CCM Acheni Utoto Huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Acheni Utoto Huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kulikoni Ughaibuni, Aug 10, 2010.

 1. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Ni dhahiri kwamba CCM ikipata mpinzani wa saizi yake inatikisika.Sio siri,tangu Chadema wamtangaze Dkt Wilbroad Slaa kuwa mgombea wao wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano katika Uchaguzi Mkuu ujao,chama hicho tawala ambacho kimekuwa madarakani kwa takriban nusu karne,kimeanza kupatwa na "mchecheto".Hakijiamini.

  Kituko cha kwanza ni uamuzi wa chama hicho kukataa wazo lililotolewa na Dkt Slaa kwamba uandaliwe mdahalo kati ya wagombea urais.Akipingana na wazo hilo,Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba alidai kwamba mgombea wao,Jakaya Kikwete,hawezi kupimwa kwa mdahalo, bali kwa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na mwekeleo wa sera za Chama.Makamba alidai, "Wananchi hawana sababu ya kumpima Rais Kikwete, kwani walishampima kutokana na utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005... utafiti wa taasisi za kimataifa umeonyesha anakubalika pamoja na serikali yake,"

  Ikumbukwe kuwa Kikwete alikacha wazo la mdahalo kwa wagombea katika uchaguzi uliopita mwaka 2005.Ungeterajia kwamba chama kilichokaa madarakani miaka nenda miaka rudi kijiamini,na kisiwe na hofu ya kumpambanisha mgombea wake na wagombea wa vyama vingine kwenye jukwaa huru ili wapiga kura wapate fursa japo moja ya kuwapima wagombea hao.CCM wanafahamu fika kuwa wazo la mdahalo kwa sasa ni hatari kwa vile wana maswali mengi ya kujibu lakini hawana majibu.Unadhani,kwa mfano, JK akiulizwa kuhusu Kagoda atajibu nini!Hizo ndizo sababu halisi zinazopelekea chama hicho tawala kuingia mitini kwa mara ya pili.

  Kabla kiroja hicho hakijatulia,CCM wametuthibitishia tena namna gani walivyopandwa na "mchecheto" baada ya kuanza "kulialia" kuwa Chadema wanakiuka taratibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati stahili.Hivi CCM wanatufanya Watanzania wote tuna akili za kitoto au?Hivi ile hotuba ya JK wakati anachukua fomu za kuwa mgombea wa CCM haikuwa sehemu ya kampeni?Na alipohutubia Bunge na kueleza mlolongo wa mafanikio ya serikali yake ya Awamu ya Nne hakuwa anajipigia kampeni?Na alichoongea majuzi alipochukua fomu ya kugombea urais hapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi sio kampeni?Jamani,mbona CCM inajiabisha kiasi hiki?Mgombea wake anatamka bayana kuwa "vipaumbele vyake akipewa ridhaa ya kuongoza tena Tanzania vitakuwa A,B,C,nk" lakini kwa mtizamo finyu wa chama hicho hizo sio kampeni.


  Kinachowatia tumbo joto CCM sio "Chadema kuanza kampeni mapema" bali ni dalili zinazoonyesha bayana kuwa chama hicho tawala kinaweza kuanguka kwenye uchaguzi ujao.Kimeanza kupaniki baada ya kuona halaiki za Watanzania wakojitokeza kwenye mikutano ya Dkt Slaa.Wametahayari baada ya kuona mgombea wao amedhaminiwa na watu elfu 14 na ushee tu ilhali Dkt Slaa kapata wadhamini zaidi ya milioni 1.Taratibu wanaanza kuona dalili ya upinzani wa dhati unaoweza kuwang'oa madarakani.

  Kwanini CCM isijibidiishe kusafisha uozo unaoendelea kwenye mchakato wake wa kupata wagombea wake?Yayumkinika kusema kuwa japo hata huko nyuma zoezi hilo lilitawaliwa na rushwa lakini hii ya msimu huu ni kubwa kuliko zote.

  CCM wanapaniki kwa vile wanamfahamu fika Dkt Slaa.Wanakumbuka vema namna alivyowaumbua na "List of Shame" (orodha ya mafisadi sugu),ambapo watajwa walitishia kwenda mahakamani lakini hakuna mmoja aliyediriki kufanya hivyo.Wanaelewa fika kuwa hoja ya ufisadi haijatolewa majibu ya kutosha na ni vigumu kwa chama hicho kujitenganisha na mafisadi wanaokilea.

