CCM tusiende tena kwenye Midahalo

CCM tusiende tena kwenye Midahalo

Sio kweli dada angu, hebu tuanzie kwenye chopa 3, kata 3. Kalenga na chalinze ndio tuseme hayo,

Kwa elimu tuliyonayo watanzania sishangai CCM kuendelea kushinda hasa huko vijijini! Miaka hamsini ya uhuru na fursa kubwa ya kila mtoto kwenda shule lakini tumevuna nini? Wananchi wengi vijijini ukiwauliza rais wa nchi watakujibu ni Nyerere. Ndio taifa linalijisifia limepiga hatua wakati watu wa nje wanakuja kusaini mikataba ambayo mTz hafaidiki chochote! Mtwara wakadai rasimali yetu tunafaidikaje nayo wakakiona cha mtema kuni..serikali sikivu ya CCM!

VIJANA MPO?

Serikali iunde Tume halafu serikali hiyohiyo iikane tume iliyounda yenyewe je hiyo serikali in watu walioenda shule au? Inakera na inasikitisha sana kwani huko tuendako inaelekea tutatumbikizwa shimoni.
 
Sio kweli dada angu, hebu tuanzie kwenye chopa 3, kata 3. Kalenga na chalinze ndio tuseme hayo,

Mkuu naona unajaribu kujitoa ufahamu.
Tunazungunzia kufeli kwa ccm kwenye midahalo. Mada ilikuwa Tanzania tuitakayo hususani Katiba mpya. Sasa naona mkuu matope yako humo kichwani bado yanakumbuka chopa 3 unazani ule ni uchaguzi mkuu?
 
Nimeuliza hivi, huu mdahalo wa Serena kautayarisha nani na fedha za kukodisha ukumbi wamezitoa wapi? na hicho kikundi kilichotayarisha huo mdahalo wana faida ipi? naomba majibu kwa hilo.

Unaleta mambo ya akina mama wakati nyinyi wenyewe ndio mnawazalisha kama kuku. Hao kina mama mimba wanajijaza wenyewe? usianze viroja. Hebu anzeni kuwacha kuwaingilia bila kinga uone kama hospitali zitajaa. It takes two to tango.

Kuzaa ni haki ya msingi ya wanandoa kama ulivyozaliwa na ulivyozaa wewe ,suala la kipato halina uhallalishi wa wewe kuzaa kitandani masikini azae chini wakati hiyo unayoita na kuhoji misaada au ufadhili ililenga kuondoa kadhia hiyo, so faida ya misaada au udhamini sio lazima kila wakati ikufurahishe au kukunufaisha wewe au kundi lako!!!! Upo hapo????!!!!!

Faida moja ya wazi ni kuwa kabla ya mjadala wanapewa taarifa wanajiaandaa na wanakuja wako na maandalizi ya kutosha, wananchi wanataarifiwa na media zinalipwa kuonesha dhamira na uwezo wa washiriki tukijua wazi kuwa wanawakilisha taasisi zao!!!!!

Wananchi wanofikiwa na media wanaona na kusikiliza na kuanzisha mijadala pacha kama huu hapa! !!!!

Hili ni kubwa kati ya faida za jumla na wazi kabisa haya weka latent functions sasa!!!!
 
Silaha ya kijinga. Na wrong timing.

Unafikiri UKAWA wana fedha kiasi gani ya kuweza kuendeleza hiyo silaha yao kwa miezi 3 mfululizo? unless wawe funded na vikundi vya nje visivyo itakia mema Tanzania. Na hizo funds ndizo zitawagawa.

Fikiri!

wakikosa pesa wapenda mabadiliko tutachangia.kwa idadi yetu kila mmoja akichangia shilingi 500 kwa mwezi inatosha sana.
 
