CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu?

Chama Cha Magamba..........hivi huyu mwenyekiti alitoka wapi na hili neno? kwa nini hawakumshauri kwamba it is a bad idea?
 
Matukio mengie yametokea siku za hivi karibuni kwenye siasa za nchi yetu. Nadhani tukio kubwa ninalokumbuka ni lile la CCM kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani akina Yusufu MAKAMBA na kuweka damu mpya ya akina January MAKAMBA.

Je ni kweli sasa CCM siyo nyoka tena bali sasa amekuwa ni mjusi tu asiyekuwa na madhara kwa watanzania tena? Swali hilo ndio sijaweza kulijibu; na ndiyo maana naanzisha thread hii ili baada ya wiki moja niweza kufahamu kama kweli magezui yaliyofanyika ndani ya CCM ni ya kweli au ni danganya toto tu. jambo moja linalokera zaidi ni kuwa gamba lililovuliwa na CCM ni lile la ufisadi, ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi ni kosa la jinai. Je ni kweli mafisadi waliovuliwa CCM watafikishwa kwenye vyombo vya sheria; yaani kuna anayeweza kuniaminisha kuwa Januari atamfikisha Yusufu kwenye vyombo vya sheria ili hali Januari huyo amefika hapo kupitia mgongo wa Yusufu?

Nadhani bado tunaishi na nyoka uvunguni mwetu; wakati wowote atatung'ata tu!!

Mkuu hapa umenena. ccm wataendelea kujidanganya na watanzania tusikubali kulala usingizi wakati jk, mkapa, mwinyi, makamba na mafisadi wanachotafuta ni immunity wa familia zao na wakiss miguu yao ili wawalinde wakiondoka maofisini. Habari ni hii, tunakuja na docs zote tutazipata na kuwaweka nyie wote ndani. Wala msidanganye mtakimbia rekodi zenu. Watch here,

"CAIRO (AP) — Egypt's ex-prime minister and two other former Cabinet members were charged with corruption Sunday in the latest step in a campaign to bring officials of Hosni Mubarak's toppled regime to justice for years of corruption, rights abuses and other crimes.
Egypt's attorney-general for public funds charged former Prime Minister Ahmed Nazif, ex-Finance Minister Yousef Boutros Ghali and former Interior Minister Habib el-Adly with wasting more than $15 million in public money and profiteering, the official news agency reported"
The Associated Press: Egypt's ex-premier charged with corruption

"A parliamentary committee recommended Mubarak face similar charges, Egypt's leading newspaper, Al-Ahram, reported Wednesday, but the public prosecutor has so far held back from accusing the former ruler of complicity in the violence surrounding the demonstrations.
The charges are in stark contrast to the almost total freedom that security forces had during Mr. Mubarak's reign, when thousands of Egyptians faced humiliations large and small — ranging in severity from torture to paying off police to dodge falsified charges"
Top Egyptian security officials charged with killing protesters - The Globe and Mail

Who thought this woild ever happened? Jk and Mafisadi Mkivua gamba au Makalivaa Tutawapeleka Jela tu​
 
Mzee wa Mdomo Mwepesi ngoje nilonge kwa hili la JK kuhifadhi mizoga yenye kutoa harufu ndani ya nyumba yake.
Nasema Loa- hasa, Rost-tam laaziz, Nimeona Kimkono, Lamba Pesa,Makongoruu Mahangamizi n.k ni mizoga ambayo imeoza siku nyingi sana. JK kwa kutumia akili ya mbayumbayu akaamua kuichukua kwa mbewmbwe za kila aina na kuiweka nyumbani kwake!!. Mizoga iliyooza yenye kutoa harufu kali na ya kutisha!!! Hii ni ajabu na maajabu haya yapo TZ tu. Baada ya kuiweka nyumbani kwake, majirani wakaanza kupiga kelele kutokana na harufu kali itolewayo na hiyo mizoga na mkusanyiko mkubwa wa inzi katika makazi yao kiasi cha kuhatarisha usalama wa afya zao.

Bila aibu huku akiendelea kutumia akili zile zile za mbayumbayu (maana za kuzaliwa hana) akaweka walizi wa kuilinda hiyo mizoga ili harufu yake isitoke nje ya nyumba yake. (Hawa walinizi ni Kamba, chingagati, nchimbili,sofy lion n.k). Maskini JK, hivi kweli unaweza kuzuia harufu ya mizoga kwa kuweka walinzi!!!. Kwa hilo pole sana kaka!!.