  Chama hicho tawala kinakabiliwa na mtihani mkubwa katika kufanya mchujo wa wagombea wake.Tayari kuna tetesi kuwa baadhi ya wagombea walioshinda wamepewa maksi pungufu.CCM inafahamu bayana kuwa baadhi ya waliokuwa wabunge wake wanaweza kuhamia Chadema na kuunganisha nguvu za chama hicho (Chadema) katika kuweka wazi uozo,madudu,ufisadi na uharamia mwingine uliofanyika katika utawala wa chama hicho.

  Ushauri wa bure kwa CCM ni kwa chama hicho kilichopo madarakani hadi muda huu kufanya vitu vya "kiutu uzima" kwa kufuata kanuni zilizopo (ikiwa ni pamoja na kukabiliana na sualam la rushwa ndani yake) kabla ya kuangalia nani anafanya nini.Of course,two wrongs do not make a right lakini kwanini walalamike kuwa Chadema imeanza kampeni kabla ya muda ilhali CCM ilianza kampeni hizo kitambo?Mkuki kwa nguruwe....

  Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha wale wote wenye uchungu na mapenzi ya dhati kwa Tanzania yetu kwamba kwa namna kampeni za ndani za CCM zilivyotawaliwa na rushwa iliyopindukia ni vigumu mno kwa chama hicho kupata wagombea safi watakaoweza kuwatumikia wapiga kura wao.Wakichaguliwa watakuwa bize zaidi kurejesha gaharama walizoingia katika kutoa rushwa wakati wa kampeni zao.Kura hizo za maoni zinapaswa kuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la chama hicho ambacho ni mahiri sana katika kuahidi makubwa lakini utekelezaji ni sifuri,zero,nada,zilch!

  CCM Acheni Utoto Huu | KULIKONI UGHAIBUNI
   
 2. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  We ndugu chagua maneno yako kadri uwezavyo. Fainali ni tarehe 30 October.
   
 3. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Yamekuuma?
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kinachomuuma zaidi ni kwamba mbinu za wizi wa kura mwaka huu huenda zikabadili siasa za Tanzania kutoka za uzuzu mpaka za ukakamavu
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Marais wote wa Marekani hufanya midahalo ipatayo mitatu au zaidi kabla ya uchaguzi; iweje rais wa Tanzania asiweze kufanya mdahalo kabla ya uchaguzi. ??
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Jirani, ukweli wa mambo ni kwamba mgombea wa CCM mambo ya midahalo sio fani yake. Yeye siyo mzungumzaji mzuri na kwa jinsi nilivyomfuatilia anaonekana siyo mtu wa kufikiri haraka on his feet. Sasa mdahalo ataumudu kweli? Labda wampe maswali ahead of time lakini na yenyewe anaweza akasahau majibu vilevile halafu akaadhirika mbele ya kadamnasi. Kwa hiyo ni bora hata wasikubali mdahalo...

  Kama unakumbuka mwaka jana au mwaka juzi mwishoni kwenye ule mkutano wa TED uliofanyikia Arusha. Jamaa alishiriki majadiliano yaliyokuwa moderated na Isha Sessay....yaani alikuwa anahangaika kutafuta cha kujibu hadi nikamwonea huruma.

  Kwingine ni Davos kwenye WEF anakoendaga kila mwaka. Huwaga anatia huruma sana. Yeye muungwana na predecessor wake ni day and night kabisa. Kama predecessor wake asingejiingiza kwenye ufisadi basi angeingia kwenye vitabu vya historia kama mmoja wa marais bora sana Afrika. Lile lijamaa acha tu bana. Linajua kuongea na linayajua mambo. Lilikuwaga linanifanya nijisikie majivuno sana lilipokuwa likituwakilisha ktk medani za kimataifa.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This is exactly wht ths guy is, ukitaka kupata kichekesho combine hiyo sifa (highlighted) na mpenda sifa, ujiko asiyejua mambo!!!!!

  Huyu jamaa kuongea ni fani yake na anapenda mno! Lakini when it comes to issues na akawa aware kwamba he is being watched and compared ni mweupe peepe pepe!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kama hawezi kuelezea analotaka kuifanyia nchi hii je atafanya nini akichaguliwa? Natamani sana CCM ifutike kama ambavyo UNIP na KANU zilivyofutika baada ya kulewa madaraka.
   
