Kifo cha CCM kimetimia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha CCM kimetimia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by activisty, Jul 22, 2012.

 1. activisty

  activisty JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 315
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ikiwa ni muda mrefu umepita,tokea watanzania tupate uhuru, tukiwa chini ya utawala wa TANU, hatimaye CCM bado mabadiliko makubwa hayajafanyika kuonesha malengo ya kulipatia taifa letu maendeleo. Awamu ya kwanza ilianza vyema, lakini mawazo ya Mwalimu JK Nyerere yalipoanza kukiukwa katika awamu ya pili, ya tatu na hatimaye ya nne ndio sasa watanzania tunaona tuko katika jehanamu iliyojaa chuki,njama,ufisadi, na umaskini uliokithiri.

  Ni ukweli usiofichika CCCM na uongozi wake wote imeshindwa kutatua matatizo yanayotukabili, na niseme imekuwa ikituongezea tabu kila kukicha. Nianze na MGOMO WA MADAKTARI, AJALI ZA ZANZIBAR, SUALA LA MUUNGANO,KILIMO n.k vyote vinatabiri kifo cha CCM, kwa kuzingatia kuongezeka kwa machafuko nchini.

  Watanzania walio wengi wenye akili timamu na hekima nadhani tayari wameshajiandaa kufanya mabadiliko makubwa 2015 ,na namini itakuwa ndio mwisho wa utawala wa kidhalimuna dhaifu wa CCM!

  NA HICHO NDICHO KIFO CHA CCM 2015!

  -------------------------------

   
 2. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mojawapo ya hadithi za kusisimua na kusikitisha katika meli iliyovuma enzi hizo na kupoteza maisha ya watu wengiNi kwamba baada ya nahodha kuona meli hiyo inazama aliwatangazia abiria kuhusu hatari hiyo ili wachukue tahadharikujiokoa na walitangaziwa na kusikia kupitia vipaza sauti na speaker zilizokuwemo melini.Abiria walisikia tangazo la hatari lkn kwa kuwa meli hiyo ilikuwa na kila aina ya starehe na burudani,ikiwa ni pamoja nana kasino viwanja vya michezo,bar nk walipuuza wakileweshwa na anasa za melini,walipuuza tangazo hilo lilipotua masikioni mwao na wengine wakadhani NI MOJAWAPO YA VIKOROMBWEZO VYA NAHODHA WA MELI!!!!Hakuna aliyedhani wala kuota kuwa meli hiyo ingekuja kuzama na kupotea kabisa ktk historia ya ulimwengu na ukweli ni kwamba MELI YA TITANIC ILIZAMA NA MAMIA YA WATU WALIPOTEZA MAISHA.Nimeilinganisha meli hii ya zamani na chama kikongwe CCM,kelele za mwangwi zinasikika kila kona zikitahadharisha anguko Kuu lake,lkn abiria(wanachama)wametia pamba masikoni wengine wakiwa wameleweshwa na anasa (ufisadi)ndani ya ccm.Wengine wakiona km kelele za wpinzani wao lkn ukweli ni kwamba si mbali chama hiki kitaanguka,dalli zote zinaonesha si mbali,ufisadi,makundi ,rushwa ,udhaifu nk ni dalili toshaBado kitambo kidogo.
   
 3. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mmoja wetu humu jukwani aliwahi kuandiks kuwa " mchwa anapojaribia kufa huota mbawa". Hii ni kuonesha mbawa zishaota sasa tusubiri yatimie.
   
 4. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanaopenda kushuhudia CCM ikisambaratika ni wengi kuliko wanaoiombea mema. Je wimbi la mabadiliko litaiacha CCM madarakani kwa muongo mmoja au miwili ijayo? Jibu wanalo viongozi wa CCM. Wanachama wa CCM wamegawanyika vipande vipande, wengine wanasema potelea pote, maana wanajihisi kutengwa na chama chao, huku wakishuhudia nguvu ya pesa katika chaguzi zote za ndani ya chama. Jambo lililo wazi ni kwamba CCM inapita katika kipindi kigumu haijawahi kutokea, na kama watavuka salama basi ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu.

  Binafsi siwaombei mabaya, lakini muda wa kujirekebisha unazidi kuyoyoma. Mdharau mwiba huota matende, viongozi wa CCM amkeni kabla jua halijakucha. Huu ni mchango huru wa mawazo, unaweza kuwa na manufaa au kupuuzwa, yote sawa.
   
 5. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  ccm ni sikio la kufa, halisikii dawa kabisa...!
   
 6. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dalili nyingine ni mparaganyiko wa wazi miongoni mwa makada waandamizi na rubani wa chama kushindwa kusimamia miiko ya chama ni ishara tosha ya anguko la chama hicho.

  Watu wanaongea kwa ndimi mbili mbili,hii ni hatari kubwa
  Wenye pesa wanaabudiwa,nivyema waadilifu wachache watakaosikia sauti ya nahodha wakajisalimisha kwa kuondoka mapema.
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,263
  Likes Received: 12,985
  Trophy Points: 280
  CCM ni sawa na Kabuli kwa nje zuri ila kwa ndani limejaa mifupa na harfu mbaya

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 8. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Wakati huo huo wajiandae woote waliofisadi hii nchi kwenda segerea na wale wezi wa kuku na waliosingiziwa kesi akiwemo NGUZA wakiachiwa huru kwa furaha siku hiyo haiko mbali yaja!!
   
 9. S

  Savannah JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WaTZ ndio wenye kauli ya mwisho wa kuimaliza ccm.
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  CCM yafaa ikae kwanza kwenye upinzani nadhani ikirudi itafanya vema zaidi
   
 11. GIUSEPPE

  GIUSEPPE JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 4,489
  Likes Received: 4,503
  Trophy Points: 280

  Can you boy wake up a dead? Dont think about it.
   
 12. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Anguko la CCM limefikia 40%...teh teh teh 2015 wanaanguka kifo cha mende! miguu juu!
   
 13. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,885
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  ila kiukweli hata mie CCM inanishangaza sana
   
 14. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama viongozi wameonywa mara zote na hawakusikia,siku mbaya inayo kuja hawatakuwa na wakumlilia zaidi ya nafsi zao.
   
 15. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  One million dollar question; is CHADEMA ready for the take over? Baada ya anguko kuu la CCM, kama kweli litatokea kama inavyotazamiwa na wengi, CHADEMA peke yao wataweza? Au waungane na CUF ili kuondoa dhana ya udini na ukanda.

  Lipumba na Mbowe watafakari kwa pamoja jinsi ya kuchukua hatamu za CCM kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu.

  Ni wazo huru, linaweza likawa la manufaa au likapuuzwa, yote sawa.
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  U-mimi, majungu na damu ya ubaguzi yote iliopata mimba na sasa kuzaa uchakachuaji sasa yaua CCM tokakila kona ya nchi.
   
 17. k

  kajima JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 866
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hilo la nne....wazee wa busara ni pamoja na Sumaye? Okay angalau nimejua leo
   
 18. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,103
  Likes Received: 6,565
  Trophy Points: 280
  Lala salama peponi.
   
 19. s

  sony wega JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumekusoma mbuyi twite
   
 20. M

  Mr jokes and serious Member

  #20
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na nukuu baba wataifa alisema watanzani wakikosa mambo ambayo wanayataka ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm,baadhi wamesha anza kuyatafuta nje,wamesha gundua kumbe hii nchi bila magamba inawezekana.
   
Loading...