Hata "sungusungu wa mtaa"nao wakaanza kusadia kuilinda hiyo mizoga kwa kufuata maelekezo ya walinzi wa nyumba ya JK. Sungusungu wakaacha jukumu la kuwalinda majirani waliowaajiri na kuwalipa mshahara, badala yake wakaanza kuwaadhibu wale wote waliokuwa wakilalamikia mizoga au harufu yake.

Majirani wote waliolalamika kuhusu harufu kali ya hiyo mizoga na kuzagaa kwa inzi mtaani kwao walipigwa na sungusungu wa mtaa ambao wametelekeza jukumu lao au kuhamishwa kwa nguvu hapo mtaani.

.Hata baadhi ya ndugu zake waishio ndani ya nyumba yake, walifukuzwa au walitishiwa kufukuzwa kutoka ndani ya nyumba kwa vile tu walilalamika hadharani kuhusu kuwepo kwa hiyo mizoga na ukali wa harufu yake.(hawa ni akina Sam Six, Mama Annie Malangu n.k). Sheria na taratibu za nyumba hii yenye kuifadhi mizoga ni kuwa mwenye tatizo hatakiwa kulalamika hadharani!!!
.
Kutokama na kuongezeka kwa mizoga na kuzidi kwa harufu kali baadhi ya majirani, marafiki zake wa karibu na hata ndugu zake walianza kumtenga. Kuna marafiki waliamua kusitisha urafiki wao na JK haradhani na hata ndugu wengine kuhama kutoka ndani ya hiyo nyumba. (hawa ni akina Sibuuda, .....n.k) Kwani JK alikuwa haambiliki wala hasikilizi mtu linapokuja suala la hiyo mizoga au harufu yake.

Siku zote JK amekuwa akiifurahia na kuisifia hii mizoga iliyoko ndani ya nyumba yake kwa kutoa harufu "nzuri".

Kuna mtoto wake mmoja alilamika hadharani hatari ya hiyo mizoga na kuongezeka kwa harufu yake. Huyu mtoto alipewa karipio kali(ambalo hakulitegemea) kutoka kwa walinzi na hata baba mwenyewe. Kilichofanyika ni kumhamisha na kumpleka kuangalia wafanyakazi wa shamba la baba yake (huyu ni Napuye alipopewa ukuu wa wilaya))

Ni ajabu na ninashagaa kusikia kwamba JK anataka kuondoa mizoga yote nyumbani kwake.!!! Kisa imezidi harufu na majirani wamelalamika sana.Hapa unawadanganya majirani na nduguzo. Mwezi wa kumi mwaka jana ulikuwa ukizunguka kwa majirani zako ukiisifia hiyo mizoga yako huku ukidai inatoa harufu ya "manukato"

Kwa kuanzia amebadilisha baadhi ya walinzi. Ndugu yangu JK, kuondoa hii mizoga ndani ya nyumba yako hakutamaliza harufu yake ambayo imeota mizizi kwa miaka mingi.

Isistoshe hata baadhi ya walinzi waliobaki, nao wana harufu ya hiyo mizoga..Hata wewe mwenyewe unayo harufu ya hiyo mizoga..

Kwanza hiyo mizoga utaiondoaje nyumbani kwako? Na utaitupa wapi??.
Na walinzi uliowaachisha kazi wataenda kuishi wapi? Maana wana harufu ya mizoga.
Japo umeandaa vijana wa kuibeba kwa ajili ya kuitupa lakini sidhani kama wana nguvu za kutosha kufanya hiyo kazi . (Mmojawapo ni M/Kiti wa UVC-M Kilimanjaro?

Kinachohitajika hapa ni kubomoa nyumba yote na kuuza kiwanja. Na hicho kiwanja kibadilishwe matumizi. Hapo ndipo utaondokana na harufu ya mizoga uliyoitunza miaka nyingi nyumbani kwako. Ona kule Misri, nyumba iliyokuwa inahifadhi mizoga imevujwa kwa amri ya mahakama!!

Sisi majirani zako, marafiki zako tuliobakia na ndugu zako tunasubiri kwa hamu kuona jinsi utakavyo itupa hiyo mizoga na jinsi gani utaiondoa harufu nyumbani kwako na wewe mwenyewe.
Pia tunataka kuona ni wapi utaenda kuitupa hiyo mizoga yako itowayo harufu kali.

Namalizia kwa kuuliza swali: Je wewe uliyekuwa ukiifadhi hiyo mizoga tukuiteje??

