CCM tusiende tena kwenye Midahalo

CCM tusiende tena kwenye Midahalo

Unaowaona pale Hospitali, mnaowapiga picha wamerundikana, wale wanangoja zamu yao ya kuzaa, hawazai pale waliporundikana, thubutu muwachiwe mkapige picha ndani ya chumba cha kuzalia, labda mzazi mwenyewe akubali na madaktari na iwe ni kwa ajili ya kufundishia, si kwa propaganda zenu za kijinga. Huzalia theater kama anavyozaa mwingine yoyote, labda awe hajawahishwa hospitali.

Haki ya kuzaa na kuzaliwa nnaijuwa vizuri sana kwani nimeshazaliwa na nimesha-zaa, hilo wala silkutie hofu.

Nimeuliza hivi:

Huu mdahalo wa Serena kautayarisha nani na fedha za kukodisha ukumbi wamezitoa wapi? na hicho kikundi kilichotayarisha huo mdahalo wana faida ipi? naomba majibu kwa hilo.


Kama unazalia theater sawa sawa sasa nakuelewa vizuri sana! !!!!!
Hebu tafuta wanawake wanaozalia theater hapa wakuambie!!!!!!
Umewahi kusikia labour ward??????!!!!
Anayesubiri kuzaa ni sawa kulala chini???!!!!

Kuweka kumbukumbu sawa hapa mimi sina haja ya propaganda na sina nasaba na chama chochote hili ulijue! !!!!!

Huwa sijibu rhettorics kamwe hata aulize mzazi wangu!!!!!
Kama unajua aliyeandaa na nia yake ukiambatanisha na sheria aliyovunja itakuwa safi sana!!!!

Otherwise ni kilio nyikani tu
 
Sasa kwanini wamekimbia bunge maalum la katiba? Hizo hoja zao mitaani zinawasaidia nini?

na hoja za ccm mtaani zinawasaidia nini wakati wameachiwa bunge peke yao wakawatukane ukawa vzr? matusi kwa wanaUKAWA nje ya bunge yanawasaidia nini ccm? matusi haya yanasaidiaje kuijenga ccm na kuleta maisha bora kwa kila mtanzania ili kuwapa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi kwa miaka mingine 5 ijayo?
 
Bado hujajibu maswali yangu, unajaribu kuyakwepa na kuyajengea hoja muflis. Wafadhili wa Serikali wanajulikana na sio siri. Na hakuna anae ifadhili Serikali bila kuwa na faida na ufadhili wake.

Sasa unapowafadhili UKAWA una faida ipi?

Tafadhali jibu maswali yangu kama hauna jibu. Kaa kimya tu kuliko kujaribu kuyajengea hoja muflis.

kwani mdahalo huu ulikuwa kwa ajili ya kuwafadhili ukawa mi sijakuelewa.
 
Duni ana hoja kali sana hakuna wa kumuweza CCM. Kuna siku alikuwa na Mwigulu Mchemba kwenye Star TV. Mwigulu alikuwa kama mtoto wa chekechea kwa Duni! Ndo maana hata Mwakyembe alutumia muda mwingi kujibu hoja za Duni kwenye Bunge la Katiba lakini bila mafanikio. Kusema kweli wazanzibari ni watu wana hoja kali kuhusus muungano. Kama alivyosema Mzee Warioba CCM hata wafanye sarakasi gani kwenye hoja ya Tanganyika kuvua koti la muungano hawatoki.
 
Duni ana hoja kali sana hakuna wa kumuweza CCM. Kuna siku alikuwa na Mwigulu Mchemba kwenye Star TV. Mwigulu alikuwa kama mtoto wa chekechea kwa Duni! Ndo maana hata Mwakyembe alutumia muda mwingi kujibu hoja za Duni kwenye Bunge la Katiba lakini bila mafanikio. Kusema kweli wazanzibari ni watu wana hoja kali kuhusus muungano. Kama alivyosema Mzee Warioba CCM hata wafanye sarakasi gani kwenye hoja ya Tanganyika kuvua koti la muungano hawatoki.

Hii comment nimeipenda 100%true
 
Kwanza jiulize hivi. hao walioandaa hiyo mada wametokea wapi? fedha za kukodisha ukumbi wamezitoa wapi? halafu wanapata faida ipi?

Sasa nakuuliza, ikiwa wana hoja nzuri za kuongelea mitaani, kwanini wamekimbia bungeni?

