CCM and UDASA, this is shameful

CCM and UDASA, this is shameful

midahalo iliyotangulia ccm walionekana kuzidiwa. ghafla leo mambo yakaonekana kugeuka na maongezi ya pale yalionyesha wazi kuwa kulikuwa na maandalizi fulani upande mmoja.Ila Mwigulu alikuwa mjanja katika hoja zake kwa ujumla alikuwa objective.
 
attachment.php




Haya maandalizi aliyakataa Kitila Mkumbo jana

Hapo CCM inawashusha watu wake


1. kwani hao watu walio hudhuria wameleta fujo yoyote?
2.kwani wao sio wananchi wanaopaswa kuhudhuria kwwenye mdahalo?
3. kwani watu wengine walikatazwa kukusanya watu wao kwa lengo la kuwaongezea eliu zaidi?
 
Wakikataa wataenda kuuza sura wapi wakati unajua kuwa wao ni wazee wa kuuza sura kwenye vyombo vya habari.

ukweli huwa haubadiliki,mtu kama TL,machali na kafulila sio watu wa kuuza sura.yeyote anaefuatilia siasa za tz anawajua vema.kaa kimya ufiche ujinga wako.
 
Si kwa taasisi hizo pekee, bali pia watu wenye majina na hadhi katika jamii walioshiriki au kuingizwa kwenye mkakati ulioandaliwa kwenye mdahalo wa leo Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakiwemo baadhi ya wachangizaji maada!

Hatuwezi kukaa kimya iwapo inafikia mahali CCM wanatumia kidhalili taasisi za elimu tena zinazohusiana na kiwango cha chuo kikuu kwa kiwango kinachotaka kufanyika leo.

Ilianza kama tetesi. Lakini sasa ni dhahiri with facts, kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa UDASA mwenye uhusiano wa kikazi na CCM, ameshirikiana na chama hicho kukodi vijana kwenda Ukumbi wa Nkrumah, UDSM kwenye mdahalo unaorushwa live na Star TV.

Ingelikuwa jambo la heri na labda kujivunia iwapo UDASA ingeingizwa Kwenye mchezo huo mchafu na aibu kwa wasomi, wanataaluma na wanazuoni, endapo tu vijana hao wangekodiwa kwenda kujifunza au kutoa mchango wao kama Watanzania.

The shameful condition is...vijana hao wengi kutokea maeneo ya Buguruni, Dar ea Salaam, waliokodiwa kwa kulipwa hela na kubebwa kwa kutumia mabasi ya ile kampuni ya umma iliyouzwa kifisadi, wamechukuliwa kwa kazi moja tu, kwenda kuzomea! That is shameful...could have been a last thing to be done by an institution like UDASA to its breathing the last!

This is how you honour people like Prof. Chachage or Prof. Haroub or Walter?

This is how you guys at UDASA in collabo with the regime of the day now are transforming the Walters', Chachage's or Haroub's dreams for this country through serious discussion and debates at the Hill?

Mkakati huo wa CCM na ki-CCM umelenga kutaka kuweka precedence (bad of course) na kulazimisha hoja za CCM za kuchakachua Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya wakati BMK linakwenda kuanza Agosti 5, mwaka huu!

Umepangwa kwa namna ile ile ulivyopangwa mkakati ule uliofanywa na Serikali ya CCM kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kukodi vijana waliokwenda kutukana matusi ya ajabu hadi kuwatakia kifo akin a Mzee Warioba na wenzake kwenye Tume ya Mabadiliko!

It becomes even more shameful when it involves those whom, we, the people of this noble nation, could trust them as intellectuals of our times!

Wangelikuwa wamefanya CCM kama ambavyo wananchi wamewazoea (kuhonga na kubeba watu kwenda kwenye shughuli yoyote ikiwemo mikutano yao tusingehangaika. Maana ni sawa na kumtoa samaki majini kisha ukategemea aishi!

Kuhusisha taasisi ya wanataaluma na wanazuoni, tena chuo kikuu ni aibu ambayo hakuna Mtanzania makini atainyamazia.

Waacheni watu watoe maoni yao naturally na automatically! Yawe ni ya kuunga mkono UKAWA au CCM au kutounga upande wowote! Kwanini kupanga au kuleta mercenaries kwenye midahalo au majadiliano! Kwanini CCM haioni aibu kujianika wazi kila siku kuwa imeporomoka na haina kabisa ushawishi wa kisiasa tena kwa Watanzania!


Tutaweka facts zaidi...

