka waondoke kwenye NEC. Tunawashauri waondoke salama wasituchokoze hivyo,"alisema.

Alisema tayari watu hao wameanza kutuma watu wao kwenda kwa viongozi wa vyama vya siasa na dini kupika uongo wa kusema jukwaani na kwenye madhabahu jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

"Hawa watu wameanza kusemwa kwa muda mrefu na wanajua hilo hata wao wenyewe kuwa si wasafi. Iweje leo waambiwe waondoke kwa ustaarabu kisha waanze kutumia baadhi ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kumchafu Mwenyekiti wetu na familia yake.

"Nataka nisisitize tena kuwa watashindana na sisi lakini hawatashinda,tutapigana hadi tuwashinde kwa kuwa tuna uhakika na kile tunachofanya,tumedhamiria,"alisisitiza Bw. Nnauye.

KWA MUJIBU WATOVUTI YA CCM ILIYONUKULIWA TAR 18 APRILI 2011 WAFUATAO HAPA CHINI NDIO WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM ILIYOCHAGULIWA NA HALMASHAURI KUU YA CCM ILIYOKETI TAR 10 APRILI 2011. HIVYO ALIYETEMWA KATIKA MZUNGUJKO WA SEKRETERIETI NA KAMATI KUU YA KUJIUZULU NI MAKAMBA, MEMBE, TAMBWE HIZZA. AMA LOWASSA, ROSTA NA CHENGE WALICHAGULIWA UPYA KUSHIKA NYADHIFA KATIKA KAMATI KUU YA CCM MPYA CHINI YA KATIBU MKUU WILSON MUKAMA; AU CCM INAWAOGOPA KUWATAJA NA KUWAFUTA RASMI KATIKA ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI KUU KWA HOFU IWAPO WATAGOMA KUJIONDOA WENYEWE NINI KITATOKEA? KWA HALI HIYO CHAMA CCM NI CHAMA KINACHOENDESHWA KISANII NA HAKIFAI KUPEWA DHAMANA TENA YA KUWAOONGOZA WATANZANIA IWAPO HAKIWEZI KUSIMAMIA MAAMUZI YANAYOFIKIWA KATIKA VIJKAO VYAKE.

KATIKA HALI INAYOTHIBITISHA USANII WA CCM, HAKUNA MAHALI POPOTE KATIKA TOVUTI YA CCM INAPOONYESHWA KUWA CCM ILIFANYA UAMUZI WA KUWAPA WANACHAMA WAKE WANOTUHUMIWA KWA TUHUMA ZA UFISADI SIKU 90 WAJITOE KATIKA NYADHIFA ZAO NA KATIKA CHAMA. KILICHOPO NI KLUGHA TAMU ZA KULEA UFISADI NA RUSHWA MIONGIONI MWA WANANCHAMA WAKE KAMA INAVYOONYESHWA KATIKA AJENDA YA TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU 2010 HAPO CHINI

1.Ndugu Kakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)

3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)

4. Ndugu Wilson Mukama - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Vuai Ali Vuai - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
13. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
14. Ndugu Nape Nnauye - Mjumbe
15. Ndugu Mwigulu Mchemba - Mjumbe
16. Ndugu January Makamba - Mjumbe
17. Ndugu Asha Abdallah Juma - Mjumbe
18. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mjumbe
19. Ndugu Anna Makinda - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23.Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30 . Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31 . Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32 . Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37 . Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf - Mjumbe

http://www.cms.ccmtz.org/index.php?page=535

Vile vile kuthibitisha kuwa Sekreterieti ya Wilson Mukama na Nape inafanya michezo ya na akili za watanzania, miniti za kikao cha Halmshauri Kuu ya CCM cha tarehe 10 Aprili 2011 zilizopostiwa katika tovuti ya CCM azionyeshi popote kufikiwa kwa mamuzi ya kuwapatia wanachama wa CCM wanaotuhumiwa kuwa Mafisadi siku 90 kujipima wenyewe na kujiondoa katika nafasi zaoa ua ndani ya CCM. ibara ya 5 ya Maamuzi ya NEC ya Tarehe 10.04.2011 hapo chini yahusika

5. KUHUSU TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU 2010

Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kujadili taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, imeagiza mambo yafuatayo:-

(a) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa Shukurani kwa wana CCM na wananchi kwa jumla kwa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi kwa kukipigia kura nyingi zilizokipa ushindi na hatimaye kuunda Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wananchi wanaombwa kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zingine zijazo.