Wewe Foxy ni mbuzi sana uelewa wako kila siku una mashaka kama wa Vuai
 
Kwanza jiulize hivi. hao walioandaa hiyo mada wametokea wapi? fedha za kukodisha ukumbi wamezitoa wapi? halafu wanapata faida ipi?

Sasa nakuuliza, ikiwa wana hoja nzuri za kuongelea mitaani, kwanini wamekimbia bungeni?

kumbe ccm huwa na hoja tu pale waandaaji wa mudahalo wanapojulikana walipotokea na kujulikana walikopata fedha za maandalizi ya mdahalo? asante kwa kutufungua macho. na ccm wanapata faida ipi ikiwa haya yote yatajulikana? ndipo huwa na akili za kutoa hoja makini?
 
Hamna kitu pale,serikali 2 tu ndio habarii ya jamii.

hapo umemaliza kuchangia au utarejea baadaye? naona kama ulikuwa unaanza kuchangia lakini tanesco wamekata umeme. umeme ukirudi usisahau kumalizia kujenga hoja--tunataka kusikia maoni yako.
 
Sasa kw akili yako ulitaka watu wanaojitambua waungane na ujingaaaaa? CCM mnastahili kuzomewa na hata kutukanwa na ili mjue nyinyi mmewachosha watanzania endeleeni kwenda kwenye midahalo mtapata majibu yenu hata msiogope ndo uvumilivu wa kisiasa unatakiwa NENDENI MKAJIPIME MPATE KUJIELEWA

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Enzi zetu wakati tunasoma Sekondari kulikuwa na MIDAHALO (DEBATE). Motion inaweza ikawa mathalani POLYGAMY IS BETTER THAN MONOGAMY! Likawepo kundi linalo support motion na kundi jingine lina oppose motion. HOJA zinashindanishwa na baadaye KURA zinapigwa kuamua kundi lililoshinda kwa hoja! Ina maana hawa CCM wazee wenzangu kuanzia akina Kikwete, Makamba Snr, Vuai Ali Vuai, Kinana (maana naye alimkimbia Dr. Slaa kwa kumtuma Nape!) walikuwa wanakimbia hizo DEBATE?! Au hawa CCM ndiyo walikuwa wakitusumbua wakati sisi tukishusha nondo, wao wanatengeneza NDEGE ZA MAKARATASI NA KUTURUSHIA/KUTUPIGA NAZO MIGOGONI!
 
UKAWA wana uwezo gani wa kuhimili gharama za midahalo na mikutano kwa miezi mitatu mfululizo? unless wawe funded na vikundi vya nje visivyoitakia mema Tanzania na hizo funds ndizo zikazowatenganisha.

Kitendo cha UKAWA ilitakiwa iwe ni protest ya siku moja tu na siku ya pili warudi bungeni. Na si kulisusia bunge kabisa, hawana vyanzo vya mapato na hapo ndipo watakapoanza kutumika. Tena kwa kukujuza tu, licha ya kutumiwa na makundi ya nje, CCM yenyewe wanaweza kuwatumia kwa fedha kiaina ili iwasambaratishe.

Kitendo cha UKAWA mimi nnakiona ni kama pweza kujipalilia mkaa mwenyewe anapochomwa.

Utanambia.

hoja iliyo mezani inahusu uwezo wa maCCM kujenga hoja, lakini naona unatulazisha tujadili hoja ya UKAWA! kwanini usifungue uzi mpya inayohusu UKAWA badala ya kutuharibia mtiririko wa hoja?
 
UKAWA wana uwezo gani wa kuhimili gharama za midahalo na mikutano kwa miezi mitatu mfululizo? unless wawe funded na vikundi vya nje visivyoitakia mema Tanzania na hizo funds ndizo zikazowatenganisha.

Kitendo cha UKAWA ilitakiwa iwe ni protest ya siku moja tu na siku ya pili warudi bungeni. Na si kulisusia bunge kabisa, hawana vyanzo vya mapato na hapo ndipo watakapoanza kutumika. Tena kwa kukujuza tu, licha ya kutumiwa na makundi ya nje, CCM yenyewe wanaweza kuwatumia kwa fedha kiaina ili iwasambaratishe.

Kitendo cha UKAWA mimi nnakiona ni kama pweza kujipalilia mkaa mwenyewe anapochomwa.

Utanambia.