FaizaFox kupanga ni kuchagua na ukiwa kiongozi wa nchi ni lazima ujue mipango yako ya maendeleo itawafikisha wapi wananchi wako ikiwa ni pamoja na idadi ya watu. Sasa kama elimu ya uzazi haitolewi unategemea nini? Watu hawana kazi unategemea nini kazi waliyonayo si kuzaliana tu? Pamoja na kuwa wanajua hawana chakula au ajira lakini mazingira yanafanya watu wazaane bila mpangilio na serikali inajua hilo sasa ilikuwa watoe elimu muafaka ikiwa ni pamoja na idadi ya watoto kwa kila kaya. La sivyo serikali ipambane na hiyo hali kwa kuboresha huduma ya afya!
 
Shukraan mkuu pembe
 
Last edited by a moderator:
Sijaona ubaya wa mdahalo wa jana,ninamshukuru sana Rose Mwakitwange ametusaidia wengi kujua mengi ndani ya rasimu ya katiba.

Nimefurahishwa pia na kauli yake tujali Tanzania na si vyama vyetu.Na alichosema Humphrey Polepole kinamantiki kwamba walichohitaji wajumbe kwanza ilikuwa kujengewa uwezo wa kujadili masuala ya katiba na kufikia muafaka wa aina ya muungano tuitakayo.

Ninauhakika ingekuwa CCM imeandaa huo mjadala tungeona pongezi kila kona kwa muandaji bila kujali nani amefadhili Mdahalo huo.Lakini kwa sababu haukuwa upande wa CCM basi maswali yote na kejeli yatapelekwa kwa aliyeandaa.Analeta vurugu,aliyefadhili mdahalo hana nia au malengo mazuri nk nk.

Kwa CCM Mtanzania wa kawaida kupata elimu ya kitu husika ni mwiko,bali Mtanzania anatakiwa alishwe chakula cha aina moja tu!Hivi afya yake kimawazo tunaidumaza au tunaihuisha?Mtoto yoyote asipopata malezi bora ndani ya familia atayapata nje ya familia na hapo itabidi mtoto mwenyewe achague afundishwe yapi mazuri au mabaya.

CCM waacheni watanzania tuelimike hata kama tukijapiga kura tupige tukijua nini tunataka na kwanini.Tafadhali msiendelee kutunyima UHURU na HAKI ya kujua mambo hususani Katiba.

Katiba ni yetu sote na si ya wanaCCM tu.Nilishawahisema ukiwa pro-CCM basi utaitwa majina yote mazuri na utabebwa kweli kweli,lakini ukiwa against CCM utapewa majina yote mabaya,Utaitwa Chaggadema,muhalifu,mleta vurugu,mpenda vurugu,muuaji nk nk,basi kwa ufupi ni Mtanzania ambaye hastahili kuishi Tanzania.Basi wangetafuta Nchi hawa walioagainst CCM wapelekwe.
 
Kuzaa ni haki ya msingi ya wanandoa kama ulivyozaliwa na ulivyozaa wewe ,suala la kipato halina uhallalishi wa wewe kuzaa kitandani masikini azae chini wakati hiyo unayoita na kuhoji misaada au ufadhili ililenga kuondoa kadhia hiyo, so faida ya misaada au udhamini sio lazima kila wakati ikufurahishe au kukunufaisha wewe au kundi lako!!!! Upo hapo????!!!!!

Faida moja ya wazi ni kuwa kabla ya mjadala wanapewa taarifa wanajiaandaa na wanakuja wako na maandalizi ya kutosha, wananchi wanataarifiwa na media zinalipwa kuonesha dhamira na uwezo wa washiriki tukijua wazi kuwa wanawakilisha taasisi zao!!!!!

Wananchi wanofikiwa na media wanaona na kusikiliza na kuanzisha mijadala pacha kama huu hapa! !!!!

Hili ni kubwa kati ya faida za jumla na wazi kabisa haya weka latent functions sasa!!!!

