CCM kuhodhi viwanja vya michezo kunarudisha nyuma juhudi za Rais Samia

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,311
12,607
Mama Samia ni Rais ambae ilikuwa kama kuota ndoto ya mchana kumpata. Mpaka sasa Mama huyu amedhihirisha kufanya mengi ambayo watangulizi wake hawakuyawaza wala kuyaota.

Ana bahati sana kwenye kipindi chake timu ya mpira wa miguu ya wanawake kufuzu kwenda kushiriki kombe la wanawake huko India, pia kuweka msukumo wa kipekee kwenye tasnia nzima ya michezo na sanaa nchini. Juzi nimemuona kahudhuria tamasha la Bongo fleva la Mr. Sugu. Sasa hivi utalii wetu umefungwa vipuli vipya kabisa kuufufua, na yale maonevu ya holela kwa wanahabari, wanasiasa, wafanyabiashara na wananchi yamepungua sana kama sio kwisha kabisa.

Hivi mama anashindwa nini kutoa tamko la CCM kurejesha viwanja vya mpira wa miguu kwa serikali ili serikali kupitia kodi za wananchinwote na TFF/CECAFA/CAF/FIFA wavihudumie viwe bora kwa michezo?

Haitawezekana kwa sasa serikali itumie fedha za walipakodi wote kukarabati miradi (viwanja) ya CCM. kama serikali itafanya hivyo ni kosa kubwa la kiufundi kwa serikali ya Mama. Itamsumbua sana kwenye mbio zake huko mbele ya safari.

CCM, viwanja na Tanzania ni vyetu sote, na hata viwanja vile vilijengwa na watanzania wote kama ilivyo kwa barabara, migodi, bandari, viwanja vya ndege, viwanda na vitu vyote ambavyo vilijengwa kabla mya mwaka 1992 wakati wa ujio wa vyama vingi. Mbona barabara, viwanja vya ndege na reli ya TAZARA vilivyojengwa kabla ya ujio wa vyama vingi hawasemi ni mali ya CCM?

Tuwe na hofu ya Mungu, sisi wote ni wapita njia tu ila nchi itabaki, vitukuu vyetu vitakuja kutuhukumu kwa dhuluma za hivi.
 
Uchawa wenu unawafanya kuwa mazuzu,Samoa in mwenyakiti was ccm na waziri was michezo no mkwr wake in an ten vanish and na hiyo mipango.
 
Tunamuomba Rais avirudishe viwanja vya Umma vilivyopokwa na ccm Serikalini
Kwanini ni viwanja vya mpira wa miguu tu, wakati nchi hii ilikuwa chini ya CCM/TANU tangu ipate uhuru? kwanini ccm isichukue mali zote kama ni hivyo.
 
Warudishe viwanja vyetu! Haiwezekani waibe kura kwenye kila uchaguzi! Waibe kodi za watanzania! Bado wadhulumu mpaka viwanja vya michezo, majengo ya serikali na maeneo ya wazi!!

Jambo hili halikubaliki. Wawekeze nguvu kwenye siasa! Watuachie viwanja vyetu.
 
Tunamuomba Rais avirudishe viwanja vya Umma vilivyopokwa na ccm Serikalini
CCM inakaribia kuuvuka mstari mwekundu kama itachukua fedha ya wananchi kuboresha viwanja vyake vya mpira wa miguu. Yaani mapato ya viwanja yanaingia CCM na sio hazina ya nchi.
 
Hii haiishii kwenye viwanja tu, inatakiwa warejeshe na ofisi zote za umma walizopora.

Chama kikongwe namna hiyo hakina hata ofisi wanazidiwa hata na vyama pandikizi ambavyo havina hata mwenyekiti wa kitongoji.. :p :p
 
Hii haiishii kwenye viwanja tu, inatakiwa warejeshe na ofisi zote za umma walizopora.

Chama kikongwe namna hiyo hakina hata ofisi wanazidiwa hata na vyama pandikizi ambavyo havina hata mwenyekiti wa kitongoji.. :p :p
Siku CCM ikianguka hainyanyuki tena abadan
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom