SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 49,973
- 75,048
Kama sikosei huyu Kashanga ndiye Tambwe Hizza, sioni mwingine awezaye kutoa pumba hizi zaidi ya TH
Hoja za kipuuzi utazijua tuu,sasa ukisema wachaga ndio chama chao, Mbona Wachaga haohao munaowatuhumu wameipa kura CCM mkoani Kilimanjaro?demokrasia ya kweli ni ile ya kusililiza cha mwenzako hata kama hupendi kusikia. La udini sina uhakika, lakini la ukabila liko saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana tu. huna haja ya kwenda darasani na kuambiwa wachagga ndiyo chama chao hicho, pamoja n wengine wengi wa kaskazini
Nafikiri tunakubaliana wote kwamba:
1. Nyoka ni utaratibu wake wa kibaolojia kwamba atajivua gamba mara kwa mara ... yaani sio mara moja tuu,
2. Akishavua gamba anang'aa anasahau ya gamba alilovua,
3. Baada ya muda gamba litakuja tena na atalivua,
4. Nyoka anabaki yule yule kibaolojia na kitabia na kila kitu
Sasa, CCM inanifanya niamini kwamba kujivua gamba ni:
1. Kila mara kutatokea ufisadi mara kwa mara na itakua inajivua gamba,
2. Ikishajivua gamba kwa danganya toto inataka ionekane ni CCM mpya,
3. Baada ya muda (sijui ni muda gani) ufisadi utarudi upya (gamba jipya),
4. CCM itabaki ile ile na ufisadi wake wa mara kwamara.
Kwa maoni yangu, tukipe hatamu chama ambacho sio nyoka maana kuvua gamba hakutuhakikishii kubadilika kwa tabia.
Mag3.. nadhani ni kwamba hawakufuata kile ambacho kinajulikana kama "the order of operation" ambayo enzi zile sisi tuliita MAGAZIJUTO. Yaani, ukipewa hesabu zenye masharti mbalimbali ya kuzifanya basi kuna mtiririko unatakiwa ufuate ili upate majibu. Hivyo, hesabu ambayo iko 34+45x23(34/10)-70 kwa mtu ambaye hajua Order of Operation ataanza kujumlisha!! Atafanya kile anachokiona lakini atafikia jibu lisilo sahihi kwani kanunu ya MAGAZIJUTO inatoa mwongozo wa kipi kifanyike kwanza kuanzia kushoto kwenda kulia.
Kwa hiyo naamini hawa jamaa pamoja na kuangalia HCF vile vile hawakufuata kanuni za MAGAZIJUTO matokeo yake wamepata majibu; tatizo ni majibu yasiyo sahihi.
Kwa tuliosoma zamani na tuliopenda namba (hesabu), twajaribu kutafuta uwiano kati ya kitendo cha CCM kuvua gamba, je walitumia HCF (Highest Common Factor) au LCD (Lowest Common Denominator) ? Samahani wana JF kiswahili chake sikijui, nimesoma zamani.
Nadhani hizi picha mbili zitatusaida kujibu hiki kitendawili, Kazi kwenu !
Tangu hawa watu wawili wanadiwe na kupewa Ubunge hata mwaka bado. Cha ajabu walionadiwa eti wanatoswa kwa kuhusishwa na ufisadi lakini aliyewanadi na kusimamia uchakachuaji wa kura anaenziwa kama shujaa na asiye na na doa - CCM ni killer poke ?
hoja za kipuuzi utazijua tuu,sasa ukisema wachaga ndio chama chao, mbona wachaga haohao munaowatuhumu wameipa kura ccm mkoani kilimanjaro?
sio siri chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwasasa lakini kimekuwa kina kashfa nyingi sana kama vile swala la udini,ingawa walijaribu kumuita kundini prof safari ili kufuta dhana ya udini lakini bado swala la udini halijafutika mioyoni mwa watu,pia liko swala la kupewa fedha na mataifa ya nje,liko swala la ukabila,pia liko swala la vurugu,mfano hai ni pale mbunge machachari Godbless Lema alipotamka live bungeni kuwa milango ifungwe watu wapigane!(mwananchi ya leo) hivi kweli mtu aliyepewa dhamana na wananchi anaweza kutamka maneno kama hayo katika chombo kikuu cha maamuzi nchini?? sasa je chadema kuvua gamba na kuwa na sura mpya katika macho ya watu?
Umetumwa.
demokrasia ya kweli ni ile ya kusililiza cha mwenzako hata kama hupendi kusikia. La udini sina uhakika, lakini la ukabila liko saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana tu. huna haja ya kwenda darasani na kuambiwa wachagga ndiyo chama chao hicho, pamoja n wengine wengi wa kaskazini