(b) Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zimetakiwa zitekeleze ipasavyo Ilani ya CCM ya 2010-2015 kwa kadri Chama kilivyoahidi wakati wa kampeni; kama zilivyo tekeleze kwa ufanisi mkubwa Ilani iliyopita iliyopita ya Uchaguzi ya 2005-2010.

(c) Serikali zote mbili ziongeze kasi ya kushughulikia matatizo ya wananchi ili kuwaondolea kero zinazowakabili, hasa tatizo la kupanda kwa gharama za maisha.

(d) Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kiongeze kasi ya mapambano dhidi ya viongozi na wanachama wanaojihusisha na rushwa. Aidha viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa wajenge tabia ya kuwajibika wenyewe kwa maslahi ya Chama wasipofanya hivyo Chama kiwawajibishe kwa maslahi ya Chama na nchi.

http://www.cms.ccmtz.org/index.php?s...ils&newsid=132
 
Ni jambo ambalo limezoeleka sasa masikioni mwa watanzania na labda nchi nyingine juu ya ccm kujivua gamba au magamba!!!? kinachonipa matatizo hapana ni mantic ya kuvua gamba. najiuliza ni gamba gani lililovuliwa? nimewahi kusema huko nyuma kwamba kwa ccm kushindwa kumkabili na labda kumwajibisha mwenyekiti wao!! kama kupo!,hiyo ndo ingeleta maana hasa ya kuvua gamba. nawashangaa watu wanazunguka nchi nzima wanasema wamevua gamba, gamba lipi? sioni mantic ya sekretarieti na kamati kuu kujiuzuru tena siyo kufukuzwa kuitwe kuvua gamba. kuvua kitu ni kuondoa kabisa. lakini pia haileti maana kwa watu walewale wanaodaiwa kuleta shida katika chama hicho kubaki bado wakiwa wajumbe wa vikao nyeti vya chama hicho kama halmashauri kuu ya taifa na bila shaka mkutano mkuu. jamani eh !kama mnaharamisha kitu haramisheni kabisa na siyo nusu nusu tunayoiona. mjumbe ambaye amekuwa haramu kamati kuu anawezaje kuwa safi kwenye vikao vingine? lakini ccm muwe wakweli, hivi kweli mmevua gamba? ni gamba gani mlilovua wakati mnawaomba wale mnaoita magamba wapime na wajiuzuru wenyewe? sijui wajiuzuru nini wakati mnadai mmeshawavua hao watu? je hizi siyo ghiliba zakisiasa? Tunawataka muwe perfomance-based badala ya porojo. mnaomba wabaya wenu wajiuzuru wenyewe, huko ni kuvua kweli? mnawaogopa? MIMI ningeona kweli dhamira yenu ya kuvua magamba kama mngechukua hatua mara moja na siyo kuomba magamba yadondoke yenyewe. mnasubiri uungwana wa mnaoita waharifu? May God help you to do things that can be seen and not the verballing of empty words as you do now. tunataka kweli tuone magamba yamevuliwa na siyo ghiliba za kisiasa.
 
Ukibishana na mwendawazimu nawe utaonekana mwendwazimu......achaneni nae anatafuta umaarufu huyo.
 
Hoja sahihi-kujivua gamba ni kuongeza ukali wa sumu na hivyo mafisadi wanaongeza namna ya kuibia watanzania. tunayo kazi nzito
 
Bora Galinoma na Butinini wamekuwa wakweli. CCM wavue gamba, wajipodoe bado machoni mwa Watanzania wengi chama hicho bado kinaonekana ni Chama Cha Mafisadi/Majambazi.
 
Danganya toto ya CCM hiyo ni kama vile kinyonga
kujibadilisha rangi ili kuwadanganya predators lakini
kwa wanyama makini kama binadamu tunajua huo
ni wizi wamchana kweupe.
 
Back
Top Bottom