Barua ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa kuhusu uchaguzi wa CCM-2022 jimbo la Hai -Kilimanjaro

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
8,248
13,206
Katibu mkuu wa CCM Taifa fika Jimbo la Hai huko Kilimanjaro ukakutane na kituko cha mwaka 2022.
Siku ya Mwisho ya wajumbe walioomba kugombea nafasi za ccm kata ilikuwa Tare 20.6.2022 saa 10.

Cha kushangaza baada ya Jana, Leo tarehe 21.6.2022 katibu wa CCM wilaya ya Hai Mr Ballo , amechukua / amekusanya fomu zote Za wagombea walizojaza nakala tatu Tatu Kila mgombea kwa kata 17 na nafasi za wenyeviti, makatibu, wenezi na wajumbe wa kata na wilaya na kuzipeleka Ofisi ya CCM wilaya kabla fomu Za wagombea hazijapita kujadiliwa na vikao vya kamati Za siasa Za Kata Ili wagombea watakao pitishwa kwa mujibu wa katiba ya ccm majina yaweze kwenda Ofisi ya ccm wilaya Kuendelea kujadiliwa na vikao vya wilaya.

Sasa Kwa Hali ilivyo kama Katibu Mkuu wa CCM Taifa hataingilia kati kuna kila dalili uchaguzi wa ndani wa ccm jimbo la Hai kuvurugwa na upinzani kwani Makatibu was ccm kata zote wameweka mgomo kutokupokea fomu Za wagombea kutoka wilayani kabla hazijajadiliwa na secretariat ya kata na kamati Za siasa Za Kata.

Na je fomu Za walioteuliwa na Majina yao Ndio yanayoletwa wilayani au ni kubeba mzingo wote waliochukua fomu na kumpelekea mwenyekiti wa ccm wa wilaya na Katibu wake?

Je Kanuni Za uchaguzi wa ccm kwenye ngazi ya matawi na kata unaelekeza mfumo alioutumia Katibu wa ccm wa wilaya kuchukua fomu zote Za wagombea ngazi ya kata na kukaa nazo hadi siku atapenda kuzirudisha?

Je mikoa mingine ngazi ya wilaya Makatibu wa ccm wa wilaya wamefanya uhuni alioufanya Katibu wa ccm Hai?
Je kwanini amechukua fomu walizojaza wagombea zaidi ya 500 kutoka kata 17 zinazounda wilaya ya Hai bila kuishirikisha sekretariet ya chama wilaya wala kamati ya siasa ya ccm wilaya ?

Akamshirikisha mwenyekiti wa ccm wilaya tu?
Je Kwanini Katibu wa ccm na mwenyekiti wa ccm wilaya wameanza kuchukua fomu ,Majina na namba Za simu Za wagombea mapema kabla ya uteuzi wa wagombea na uchanguzi?

Kuna agenda gani kama Sio kuharibu na kuvuruga uchaguzi wa ccm?
Kuna kikundi cha vijana kiliundwa na Katibu wa ccm na kutumia mbinu kikabarikiwa na Halmashauri kuu ya ccm wilaya kinaitwa kikundi cha tehama ndicho kinatumika kuratibu uchaguzi na kinafanya kazi za uchaguzi kwa kutumwa na katibu wa ccm bafala ya sekretariet ya chama wilaya kinyume na kanuni za uchaguzi ndsni ya chama,na kutafuta majina ya mwenyeviti wa vijiji na mitaa ili kusaidia uchaguzi wa chama.
Ninashauri kikundi hiki kifutwe kinavuruga uchaguzi ndani ya chama na kinatoa siri zote za chama kwa vijana wa chadema wilaya. Pia kikundi hiki kinalikisha siri za usalama wa Taifa kikijifanya ni usalama wa Taifa jambo ambalo sio.
Je mkoa wa Kilimanjaro una wilaya zaidi ya saba je wilaya zingine Makatibu wa ccm wa wilaya Wanafanya ujinga kama huu wa kuchukua fomu Za wagombea kabla ya vikao vya chama kwenye ngazi Za chini kujadili Majina na mapendekezo?

