Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
MJADALA mkali umeibuka bungeni kuhusu upasuaji kurekebisha maumbile, ikiwamo kupunguza au kuongeza ukubwa wa makalio katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa (CCM), ndiye aliyeibua zogo bungeni jijini, alipotoa hoja kwamba MNH-Mloganzila imeanzisha huduma hiyo kinyume cha Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007.
"Hakuna mahali kwenye Sera ya Afya yetu ya Mwaka 2007 imeruhusu jambo hili. Operesheni ya matibabu, operesheni kwa ajili ya kuongeza makalio; ni operesheni ya kimapambo (cosmetic surgery), si ya mtu ambaye ana changamoto yoyote ile ya afya.
Baada ya Mpina kutoa kauli hiyo, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby, alisimama na kumpa taarifa Mpina, akisema hata kiuno kikikaa vibaya nayo ni changamoto ya kimatibabu.
"Kwahiyo, kukiweka kiuno vizuri, ni kusababisha binadamu atembee vizuri na aweze kuwa na umbo zuri," alisema Shabiby.
Hata hivyo, Mpina alikataa kupokea taarifa hiyo ya mbunge mwenzake, akisisitiza serikali imeanzisha huduma hiyo bila kibali cha Bunge wala hakuna sheria, kanuni na mwongozo wa utoaji huduma hiyo.