 9. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MWEZI OCTOBER NI MWEZI AMBAO MBIVU NA MBICHI ZITAJULIKANA........WAFUASI WA VYAMA MBALIMBALI KADRI WALIVYOJIANDAA WASITAFUTE VISINGIZIO PINDI MATOKEO YATAKAPOTANGAZWA............sababu za wizi wa kura,masanduku kuchelewa kufika,kura kuharibika n.k zitakuwa zimepita KAMA MMEJIANDAA VYEMA NAJUA MMETAFUTA MBINU ZA KUDHIBITI YOTE HAYO..........TUTAKUJA NA SABABU GANI TENA? PINDI MATOKEO YATANGAZWAPO?
   
 10. Mwanahakij

  Mwanahakij Senior Member

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa akina Makamba na Msekwa na pengine, CCM wana kumbukumbu ndogo sana. Walivyo maliza mkutano wao Chimwaga, wakampitisha JK na Bilal kugombea urais wa bara ( muungano) na Dr Shein kusukumiwa Zenji, walianzia kampeni pale jamhuri stadium. Wakahutubia wee, na kukampeni kwa kisingizio cha kutambulisha wagombea wao. Kama vile, haitoshi, wakaja Dar, wakafanya kampeni pale jangwani. Wakavuka maji, wakaenda Zanzibar na baadae Pemba, ambapo Dr shein na Dr Bilali, walienda kujitambulisha. Walipotosheka wakamalizia na kampeni za kura za maoni, wakizunguka Tanzania zima hadi vitongojini? Je hii si kampeni?

  Sasa ChADEMA, wakaamua kuwashinda CCM, katika kamchezo kao wenyewe. Wanachofanya CHADEMA, ni kutambulisha mgombea wao, kama CCM walivyofanya, Dodoma, Dar, zenj na Pemba. CHADEMA wao wajanja, wameanzia pale hawa ccm wasahaulifu walipoishia! Tatizo, ccm walidhani wapinzani hawatakuwa na fedha za kuzunguka kama wao, sasa wamenasa kataika mtego wao wenyewe! Ama kweli mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu!
   
 11. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwani tupo marekani hapa, hii kasumba ya kuiiga marekani itaisha lini?
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Mbona tumeiga kupiga kura?...niambie hii ni mila ya kabila gani kati ya 120 tulonayo?.......hata hicho cheo cha urais ni cha kabila gani?(neno lenyewe la kiarabu)
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi kukaa kimya huwezi mbona unawashwa sana
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ..AAIIMEN! That Day Is Very Soon Coming...!

   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,684
  Likes Received: 21,946
  Trophy Points: 280
  Hapo hujaongea kitu, unaishi ulimwengu upi wewe?
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa mbona vitisho babu vipi???????????? Taratibu!!!!!
   
 17. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Tukienda kwenye uchaguzi tukitaraji maendeleo endelevu hatuwezi chagua CCM....
  Tukienda ki-ushabiki tutazidi kuwapa ulaji kundi dogo la wateule na vitegemezi vyao...
  Tutumie busara...
   
 18. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli, cha zaidi ni pale CCM wanapoona baadhi ya wakongwe kama Shibuda kutishia kuhamia upinzani na jana wanachama kama 70 wamerudisha kadi za CCM na kujiunga na upinzani, kingine ni pale TUCTA walipokaa na kusema watatoa tamko kuwa ni rais gani wamchague mwaka huu, "POOR CCM NA SHAME ON YOU" Wametunyanyasa, wemetutesa na kutudhalililisha vya kutosha na sasa saa ya ukombozi imefika na na CHADEMA ndio mkombozi wetu, kilikuwepo KANU je mbona kiling'oka? na hao tume ya uchaguzi wakiwasikiliza CCM na kumzuia Slaa kugombea uraisi tutaanzisha maandamano ya amani kuhamasisha wananchi kugoma kupiga kura hapo Oktoba. CCM ACHENI UOGA. "PIGANENI KWA SERA SIO KWA SARE"
   
 19. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa wale wanaosema kuwa si lazima kufanya mdahalo na haijatokea hivyo, wanakosea. Mimi ninayo hapa mbele yangu video casette iitwayo 'Mada Moto-Uchaguzi 1995. Video hiyo inaonyesha mdahalo kati ya wagombea uraisi wa vyama mbalimbali kwa mara ya kwanza Tanzania. Katika video hiyo mojawapo ya walioshiriki mdahalo alikuwa Raisi Ben Mkapa, Lipumba, Mrema na wengine. Sioni kwa nini mdahalo usifanyike sasa wakati ambapo Tanzania imekuwa na uzoefu wa vyama vingi, kuliko pale ilivyokuwa mwaka wa 1995.
   