Unaowaona pale Hospitali, mnaowapiga picha wamerundikana, wale wanangoja zamu yao ya kuzaa, hawazai pale waliporundikana, thubutu muwachiwe mkapige picha ndani ya chumba cha kuzalia, labda mzazi mwenyewe akubali na madaktari na iwe ni kwa ajili ya kufundishia, si kwa propaganda zenu za kijinga. Huzalia theater kama anavyozaa mwingine yoyote, labda awe hajawahishwa hospitali.

Haki ya kuzaa na kuzaliwa nnaijuwa vizuri sana kwani nimeshazaliwa na nimesha-zaa, hilo wala silkutie hofu.

Nimeuliza hivi:

Huu mdahalo wa Serena kautayarisha nani na fedha za kukodisha ukumbi wamezitoa wapi? na hicho kikundi kilichotayarisha huo mdahalo wana faida ipi? naomba majibu kwa hilo.
 
CCM siku zote hawajawahi kufanya vizuri kwenye midahalo tangu ule wa urais wa 1995 wakiwakirishwa na mzee mkapa ulioongozwa na mzee Simbeye.
lakini pia hiyo ndo taawira halisi ya viongozi wanao liongoza taifa hili ndo maana hata katika bunge hoja zao ni hafifu sana na mwisho kuishia kulazimisha maswala.
hata hivo Vuai asingekuwa na hoja yoyote kwa kuwa siku zote kuutetea uongo ni ngumu sana, maana ukweli anaujua.

Hivi huu UWOGA wa midahalo kwa wana-CCM umesababishwa na nini? Mbona Nyerere alikuwa haogopi midahalo? Hata Mkapa 1995 alifanya vizuri tu kwenye mdahalo dhidi ya mzee wa Kiraracha Mrema. Ingawa naye baada ya miaka 5 akawa MUOGA wa midahalo? Kuna jambo ngani limejificha hapo. Hivi kweli kama Obama au Uhuru Kenyetta wangekimbia midahalo ya president candidates wangeweza kweli kuchaguliwa kuwa marais wa nchi zao. Majabu ya Tanzania wakimbia MIDAHALO ndiyo wanachaguliwa kuwa MARAIS wa Tanzania? Kweli Tanzania tuna uwezo DUNI wa kufikiri (IQ)
 
Kwa hiyo ule ulikuwa uchaguzi? Pole pole amepata kura ngapi?

haukuwa uchaguzi, bali hoja za ccm hazikuwa na mashiko, hata waliomtegemea kusaidia kutoa maelezo ya kina, kwanini wachomekee hoja ya serikali mbili , alikosa majibu na kubaki kuzomewa.ndo ubaya wa kulazimisha mambo ambayo umma unaona ni kuendeleza ghiriba na hila za kuendeleza utawala usio na masilahi na kuleta usitawi wa umma.kama alivyothibitisha kinana kwenye mkutano wa kibanda maiti kuwa ,"hata kama tutapata katiba mpya,haiwezi kuleta maendeleo na usitawi wa umma".maanake, wao wanataka tuendelee na katiba mbovu kwa masilahi ya matumbo yao na si umma.
 
CCM hawawezi midahalo ya takwimu bali wanaweza mipasho
 
Nimeuliza hivi:

Huu mdahalo wa Serena kautayarisha nani na fedha za kukodisha ukumbi wamezitoa wapi? na hicho kikundi kilichotayarisha huo mdahalo wana faida ipi? naomba majibu kwa hilo.

Kwahiyo ukishafahamu waandaji wa mdahalo na wafadhili ndiyo Vuai Ali Vuai atapata AKILI ZA KUONGEA POINT? This remind me the old adage which goes like "MBAAZI AKIKOSA MAUA HUSINGIZIA JUA!
 
Bado hujajibu maswali yangu, unajaribu kuyakwepa na kuyajengea hoja muflis. Wafadhili wa Serikali wanajulikana na sio siri. Na hakuna anae ifadhili Serikali bila kuwa na faida na ufadhili wake.