Swali hili Katibu wa ccm wa mkoa aliulizwa hakutaka kujibu wala kuelezea kanuni Za uchaguzi ndani ya chama.
Katibu wa ccm wa wilaya ya Hai anaendesha uchaguzi wa ccm kibabe na kihuni bila kufuata kanuni na miongozo ya ccm kama chama tawala.

Katibu Ajajifunza na kuelimishwa kuwa wilaya ya Hai ni wilaya ya kimkakati hivyo akicheza na uchaguzi huu, mwisho kutakosekana wagombea wanaotokana na ccm na uchaguzi kutokafanyika au ukifanyika wateule watakuwa zao la CDM na mwisho atakushababishia chama kuwa chama cha upinzani kwenye Jimbo kama kilipotokea.

Tume Wasiliana na Katibu wa ccm mkoa wa Kilimanjaro Mh Mabya simu yake ilikuwa inaita tu ila Tumetuma ujumbe kwa sms na ulipokelewa na haujajibiwa.
Tunashauri na kupendekeza Katibu wa ccm Hai ambaye anayumika upande wa pili unampatia mlungula ili ccm ipate mgombea weak asimamishwe ,kusimamia uchaguzi wa ccm mapema na haraka kukinusuri chama kipindi hiki cha uchsguzi utakao pelekea ccm Hai kushinda uchaguzi mkuu 2025 na serikali za mitaa 2024.
Ushauri:
1. Katibu wa ccm Mkoa wa kilimanjaro ukimya wako ofisini kwako bila kupiga hodi Hai kufuatilia mwendo mzima wa uchaguzi wa ccm Hai, maana yake unaliweka jimbo rehani.
2. Fuatilia mwendo mzima wa Katibu wa ccm Hai, ukizingatia ni mgeni Hai, ni mgeni kwa kuteuliwa kuwa katibu wa ccm wilaya na jimbo la Hai lilikuwa chadema miaka mingi na hiki ni kipindi cha uchaguzi ndani ya chama.
3. Uchaguzi wa ndani wa ccm usimamiwe na Katibu wa ccm mkoa Ili kuepuka anguko la ccm jimbo la Hai mwaka 2025 , Kwa kuepuka kuchagua viongozi ambao wamejaza fomu walio wengi ambao ni wanachama wa upande wa pili.
4. Kuna Kila dalili akaharibu uchaguzi wa chama. Ili kuzuia hili lisitokee ninashauri sekretariet ya chama mkoa wa Kilimanjaro ihamie Hai ishirikiane na sekretariet ya chama Hai kuongoza na kuratibu uchaguzi huo.
5. Ili kuepuka matatizo yaliyowahi kutokea kwa Hai , ninashauri michango kutoka kwa wafanyabiashara inayokusanywa na Katibu wa ccm ipate kibali maalum kutoka kwa Katibu wa ccm mkoa na Michango hiyo ifunguliwe account maalum na fedha zitolewe na kamati maalum itakayoundwa vinginevyo Michango yote Unaishi mifukoni mwa mtu mmoja Mwisho kukiua chama.
6. Fedha Za uchaguzi ndani ya wilaya ya Hai ziwekwe wazi kwa watumishi wa ccm Hai. Kwa sasa fedha zote Za uchaguzi ni mali na Siri ya Katibu wa ccm wa wilaya.
7. Katibu wa ccm Mkoa wa Kilimanjaro kuitisha kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya ccm wilaya ya Hai kujadili jambo hili na kulipatia hatma yake kwa haraka.
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
4,726
12,860
Hama ccm wewe unachelewesha maendeleo ya nch hii

Ccm wiz na uhuni ndio.jad yao nashangaa unavyoshangaa

Huyo mbunge wa hapo mwenyewe analijua hilo
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom