Catherine Magige hajui jina wala jimbo la Luhaga Mpina

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,575
11,194
Nimeshangazwa sana na video ya mbunge wa vijana (CCM) Catherine Magige ambaye hana hata jina katika nchi hii akimshambulia mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM).

Katika video hiyo, ameonekana akimuita Luhanga mpina jambo ambalo dhahili linaonesha hafahamu jina lake labda kwakuwa sio mfuatiliaji wa vikao vya Bunge na mijadala ya kitaifa.

Si hivyo tu, amethubutu kusema "Luhanga Mpina ni mbunge wa jimbo la  Meatu" jambo linalothibitisha kuwa hafahamiani hata na wabunge wenzie wakiwemo mbunge wa Meatu na mbunge wa Kisesa!

Kwangu mimi hii ni fedheha kubwa naiona kwa kuwa na mbunge asiye na uelewa wowote wa siasa ya nchi hii.

Inasikitisha!!!

Msikilize hapa Catherine Magige: Luhaga Mpina ni mtu wa ovyo ambaye haamini uongozi wa mwanamke
 
🤣🤣🤣🤣🤣 hao wanapewa ubunge Kwa sababu ya kelele za Midomo, ila vichwan ni weupee.

Unashindwa kujua hata Jimbo la mbunge ambaye pengine Umekaa ukashauriwa umshambulie??.

Sasa huyo kweli anaweza chambua Report za CAG ?.
 
Sio kakosea kwa makusudi kukwepa kushtakiwa kwa ushahidi wa moja kwa moja so akayumbisha baadhi ya vipengele ila ujumbe unajulikana ni wa fulani? Maana Mpina sio mwepesi.
 
Sio kakosea kwa makusudi kukwepa kushtakiwa kwa ushahidi wa moja kwa moja so akayumbisha baadhi ya vipengele ila ujumbe unajulikana ni wa fulani? Maana Mpina sio mwepesi.
Huyu kilaza hana akili hiyo ila pia inaonekana ni muoga wa kamera labda hajazoea kurekodiwa na kuzungumza mbele ya kadamnasi
 
Wewe ndiyo hujui usishabikie ujinga. Kisesa ni "Uanangwa", ni Utemi wa Meatu sawa na Mwanga ilivyotoka Same.

Indeed, actually kwao Luhaga ni huku Meatu lakini kwa sababu ni watu wamoja hawaoni ubaya kuwa wanafiki kama wewe wajifiche, kugombea Meatu-Kisesa bado akapata.
 
Back
Top Bottom