kama kweli unafuatilia au mfatiliaji mzuri wa midaharo,hasa wa leo STAR TV ni rahisi kuelewa. Kwa kifupi Lukuvi kamuomba Dr.Kitila kufanya utafiti kama UKAWA wana nia nzuri ya kuleta katiba mpya.huelewek mzee try to write in gud sense ukiwa unatoa hisia zako
Washaurini UDASA waandae mdahalo utakaokuwa balanced kama mnafikiri huu haukuwa wa kwao!Moderator.
Kwa heshima na taadhima naomba tafadhari usifute wala kuunganisha thread hii.
Natambua kwa miaka mingi iliyopita chuo kikuu cha Dar es salaam kilijijengea heshima kwa kuwa tanuru la kuchakata na kuoka fikra na tafakuri tunduizi. Natambua kuwa katika miaka ya nyuma maswala yote magumu ya mkwamo kwenye nchi yalikuwa yakijadiliwa objectively kwenye viunga vya chuo kikuu cha dar es salaam kwa weledi na kwa usawa wa hali ya juu.
Leo kwenye mdahalo wa nini kifanyike bunge la katiba likiendelea wiki ijayo, nimeona kwa dhahiri mdahalo huu umeitishwa tu kwa jina la UDASA lakini ukweli ni kwamba ilikuwa mdahalo wa CCM ukimshirikisha Tundu Lissu kwa minajili ya kufunika kombe ili mwana haramu apite. Na hili limedhihirishwa na kauli ya Lukuvi akimsifu Lissu na kumuona kama ka mzizi ka UKAWA.
Ukiangalia namna wazungumzaji walivyo kuwa wanapewa fursa za kuchangia kwenye mdahalo ule, bila chembe ya shaka utagundua kuwa hakukuwa na fursa sawa ya uchangiaji. Sikuona mantiki ya kumuita Mwigulu Nchemba na kuacha kumuita miongoni mwa washiriki walio tambuliwa awali kama Mheshimiwa Machali na David Kafulila lakini wakati huohuo nafasi ya kuchangia akipewa kada Kunambi wa Ccm.
Haikuwa sahihi kuacha kumpa nafasi ya kuchangia mtu wa kariba ya Prof Sheriff na kumpa nafasi kijana kutoka zanzibar ambaye hata historia ya Zanzibar aliipotosha huku pia akiongea kwa kujiamini lakini kwa kupotosha kuwa tume ya Warioba haikwenda kuchukua maoni Zanzibar.
Kulikuwa na vigezo gani kumpa nafasi ya kuchangia Prof Tabaijuka aliyekiri kuwa hata katiba mpya isipo patika bado ni ushindi kwa ccm na jk huku akiacha Prof Sheriff na Dr Lwaitama tena bila hata kutambuliwa kuwa wako ukumbini?!
Nimebaki najiuliza, wale vijana walio kuwa wanaitwa kuchangia ikiwa ni pamoja na baadhi ya wazee walio ishia kuzomewa, majina yao yalipatikana vipi na ni utaratibu upi ulio tumika?
Umetumika utaratibu upi na vigezo gani vya kuwa na wazungumzaji wengi wa ccm kuliko wazungumzaji wanao unda kundi la ukawa?! Kwa nini hakukuwa na usawa wa wachangiaji?!
Kwa nini mdahalo wa UDASA uhitimishwe na Lukuvi (mccm) nasi mwenyekiti wa UDASA?!
Nabaki najiuliza? Mdahalo ulioandaliwa chuo kikuu ulikuwa wa Udasa au Ccm?! Kama ccm imefanikiwa kuingilia mpaka uhuru wa vyuo vikuu tunaachaje kuamini kuwa elimu pamoja na taasisi zilizo heshimika za elimu ya juu ziko shakani kwa kuendeshwa kwa remote control na kutumika kisiasa?!
Hakuna lolote hayo ni maneno au maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi hakuna utekelezaji.
Hivi UDA tatu zinaweza jaza Nkuruma? Mimi mwenyewe nilikuwa pale and majority tulikuwa wanachuo tunaofahamiana - hivi Mnyaa, Kafurila, Lweitama, Makaidi, etc nao waliletwa na UDA?Tumaini Makene mbona iko wazi kuwa UDASA inaongozwa na mwenyekiti Dr Francis Michael ambaye ni mjumbe wa bunge la katiba ambaye ni CCM wa kutupa. Katibu ni Faraja Kristomus ambaye ni CCM damu. What do you expect?
Udasa inatumiwa vibaya sana sana na ni aibu ya mwaka. Wanafunzi udsm wako likizo wote lakini hapa wanasingizia waliomo ndani ni wasomi. Nimewashuhudia wakiletwa na mabasi matatu ya uda mbele ya utawala ili kuja kushangilia wanaccm wanaochangia. Shame on Udasa!
Bado mnapambana na Dr. Kitila? Kama ccm kusomba watu wao tumewazoea lakini hii ya udassa inalalamikiwa.Si kwa taasisi hizo pekee, bali pia watu wenye majina na hadhi katika jamii walioshiriki au kuingizwa kwenye mkakati ulioandaliwa kwenye mdahalo wa leo Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakiwemo baadhi ya wachangizaji maada!
Hatuwezi kukaa kimya iwapo inafikia mahali CCM wanatumia kidhalili taasisi za elimu tena zinazohusiana na kiwango cha chuo kikuu kwa kiwango kinachotaka kufanyika leo.
