CCM chini ya Mwenyekiti wetu Dr. Samia Suluhu Hassan imekuwa maarufu kama Marekani Dunia yote inaiongelea Marekan hii ndo siasa Sasa.

Umaarufu wa CHAMA CHA MAPINDUZI TANZANIA umezidi kukua maradufu Tangu Mwenyekiti wetu jemedali wetu wa siasa za kisayansi DAKTARI Samia Suluhu Hassan aingie madarakani.

Tuwe wakweli Jamani Samia anaujua uongozi, anaijua siasa, yupo very focused Hana papara, kwakweli nampongeza sana, sijui bunge la Ulaya sijui nani kujihudhuru walaaa! ...yy yupo na Tanzania, yy ni Tanzania kwanza, yy ni kazi, yy na Watanzania.

Hamjakaa mkatulia kidogo kawapiga na Google meeting 🤣🤣👏👏 upepo umehamia kwenye Google meeting.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Dr. Samia ameuthibitishia ulimwengu na Tanzania kuwa wanawake wanauwezo mkubwa wa uongozi.

Dr. Samia AMEONDOA KELO ZOTE ZA WATANZANIA KWA MUDA MFUPI TU, sijui madaraja ya Watumishi, sjui mazingira ya uwekezaji yamefanyaje, sjui ajira, sjui masoko, sijui nyongeza za mishahara, sijui mbolea za ruzuku, sjui Nini vyote ame CLEAR!

HONGERA SANA RAIS WETU KWA UTHUBUTU WAKO WA KUTUTUMIKIA SISI WANANCHI WAKO.

MUNGU AKUBARIKI SANA MH. RAIS SAMIA.
Kwanza, hakuna anayepinga kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameleta mtindo wa uongozi wenye utulivu na busara ya kidiplomasia. Hilo ni jambo linalojieleza wazi. Hata hivyo, kudai kwamba “ameondoa kero zote za Watanzania kwa muda mfupi” ni kauli ya kupindukia na isiyoakisi hali halisi. Bado taifa linakabiliwa na changamoto kubwa katika sekta ya afya, elimu, ajira kwa vijana, gharama za maisha, na hata ukomo wa uhuru wa kisiasa kwa baadhi ya makundi.

Pili, si sahihi wala sahiba kulinganisha umaarufu wa CHAMA CHA MAPINDUZI na taifa kama Marekani. Marekani ni dola kuu duniani kwa misingi ya nguvu za kiuchumi, kijeshi, kiteknolojia, na ushawishi wa kidiplomasia duniani. CCM, kwa heshima yake ya kihistoria ndani ya Tanzania, haiwezi kuwekwa katika mizani moja na taifa lenye nguvu za kiulimwengu.

Tatu, kauli inayosema “Samia ni Tanzania” ni hatari kwa afya ya demokrasia.
Tanzania ni taasisi ya watu milioni zaidi ya sitini, si jina la mtu mmoja. Rais ni kiongozi wa nchi, lakini nchi si mali ya Rais.

Ni wakati wa kuacha siasa za porojo na kusifu kila jambo kwa mihemko. Tupongeze palipo na sababu ya kweli, lakini tusipoteze uwezo wa kutoa hoja kwa hofu ya kuitwa wapinzani. Maendeleo halisi yanayoguswa na maisha ya watu ndiyo kipimo sahihi cha mafanikio ya kiongozi.

Tuzungumze kwa hoja. Si kwa ushabiki.
 
Kwanza, hakuna anayepinga kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameleta mtindo wa uongozi wenye utulivu na busara ya kidiplomasia. Hilo ni jambo linalojieleza wazi. Hata hivyo, kudai kwamba “ameondoa kero zote za Watanzania kwa muda mfupi” ni kauli ya kupindukia na isiyoakisi hali halisi. Bado taifa linakabiliwa na changamoto kubwa katika sekta ya afya, elimu, ajira kwa vijana, gharama za maisha, na hata ukomo wa uhuru wa kisiasa kwa baadhi ya makundi.

Pili, si sahihi wala sahiba kulinganisha umaarufu wa CHAMA CHA MAPINDUZI na taifa kama Marekani. Marekani ni dola kuu duniani kwa misingi ya nguvu za kiuchumi, kijeshi, kiteknolojia, na ushawishi wa kidiplomasia duniani. CCM, kwa heshima yake ya kihistoria ndani ya Tanzania, haiwezi kuwekwa katika mizani moja na taifa lenye nguvu za kiulimwengu.

Tatu, kauli inayosema “Samia ni Tanzania” ni hatari kwa afya ya demokrasia.

Ni wakati wa kuacha siasa za porojo na kusifu kila jambo kwa mihemko. Tupongeze palipo na sababu ya kweli, lakini tusipoteze uwezo wa kutoa hoja kwa hofu ya kuitwa wapinzani. Maendeleo halisi yanayoguswa na maisha ya watu ndiyo kipimo sahihi cha mafanikio ya kiongozi.