"MUNGU IBARIKI TANZANIA"
 
mdomo mwepesi mwambie huyu............sisi tulisema hataki kusikia......wakati kijua kinawaka tulimwambia auanike lakini hakusikia.....sasa kijua kimezama analazimika kuutwanga mbichi
 
Waheshimiwa! viongozi,makada na wafuasi wa ccm,,
wanazuoni na wasomi wa siasa na falsafa,,
wadau mbalimbali mnaopitia jamii forums,,wanajf wenzangu...
natanguliza heshima zangu kwenu!
Ningependa tuijadili kwa kina falsafa hii mpya ya KUJIVUA GAMBA kwa kujibu maswali yafuatayo;

MOSI:je gamba hili la ccm lililovuliwa hivi karibuni liliota lini?je ni toka kuzaliwa kwa ccm au liliota kuanzia mwaka 2005.

PILI:je gamba hili litachukua muda gani kuota tena?mimi sio mtaalamu wa biolojia sana lakini naamini nyoka huwa na muda maalumu kabla ya kwenda kwenye jiwe na kujivua gamba.

Naomba mwenye majibu au maswali zaidi ayaanike hapa jamvini.

Naomba kutoa hoja...
 
Nnavyodhani mimi, kati ya maswali yako MOSI & PILI jibu lake, HAKUNA JIBU!... Hakuna gamba lolote lililovuliwa, ni maigizo tuu yaliyolenga kufanikisha harakati zao za kuteka imani ya watanzania!..
 
kwa ufupi kabisa ccm hawakua na GAMBA bali ule ni UKURUTU ambao uliletwa na matendo yao machafu yalokua yakifugwa tangu ccm imechukua nchi. M nadhan kwa uchafu huo ulokithiri suluhu haikua kujivua gamba bali kunywa sumu wapotee kabisa kwny ramani then wasubiri kuzaliwa upya na jina jipya... Mwisho wa kuwasilisha. Naitwa upenyo mdogo.
 
Hakuna gamba lolote lililovuliwa, ni maigizo tuu yaliyolenga kufanikisha harakati zao za kuteka imani ya watanzania!..
yawezekana uko sahihi kwamba kilichofanyika ni maigizo tu.lakini jaribu kuelezea falsafa hii ambayo jk aliisema kabla ya mabadiliko ya kamati kuu hivi karibuni ilimaanisha nini?
 
Kama kweli CCM wameamua kujivua GAMBA wangesema pia gamba lingine litavuliwa lini. Isije ukawa ni ukurutu tu wakadhani gamba limevuliwa.
 
Ndugu zanguni hata hili linachukua muda kulitambua,
Kujivua gamba kwa ccm ni kiini macho kitu ambacho kila mtu anapaswa kukifahamu.
siku zote gamba laanza kuvuliwa kichwani na kumalizikia mkiani, sasa hili kamba la kuvua kifuani tu ni gamba gani? la mjusi ,kenge, mamba au JK gamba?
Alipaswa kuanza yewe then wengine wafuate.
JK aka kilaza anafikiri wa TZ wa sasa ni wa karne ya 15 la hasha
 
majibu sahihi
anayo mukamua.
akija jibu tafadhali atujuze je anajua kiumbe akijivua gamba(moulting/ecdysis)inabidi akae/ajifiche kwa muda mpaka liote jipya?kama ndiyo nyoka wetu(sisi si M)wametimiza vigezo hivyo au maneno
 
GAMBA- Ni kitu muhimu sana kwa mnyama kwa ajili ya kuhakikisha usalama wake, kwa mfano rahisi Kobe, hebu fikiria mazingira ya mnyama kobe jinsi gamba lake lilivyo muhimu katika kujilinda na maadui, kwa kifupi kobe hawezi kuishi bila gamba na ikibidi kufa atakufa nalo. Na ndio hivyo hivyo Chama chetu hakiwezi leo kuvua gamba, gamba ndio ngao yake na kitakufa na gamba lake. Nyoka hana gamba bali ana ngozi, nyoka huwa anajitoa ngozi yake na si kuvua gamba. Mnyama yeyote mwenye gamba akilivua tu lazima afe na vivyo hivyo Chama chetu.
 
Kujivua Gamba huanzia kichwani na ukichumguza utakuta matundu yanapokaa macho ya nyoka aliyejivua gamba. Sasa juzi CCM wajivua gamba kwa kanzia kiwiliwiwli. Vinara wa Ufisadi Mkapa na Kikwete wamebaki katika Kamati Kuu ya CCM. Hii ni ghiliba tuu
 
Kama ukifuata mfano wanyoka basi ni dhahiri baada ya muda mfupi gamba jipya litawaota hawa wanaodai kuwa wamejivua gamba. Lakini cha kushukuru ni kuwa nyoka akishajivua gamba mara kadhaa kinachofuata ni mwisho wa maisha yake kwani kujivua gamba hakumuongezei urefu wa maisha yake. Kwa hao waliovua gamba wajue kuwa mauti yao iko karibu licha ya kutaka kujionyesha wapya!
 



