CCM and UDASA, this is shameful

CCM and UDASA, this is shameful

Moderator.

Kwa heshima na taadhima naomba tafadhari usifute wala kuunganisha thread hii.

Natambua kwa miaka mingi iliyopita chuo kikuu cha Dar es salaam kilijijengea heshima kwa kuwa tanuru la kuchakata na kuoka fikra na tafakuri tunduizi. Natambua kuwa katika miaka ya nyuma maswala yote magumu ya mkwamo kwenye nchi yalikuwa yakijadiliwa objectively kwenye viunga vya chuo kikuu cha dar es salaam kwa weledi na kwa usawa wa hali ya juu.

Leo kwenye mdahalo wa nini kifanyike bunge la katiba likiendelea wiki ijayo, nimeona kwa dhahiri mdahalo huu umeitishwa tu kwa jina la UDASA lakini ukweli ni kwamba ilikuwa mdahalo wa CCM ukimshirikisha Tundu Lissu kwa minajili ya kufunika kombe ili mwana haramu apite. Na hili limedhihirishwa na kauli ya Lukuvi akimsifu Lissu na kumuona kama ka mzizi ka UKAWA.

Ukiangalia namna wazungumzaji walivyo kuwa wanapewa fursa za kuchangia kwenye mdahalo ule, bila chembe ya shaka utagundua kuwa hakukuwa na fursa sawa ya uchangiaji. Sikuona mantiki ya kumuita Mwigulu Nchemba na kuacha kumuita miongoni mwa washiriki walio tambuliwa awali kama Mheshimiwa Machali na David Kafulila lakini wakati huohuo nafasi ya kuchangia akipewa kada Kunambi wa Ccm.

Haikuwa sahihi kuacha kumpa nafasi ya kuchangia mtu wa kariba ya Prof Sheriff na kumpa nafasi kijana kutoka zanzibar ambaye hata historia ya Zanzibar aliipotosha huku pia akiongea kwa kujiamini lakini kwa kupotosha kuwa tume ya Warioba haikwenda kuchukua maoni Zanzibar.

Kulikuwa na vigezo gani kumpa nafasi ya kuchangia Prof Tabaijuka aliyekiri kuwa hata katiba mpya isipo patika bado ni ushindi kwa ccm na jk huku akiacha Prof Sheriff na Dr Lwaitama tena bila hata kutambuliwa kuwa wako ukumbini?!

Nimebaki najiuliza, wale vijana walio kuwa wanaitwa kuchangia ikiwa ni pamoja na baadhi ya wazee walio ishia kuzomewa, majina yao yalipatikana vipi na ni utaratibu upi ulio tumika?

Umetumika utaratibu upi na vigezo gani vya kuwa na wazungumzaji wengi wa ccm kuliko wazungumzaji wanao unda kundi la ukawa?! Kwa nini hakukuwa na usawa wa wachangiaji?!

Kwa nini mdahalo wa UDASA uhitimishwe na Lukuvi (mccm) nasi mwenyekiti wa UDASA?!

Nabaki najiuliza? Mdahalo ulioandaliwa chuo kikuu ulikuwa wa Udasa au Ccm?! Kama ccm imefanikiwa kuingilia mpaka uhuru wa vyuo vikuu tunaachaje kuamini kuwa elimu pamoja na taasisi zilizo heshimika za elimu ya juu ziko shakani kwa kuendeshwa kwa remote control na kutumika kisiasa?!
 
Huo ndo ukweli na ndio maana ccm wamewapeleka vijana wa vyuo vikuu jeshi ili wawe waoga wa kutii tu hataka unajeuzwa nyuma
 
Wee Mtoi unaishi Bongoland au Sayari ya Mars? Mbona hicho Choo Kikuu cha DSM kilishafanywa kitengo cha Magambas siku nyingi. Maprofesa inabidi wajipendekeze kwa CCM ili wasifukuzwe kazi au wapewe concultancy za serikali! Nimemwona profesa mmoja alikuwa mashuhuri sana siku hizi anabeba mikoba ya Membe! Wanafunzi wanaogopa kunjega na kueleza fikira tunduizi na mbadala kwa kuofia kuwekwa kwenye black list na hivyo kubaguliwa wakati wakitafuta ajira!! Hapa tuko kwenye vicious circle - Taaluma iliyopaswa kuwa mkombozi wa jamii imebakwa!
 
mimi nilishtuka nilipoona nyuso za watu na akinamama waliokuwa wamevaa kanga nikasema hawa wamekodishwa toka Manzese. Zaidi ya yote Lukuvi akapewa nafasi ya kufunga mdahalo!!!. Hivi kweli UDASA walijipanga?.
 
