CCM mbona kimya kingi kuhusu kifo cha Mabina?

shangaa hawa manyangau Ccm walivyo huyo kijana wa miaka 12 aliyeuawawa kabla ya yeye kuuwawa hawamsikitii
kwasababu sio maarufu na hakuwa na utajiri.
pia nimesikia mabina alishauza hilo shamba kwa NSSF kwa billion 2 nashangaa kilichompeleka huko
 
Tanzania bana...very kontradikitingi

Wananchi tunaambiwa tutii sheria bila shuruti

viongozi wanavunja sheria bila shuruti...

Kuna mtu alikuwa anauza ARV feki, hadi leo hajachukuliwa hatua zozote...na ni kiongozi mkubwa wa CCM yao...

anaitwa RAMADHANI MADABIDA , hakuna haja ya kumung'unya maneno , ni Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Dar es salaam , ANGALIZO - KUNA HAJA YA KUCHUNGUZA MWENENDO WA KILA MWANA CCM ULIYEKARIBU NAYE .
 
Habari zilizopo ni kwamba katika kutafuta ungwaji mkono kanda ya Ziwa ambako chama hicho kipepoteza kukubalika kutokana na matatizo mbalimbali yanayo wakumba wananchi wa kanda hiyo hususani Serikali kushindwa kuendeleza kikamilifu zao la Pamba, huduma hafifu za jamii n.k

CCM imeona ni vyema kutoshiriki mazishi ya aliyekuwa Diwani na Mwenyekiti mstaafu wa ccm mkoa, hoja yao ni kwamba endapo watashiriki mazishi hayo itaonekana wanaunga mkono watu uvunjaji wa sheria kwani marehemu Mabina alijichukulia sheria mkononi kwa kumuua kijana wa miaka 12 asiyekuwa na hatia.

Angalizo:
CCM kimejaa watu wengi waharifu na wanaopenda kuvunja sheria, tumeona watu wakipigwa kwa kukatwa mapanga kwenye chaguzi, kuchomewa moto mali zao kwenye chaguzi, kupora mali za wanyonge n.k. Sioni kama ni suluhu kwa chama hicho kutoshiriki mazishi ya kiongozi huyo bali suluhu ni kukisafisha chama chao kwa kuondoa watu wote aina hiyo
kwa kuwa jambo hilo wanalifanya kwa hila lazima litawaletea haibu na kuipaisha chadema, kila wakati nawaambia ccm waache kufanya mabo kwa hila,na hasa kuwafanyia hila chadema hawanisikii, ccm ni sikio la kufa
 
Maiti huwa haitupwi bila shaka watamzika
Hata magamba wakigoma basi Jiji litahusika.
 
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?

Wanakimbia kivuli chao.,pia wasisahau hiyo ni salamu kwa wasaliti wote kuanzia huyo diwani matata na mazuzu wenzie."Sipati picha hiyo zomeazomea kwa magamba kunako uchaguzi wa marudio".
 
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?
Ah,"Ukifanya fujo,ukiambiwa usifanye hiki utapigwa tu!maana tumechoka sasa"Si tuliambiwa hivyo,au umesahau ndugu? Au ndiyo vile Mkuki kwa ngurue?
 
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?

Hayakuhusu.
 
Tanzania bana...very kontradikitingi

Wananchi tunaambiwa tutii sheria bila shuruti

viongozi wanavunja sheria bila shuruti...

Kuna mtu alikuwa anauza ARV feki, hadi leo hajachukuliwa hatua zozote...na ni kiongozi mkubwa wa CCM yao...

Mkuu umenikumbusha nilishasahau hiyo sinema. Anaitwa Madabida (?), hata majina yanafanana fanana. Kweli ccm majanga! Wameoza wote...
 
Mh we ni mchokozi sana. Hiyo ni kesi ya jinai hivyo CCM hawawezi kusema lolote kwani wataharibu ushahidi. Isitoshe hawakumtuma amditopile yule mtu anyedaiwa kuditopiliwa!
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?
 
Mimi nimetoka Mwanza jana na kila mtaa niliopita wananchi wengi nilioongea nao walikuwa wanafurahia mno kifo cha mabina huku wakisema amebaki mwanasiasa mmoja ambaye ni mbabe kama marehemu ambaye ubabe wake kwenye halmashauri ya jiji umepita kiwango. Kilichonishtua pia ni ile hali ya wananchi kudai kuwa sasa hakuna kuogopa bunduki tena, kwani atauawa mmoja wengine tunasonga mbele na mawe, ukweli ni kuwa kama hali ndo hiyo basi tumefika pabaya kwani hata mabomu ya machozi si chochote wala lolote. Mara nyingi CCM hufikiri kuwa wananchi wanakichukia kwa sababu ya Chadema na hivyo kutumia pesa nyingi na mikakati mingi ili kukifuta chadema!!! Kumbe sivyo, wanakosea sana kwani Jibu limepatikana wazi wazi huko Kisesa na msipowaondoa hao magamba, wengi watakufa kifo cha Paka Mwizi kama Marehemu Mabina. Mungu niweke hai nishuhudie Vita vya mawe na Bunduki 2015....
 
Back
Top Bottom