CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Apr 18, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Matukio mengie yametokea siku za hivi karibuni kwenye siasa za nchi yetu. Nadhani tukio kubwa ninalokumbuka ni lile la CCM kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani akina Yusufu MAKAMBA na kuweka damu mpya ya akina January MAKAMBA.

  Je ni kweli sasa CCM siyo nyoka tena bali sasa amekuwa ni mjusi tu asiyekuwa na madhara kwa watanzania tena? Swali hilo ndio sijaweza kulijibu; na ndiyo maana naanzisha thread hii ili baada ya wiki moja niweza kufahamu kama kweli magezui yaliyofanyika ndani ya CCM ni ya kweli au ni danganya toto tu. jambo moja linalokera zaidi ni kuwa gamba lililovuliwa na CCM ni lile la ufisadi, ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi ni kosa la jinai. Je ni kweli mafisadi waliovuliwa CCM watafikishwa kwenye vyombo vya sheria; yaani kuna anayeweza kuniaminisha kuwa Januari atamfikisha Yusufu kwenye vyombo vya sheria ili hali Januari huyo amefika hapo kupitia mgongo wa Yusufu?

  Nadhani bado tunaishi na nyoka uvunguni mwetu; wakati wowote atatung'ata tu!!
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na John Daniel

  SEKRETARIET mpya ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimebaini mbinu chafu za mafisadi waliopewa siku 90 kujiondoa ndani ya Halmashauri Kuu
  (NEC), kuanza kujihami kwa kukihujumu chama hicho na kumhujumu Rais Jakaya Kikwete.

  Wamesema wamebaini mbinu hiyo inayolenga kuvuruga hoja ya kuwaondoa ili waonekane kuwa hawana hatia kwa kuwapakazia watu wengine akiwemo Rais Kikwete na familia yake vitendo vya kifisadi kwa lengo la kuondoka na kundi kubwa au kufuta hoja ya kuwaondoa.

  Akihutubia mkutano wa hadhara ya kuwatambulisha kwa wana CCM katika uwanja wa Manzeshe maarufu kama Bakhresa jana, Katibu wa NEC Ikitikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, alisema wamebaini watuhumiwa hao kuwatumia baadhi ya vyama vya siasa na viongozi wa dini kufanikisha azma yao.

  "Tumebaini kuwa baada ya kuchukua uamuzi wa kuwaondoa mafisadi kwenye NEC kule Dodoma, wameanza kutumia baadhi ya vyama vya siasa kuhujumu chama, kibaya zaidi wanaelekeza hujuma zao kwa mwenyekiti wetu na familia yake.

  "Licha ya kutumia viongozi wa baadhi ya vyama pia wanatumia hata baadhi ya viongozi wa dini kutaka kuhalalisha hoja yao, kudanganya Watanzaia na kutaka kufuta dhambi zao mbele ya jamii ili ionekane chama chote hakifai na si wao,"alisema Bw. Nape na kuongeza.

  "Nataka niwaonye kuwa wasianzishe vita vya mawe wakati wanaishi kwenye nyumba ya vioo, tulipoanzisha vita vya ufisadi hatutanii, sababu tunayo, nia tunayo na uwezo tunao,"alisisitiza Bw. Nnauye.

  Alisema uamuzi wa kuwapa nafasi ya kutumia busara zao kujiondoa wenyewe ilikuwa ya makusudi hivyo wasithubutu kukihujumu chama hicho na Mwenyekiti wake Rais Kikwete kama walivyoanza.

  Alisema CCM haina ugomvi na vyama vya siasa kwa kuwa inapenda kukuza demokrasia nchini ndio maana hata wakisema maneno ya kashfa na uchochezi haiwachukulii hatua japo ina uweo wa kufanya hivyo.

  "Sisi tunasema hatutaki malumbano na vyama vingine kutokana na hujuma za mafisadi tunaotaka waondoke kwenye NEC. Tunawashauri waondoke salama wasituchokoze hivyo,"alisema.

  Alisema tayari watu hao wameanza kutuma watu wao kwenda kwa viongozi wa vyama vya siasa na dini kupika uongo wa kusema jukwaani na kwenye madhabahu jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

  "Hawa watu wameanza kusemwa kwa muda mrefu na wanajua hilo hata wao wenyewe kuwa si wasafi. Iweje leo waambiwe waondoke kwa ustaarabu kisha waanze kutumia baadhi ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kumchafu Mwenyekiti wetu na familia yake.

  "Nataka nisisitize tena kuwa watashindana na sisi lakini hawatashinda,tutapigana hadi tuwashinde kwa kuwa tuna uhakika na kile tunachofanya,tumedhamiria,"alisisitiza Bw. Nnauye.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,670
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kichuguu habari za masiku? Umeadimika hapa jamvini siku za karibuni.