Sasa unapowafadhili UKAWA una faida ipi?

Tafadhali jibu maswali yangu kama hauna jibu. Kaa kimya tu kuliko kujaribu kuyajengea hoja muflis.

kadiri unavyojitahidi kuitetea ccm ndio unavyozidi kujichanganya. Unasema misaada ya serekali sio siri, mikataba mingapi ni siri? Na je unajua ile mikataba 16 ya juzi na uchina watz hatujui ni nini zaidi ya ccm kujua kilichomo.
 
Silaha ya kijinga. Na wrong timing.
MAMA wewe tunakujua napenda serikali tatu hapa unatuzuga tu sisi wanaCCM.
Unafikiri UKAWA wana fedha kiasi gani ya kuweza kuendeleza hiyo silaha yao kwa miezi 3 mfululizo? unless wawe funded na vikundi vya nje visivyo itakia mema Tanzania. Na hizo funds ndizo zitawagawa.

Fikiri!
Sisi tunakujua wewe ni serikali tatu hapa unatuzuga tu sisi wanaCCM
 
Msilalamike sana hamjui kufanya siasa mnajua kuhujumu wapizani tu, Tangu muanze kuingia kwenye midahalo sijawahi kuona mnashinda, zaidi huwa mnaishia kutishia kuwa ninyi mmeshikria dola.
Nakushauri muongeze kozi ya midaharo kwenye chuo chenu cha pale Iringa.

Leo nilikuwepo Serena Hotel kuhudhuria Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi moja binafsi nchini (jina limenitoka). Nimesahau hadi jina la Taasisi kwa yaliyotokea pale. Mdahalo huo ulikuwa ukiongozwa na Bi.Rosemary Mwakitwange na kurushwa moja kwa moja na ITV na Radio One. Pamoja na washiriki wengine,meza kuu iliwajumuisha watu 'wazito'.

Mdahalo ulijikita katika Mada: Tanzania Tuitakayo.Lakini hasa ilizungumzwa sana Rasimu ya Katiba mpya.Meza kuu ilikuwa na Wageni kama Ndugu Juma Duni Haji (Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF),Ndugu Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar) na Humprey Polepole (Mjumbe wa zamani wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba).

Kiufupi,CCM tumedhalilishwa,tumezomewa,tumejichanganya,tumepoteana,tumejiharibia na kukosea kuhudhhuria pale. Vuai hakutusaidia. Alibaki kutetema kwa hasira na kushikwa na tashwishwi zisizo na maana. Eti alidai watu 9000 ni asilimia 5 ya watu wote wa Zanzibar.Kweli?! Hivi hata kama Zanzibar ina watu milioni moja kamili,asilimia 5 ni watu 9000?

Duni na Polepole walitamba walivyoweza.Walishangiliwa.Walifunika.Walimpotezea mbali Vuai. Walishinda kirahisi kutokana na mwakilishi wa CCM kukosa hoja za haja na kubaki kubwabwaja. Sikuamini macho yangu.Watanzania watatuonaje kiuongozi kama watu waliopo ni watu aina ya Vuai? Tusiende tena kwenye Midahalo

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
CCM tusiende tena kwenye Midahalo
- Hivi unajua kilichomuondoa Mzee Tido TBC?
- Kwa hiyo unakubaliana na Mzee Makamba kuwa alikuwa sahihi kuzuia midahalo?
- Pia unakubaliana na 'busara' za mwenyekiti kukimbia mdahalo (kama Nape) wakati wa kampeini uchaguzi?
Asante kwa kusimamia ukweli katika bandiko lako.

Kwa nini msitumie yale yaliyotokea pale kuwa fundisho kwa siasa zenu nchini. Mnatumia nguvu bila hoja. Itafika wakati hata wanaowashabikia watalijua hilo
 
Back
Top Bottom