Kashaga umenifurahisha sana leo si kwa kazi nzuri uliyofanya bali siamini kama kuna watu kama ww na wanajiita great thinker...kwanza badala ujibu au utetee hoja unazoulizwa unaanza uliza muda wa aliyekuuliza inashangaza sana. Kuhusu post yako ni upupu mtupu.
Kwanza hilo gamba la CCM limevuliwa baada ya miaka zaidi na 40 ya upupu wao.
Pili hoja ya CDM na udini haina maana maana ni jana tu waislamu wametoa tamko kusifu kazi ya CDM na kuwaponda viongozi wa Bakwata kwa hoja za upupu kama yako.
Tatu hoja ya ukabila inashangaza sana maana viongozi hawa wa CDM kina Dr. Slaa, Zitto, Lissu, Mdee, Mnyika nk. na watanzania zaidi ya 40% waliopigia CDM kura ni kabila moja?
Suala la vurugu pia ni upupu maana mtu kudai haki yake kihalali sidhani kama ni vurugu. Ungekuwa waongelea vurugu kama za CCM kumwaga damu ZNZ, Mwembechai nk kwa ajili ya wizi wa kura hizo sasa ndo vurugu.
Jichunguze ujipange na ujikane mwenyewe kabla hujapita anga za CDM