CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Yaani, CCM wametupa kweli wajinga sisi watanzania!! Ili kuiondoa CCM lazima kuwe na chama kimoja tu cha upinzani ambacho itikadi yake ni ANTI_CCM, that is it.
Yaani kazi kweli kweli

Huwezi kuwa na chama cha itikadi ya anti-CCM! Ndio makosa makubwa ya upinzani uliopita; tunataka chama chenye itikadi ya kusimamia nini! CCJ ndiyo chama pekee kwa itikadi yake ni kinyume kabisa na zile za utawala uliopo sasa.
 

Mkandara, Katiba uliyoisoma ya CCJ ni katiba ya muda (provisional constitution) ili kukiwezesha kuanza kazi za kisiasa na kupata usajili wa muda. Mara baada ya kupata usajili wa kuduma Katiba mpya itaundwa na uongozi mpya wa kitaifa na kwenye mikoa utaundwa. Vyovyote unavyovisoma kwenye Katiba sasa hivi ujue ni vya muda tu.
 
Lakini hiyo ndio dira (msingi na malengo) ya chama hiki.. Hivyo katiba itakayofuata ni ktk kuweka taratibu za kisheria zinazojenga safari nzima kufikia malengo haya. Mkuu kama unataka kuwapeleka wananchi Canada kuhudhuria Caribana la msingi ni kuwafikisha wananchi hao huko. Nachopinga mimi ni pale CCJ wanaposema tutasafiri na chombo chetu wanaotaka kuja nasi waje wakitumaini watu wengi watawafuata hali upo usafiri mwingine. Tunacho shauri sisi ni kukaa kwa pamoja na kujadili safari hii kwa pamoja iwe kwa bus au ndege lakini sote tufike tunakotaka kwenda pamoja. Haya maswala ya vyama 14 vyote kufikiri wana nafasi ya kushinda (kufika) ni upotoshi mkubwa sana kwa sababu kila chama kinakuwa kinafikiria ushindi wa mtu mmoja mmoja kama usafiri binafsi wa kwenda Canada akichukua abiria wanaotaka kwenda naye. Mkuu tupande ndege moja tutafika sote, kama wewe una malengo ya kulala hotelini utalala hakuna anayekuzuia, ila waache wanaotaka kukaa kwa Mkandara wakakae wao - muhimu sote tumesha fika Canada...

Halafu kama sikosei tukumbuke kwamba mfumo wa uchaguzi ni mbaya na hasi kwa wapinzani..sijui kama kuna sheria ya mshindi lazima apate zaidi ya kura 51 kushinda..Winner take all unatugawa vibaya sana kiasi kwamba hata kama CCM watashinda kwa asilimia 40, CCJ kura 30, CUF 20 na vyama vingine kwa ujumla wake kufikia asilimia 60. CCM atachukua ushindi na kuongoza nchi hakuna cha serikali ya mseto. Hili tumeliona ktk uchaguzi uliopita huko Zanzibar tofauti na tulivyoona Uingereza. Kwa hiyo mfumo mzima wa uchaguzi ni against vyama vya Upinzani na the only way wanaweza kubomoa nguzo hii ni wao kuungana na kuunda team moja. Ni kwa ujumla wao tu wanaweza kuwa mbele ya CCM ktk uchaguzi kiyasansi..Hakuna habari ya ramli na bao (siasa nyingi) litakalo wawezesha.

Mkuu haijalishi kama CCJ itamsimaisha mtu kama Salim ambaye nampa kura zangu zote., bado atashindwa kuvuta kura za wana CUF, Chadema, NCCR na TLP jambo ambalo litaangusha nguvu kubwa ya upinzani. The only way Salim anaweza kumshinda Kikwete ni kugombea ndani ya CCM yenyewe since JK mwenyewe kaweka sheria ya mgombea kuchaguliwa na wanachama sio kamati za chama. Sheria hii pekee ndiyo inaweza kumgeuka JK mwenyewe ktk uchaguzi ndani ya chama chake akisimama mtu anayeaminiwa zaidi yake. Akigombea nje ya hapo ni lazima vyama vyote vya upinzani visimame nyuma ya mtu huyu laa sivyo itakuwa vichekesho... mark my word on that.
 
Mkuu huwa unafuatilia mjadala kabla ya kuposti? hiyo itasaidia sana.