 20. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #20
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Politics ina mbinu nyingi sana..zipo safi na chafu na hata umafia hufanyika katika siasa so sioni kwanini tuumize vichwa wakati tunajua kuwa vita ilishaanza kitambo na yanayoendelea ni mapambano ya chini kwa chini kujaribu kunyimana usingizi na tunapoelekea Oktoba 31 ambapo mbivu na mbichi zitaonekana ambapo itafahamika kama kadi zilizorudishwa CCM zitaupa upinzani ushindi au la...pia ishu ya mdahalo uwepo usiwepo siku hiyo ndio itaamua kwa hiyo mi nadhani ishu ni mbinu gani itakuweka madarakani....watanzania walio wengi ambao ni wa kipato cha chini nathubutu kusema kuwa huwa wanaamuliwa mambo mengi na wachache wenye platform ya kusema mambo mfano ni hii mitandao ambayo nadhani ni tabaka la watu wachache ndio wana access na waliobaki wengi hata magazeti huyasoma ubaoni au kusikia chambuzi zake redioni.hivyo bado watapiga kura kwa itikadi za chama na kusapoti vyama vyao kwa hiyo kwao mdahalo si kitu muhimu, au kuwa flani kapata udhamini wa watu wangapi si hoja sana maadamu amefikisha kiwango kilichowekwa na tume ya uchaguzi..

  kwa hiyo nadhani mambo mengine ni mazuri kuyaweka kwa mijadala na mengine yanayohitaji utekelezaji nadhani walio wengi ambao hawashiriki hii mijadala kama huu ndio waamuzi wakubwa na ndio maana tunabaki kulia faulo kuwa kura ziliibwa au hili au lile kwakuwa huwa tunaamini tunawakilisha kilio cha kila mtanzania kumbe wao pamoja na kero zao bado wanapoenda kupiga kura hupigia kura mtu ''waliemzoea'' kwani zimwi likujualo... nadhani politics tunaijua so ni bora kujenga misingi bora toka vitongojini kitu ambacho CCM walifanya enzi tlipopata uhuru so wana base...leo hii chama cha upinzani hakina base nzuri kitongojini na kinaota kuitoa CCM madarakani..hizi ni siasa!!! tuambiane ukweli kuwa upinzani uweke madiwani wa kutosha,wenyeviti wa mitaa,na ndipo wabunge wao wataongezeka na hapo nathubutu kusema ndoto yao ya kutwaa taasisi ya Uraisi itatimia ambayo itawachukua miaka mingi kuitimiza.

  nadhani pia iko haja ya kuiga kwa wenzetu ambako pamoja na utitiri wa vyama vya siasa, vyama vinavyogombea si vyote na hii hutoa upinzani wa ukweli. mi namsifu sana Mtikila coz anajua kufanya politics hata kama chama chake hakina mbunge.. anajua nini afanye kwa manufaa ya Taifa kama ilivyokuwa kwa mgombea binaafsi na ameshinda kesi..wengine wanalia tu na kulalama utendaji wa serikali ya CCM. sawa wana haki kulalamika ila kuna mambo makubwa ya kufanya kama alivyofanya mtikila alipochallenge katiba kuhusu mgombea binafsi ambapo hiyo itatoa fursa kwa watanzania wenye uwezo kuomba kuongoza nchi kikatiba..

  ushauri wangu ni kwa watu kufanya siasa katika maana hasa ya siasa na tutasikia mengi kuhusu rafu kabla ya uchaguzi so hizi ni rasha rasha tu...upinzani waweke base nzuri vitongojini na watu wanaojitokeza kushangilia mikutanoni wawe kweli wameandikishwa na wapige kura coz watu hawapigi kura siku ikifika na hii ndio hufanya wengi tudhani kuna michezo imechezwa japo huwa kuna kaukweli kwa pande zote japo huzidiana ujanja
  lets be realistic..THIS IS POLITICS na tuzifanye katika definition ya Politics (yoyote tunayoichagua coz hakuna universal definition).
   
Loading...