Wasalaam

Makene

udasa ssssm damu damu siku hizi kwa matangazo kwanza hakuna
 
Vijana tunatakiwa tujue kwamba tutavuna tulichopanda yaani unapewa elfu kumi halafu kesho unanyang'anywa milioni moja...jamani tufunguke uoga wetu ndo umasikini wetu
 
midahalo iliyotangulia ccm walionekana kuzidiwa. ghafla leo mambo yakaonekana kugeuka na maongezi ya pale yalionyesha wazi kuwa kulikuwa na maandalizi fulani upande mmoja.Ila Mwigulu alikuwa mjanja katika hoja zake kwa ujumla alikuwa objective.

mwigulu mjanja sana,anajua ukawa wana hoja.
 
Kwa mdaharo wa leo nimejifunza mambo mengi sana ya ajabu kwa wasomi wetu. Na kilichonisikitisha ni wasomi kutoka chuo kipi?. Sehemu ambapo inaaminiwa na watu wengi kuwa greater thinkers wa Tanzania ndipo walipo au wanategemea kutoka....duuuuuu!!!!. Niachane na hilo nirudi kwenye maada yangu niliyokusudia kuitoa.

Dr.kitila kasifiwa leo na CCM hasa Lukuvu kuwa ana akili sana,na Lukuvi amesisitiza na kumuomba Kitila afanye utafiti kuhusu kama kweli Muungano wa watu watatu yaani UKAWA una nia thabiti au njema ya kupata katiba mpya?. Wamekuomba wao,na ukifanya hivyo watakusaidia sana maana watawala wanapenda kusifiwa.

Mfano,lukuvi anajua kabisa Kitila na CHADEMA wana UGONVI, ivi mtu mwenye akili unategemea huyu atakuja na majibu ambayo kweli yanaonyesha uhalisia wa utafiti....maana yeye mwenyewe ana interest. Dr. Fanya hicho kitu haraka sana na watakupa pesa nyingi na utakuja na majibu wanayotaka wao ili wayatumie kwenye midaharo..fanya....fanya haraka. Unaweza ukajifungia hotelini siku tano au wiki ukamaliza machezo.

Nilitegemea angalau AWAAMBIE wana UDASA kwa ujumla na si Dr.Mkumbo. Dr. Dili hilo fanya na pesa ipo nadhani maana wao ndio wamekuomba. Usiwape majibu tofauti baada ya utafiti maana hawatakupa hizo pesa.
 
Kilichoniuma Ni Jinsi Upendeleo Wa Wazi Kwa Wachangiaji Yaani WacCm Kibao Halafu Mwishoni Walisema Dk Mbili Wakampa Lukuvi Dkika 45 Amalizie, Haya Nikasema Nikajiliwaze Na Matokeo Ya Taifa Starz Nako Tumechezeia, Nchi Hii! Aaah Cjui Niende Wapi?
 
blah blah nyingi lakini kwa ujumla nakubaliana na 50% ya hoja

Hakuna jipya kwenye hii midahalo mingi yake ina malengo mahsusi yalijificha,Na ikiwa kama wale wanaojiita wasomi wanashindwa kujenga hoja makini kuwashaishi kukubaliwa kwa hoja zao mjengoni basi wanapoteza mda wao bure.wananchi tutashawishika kwa hoja zenye mantiki na sio hoja shawishi.nakubariana kidogo na Mwiguru leo. nchi hii kuna kundi la watu wameamua kwa makusudi kuwafanya wananchi kama manyumbu yanapelekwa tu na wanasiasa hao wanajiita wasom lakini kiukweri ni watu waliobeba ajenda yao.walaaniwe wote.
 
Kiukwel mie nahisi watanzania tunahitaji elimu sana kuondoa mgando wa fikra, tunawezaje kuwa na wasomi ambao wanabailika badilika katika mawazo yao ambayo wameyaandika katika vitabu vyao mbalimbali? kiukwel mie kama mwanafunzi sijui nijifunze nini kutoka kwa hawa ma prof na ma dr ambao wanatuasa tusome vitabu vyao. Inakuaje prof unashindwa kujenga, kupambanua hoja na hata kujieleza tu kwel? Kama wasomi wetu ndo hawa basi tunasafari ndefu sana
 
Mkuu Makene, kwa welevu walioangalia kongamano hilo ni wazi atagundua udasa imeanza kutumika kama ile bidhaa ya wapenzi c.nd.m. Taasisi ya juu namna hiyo inageuzwa kitengo cha propaganda ya CCM. Cha ajabu zaidi wazungumzaji walikuwa wamepangwa na walikuwa wamelishwa maneno, hawakuwa huru na nafsi zao ziliwasuta na zitaendela kuwasuta.