Ilianza kama tetesi. Lakini sasa ni dhahiri with facts, kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa UDASA mwenye uhusiano wa kikazi na CCM, ameshirikiana na chama hicho kukodi vijana kwenda Ukumbi wa Nkrumah, UDSM kwenye mdahalo unaorushwa live na Star TV.
Ingelikuwa jambo la heri na labda kujivunia iwapo UDASA ingeingizwa Kwenye mchezo huo mchafu na aibu kwa wasomi, wanataaluma na wanazuoni, endapo tu vijana hao wangekodiwa kwenda kujifunza au kutoa mchango wao kama Watanzania.
The shameful condition is...vijana hao wengi kutokea maeneo ya Buguruni, Dar ea Salaam, waliokodiwa kwa kulipwa hela na kubebwa kwa kutumia mabasi ya ile kampuni ya umma iliyouzwa kifisadi, wamechukuliwa kwa kazi moja tu, kwenda kuzomea! That is shameful...could have been a last thing to be done by an institution like UDASA to its breathing the last!
This is how you honour people like Prof. Chachage or Prof. Haroub or Walter?
This is how you guys at UDASA in collabo with the regime of the day now are transforming the Walters', Chachage's or Haroub's dreams for this country through serious discussion and debates at the Hill?
Mkakati huo wa CCM na ki-CCM umelenga kutaka kuweka precedence (bad of course) na kulazimisha hoja za CCM za kuchakachua Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya wakati BMK linakwenda kuanza Agosti 5, mwaka huu!
Umepangwa kwa namna ile ile ulivyopangwa mkakati ule uliofanywa na Serikali ya CCM kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kukodi vijana waliokwenda kutukana matusi ya ajabu hadi kuwatakia kifo akin a Mzee Warioba na wenzake kwenye Tume ya Mabadiliko!
It becomes even more shameful when it involves those whom, we, the people of this noble nation, could trust them as intellectuals of our times!
Wangelikuwa wamefanya CCM kama ambavyo wananchi wamewazoea (kuhonga na kubeba watu kwenda kwenye shughuli yoyote ikiwemo mikutano yao tusingehangaika. Maana ni sawa na kumtoa samaki majini kisha ukategemea aishi!
Kuhusisha taasisi ya wanataaluma na wanazuoni, tena chuo kikuu ni aibu ambayo hakuna Mtanzania makini atainyamazia.
Waacheni watu watoe maoni yao naturally na automatically! Yawe ni ya kuunga mkono UKAWA au CCM au kutounga upande wowote! Kwanini kupanga au kuleta mercenaries kwenye midahalo au majadiliano! Kwanini CCM haioni aibu kujianika wazi kila siku kuwa imeporomoka na haina kabisa ushawishi wa kisiasa tena kwa Watanzania!
Tutaweka facts zaidi...
Wasalaam
Makene
Hili jambo lina sehemu mbili, inavyoonekana watu wanaongozwa na hisia na ushabiki.Dr Kitila , hapa kuna hoja kuu mbili muhimu na kwa bahati mbaya sana unaonekana kuongozwa na jazba bila kuzitambua
1. Ni kweli kuwa umeshiriki sana kuandaa makaongamano mbali mbali.
Ni kweli kuwa UDASA imefanya hivyo kwa muda mrefu.
Na sasa ni ukweli kuwa umethibitisha kuandaa kongamano la Jumapili.
Hadi hapo hakuna tatizo la aina yoyote ile.
2. Upo uwezekano wajanja (opportunists) wakatumia nafasi ya kongamano lako kutimiza haja zao za kisiasa.
Hivyo kusema kuwa Rochi hayupo unakuwa hujitendei haki wewe mwenyewe.
Kwa maneno mengine unathibitisha kuwa hakuna opportunists kama Rochi wanaoweza kutumia kongamano lenu lenye nia njema kufanikisha nia zao ovu.
Hapa ndipo naona unajiweka katika 'hook'
Kwa bahati mbaya ikithibitika kuwa kuna watu waouvu wanataka kulitumia kongamano lenu bila ninyi wenyewe kujua, kwa utetezi wako kuwa 'Rochi' hayupo utakuwa umejenga mazingira tatanishi sana na pengine kujikuta ni Mhusika Mkuu(MM) bila kutarajia.
Ushauri wangu kwako ni kuwa, simamia azma ya kongamano lako kama kongamano la UDASA.
Acha uwakili wa akina Rochi maana mwisho wa siku unaweza kujiweka katika nafasi ngumu zaidi ya hii inayoonekana.
Hili la akina Rochi linaweza kuwa kweli au si kweli, usiingie kwa kusukumwa na jazba.
Usithibitishe au kukanusha bila kuwa na ushahidi.
Nakushauri uangalie na kupima kauli zao kulingana na mazingira yanayokuzunguka kwa sasa na huko nyuma. Kuongozwa na jazba hakusaidiii .
1. kwani hao watu walio hudhuria wameleta fujo yoyote?
2.kwani wao sio wananchi wanaopaswa kuhudhuria kwwenye mdahalo?
3. kwani watu wengine walikatazwa kukusanya watu wao kwa lengo la kuwaongezea eliu zaidi?
kama usomi unaomaanisha ujipendekeze kwa wanasiasa kama wana UDASA, acha nikose huo usomi.Kajipange huna cha kumjibu msomi kama kitila