CCM mbona kimya kingi kuhusu kifo cha Mabina?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
2,000
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?
 
Lusam

Senior Member
Apr 4, 2013
195
0
Ni aibu kwa kiongozi kama yeye kuuliwa na wapiga kura wake, isitoshe kesi ilikua Mahakamani Kutokana na ubabe wa wana CCM kwa wapiga kura wao akaamua kuvunja Sheria.
 
Jahman

JF-Expert Member
Dec 25, 2011
469
250
Kwani walitoa tamko dhidi ya mbakaji Kapuya? Waache wafu wazike wafu wenzao

Wamekuwa kimya mno jamani, kama vile hawajapata msiba, nasubiri historia ya marehemu, ile aya ya sababu za kifo cha marehemu
 
M.G.

Member
Nov 13, 2013
42
95
Utawala wa sheria.Kesi mahakamani.Mabina kwenda kupanda miti kwa sababu ni msimu wa mvua.Pagumu hapo.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,536
2,000
Bwana mdogo Kiwi,
Hayo si mambo madogo kama weye ulivyo mdogo. Aliye kufa ni diwani, aliyeuawa na wananchi wake kwa hasira zao juu ya ufisadi wake.
Tayari hilo pekee linatosha kuonesha kuwa kata hiyo sio ya ccm tena. Sasa, kupokwa kata mchana peupe, uongeze na sile za Arusha ambapo kidonda bado kibichi kabisa!!! Yataka moyo atii kuamini.
CCM bado hawaja amini. Nape hajaamini kuwa aibu nyingine inamngoja ya kupoteza tena kata hiyo.
Poleni sana wafiwa wa mtoto asiyestahili bali amenyang'anywa uhai wake mapema mno. Mungu ampokee tu na amlipe aliyemtuma huko kabla.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
2,000
Roho ya mtoto wa miaka 12 ipumzike kwa Amani na aliye muua ahojiwe na Mungu
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
2,000
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?

Mkuu hiyo Kata sina hakika kama CCM wataenda kuomba kura .Maana alikuwa Diwani wao na akaamua kuwatenda .Sijui wacha tuone maana CCM hawakuumbwa na aibu .
 
Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,118
2,000
...magamba ndoano imewakwama kooni,kumeza wanashindwa kutema imeshindikana..."wananchi wakiikosa haki mahakamani wataitafuta hata kwenye mawe"....
 
Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
2,000
Bwana mdogo Kiwi,
Hayo si mambo madogo kama weye ulivyo mdogo. Aliye kufa ni diwani, aliyeuawa na wananchi wake kwa hasira zao juu ya ufisadi wake.
Tayari hilo pekee linatosha kuonesha kuwa kata hiyo sio ya ccm tena. Sasa, kupokwa kata mchana peupe, uongeze na sile za Arusha ambapo kidonda bado kibichi kabisa!!! Yataka moyo atii kuamini.
CCM bado hawaja amini. Nape hajaamini kuwa aibu nyingine inamngoja ya kupoteza tena kata hiyo.
Poleni sana wafiwa wa mtoto asiyestahili bali amenyang'anywa uhai wake mapema mno. Mungu ampokee tu na amlipe aliyemtuma huko kabla.

Duu,

Mkuu nimekuwa bwana mdogo?
Ninafikiri kiumri ni mmoja wa wanajamvi wenye umri mkubwa humu JF.
Shahada yangu ya kwanza niliipata mwaka 1981 UDSM, sina haja ya kueleza nina shahada ngapi mpaka sasa wala wasifu wangu hauna haja ya kuanikwa humu jamvini. Mahali panapohusika na kwa wanaonifahamu wanajua hayo.
Nimekusamehe bure mkuu...
 
justuskipara

Member
Oct 21, 2013
76
0
Maccm hapa mwanza hayaongei kabisa utafikiri hayana musiba,yanaongelea mpira. Wamekufa na musiba wao aibu imewakuta na nitaenda kusikiliza historia ya marehemu nitawajuza aibu yao wana jf tulia.
 
jerry voice

Member
Dec 16, 2013
10
0
Hii inaonesha wazi kuwa hamna walio juu zaidi ya nguvu ya uma wakichoka madhara yake ndio hyo viongozi wa ccm wanapaswa kujua wananchi wamekichoka chama na udhalimu unaoendelea ndani ya chama mwananchi wa tanzania usifanye makosa 2015!!
 
Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
588
1,000
Duu,

Mkuu nimekuwa bwana mdogo?
Ninafikiri kiumri ni mmoja wa wanajamvi wenye umri mkubwa humu JF.
Shahada yangu ya kwanza niliipata mwaka 1981 UDSM, sina haja ya kueleza nina shahada ngapi mpaka sasa wala wasifu wangu hauna haja ya kuanikwa humu jamvini. Mahali panapohusika na kwa wanaonifahamu wanajua hayo.
Nimekusamehe bure mkuu...

Pole sana mkuu watoto wa humu jamvini we wachukulie poa tu maana wanajibu kama wapo kijiweni.. Ilo nakupa salute mkuu ila gamba la bachelor umechukua long time sana yaani kama mvungi. Baba unatisha.
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,694
2,000
1463705_480534795397627_448780611_n.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom