PICHA HALISI YA MDAHALO WA LEO STAR TV.
Ndg watazamaji, wasomaji na wafuatiliaji wa MIDAHALO hii mbalimbali ya Katiba mpya, naamini kwamba, leo 03/08/2014 siku ya Jumapili mmepata wasaa mzuri wa kuutazama mdahalo wa leo uliofanyika katika ukumbi wa NKRUMAH pale mlimani Chuo Kikuu, kupitia Kituo cha Television cha Star tv.
Kama ilivyo kawaida yao watawala, huandaa midahalo inayohusu masuala ya Kitaifa kwa kujikita zaidi katika misingi ya uchama zaidi, na hii imedhihirika leo pale UDSM.
Ni mdahalo ambao watu maalumu wa kuzungumzia hoja za kuibeba CCM katika issue nzima ya mchakato wa Katiba mpya, tayari walikuwa wamekwishaandaliwa kwa majina kama tulivyoona wakisomwa majina mmoja baada ya mwingine, na kulipuka kama mabomu yalokuwa yametegwa.
KISA CHA MIMI KUZUILIWA MARA MBILI KUZUNGUMZA PALE JUKWAANI LEO.
Mimi Francis, nilikuwa nimekaa line ya mbele kabisa chini kwenye floor pale ndani Nkrumah Hall, kushoto kwangu alikuwepo Adams Chagulani, nyuma yangu walikuwepo Habib Mchange na Mtela Mwampamba, sasa basi, wakati nikiendelea kuandaa hoja zangu pale chini ili nikaziwasilishe kwa niaba ya Watanzania hasa wale wote wenye Imani na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kumbe wakati huo akina Chagulani walikuwa wananichora na kunilia target ya kunidhibiti kwa namna yoyote ile, ili mradi nisipate nafasi ya kuwasilisha yale yote niliyoyaandaa kwenye Document zangu, hivyo ili kutimiza azma yao hiyo ikawalazimu kula dili na maafisa usalama waliokuwepo pale ndani bila ya mimi kuugundua mchezo kwamba unanihusu mimi.
Niliponyanyuka mara ya kwanza na kufika jukwaani ghafla nimevamiwa na watu zaidi ya watatu na kushushwa chini na hatimaye tena nikapanda mara ya pili, lakini sikuweza kufua dafu kwa sababu tayari walikuwa wamejenga mtandao mkubwa wa kunidhibiti pale ndani.
Ishaalah nashukuru mola tumehitimisha salama bila mtafaruku wowote, ingawa CCM wameangukia pua
vibaya sana!