Nafuatilia sana ndugu yangu ndio maana nikamuuliza kinaganaga kama ni mwanachama kwa kuwa analikimbia kiaina hilo swali - nioneshe alipolijibu kwa uwazi kabisa!
 

Tatizo ni kwamba huo usafiri mwingine hauendi tunakotaka kwenda au malengo yake siyo kama ya wasafiri sisi; sasa hatuwezi tu kudandia gari la wengine kwa sababu tu kwa kuja na gari letu wenyewe abiria wanaweza kuacha lile gari jingine. Kama watu wanataka kwenda kwa usafiri wa gari fulani na wanaamini madereva wake na huko linakotaka kwenda basi watu wana haki ya kupanda gari hilo. Ndio maana utaona hatuna sababu ya kupiga vita vyombo vingine vya usafiri.

Tunacho shauri sisi ni kukaa kwa pamoja na kujadili safari hii kwa pamoja iwe kwa bus au ndege lakini sote tufike tunakotaka kwenda pamoja.

Huu ndiyo ushauri ambao wengine tumeukataa mapema kwa sababu kila wenye magari wanajua wana safari zao na wanataka kwenda wapi. Kama hivyo vyombo vingine vinakubaliana na chombo chetu cha usafiri basi wao waje upande wetu kwanini sisi twende kwao wakati hatukubaliani nao?
Haya maswala ya vyama 14 vyote kufikiri wana nafasi ya kushinda (kufika) ni upotoshi mkubwa sana kwa sababu kila chama kinakuwa kinafikiria ushindi wa mtu mmoja mmoja kama usafiri binafsi wa kwenda Canada akichukua abiria wanaotaka kwenda naye.

Hili nalo ni tatizo; nyinyi mnataka tuungane ili "tushinde"; hii haiwezi kuwa sababu ya muungano. Kuungana kwa ajili ya kushinda kumetokea Kenya! Muungano kwa lengo la kushinda ni muungano katika udhaifu siyo katika nguvu.

Mkuu tupande ndege moja tutafika sote

Ni kweli tukipanda ndege moja sote tutafika lakini je sote tutafika tulikotaka wote kwenda? Maana tunaweza kupanda ndege tukafika sote Iringa, lakini kumbe wengine wanataka kwenda Mwanza, wengine wanataka kwenda Kigoma, Mbeya au Zanzibar! Sasa kupanda ndege na kufika kwa pamoja haina maana wote wanafika walikokusudia. Ni muhimu wale wanaotaka kupanda ndege ya kwenda Iringa na lengo lao ni kufika Iringa basi wapande ndege hiyo na kwenda Iringa; wale wanaotaka kwenda Mwanza kama hakuna ndege basi hata wapande mabasi na kuzunguka hadi Kenya au kukata Serengeti au kupitia ya Dodoma - Nzega.. Lakini kusema "wote" tupande ndege moja kwa sababu "wote" tutafika kwa "pamoja" hakuzingatii watu wanataka safari gani na ya kwenda wapi.

, kama wewe una malengo ya kulala hotelini utalala hakuna anayekuzuia, ila waache wanaotaka kukaa kwa Mkandara wakakae wao - muhimu sote tumesha fika Canada...

Ni kweli, lakini je ni wote wanataka kwenda Canada?

Ni kweli, lakini kama upinzani ukiwa na kura nyingi wanaweza (baada ya kushinda) kukaa na kuamua kuunganisha nguvu na kupiga kura kama kundi moja na hata kuchagua Waziri Mkuu. Katiba haisemi Waziri Mkuu ni lazima atoke chama kilichoshinda; inasema aidha atoke kwenye chama chenye wabunge wengi; au mbunge anayeungwa mkono na wabunge wengi zaidi!


Bado napinga muungano kwa ajili ya kushinda au kuiondoa CCM; huo ni muungano katika udhaifu. Muungano wa kweli ni lazima uwe muungano wa nguvu yaani itikadi, malengo, na mbinu za kuongoza. Nje ya hapo muungano haufai. Na kama muungano ungekuwa ni suluhisho wapinzani watanzania wangekuwa wamekwisha ungana sasa!


Mkuu haijalishi kama CCJ itamsimaisha mtu kama Salim ambaye nampa kura zangu zote., bado atashindwa kuvuta kura za wana CUF, Chadema, NCCR na TLP jambo ambalo litaangusha nguvu kubwa ya upinzani.

