Wanabodi,
Nikiwa hapa Dom, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na viti maalum ndio usiseme kabisa, wengi ni makapi tuu, kama sio vidumu, basi ni kwa ajili ya kutoa huduma na kibinaadamu, na hili litathibitishwa na michango yao kikao cha Januari.
Nilipoongea na wale makamanda walikata magogo kanda ya ziwa, nao ni wa kawaida tuu, hivyo nimefikia jibu moja la uhakika, CCM imechokwa baadhi ya maeneo, upinzani hata ungesimamisha jiwe, lingechaguliwa, nadhani ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi hawakujitokeza waliona ni kujisumbua.
Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa toka Asilimia 80% niliyohakikishiwa na mwana CCM mwandamizi mpaka asilimia 60% ni uthibitisho tosha, Watanzania wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzania kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani hawajaonyesha wako tayari kukamata dola.
Najua kwa dhati, japo JK anafurahia ushindi kwa furaha ya machoni, lazima atakuwa na huzuni moyoni kwa kukataliwa na hiyo asilimia 20% kukataliwa ni kukataliwa tuu, kunauma. Hivyo CCM lazima watakaa na kujiuliza kulikoni, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange vipi, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down.
Dawa pekee ya kuitibu CCM, kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba should go first with his old guards team. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaweza siasa za kisasa za dot com type.
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja, huku sio kukua bali ni kupaa, tazizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga.
Kichama, wanachadema mkubali msiku chama chenu bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa, Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.
Kwanza Freeman Mbowe, ajiuzulu uenyekiti, ampishe Dr. Slaa kwenye Usukani, Katibu Mkuu mpeni Zitto, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, ili Walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kuwapigia kura 2015.
Kitendo cha kuihodhi kambi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani, Chadema peke yenu hamuwezi!.
Nasisitiza Chadema hamjajipanga vyema na tatizo lenu kubwa ni ubinafsi wa viongozi wenu na ugonjwa wa umimi. Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Zitto Kabwe na Uwezo wa Freeman Mbowe katika kukata issue. Mbowe sio born leader, ni made leader, tena ameletewa uongozi kwenye kisaani cha chai. Zitto ni born leader na amepambana kufika hapo alipofika.
Kitendo cha Mbowe kuwa ndie kiongozi rasmi wa upinzani Bungeni is a waste. Mbowe hana features za promising great leader, Zitto anazo. Mbowe hana powers from withing to make things happen, Zitto is powerful from within who can make things happen, he is a force to recon with. Juzi wakati wa kampani za Marando, alimgomea kata kata Ole Sendeka kuzungumzia kisemeo cha Marando, alisimama, akagonga meza na kusema kwa sauti kubwa "we can't allow such a thing, never on earth!" Spika Makinda ndipo akakazia msimamo na Ole Sendeka kufurushwa!.
Kiongozi sahihi wa upinzani bungeni should be Zitto not Mbowe. Naibu kiongozi wa upinzani alitakiwa awe Hamad Rashid. Chief Whip Lissu is ok.
Kama CCM iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?.
Angalizo: Pasco wa Jamii Forums ni political analyst ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya ubunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!