CCM mmetuaibisha Katesh kwa kutumia vifo na madhara yetu kama mtaji wa siasa

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Mimi na wenzangu raia wa Mkoa wa Manyara hakika mmetuaibisha sana sisi wakazi wa Kateshi kwa kutumia shida na machungu yetu kama mtaji wenu CCM katika harakati zenu za siasa kuelekea uchaguzi wa mitaa 2024 na ule mkuu 2025.

Nini hasa kimepelekea nyie mjivishe jukumu la nani aje atupe pole na misaada na nani asikanyage Kateshi?
Msiba ni wetu, nyie ni nani mnataka kutufanya sie ni mbumbumbu kiasi mnafikia kumzuia Mwenyekiti wa Chadema na ujumbe wake mdogo kuja kutusabahi? Mlichofanya ni kama mnatuchulia na misiba itajirudia kama sie hatutafanya zindiko la kuondoa hilo balaa mlilotuangushia bila nyie kujua.

Kikwetu kwenye msiba ukimbagua mtu yeyote basi elewa utazika mfululizo hadi umuombe radhi uliyembagua wakati kaja kwako kwa moyo mmoja.

Tafadhali sana muombeni msamaha Mbowe na watu wake, msibani hakuna mgeni mashuhuri kuliko mwingine, vinginevyo tutawachukia kama mlivyochukiwa na kabila fulani ambalo mlikula hadi rambirambi zao kwa kashfa na kejeli nyingi.

Tunajua hata tusipo wapa kura kama huko mtaiba tuu, lakini bora mjue mnaiba kura kwa vile tumewachukia kwa mliyotenda.

Wazee wetu watakaa na kulishughulikia hili kama mtadharau kutuomba radhi na kumuomba radhi mgeni wetu aliyekuja kwa moyo mwema.

Pia soma> Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 63
 
CHADEMA walitaka kuleta siasa kama kawaida yao,bila kujuwa kuwa watu wanahitaji misaada,faraja na kutiwa moyo kutokana na yale yaliyowakumba. Sasa wao CHADEMA wakataka waweke kama ndio jukwaa la kufanyia propaganda.
CCM ni shetani ambaye anaonea wivu mpaka maiti. Namheshimu na kumkumbuka sana Baba wa Taifa. Lakini hii CCM shetani ya sasa, siyo sahihi ka isa kuishikamanisha na Mwalimu Nyerere.
 
CHADEMA walitaka kuleta siasa kama kawaida yao,bila kujuwa kuwa watu wanahitaji misaada,faraja na kutiwa moyo kutokana na yale yaliyowakumba. Sasa wao CHADEMA wakataka waweke kama ndio jukwaa la kufanyia propaganda.
Manyara na huko khatesh babati
Ilishakuwa ngoma ya cdm,
Ccm nyie hapo ni wajuzijuzi
Cdm wana haki nao hapo

Ova
 
CHADEMA walitaka kuleta siasa kama kawaida yao,bila kujuwa kuwa watu wanahitaji misaada,faraja na kutiwa moyo kutokana na yale yaliyowakumba. Sasa wao CHADEMA wakataka waweke kama ndio jukwaa la kufanyia propaganda.
Since day one nilikuambia mmefurahia hilo janga ili mfanye siasa. Na Sasa imedhihirika nilichokuambia baada ya kuvaa sare za ccm kana kwamba ni mkutano wa kampeni.

Na mmejiacha uchi zaidi baada ya kuwazuia viongozi wawili watatu wa cdm kwenda huko. Mmeamua kujimilikisha msiba, na nani asihudhurie.

Wivu wa kisiasa, na siasa za kishamba kuwa nyie ndio mliowajali wananchi zimepotezwa na viongozi wachache sana wa cdm. Kweli majizi ya kura Leo mmetia aibu sana. Cdm wako level nyingine zaidi yenu chama la majizi.
 
CCM ikatawe popote!
Ilisha kataliwa kutambo kwa kutumia kwake majanga kama Kiki kwao.
Habari mpya ni kuwa baada ya Mbowe kuamua kuondoka eneo hilo viongozi wa serikali wakagundua haraka sana mchezo walio ucheza ubaya wake na athari zake na kumuita haraka kuwa zuio la kutoingia Kateshi limeondolewa sasa anaweza kufanya shughuli iliyo mpeleka.
Kwa kweli ilikuwa picha mbaya sana kwa watoa misaada ndani na nje ya nchi kama ubaguzi huo ungeendelea au kilichotokea kingeachwa kiandikwe kama historia.
Hisia za Wana Kateshi na Watanzania wengine kwa CCM na serikali yake zingezidi kuwa negative.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
CHADEMA walitaka kuleta siasa kama kawaida yao,bila kujuwa kuwa watu wanahitaji misaada,faraja na kutiwa moyo kutokana na yale yaliyowakumba. Sasa wao CHADEMA wakataka waweke kama ndio jukwaa la kufanyia propaganda.
Wote, hata CCM tunatumia hilohilo.
 
UBAGUZI NI KITU KIBAYA SANA.
KIPO CCM NA VYAMA VINGINE.
HAKUNA MZURI KWA HILI....
 
Back
Top Bottom