CCM ni lazima kujitenga na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,973
2,000
Wanajamvi heshima kwenu,

Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?Tulio wanachama wa CCM toka enzi za TANU kulikuwapo na msemo uliokuwa unaaminiwa kama sala miaka hiyo.

CHEO NI DHAMANA.

Tukio la kusikitisha lilotokea eneo la Kisesa nje kidogo ya mjo wa Mwanza, ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili lazima liangaliwe katika msimamo unaostahili.

Mpaka sasa tunapata habari kutoka vyanzo vya habari toka sehemu mbali mbali, pamoja na taarifa ya polisi.
Clement Mabina -aliyekuwa Mwenyekiti waCCM wa Mkoa wa Mwanza , mpaka kifo chake, saa 3 au nne hivi asubuhi, alienda kulishughulikia shamba ambalo wananchi wa karibu walikuwa na ugomvi naye , ugomvi wa umiliki wa shamba hilo.
Kosa la kwanza ni kulishughulikia shamba ambalo Mabina ni dhahiri alikuwa na ugomvi na majirani zake.

Pili . wananchi waliokaribu wakahoji ni vipi Mabina aingie kwenye shamba, tena bila kutoa taarifa kwa wagomvi wake na kuendelea kulishughulikia shamba hilo.

Tatu katika inaelekea mabishano na wanakijiji waliohoji , Bwana Mabina aliktumia bunduki aina ya shotgun kumuua mmoja wa wanakijiji aitwae Temeli Malemi, kijana wa miaka 13-14 hivi.

Wana kijiji wakacharuka na kujichukulia hatua ya kumpopoa muheshimiwa huyu mpaka mauti.
Kwa wanaouelewa mkoa wa Mwanza , jiwe ni a weapon of choice, huendi mita moja bila kukuta jiwe l aina yoyote.

CHEO NI DHAMANA, na mwenzetu huyu hatuna haja ya kumhukumu lakini alitumia cheo chake bila ridhaa ya waliomuweka madarakani-wananchi.
Mbaya zaidi yaliyofanyika na mwenzetu huyu ni masuala ya JINAI, masuala ambayo CCM hairidhii wala haikumtuma.
Ametumia ubabe, na ubabe wa wanachi umedhihiri.

Ni kwa vile nchi hii ni ya sheria , lakini CCM kujihusisha na tabia za namna hii ni kujitakia kifo.

CCM lazima ijitenge na kifo cha mwenzetu huyu, ambaye alitumia dhamana yake vibaya.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,241
2,000
Kuna yeyote ndani ya CCM ambaye hatumii cheo chake vibaya kwa manufaa yake binafsi badala ya yale ya nchi? Kama wapo basi basi majina yao yawekwe hapa ili na wengine tuwafahamu.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,979
2,000
Kuitofautisha ccm na tukio la kifo cha Mabina ni ngumu sana.

Mabina aliuawa akiwa katika kutekeleza ila ya ccm ya kuwanyang'anya ardhi wananchi maskini wa Kisesa
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,973
2,000
Kuna yeyote ndani ya CCM ambaye hatumii cheo chake vibaya kwa manufaa yake binafsi badala ya yale ya nchi? Kama wapo basi basi majina yao yawekwe hapa ili na wengine tuwafahamu.
Mawazo kama haya ni kama yale ya wanaosema CDM ni chama cha kina Mangi, wengine wote ni chasaka wa kisiasa.
 
microX

JF-Expert Member
Feb 6, 2011
482
500
Ccm kuna msemo mmoja tu utatumika kama co.n.dom naona mnatekeleza kwa vitendo ,vipi kama angejeruhiwa tu, mngemtupa??
 
Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,663
2,000
Masopakyindi, ushahuri wake si sahihi. Ukiwa na mwanao mwizi akauawa kwa matendo yake utamkana? Nafikiri ukifanya hivyo wananchi hawatakuelewa na watakuona hufai katika jamii. Ukichukua wajibu wako ukamkubali ni mwanao na ukamsitiri kwa heshima inayostahili, utanapa heshima zaidi na watu watakupa heshima yako. Pamoja na madhaifu yake marehemu aliitumikia CCM mpaka mwisho wa maisha yake na hivyo CCM wanatakiwa wamzike kwa heshima hiyo. Ni suala la utu tu.
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
Sumaye ana ardhi kila kona,ni sera ya chama cha mizigo kukwapua ardhi ya walala hoi
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,241
2,000
Badala ya kujibu ulichoulizwa unaenda kushambulia CHADEMA na Mangi!!!! Wakati huu uzi uliouanzisha hauna uhusiano wowote na CHADEMA au Mangi!!! Dah!!!!