Hili si tatizo; huwezi kupata kura za watu wote. Lakini bado mnasisitiza sana "upinzani" I really don't think much about that.


I'm marking your words..
 
Mkuu hapa sasa ubabaisha kujaribu kuupangua mfano wangu kwa herufi kubwa.
Hakuna chama Tanzania chenye malengo nje ya safari ya kumkomboa Mtanzania, kuboresha maisha yake kiuchumi na kadhalika. Hata hao CCM wenyewe waliahadi haya, tatizo ni kwamba sisi sote tunataka kwenda nchi ya kusadikika. Hakuna kati yetu anayejua Iringa, Mwanza au Bukoba inafanana vipi nikiwa na maana hakuna Mtanzania hata mmoja anafahamu hivi vyama vitaweza vipi kutufikisha ktk nchi ya kusadikika. Hivyo napozungumzia Canada na shehere za Caribana ujue kwamba wasafiri wote hawajui hiyo Canada zaidi ya jina na picha za TV kisha hawaji Canada kwa sababu wanataka kuja Canada ila kuna sababu zaidi ya kusafiri tu. Ndege yetu ya CCM (chombo) imeanguka kisiwani na sisi survivors tunajaribu kutoka ktk kisiwa hiki baadala ya safari ya awali toka tupate Uhuru.. (sinema ya LOST).. So who U trust itachukua nguvu zaidi ya uzuri wa mashua, bus, dereva au tingo ila mpango madhubuti kulingana na wingi wa wasafiri wanaotaka wote waokolewe...

Haya maswala ya chaguo la mtu ni pale msafiri kisha fahamu Mbeya ni wapi tofauti ya Mwanza na Mbeya na unachukua usafiri upi rahisi...Kumbuka hii ni nchi ya Wajinga na Malimbukeni usifanye mzaha hata kidogo kwani sisi wote hatufahamu nini maendeleo zaidi ya kuiga yale tunayoyaona ktk TV, na isije kuwa kutofahamu kwetu iwe sababu ya kutuburuza kama CCM walivyotuburuza..
Nyote CCM, CCJ, Chadema CUF mnatupa picha ya usafiri mkitumia navigation system (katiba) mlo tengenezewa pasipo hata nyie kujua huko tuendako kunafanana vipi..Kifupi ktk hatua tuliyopo, mafanikio ya Mtanzania kwenda nchi ya kusadikika ni kuondoka ktk hali hii kwanza iwe hata kwa kudandia gogo..itachukua umoja wenu kuweza kumudu majanga ya kisiwa hiki cha LOST.
 

kama unayoyasema ni kweli kwanini vyama vya upinzani vilivyopo sasa visijiunga na CCM?
 

Jmushi1 usipende kuamini watu kabla hujajiamini wewe mwenyewe, utakuwa mtumwa daima! Kama hiyo itikadi ya chama unaiamini ndiyo itakayorudisha taifa katika mstari vipi usubiri wengine wafanye na wewe u free ride? Hiyo ni lack of confidence, a sign of fear and unboldness! I wish I could give my heart and impert into you the boldness that would make you dare to do what you believe is right to be done for your self first and for others.

Labda nikupe mfano, Mwl JKN alipotangaza vita vya Uganda alisema maneno haya bila ku nukuu sababu tunayo, nia tunayo na uwezo tunao wakumpiga adui yetu ambaye ni Idd Amin. Labda nikuulize je hiyo kweli ilikua imani ya watanzania wote? Je wote hatukuingia vitani? Na je garama ya hiyo vita ilikuwa juu ya Nyerere pekee au hata wale ambao hawakua na nia, sababu wala uwezo? What am I trying to say...

Hata kama hakua sahihi aliamini hivyo alivyo sema na kwasababu ya nguvu iliyokua ndani yake alisababisha wote tukafanya kama alivyo amini yeye and so we all did as he believed and said....Then he proved to be strong and he conqured the weak, how...Because he believed in HIMSELF and the power inside HIM and not into others....Thats what I exactly want every body of us to know.....If you believe differently then dont wait others to do what you believe in do it yourself for they might be believing differently..