LUMUMBA ON DUTY!!:majani7: tunasubiri tukuone hivii :mimba:
 
WATANGANYIKA MMELIONA HILI
Siku zote huwezi kuzuia hoja yenye nguvu wengi wasio na hoja wanachokifanya ni kuvuruga mada na kujaribu kuleta hoja juu ya hoja ili kuharibu hoja ya msingi swala la katiba ukisikiliza hoja bungeni ,kwenye taasisi au hata vijiweni kwa watu wa kawaida kabisa yale mawazo yaliyopewa jina la mawazo ya wachache yana nguvu za hoja kuliko yale yaliyopewa jina la mawazo ya wengi kinachonipa shida ni hizi hoja zinazosindikiza hoja ya msingi watu wamezunguka nchi nzima kwa pikipiki wakahitimisha kwa kupokewa na mkuu na hotuba bado wqnawaona waliohutubia mkutano miwili tu Zanziba kuwa ni wachochezi bila kutueleza wanachochea nini na kwanini? Naomba mnisaidie kunielewesha ukawa wanachochea nini
 
Duni aliongea uzuri sana kihoja kumzidi vuai,vuai alinifurahisha aliposema zanzibar kunatatizo kuipata 2/3 kitu ambacho ccm wachache sana wanaoweza kuusema ukweli huu
 
CCM wamebaki tu kuseme "mbili zatosha". Wakiulizwa zatoshaje? Kila mtu anawahi kutoa mapungufu ya serikali tatu badala ya kutushawishi mbili zinatosha vipi!. Acheni umaamuuma, watu wameamka sasa hivi, wanataka hoja.
 
Leo nilikuwepo Serena Hotel kuhudhuria Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi moja binafsi nchini (jina limenitoka). Nimesahau hadi jina la Taasisi kwa yaliyotokea pale. Mdahalo huo ulikuwa ukiongozwa na Bi.Rosemary Mwakitwange na kurushwa moja kwa moja na ITV na Radio One. Pamoja na washiriki wengine,meza kuu iliwajumuisha watu 'wazito'.

Mdahalo ulijikita katika Mada: Tanzania Tuitakayo.Lakini hasa ilizungumzwa sana Rasimu ya Katiba mpya.Meza kuu ilikuwa na Wageni kama Ndugu Juma Duni Haji (Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF),Ndugu Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar) na Humprey Polepole (Mjumbe wa zamani wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba).

Kiufupi,CCM tumedhalilishwa,tumezomewa,tumejichanganya,tumepoteana,tumejiharibia na kukosea kuhudhhuria pale. Vuai hakutusaidia. Alibaki kutetema kwa hasira na kushikwa na tashwishwi zisizo na maana. Eti alidai watu 9000 ni asilimia 5 ya watu wote wa Zanzibar.Kweli?! Hivi hata kama Zanzibar ina watu milioni moja kamili,asilimia 5 ni watu 9000?

Duni na Polepole walitamba walivyoweza.Walishangiliwa.Walifunika.Walimpotezea mbali Vuai. Walishinda kirahisi kutokana na mwakilishi wa CCM kukosa hoja za haja na kubaki kubwabwaja. Sikuamini macho yangu.Watanzania watatuonaje kiuongozi kama watu waliopo ni watu aina ya Vuai? Tusiende tena kwenye Midahalo

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mimi namfahamu vizuri sana maalim Juma Duni ni kada aliyekomaa sana amekuwa katika CC ya CCM na kuwa mjumbe wa NEC ya CCM tokea 1977 kwa zaidi ya miaka 15. Na aliwahi mpaka kuwa makamo mwenyekiti wa shirika la uchumi la CCM yaani SUKITA kwa miaka mingi tu. Lakin kubwa ameshika nyadhwifa mbalimbali za juu katika Serikali ya Znz kwa kipindi kirefu hivyo ana uzoefu mkubwa sana katika siasa za ZNZ na hata za CCM Tgk.

Kumpambanisha Maalim Duni na Nape au Vuai ni kama kulinganisha kichuguu kwenye mlima mrefu kuliko Kilimanjaro. Kwa Duni ilibidi CCM aje MSEKWA au Malecela au hata Mangula kidogo angejaribu.

Msimlaumu Vuai, Duni sio saizi yake.

Jipangeni katika uchaguzi wa watu katika midahalo na sio bla bla.

 
Back
Top Bottom