Mawazo kama haya ni kama yale ya wanaosema CDM ni chama cha kina Mangi, wengine wote ni chasaka wa kisiasa.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,542
2,000
Masopakyindi;
Weye ni mtu shujaa sana, umeweza kujieleza kabisa kuwa huyo marehemu alikuwa mtu wenu. Sasa, fanyeni uungwana tu. Mpokeeni marehemu Mabina, kwa heshima zoote za chama chenu sikivu, mlazeni pema kwa heshima zoote na baadaye mtafute njia na neno la kusema kwa familia ya yule aliyeuawa na Mabina.
Kuomba samahani si vibaya. Kinyume cha hapo, mnadhihirisha kuwa mnawatumia watu kama ko.ndo.m tu. Akishatumika tupa kuleee chukua mpya
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,014
2,000
watu tunasubiri kwa hamu hayo mazishi tuone watasemaje, alazwe mahali pema peponi au motoni kabsa?

hivi c ijumaa eeee?
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Tulio wanachama wa CCM toka enzi za TANU kulikuwapo na msemo uliokuwa unaaminiwa kama sala miaka hiyo.

CHEO NI DHAMANA.

Tukio la kusikitisha lilotokea eneo la Kisesa nje kidogo ya mjo wa Mwanza, ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili lazima liangaliwe katika msimamo unaostahili.

Mpaka sasa tunapata habari kutoka vyanzo vya habari toka sehemu mbali mbali, pamoja na taarifa ya polisi.
Clement Mabina -aliyekuwa Mwenyekiti waCCM wa Mkoa wa Mwanza , mpaka kifo chake, saa 3 au nne hivi asubuhi, alienda kulishughulikia shamba ambalo wananchi wa karibu walikuwa na ugomvi naye , ugomvi wa umiliki wa shamba hilo.
Kosa la kwanza ni kulishughulikia shamba ambalo Mabina ni dhahiri alikuwa na ugomvi na majirani zake.

Pili . wananchi waliokaribu wakahoji ni vipi Mabina aingie kwenye shamba, tena bila kutoa taarifa kwa wagomvi wake na kuendelea kulishughulikia shamba hilo.

Tatu katika inaelekea mabishano na wanakijiji waliohoji , Bwana Mabina aliktumia bunduki aina ya shotgun kumuua mmoja wa wanakijiji aitwae Temeli Malemi, kijana wa miaka 13-14 hivi.

Wana kijiji wakacharuka na kujichukulia hatua ya kumpopoa muheshimiwa huyu mpaka mauti.
Kwa wanaouelewa mkoa wa Mwanza , jiwe ni a weapon of choice, huendi mita moja bila kukuta jiwe l aina yoyote.

CHEO NI DHAMANA, na mwenzetu huyu hatuna haja ya kumhukumu lakini alitumia cheo chake bila ridhaa ya waliomuweka madarakani-wananchi.
Mbaya zaidi yaliyofanyika na mwenzetu huyu ni masuala ya JINAI, masuala ambayo CCM hairidhii wala haikumtuma.
Ametumia ubabe, na ubabe wa wanachi umedhihiri.

Ni kwa vile nchi hii ni ya sheria , lakini CCM kujihusisha na tabia za namna hii ni kujitakia kifo.

CCM lazima ijitenge na kifo cha mwenzetu huyu, ambaye alitumia dhamana yake vibaya.

KWELI KUFA NI NOMA, SIKU ZOTE CCM ILIMPITISHA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI IKIWEMO UDIWANI, MWENYKITI WA HALMASHAURI na MWNEYEKITI WA MKOA WA CCM, leo amekufa mnafanya kama kwamba hamkujui sifa zake mbaya??? leo mnamtelekeza wakati wote mko kama yeye tofauti yeye mauti imemkumba eneo la tukio, Ukibisha mifano iko kibao Mkuu wa MKOA TABORA Je?? DITOPILE etc
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom