Priscus Tarimo alilia maboresho viwanja vya Soka na gofu

Jun 20, 2023
54
51
Kilimanjaro,

Serikali imeahidi kutuma watalamu kwa ajili ya kufanyia tathimini uwanja wa michezo wa Memorial ulioko Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ili kuuwekea nyasi mbadia na kuwezesha uwanja huo kutumika kwa ajili ya mechi za kitaifa.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa utamaduni, sanaa na michezo Damas Ndumbaro kwenye viwanja vya chuo kikuu cha ushirika Moshi muda mfupi baada ya kutoa zawadi kwa washindi wa mbio za Kilimanjaro international marathon msimu wa 22.

Hatua hiyo ilitokana na ombi la mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo kuhusu umuhimu mkubwa wa kuboresha uwanja huo ili uweze kutumika katika mechi za kitaifa.

Amesema kuwa mwaka 2027 Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano Afcon ambapo jijini Arusha kutakuwa na Miata na uwanja utakaotumika kwa ajili ya michuano hiyo na kwamba Moshi na Arusha ni majirami hivyo upo umuhimu wa uwanja huo kujengwa ili timu zitakazoshiriki zimeweka kambi Moshi na kutumia kwa ajili ya mazoezi.

Amesema kama serikali amelipokea ombi hilo na kwamba wiki hii watakuja watalamu kutoka TFF kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kufanya thamini ili ujenzi uanze.

"Uwanja wa Memoria wiki ijayo (wiki hii)nitaleta wataalamu kuangalia uwanja ule nakuanza kufanyia kazi kwa haraka ili uweze kutumika katika michezo ya kimataifa kwa ajili ya afcon mwaka 2027,"amesema Waziri.

"Lazima fedha zitafutwa ule uwanja ujengwe ili tuweze kutumia katika mashindano ya Afcon, Arusha Moshi ni majirani hivyo nirahisi timu shiriki kuja Moshi,"amesema.

Akizugumzia uwanja gofu wa Moshi club alitoa maelekezo kwa viongozi wa Moshi Club kwendav wizarani ili waweze kujandili kwa pamoja namna ya kuuboresha uwanja huo

Amesema Kuwa Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya afcon ni matunda ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kufungua fursa mbalimbali.

"Tunawaahidi wananchi tutafanya kila linalowezekana kuboresha viwanja vya michezo,"amesema.

Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo amesema uwanja wa Memoria unamanufaa makubwa na ukijengwa unaweza kuleta mabadiliko makubwa kiuchumi kwa Wananchi wa mji wa Moshi na Taifa kwa ujumla.

Amesema endapo uwanja huo utajengwa utachochea uchumi wa wananchi wa Moshi mjini pamoja na mkoa Kilimanjaro kutokana na kwamba utatumika kuleta timu kubwa kuja kuweka kambi na kutumika kwa ligi kuu.

"Mheshimiwa waziri tuna uwanja mwingine wa gofu wa Moshi Club naomba nikuombe tusaidi uwanja ule uboreshwa ili uweze kutumika katika mechi za kitaifa kwa upande wa michezo ya gofu,"amesema.

Mwisho...
 
Back
Top Bottom