Tuzungumze kwa hoja. Si kwa ushabiki.
Hivi ni raisi wa mpito ,? Au akigombea hii anaanza mitano yake mpya? Au atamaliza mitano yake awe kahudumu kama raisi miaka 9na nusu? Au atarudi tena ahudumu mika 14?
 
Kwahyo hujui nafasi ya Rais mbona ni civics ya kidato Cha pili
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
"Endapo Rais aliyeko madarakani atafariki dunia au kushindwa kuendelea na madaraka, Makamu wa Rais ataapishwa na kushika madaraka ya Rais kwa kipindi kilichobaki cha muhula huo."

Rais SSH alitekeleza ibara hii aliposhika madaraka Machi 2021 kufuatia kifo cha Rais JPM. Kwa kuwa muhula huo ulianza Novemba 2020, Samia alihudumu kwa zaidi ya nusu ya muhula uliobaki.

Hili linafafanuliwa bayana na Ibara ya 40(3) ya Katiba:
"Mtu yeyote atakayeshika madaraka ya Rais kwa kipindi kinachozidi nusu ya muhula wa miaka mitano atahesabika kuwa ameshahudumu muhula mmoja kamili wa urais."

Kwa muktadha huu wa kikatiba, Rais Samia anahesabika kisheria kuwa tayari amehudumu muhula mmoja kamili wa urais, japokuwa hakuchaguliwa moja kwa moja mwaka 2020.

Aidha, Ibara ya 41(2) ya Katiba inazuia mtu kushika nafasi ya Rais kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano:
"Rais atachaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano, na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kama hicho, lakini si zaidi ya hapo."

Hii ina maana kuwa Rais Samia anayo haki kisheria ya kugombea muhula mmoja zaidi mwaka 2025. Akichaguliwa, atahitimisha vipindi viwili vinavyoruhusiwa kikatiba.

Kwa mantiki hiyo:
  • Samia SI rais wa mpito, bali ni rais wa muhula wa kwanza kamili kisheria.
  • Ana haki moja ya kugombea mwaka 2025.
  • Akiwachaguliwa tena, muhula huo wa pili utakuwa wa mwisho kwa mujibu wa Katiba.
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Rais SSH alitekeleza ibara hii aliposhika madaraka Machi 2021 kufuatia kifo cha Rais JPM. Kwa kuwa muhula huo ulianza Novemba 2020, Samia alihudumu kwa zaidi ya nusu ya muhula uliobaki.

Hili linafafanuliwa bayana na Ibara ya 40(3) ya Katiba:

Kwa muktadha huu wa kikatiba, Rais Samia anahesabika kisheria kuwa tayari amehudumu muhula mmoja kamili wa urais, japokuwa hakuchaguliwa moja kwa moja mwaka 2020.

Aidha, Ibara ya 41(2) ya Katiba inazuia mtu kushika nafasi ya Rais kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano:

Hii ina maana kuwa Rais Samia anayo haki kisheria ya kugombea muhula mmoja zaidi mwaka 2025. Akichaguliwa, atahitimisha vipindi viwili vinavyoruhusiwa kikatiba.

Kwa mantiki hiyo:
  • Samia SI rais wa mpito, bali ni rais wa muhula wa kwanza kamili kisheria.
  • Ana haki moja ya kugombea mwaka 2025.
  • Akiwachaguliwa tena, muhula huo wa pili utakuwa wa mwisho kwa mujibu wa Katiba.
Ningependa swali langu lisijibiwe na chawa , ila Nashukuru tu.
 
Kwahyo hujui nafasi ya Rais mbona ni civics ya kidato Cha pili
Kwahiyo kwa ambaye hakusoma kidato cha pili vipi hajui nafasi ya rais?

Tanzania ni taasisi ya watu milioni zaidi ya sitini, si jina la mtu mmoja.

Rais ni kiongozi wa nchi, lakini nchi si mali ya Rais.
 
Ningependa swali langu lisijibiwe na chawa , ila Nashukuru tu.
Majadiliano ya hoja hayahitaji matusi wala kejeli.

Ukianza na dhihaka kama “chawa,” tayari umejiondoa kwenye msingi wa hoja na kuonesha upungufu wa hoja za msingi.

Kama una hoja, itoe kwa heshima. Ukitukana badala ya kujenga, unathibitisha kuwa huna msingi wa kueleweka.

Hili ni jukwaa la hoja, si jukwaa la kihoro.
 
Basi sawa nikajua chawa ni wafuasi wa mama samia!! Na wao wanajiita chawa wa samia , kumbe ni kejeli bwashee ? basi Samahani
 
Back
Top Bottom