CCM mbona kimya kingi kuhusu kifo cha Mabina?

CCM mbona kimya kingi kuhusu kifo cha Mabina?

Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?


Sidhani kama unahitaji akili ya ziada kufahamu kuwa ccm sio mahakama ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine,vya siasa.Pengine ulihitaji watu wasingizie cdm ndi wamemua kupitia kauli yao mbiu ya kuua raia wakiita nguvu ya uma? shame on you.tuacheni vyombo husika kufanya kaz zake.
 
1463705_480534795397627_448780611_n.jpg
safi sana na wewe uliua wengi lakini hukujua kama nawe utakufa hv, bado rafiki yako
meya wa kijina bwana Matata. safi,safi, safi, safi, safi, safi, safi, safisana. na viwaja umeviacha
 
Habari zilizopo ni kwamba katika kutafuta ungwaji mkono kanda ya Ziwa ambako chama hicho kipepoteza kukubalika kutokana na matatizo mbalimbali yanayo wakumba wananchi wa kanda hiyo hususani Serikali kushindwa kuendeleza kikamilifu zao la Pamba, huduma hafifu za jamii n.k

CCM imeona ni vyema kutoshiriki mazishi ya aliyekuwa Diwani na Mwenyekiti mstaafu wa ccm mkoa, hoja yao ni kwamba endapo watashiriki mazishi hayo itaonekana wanaunga mkono watu uvunjaji wa sheria kwani marehemu Mabina alijichukulia sheria mkononi kwa kumuua kijana wa miaka 12 asiyekuwa na hatia.

Angalizo:
CCM kimejaa watu wengi waharifu na wanaopenda kuvunja sheria, tumeona watu wakipigwa kwa kukatwa mapanga kwenye chaguzi, kuchomewa moto mali zao kwenye chaguzi, kupora mali za wanyonge n.k. Sioni kama ni suluhu kwa chama hicho kutoshiriki mazishi ya kiongozi huyo bali suluhu ni kukisafisha chama chao kwa kuondoa watu wote aina hiyo
 
Mbona alipofariki Hayati Ditopile Mzuzuri pamoja na kuwa na kesi ya kumua kijana mwendesha daladala lakini CCM ilishiriki mazishi yake.

CCM walikwisha kosa MSHIPA WA AIBU.
 
Mbona alipofariki Hayati Ditopile Mzuzuri pamoja na kuwa na kesi ya kumua kijana mwendesha daladala lakini CCM ilishiriki mazishi yake.

CCM walikwisha kosa MSHIPA WA AIBU.

Hawakuwa na jinsi ya kukwepa maana licha ya kuua kwa kukusudia, DPP (mwendesha mashitaka na Jamuhuri) alimshitaki eti kwa kosa ya kuua bila kukusudia!
 
aliyekufa alikuwa mzigo, na mizigo wengine watashiriki tu
 
safi sana na wewe uliua wengi lakini hukujua kama nawe utakufa hv, bado rafiki yako
meya wa kijina bwana Matata. safi,safi, safi, safi, safi, safi, safi, safisana. na viwaja umeviacha

BADO lameck Airo/Nakairo na Kitano Chacha/Chinjachinja majini
 
Bado Lameck Airo/Nakairo na Kitano Chacha/Chinjachinja Majini huku wamevaa gwanda la kijani/CCM Mabina alikuwa ni Jambazi sugu na wasikunyingi sana kwa vile alikuwa ndani ya nguo ya kijani alifikiri atafanya kila kitu atakavyo
1463705_480534795397627_448780611_n.jpg
[/QUOTE]
 
HISTORIA YA MSIBA
Chanzo:-viongozi kujivika umungu Mtu.
Sababu:- ni ukosefu wa utii wa sheri,yaani:-
mabina, Dpp na wananchi.
Hitimisho:-hofu juu ya Mungu itawale maisha yetu.
 
Mungu yupo
kila siku nawaambia
wanafikiri uonevu huu hauna mwisho?
na mwisho wake mbaya km hiv
 
Tanzania bana...very kontradikitingi

Wananchi tunaambiwa tutii sheria bila shuruti

viongozi wanavunja sheria bila shuruti...

Kuna mtu alikuwa anauza ARV feki, hadi leo hajachukuliwa hatua zozote...na ni kiongozi mkubwa wa CCM yao...
 
ukiondoa watu wa aina ya MABINA ndani ya ccm basi bila shaka chama hicho kitabakiwa na majengo matupu .
 
ccm walikwisha mkana mungu siku nyingi,wamebaki wanaabudu kijani na njano.
 
Back
Top Bottom