CCM "wakiharibu" wimbo wa Taifa: Jicho la Mutungi lina makengeza?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,199
103,733

Katibu Mkuu wa BAVICHA Nusrat Hanje na mratibu wa uhamasishaji taifa Twaha Mwaipaya wapo gerezani yapata mwezi sasa kwa kile kinachodaiwa kuuharibu wimbo wa taifa kwa kusema "Mungu ibariki Chadema, wabariki viongozi wake". Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi nae kakipa onyo Chadema kwamba jana wakati wa ufunguzi wa Baraza kuu, wanachama waliongeza ubeti wa 3 kwenye wimbo wa taifa kwa kusema "Mungu ibariki Chadema, wabariki viongozi wake"
_
Wafuasi wa CCM wakashangilia kauli ya Mtungi na wakafurahia akina Nusrat kusota jela kwa madai eti wameharibu wimbo wa taifa. Sasa nawauliza hawa wafuasi wa CCM wenye vichwa kama "Mtungi" je hiki kilichofanywa na vijana wa CCM Temeke ni sawa? Pia muulizeni huyo mwenye "Mtungi" wake hiki ni nini? Je CCM hapa hawajaharibu wimbo wa taifa? Hizi double standard ndio zinafanya Mtungi aonekane Mtungi kweli. Mtungi bhana.!

Credit: Malisa Godlisten

117195765_3213508722074131_2911542144163865371_n.jpg
 
Hicho ni kiherehere tu cha Jaji Mutungi......

Hivi kosa likifanywa na Chadema peke yake na likifanywa na CCM siyo kosa?

Hii double standards inayoendeshwa nchi hii na watendaji wa serikali kwa ajili ya kumfurahisha Jiwe, italifikisha Taifa hili pabaya
 
ila CHADEMA nao wanazingua aisee kwann wanajitaftia sababu wenyewe za kusumbuliwa?

wanazingua aisee mambo ya kitoto hayo
Wimbo wa Taifa kimsingi uligomea kwenye ubeti wa pili, ubeti wa tatu ni wimbo tuu ulioimbwa kumuomba Mungu aibariki Chadema na wala kufanya hivyo siyo dhambi maana wanaomba baraka kwa Chadema baada ya kuomba kwa Afrika na Tanzania. Mutungi anawehuka tu hovyo!
 
View attachment 1527153

Katibu Mkuu wa BAVICHA Nusrat Hanje na mratibu wa uhamasishaji taifa Twaha Mwaipaya wapo gerezani yapata mwezi sasa kwa kile kinachodaiwa kuuharibu wimbo wa taifa kwa kusema "Mungu ibariki Chadema, wabariki viongozi wake". Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi nae kakipa onyo Chadema kwamba jana wakati wa ufunguzi wa Baraza kuu, wanachama waliongeza ubeti wa 3 kwenye wimbo wa taifa kwa kusema "Mungu ibariki Chadema, wabariki viongozi wake"
_
Wafuasi wa CCM wakashangilia kauli ya Mtungi na wakafurahia akina Nusrat kusota jela kwa madai eti wameharibu wimbo wa taifa. Sasa nawauliza hawa wafuasi wa CCM wenye vichwa kama "Mtungi" je hiki kilichofanywa na vijana wa CCM Temeke ni sawa? Pia muulizeni huyo mwenye "Mtungi" wake hiki ni nini? Je CCM hapa hawajaharibu wimbo wa taifa? Hizi double standard ndio zinafanya Mtungi aonekane Mtungi kweli. Mtungi bhana.!

Credit: Malisa Godlisten

View attachment 1527154
Nakumbuka miaka hiyo nikiwa nafanya kazi serikalini,mzee mmoja akawa anatumia madaraka yake kuninyanyasa,siku moja nikaamua kumchapa ngumi ofisini kwake humo humo,nakuambia kuanzia hapo nidhamu ikawa juu sana.Hawa akina mtungi bila nguvu kutumika wataendeleza hizo double standards had kesho kutwa?
 
Back
Top Bottom