Wana JF Habari...........

Hii inasikitisha sana kwa kweli. Naomba tuchangie kwa uzito wake unaostahili.



  • Ni kweli kwamba UDASA wameandaa huu mdahalo mbona kama umepangwa na ama SERIKALI au CCM?.
  • Sio tu kwamba unaegemea upande wa CCMna serikali bali hata management ya muda ya watoa mada wakuu na wachangiaji wengine mbona kama haman balance?
  • Hiyo zomeazomea iliyoanza ni ilipangwa au ime tokea tu?

Mwenye tetesi tafadhali........................................
 
mimi nilishtuka nilipoona nyuso za watu na akinamama waliokuwa wamevaa kanga nikasema hawa wamekodishwa toka Manzese. Zaidi ya yote Lukuvi akapewa nafasi ya kufunga mdahalo!!!. Hivi kweli UDASA walijipanga?.

Nimeshangaa kuona Lukuvi anahitimisha kama nani
 
Walinunuliwa na maccm hilo lipo waxi. Wew hukuona mamluki walioletwa na maccm ili kuzomea nakushangilia eti ili wtz waone ccm ina watu wengi nyuma yao so wana nia njema na katiba. Watz hatudanganyiki na mavi zenu.
 
nimeshangaa sana LISSU kuzomewa, wale vijana ni wakina nani..?
 
Ccm inaharibu nchi.Mpango upo pia kwa waandishi wa habari. Sikilizeni kesho headline
 
yyan ccm ni kichaka cha wahuni na wazindiki,, alafu yanatoka kama mazuzu vile,, majinga hata kudanganya hayajui pumbuvvuuuuuu ,,,,,,,
 
Pamoja na yote hayo,leo Mh,Mwigulu ameongea kiutu uzima sana!Kwa mara ya kwanza mimi namsikia akiongea kama Mzalendo halisi.Sasa sijajua hiyo ni JANJA YA NYANI au.......? Maana inaoneka mkutano ulikuwa kimkakati zaidi kwa kutoruhusu maswali,kwani ukiruhusu maswali mambo mengi wenzetu huwa hawana maelezo yanayo jitosheleza mbele ya wananchi na kuishia kuzomewa!
 
Ili kuthibitisha kuwa hii ilikuwa ni colabo kati ya CCM and UDASA aliyetoa neno lamwisho alikuwa mnyalu Lukuvi.
 
Mkuu huwa nashangaa sana pale watu wote wanaotaka UKAWA warudi bungeni hawesemi chochote kama watarekebisha kile kinacholalamikiwa na UKAWA au juu ya madai yaliyosababisha UKAWA wasusie bunge. kama wameyarekebisha na kama watayarekebisha je kutakua na maandishi yoyote kama kumbukumbu? UKAWA wana madai mengi ya msingi LAKINI DAI KUU NA LA MSINGI NI KUJADILI maoni ya wananchi kama yalivyowasilishwa na TUME ya Jaji Warioba.Hata hivyo naungana na wewe kabisa mdahalo huu una mkono wa CCM.Hata mimi sikuridhika na Lukuvu kuhitimisha naona kama ni propaganda tu na jinsi alivomalizia ni ujanjaujanja tu.mfano aliposema Bunge la keshokutwa wanakwenda kujadili mambo ya wanafunzi kusoma bure,jinsi ya umiliki wa ardhi n.k Hii ni kuwa laghai wananchi ili waone UKAWA hawawatetei wananchi. Nakubaliana na wewe kwa ulichoandika mkuu.
 
Back
Top Bottom