………….CCM imejivua gamba…………

Hii ndio kauli inayoendelea kutikisa vichwa vya habari nchini Tanzania kwa sasa kufuatia kikao cha Dodoma kilichokuja na safu mpya ya uongozi ndani ya CCM, ajabu ni kuwa wanahabari wengi wamekumbwa na kamsemo haka pasipo kufikiri mara mbilimbili nini maana sahihi ya msemo huu halikadhalika uhalisia wake upo wapi?
Naomba niweke wazi kuwa kutokana na CCM kufinywangwa ndani ya kashfa za ufisadi hasa kwa baadhi ya vigogo wake hakuna ubishi kuwa damu ya CCM ilichafuka na gamba lake likazeeka lakini kwa watanzania wengi hata CCM yenyewe imekuwa gamba sasa kutokana na maisha magumu kwa wananchi CCM ndiyo gamba sasa watu wanashangaa
CCM imejivua nini? Wao CCM watulie waone watanzania watakavyojivua gamba mwaka 2015.
Hata kama imejivua gamba wenye busara wanauliza kwani gamba la nyoka lina athari gani kwa binadamu? Badala yake ni kuwa nyoka akijivua gamba ndio anakuwa na kasi zaidi ya kutembea hivyo ndio anakuwa hatari zaidi kwa binadamu kwani anaweza kung’ata bila shida, sasa CCM kujivua gamba ina tafsiri gani kwa walalahoi?
Ipo wazi kuwa licha ya CCM kujivua gamba tena kwa kujilazimisha hakuna hoja ya msingi kwani sumu ya nyoka ipo kwenye damu sio gamba hivyo damu ya CCM ina sumu haifai na hili hata Kikwete analifahamu na anafahamu naposema damu ya CCM na maana gani? Hivyo hii ya CCM kujivua gamba ni bora mjadala ukafungwa rasmi kwani hauna maana kwa maana nani kasema sumu ya nyoka ipo kwenye gamba?..Tafakari!

Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,

Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai,

Nova Kambota Mwanaharakati,

Nipigie; 0717-709618(Tanzania) au +255717-709618(Nje ya Tanzania)

Niandikie; novakambota@gmail.com

Nitembelee; www.novatzdream.blogspot.com

Tanzania, East Africa,
Jumatano 20 April, 2011.

 
Wanajf naomba mwongozo nini maana ya kujivua gamba? Hivi nyoka anapojivua gamba anabadilika na kuwa ng'ombe au kuku?
 
Matukio mengie yametokea siku za hivi karibuni kwenye siasa za nchi yetu. Nadhani tukio kubwa ninalokumbuka ni lile la CCM kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani akina Yusufu MAKAMBA na kuweka damu mpya ya akina January MAKAMBA.

Je ni kweli sasa CCM siyo nyoka tena bali sasa amekuwa ni mjusi tu asiyekuwa na madhara kwa watanzania tena? Swali hilo ndio sijaweza kulijibu; na ndiyo maana naanzisha thread hii ili baada ya wiki moja niweza kufahamu kama kweli magezui yaliyofanyika ndani ya CCM ni ya kweli au ni danganya toto tu. jambo moja linalokera zaidi ni kuwa gamba lililovuliwa na CCM ni lile la ufisadi, ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi ni kosa la jinai. Je ni kweli mafisadi waliovuliwa CCM watafikishwa kwenye vyombo vya sheria; yaani kuna anayeweza kuniaminisha kuwa Januari atamfikisha Yusufu kwenye vyombo vya sheria ili hali Januari huyo amefika hapo kupitia mgongo wa Yusufu?

Nadhani bado tunaishi na nyoka uvunguni mwetu; wakati wowote atatung'ata tu!!

Mtu makini atajiuliza walikuwa wapi siku zote hizo.Tulishasema siku nyingi kwamba walikuwa wametukosea sisi wananchi katika maeneo mengi kwa hiyo iliwapasa kuomba radhi na kuanza upya lakini hawakusikia.Why now.Kwanza hata kuomba radhi kwa uovu wote waliotufanyia hawajaomba.Waendelee na kujivua magamba kama nyoka,to us ni nyoka wale wale bado wana uwezo wa kuuma.Kwani nyoka akijivua gamba ana cease kuwa nyoka.Mawazo duni kweli.
 
Back
Top Bottom