  Nadhani Watanzania tuna haki ya kuuliza maswali yafuatayo ambayo labda kada/makada wa CCM wanaweza kutujibu
  1. Je, hili gamba walivalishwa lini?
  2. Ni nani aliyewavalisha gamba hilo?
  3. Walivalishwa katika awamu ipi? (Ya Mwinyi, Mkapa au Kikwete)
  4. Tangu walipovalishwa gamba hilo muda wote uliopita walikuwa hawajagundua kama wana gamba hadi 2011?

  Mimi kwa maoni yangu huu ni msamiati wa kujaribu kutuzuga Watanzania kwamba CCM sasa ni safi wakati ukweli ni kwamba bado kuna mafisadi wengi tu ndani ya chama hicho na sidhani kama kuna juhudi za kweli za kujisafisha bali ni usanii tu. Itakuwa poa sana hao wanaotaka kufukuzwa CCM wakiamua kupambana ndani ya chama hapo si ajabu tutazijua siri nyingi sana tena nzito za ndani ya chama hicho ambazo zinaweza kabisa kukisambaratisha.
   
 5. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninavyo juwa mimi kujivua gamba kwa nyoka ni kutoka katika ali ya uzee na kurudi ujanani. sasa awa jamaa wamevua uhoza wa kale sasa wameaza na uhoza mpya, akuna aliye mwema katika icho chama issue ni kuwatoa kabisa kwenye system.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,670
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Dk Slaa ampa JK siku 90 kudhihirisha gamba jipya Sunday, 17 April 2011 21:06
  Godfrey Nyang'oro, Urambo
  Mwananchi

  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete awataje watuhumiwa wa ufisadi na kisha kuwavua nyadhifa zao zote na kisha kuwafikisha mahakamani katika muda wa siku 90 kama kweli anataka kukivua gamba chama hicho.

  Kauli hiyo ya Chadema kwa Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya CCM kuchukua hatua katika kile ilichokiita kujivua magamba kwa kuwataka watuhumiwa wote wanaotajwa kuhusika katika kashfa kadhaa za ufisadi, kujiondoa wenyewe katika nafasi zao ndani ya chama hicho katika kipindi cha miezi mitatu vinginevyo watawajibishwa.

  Jana, akiwa kwenye Uwanja wa Kaliua, Urambo Magharibi, Dk Slaa alisema kama kweli Rais Kikwete amedhamiria kukivua gamba chama chake, anapaswa kuuthibitishia umma kwa kufanya hivyo vinginevyo itakuwa ni ‘usanii.'

  Kwa mujibu wa Dk Slaa, endapo watuhumiwa hao watatajwa na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuvuliwa nafasi zao na uanachama na kupoteza ubunge au kufukuzwa serikalini, dhana hiyo ya kujivua gamba itakuwa na mantiki. (Kikwete hana ubavu wa kuyafanya haya)

  Dk Slaa alisema, Watanzania wanataka kuona fedha zao zilizoibwa na mafisadi zinarejeshwa na watuhumiwa kufikishwa mahakamani, hivyo haitoshi kusema neno kujivua gamba.

  Mwanachama mwingine maarufu wa Chadema, Frederick Mpendazoe ambaye aligombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Jimbo la Segerea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alisema endapo CCM kitashughulikia watuhumiwa hao wa ufisadi ndani ya siku 90 ni dhahiri kutafanyika uchaguzi kutokana na kile alichodai kwamba ni kuwa na wabunge wengi waliingia madarakani kwa njia ya rushwa.

  Alidai kwamba CCM imepoteza mwelekeo kutokana na kuhodhiwa na watu wenye malengo ya kibiashara ambao huchochea ufisadi unaokigharimu sasa.
  Mpendazoe ambaye aliwahi kuwa kada wa chama hicho tawala alisema miaka ya nyuma wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, CCM kilikuwa madhubuti kutokana na kuwa na viongozi waliokuwa tayari kupambana na rushwa na ukosefu wa maadili ya uongozi, hali ambayo ni tofauti kwa sasa.
  Mpendazoe ambaye alijiondoa CCM kutokana na kile alichodai kuwa ni fitina za mafisadi alisema uongozi ndani ya chama hicho tawala kwa sasa ni uwekezaji akisema asiye na fedha ni vigumu kupata uongozi.

  Alisema kutokana hali hiyo, hata ile misingi ya waasisi iliyojengwa katika miaka ya 1960 na 1970 imebomolewa na mafisadi kushika hatamu za uongozi wa chama hicho tawala.

  Mpendazoe alisema Serikali iliyopo ni ya kidemokrasia lakini imekuwa ikiyapa kisogo matatizo ya wananchi wa tabaka la chini na kukumbatia wafanyabiashara ambao wana nguvu ndani ya chama hicho.

  Kuhusu muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, alisema hadi sasa serikali imeuondoa muswada huo bila kuweka mambo wazi na kuonya kama ukirejea kama ulivyo na tume ikiundwa na rais chama hicho kitaandamana.