Namheshimu sana Fred Mpendazoe kwani alisema maneno yenye msingi sana... kwamba hata kama hata fanikiwa katika yale aliyodhamiria kuyafanya bado hatajuta kwani amefanya sawa sawa na dhamira yake....Watch my words ni mara chache sana watu wenye imani kama hiyo kushindwa kwani yuko tayari kwa lolote and according to natural law because he does not fear anything then there is extra power to take him forward! Na hata kama atashindwa atakua amepanda mbegu ambayo haita kufa daima dawamu bali itakua taratibu na matunda yake yatafaidi wengine and thats what exactly Obama benefitted from...He had a reference from people like Luther King jr and the like... So to say better late than never...ONCE AGAIN JOIN US in the move to bring back the lost hope!
 
kama unayoyasema ni kweli kwanini vyama vya upinzani vilivyopo sasa visijiunga na CCM?
Kwa sababu ndege ya usafiri wetu CCM imeanguka, vyama vya Upinzani walikuwa na wasiwasi nayo toka mwaka 1992, wakati hawa CCJ wakiwa wahudumu na waajiriwa wa shirika hili. Sasa baada ya kuanguka ndipo tunapata mawazo mengine toka kwao ya kutuchanganya akili zaidi..Kumbuka mkuu wangu wewe unazungumza kama mwanaCCJ sijui kama umesimama kama mpiga debe au mmoja wa viongozi hali mimi nazungumza kama mwananchi nayetaka kuokolewa..Imani yangu mwananchi kwako ndiyo muhimu kuliko maelezo yoyote yale na lazima ujali zaidi hofu ya mwananchi kuliko fikra zako wewe..

Nitarudia kusema hivi ile ndoto ya Ushindi haiwezi kuwepo kama hakuna muungano wa vyama. CCJ could be anything.. pengine ni watu wa Lowassa, Mkapa, Sumaye who knows..au hata JK mwenyewe anataka kujiengua CCM ya wazee na kuunda wagombea wapya through CCJ kama alivyofannya yule rais wa Malawi. Kifupi Ujio wa CCJ unatuchanganya zaidi sawa na hiyo misaada inayotolewa hivi karibu ya uchaguzi kama ni takrima au ndio ilikuwa Ilani ya mgombea. Mkuu mnatuvuruga tu akili zetu kuweni wazi. wakweli na kutazama ishara za wakati na ushindi, haya maswala ya kila kila mtu na usafiri wake ni maswala ya kutafuta orodha ya wanachama sio ushindi kwa Taifa zima.
 
Chama ambacho kimedaiwa ni gelesha na kisicho na jina kubwa kinaendelea na wimbi lake la kushawishi wananchi kuweza kukikubali. Jana (Jumamosi) kilifanya mkutano wake huko Mbagala (katika kile kinachoitwa Meet and Greet - kuonana na kuwasalimu wananchi) ambapo Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Temeke pamoja wanachama kadhaa wa CCM na CUF wameamua kurudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na chama hiki chenye usajili wa muda kikiendelea kusubiri usajili wa kudumu.

Kuna nyaraka mbili za hotuba za kuwakaribisha watu CCJ. Zinajaribu kujibu maswali mbalimbali.
 

Attachments

  • HOTUBA KUWAOMBA WANANCHI 2.doc
    53.5 KB · Views: 129
  • HOTUBA CCJ 2.doc
    46.5 KB · Views: 139
Kwa sababu ndege ya usafiri wetu CCM imeanguka, vyama vya Upinzani walikuwa na wasiwasi nayo toka mwaka 1992, wakati hawa CCJ wakiwa wahudumu na waajiriwa wa shirika hili.

Karibu waanzilishi wote wa CCJ hawakuwa katika nafasi za uongozi wa CCM au kuwa wahudumu wa hiyo ndege.


Hili ni kweli.



CCJ siyo zao la kina Lowassa, Mkapa au Sumaye; siwezi kuwa meli moja na Lowassa au Mkapa! Na Kikwete hawezi kuhusishwa na CCJ kwani uwepo wa CCJ unatishia uwepo wa Kikwete madarakani.

Kifupi Ujio wa CCJ unatuchanganya zaidi sawa na hiyo misaada inayotolewa hivi karibu ya uchaguzi kama ni takrima au ndio ilikuwa Ilani ya mgombea.