Viti vyote pale chini walikuwa wale vijana wa kukodiwa na wachache pale juu. Kuna mwana JF alisema wameandaa vijana wa kukodi na kwamba akiingia ukumbini anaingizwa kwenye payroll tukampuuza ila leo wametuaminisha.

Tunawashukuru kwa kutufumbua macho watanzania kwa kujua mbinu chafu na hila zao (CCM) na kwamba UKAWA kamwe msidanganyike mkarudi Bungeni. Wanaposema njooni tutaelewana ni mtego mbaya sana na mkidhubutu watanzania tulio nyuma yenu hatutawaelewa kabisa na mtakuwa mmetutusi sana. Chonde chonde msirudi bungeni.

Eti mchangiaji (Lukuvi) ndo anakuwa wa kuweka hitimisho tena kwa nusu saa ila watoa mada dakika 2. CCM shame on you.
 
Mambo ya kawaida kwenye demokrasia, sasa upinzani hata hamtaki cha kibisha?! Wengine tunapenda yawepo kama challenge kwenu upinzani, hasa ukichukulia upinzani wenyewe ni kama wa kichaga au kipemba..
 
Hii imetokea leo baada ya yeye na mwenzake Robert Gwanchele kukutwa akiwa na Vijana wa Uvccm mr Assenga na Paul Makonda akizomea vibaya Wazungumzaji wa UKAWA na kuishabikia CCM hasa wakati ambapo Mwigulu na Wasila walipokuwa wakizungumuza katika kongamano la Katiba ukumbi wa Nkuruma chuo kikuu cha Dar es salaam leo jioni.

Huyu bwana hivi karibuni ameonekana akiwa na viongozi wa Act wakipanga mikakati ya kununua baadhi ya makada wa CHADEMA wajiunge na ACT chaajabu leo tena alikuwa bega kwa bega na vijana hawa wa CCM wakizomea kwa pamoja UKAWA na akisahau kabisa kuwa kiongozi wake Dr mkumbo amewaunga mkono UKAWA, hivi hao waliomuchagua anawatumikia saangapi kama ndo kila siku kubadili vyama vya siasa nawapambe wake akina Gwanchele?

Vijana jamani kuna haja ya kulazimishana wote kujitambua kama ni nguzo na msaada mkubwa saaana wa taifa hili hapo baadaye badala ya kuendelea kuwa wabeba mabegi ya wanasiasa kama hawa marafiki zangu Chagulani begi la mwigulu na Robert Gwanchele begi la Chagulani.Kijana mwenzangu wewe unasemaje katika hili la kutumikia vyama viwili na kubebea watu mabegi yao kama mtu uliyekomaa kifikira?
 
Ni aibu ya mwaka.Hicho si chuo kikuu tena.Nchi haina think tank tena. Huko ndiko waliko wasomi wanaoitwa Benson Bana,ukimsikia akichangia mada utafikiri hakwenda shule.
Mdahalo huu umeandaliwa na ccm kwa jina la udasa ndiyo maana walijaa viongozi wa ccm na kuwa wazungumzaji.
Kwa nini hawa Udasa wawakilishi wa ccm kwenye mdahalo huu hawakuwaita waliokuwa wajumbe wa tume ya Warioba ili watoe ufafanuzi wa mambo yote yanayobishanishiwa? Shame on you Udasa


acha porojo wew bana ni mjenga hoja mzuri sana cie anaetufundisha tunamfahamu vizuri na tunamkubali hana bias ccm au chadema wakiboronga huwa hakwepeshi,acha mawazo ya kibavicha.
 
Makene...

Ni kwa nini Tundu Lissu asingekataa mwaliko?...

Ilishaelezwa hapa nini CCM wanafanya kuhusiana na Kongamano hilo...Nimeshangaa sana kuwaona Lissu, Machali , Kafulila na wajumbe wengine wa UKAWA kama sehemu ya Kongamano hilo...

Bala,
Hoja ya Makene ni CCM kuitumia taasisi ya UDASA kukodi vijana wahuni kuja kuharibu mdahalo.
Hio haihusiani kabisa na Presence ya UKAWA pale.
By the way,Kama UKAWA wasingekuwepo wangemzomea nani wale wahuni /
 
Hata wasira kuchelewa ilikuwa janja tu ... Everything was planed !! But we are brave ! We can
 
Back
Top Bottom