   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kobe akijivua gamba anakuwa........
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu Nape anataka kudanganya umma. Ugomvi wa mafisadi wa CCM ni ugomvi wa ndani ya CCM. Hakuna cha viongozi wa dini wala kutumiwa kwa vyama vya siasa. Chenge alishaapa siku nyingi kuwa hawezi kuanguka peke yake. Kama atatoswa atahakikisha na madhambi ya Kikwete nayo yanafahamika. Sasa wameshaanza kutekeleza mkakati huo kwa kutumia magazeti ya Rostum lakini Nape anataka kutudanganya kuwa vyama vya upinzani vinatumiwa. Huu ni uongo usio na mshiko. Kikwete angekuwa msafi asingekuwa na wakati mgumu kama alio nao hivi sasa. Anashindwa kuwafukuza rafiki zake badala yake anawapa siku 90 wajiengue wenyewe. Ulishayasikia wapi hayo?
   
 9. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Moyoni kwa viongozi wote wa CCM kumejaa ufisadi..

  Mwilini wamejivua Gamba.. WHAT A JOKE!!

  Simply this make things worse ... and very confusing..

  Kwani sasa kwa kuwatizama huwezi kujua kwani maneno na matendo wooote ..wanaimba ... kujivua kujivua...Lakini moyoni?

  Mabadiliko ya kweli ni moyoni si mwilini lilipo gamba!!

   
 10. F

  Falconer JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Jamani hakuna mpya CCM. Hizi ni njama za kuwadanganya wananchi. Wamewachagua viongozi walioshindwa Zanzibar kuwakilisha Zanzibar katika baraza lao. Hhahahahahahha - OVYO.
   
 11. H

  Haruna S Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dont live in denial Nape! Ufisadi wa Kikwete haukuanza kutajwa jana.

  Kwa mtazamo wangu,CCM walikosea mambo mawili wakati wa kujivua gamba:

  Mosi,kuwapa mafisadi siku 90 wawe wameshajiondo ilikuwa ni kufungulia milango siasa za maji taka,It really suprise me has taken Nape about a week to know that.Scandals zote ambazo zilikuwa “funika kombe mwanaharamu apite” zitafunuliwa, baada ya siku tisini kutakuwa hakuna ambaye ndani ya CCM anaweza kumnyooshea mwenzake kidole.

  Pili, kusema watuhumiwa wote wa ufisadi watoke hata kama tuhuma zao hazina ushahidi wowote.Sasa ni nani CCM anaweza kusimama kifua mbele aseme sijawahi kuhusishwa na ufisadi.

  Kazi ya kujisafisha na ufisadi CCM ni ngumu wakati walishasema kama unataka mambo yako ya kunyooke jiunge na CCM.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ndo maana kila siku nasema huyu Nape hana akili timamu..anaropoka ropoka tu nadhani hajui anachoongea..yaani JK anadhani kwa kumuweka nape an january kwa kuwa ni vijana basi ndo ame wim mass ya vijana wa kitanzania??? Ujinga ni nugonjwa mbaya sana maishani ...JK anapaswa kujua kwamba CCM ni kama chuma chakavu halina mvuto wala kazi tena
   
 13. S

  Straight JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika cku za karibuni, ndugu ze2 ccm wamekuja na kali ya mwaka eti ....kujivua gamba. ndugu zangu mtakubaliana na mimi kuwa nyoka anapofika stage fulani uhitaji kuvua gamba na kubaki na ngozi mpya... kwa maana anakuwa mpya., lakni msisahau ki2 kmoja muhimu NYOKA ATABAKI KUWA NYOKA kwa maana hyo uhasi wake kama nyoka unaimarika maradufu.. so pls let us b careful wit CCM cuz nothng has changed CCM NI ILE ILE this tym watakuja na uhasi na wizi mpya zaidi... plz ma fellow don b fools wit ths ccm drama.
   
 14. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  in this way,ccm finish! it will remain history!
   
 15. fige

  fige JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hata sumu yake haipungui na akizaa huzaa nyoka.

  Tabia ya kurithishana madaraka ambayo wenzetu wa Libya ni chanzo cha mgogoro haiwezi kuisha ,angalia sekretariat mpya Nape,January koo zilezile
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  NDIO niliwashauri CCM wajivue govi ndio lenye heshima na sio gamba! '1*kwani wao nyoka???
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Huyu naye BORGUS tu naona analalamika kama kiranja wake, hao mafisadi kwani wako CDM au CCM?
   
 18. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani huyo mwenyekiti wao ni Mungu yeye hata asisemwe; hao wanajuana ndo maana wanashangaa kwa nini wao waondolewe huku wakimwacha fisadi mwenzao akizidi kuvinjari? Lakini nyerere alisha sema huyo hafai
   
 19. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sikio la kufa halisikii dawa,sio kuwa hawasikii ni kuwa alama za nyakati zinazonyesha ChiChieM kushney.
   
 20. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2011
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu katika Jina la Yesu atamlinda Nape. Hakuna atakayemgusa kwa kuwa Malaika wa Mungu aliyehai wanaomlinda ni wengi kuliko Majini yatakayotumwa na wabaya wake ili kumdhuru.

  Mungu aendelee kumlinda Nape Nnauye
  .
   
Loading...