CCJ haimchanganyi mtu yeyote; watu wanajichanganya wenyewe kwa sababu bado hawaamini kuwa CCJ ni wazo na zao la Watanzania wa kawaida kabisa waliochoshwa na siasa zilivyo sasa na ambao wameamua kuyaleta mabadiliko wanayoyataka wao wenyewe. CCJ haina matajiri wa kukifadhili, haina uwezo wa kulipa makada wake, na hakina uwezo wa kuweza kujenga maofisi makubwa au magari ya hapa na pale. Ni chama ambacho kinajengwa toka chini moja kwa moja. Ni wananchi wenyewe wanakijenga na ni lengo la CCJ kuhakikisha kuwa wananchi wanabakia nakuwa na nguvu ya kukisimamia.

Mkuu mnatuvuruga tu akili zetu kuweni wazi. wakweli na kutazama ishara za wakati na ushindi, haya maswala ya kila kila mtu na usafiri wake ni maswala ya kutafuta orodha ya wanachama sio ushindi kwa Taifa zima.

Napendekeza hivyo vyama vingine vijiunga na CCJ ili iwepo meli moja ya ushindi. Wafanye hivyo kwa hiari yao sasa ama sivyo watajikuta wanalazimishwa na historia.
 

Mkuu did you mean chenye usajili wa muda kikingojea usajili wa kudumu au? Because your statement seems vice versa.
 
Mkandara sorry am not trying to attack you but please bare with me....Hii ni mentality ya watu wengi kwamba kama yeye hana solution basi anadhani kila mtu yuko kama yeye...VERY WRONG!

Some of us are carrying dreams since our childhood ya jinsi ya kuitengeneza nchi tulikua tukitafuta opportunities tu and I believe am not alone wako wengi talented na wenye vision nzuri tu ambazo zinatafuta nafasi tu ya kuonyesha njia ili wengine wafuate. Tu ache tabia ya kugeneralise issues, tuwe wastaarabu if you think you can not do something better ask for others to help na hapo wenzetu wa dunia nyingine ndo walipotuacha mtu akiona hana uhakika na jambo ana admit this one is out of my capacity wenye uwezo wana take charge....

Even in the bible which is the only book of faith I know sorry for this I would have probably used other reference if I had... there was a prophet who told God that ...God I am the only one left in Israel and here I am they also want to kill me... God told Him come on....inside Israel I have more than 500 people who dont worship Baal...

Hi mentality ya kushindwa kwa mmoja na pengine wale anaowafahamu tu ndo wenye uwezo kushindwa na hivyo kudhani wote wameshindwa ni mbaya mno na ndiyo inayotusababisha tusitoke kwenye umaskini..... In Tz there are a lot of abled people to take us to a dream land!
 
duh.. sorry.. unajua tena wakati mwingine mawazo yanafikiria kinyume nyume.. .. masahihisho yamefanyika. Shukrani. Niwaache mjisomee hayo wakati naenda kuwaunga mkono wazawa hapa..
 
Kwa sasa nibakie kuwa ni mwanachama tu sina cheo chochote na sitamani cheo chochote zaidi ya kuwa mpiga prapaganda mkuu (in the tradition of Caville na Rush).
Mzee Mwanakijiji, let me be frank and open, numekuwa nikusoma muda mrefu nikajiridhisha wewe ni/ulikuwa CCM Damu.
Of late nimenotice change of heart against CCM, ila hili la kuwa mwanzilishi na mpiga debe wa CCJ, nalitafsiri kwa mawili
1. Kwanza: CCJ is for real, and its more that what we see and hear mpaka mtu wa calibre ya Mzee Mwanakujiji kujiunga. Ili nijiridhishe, its for real, natamani kuijua 'the motive behind Mzee Mwanakijiji ndani ya CCJ'.
2. Pili inawezekana kabisa Mzee Mwanakijiji ukawa uko Kazini, na hii piga debe yote ikawa ni sehemu tuu ya majukumu tuu ya kazi

Its just thinking aloud!,
 
Whether CCJ is for real or not is yet to be seen. I am a bit skeptical because of the history of opposition parties in Tanzania and also not enough exposure to the party and it's philosophy. Yes CCJ has it's philosophies on paper but so do CCM, Chadema, CUF and every other political party. On paper it is ok but I am yet to see the practicality of it all. After all they say you don't truly know your spouse until the day you marry them. So I'm waiting to see the performance of a few of their leaders who will be lucky enough to win representation.

Now beyond the above point I think it is going to take a while until CCJ truly establishes itself. So I'm not thinking of CCJ in 2010 but 2015. Will they attract charismatic leaders who can inspire people to rally around them? Can they practice what they preach? For the time being I think this Greet and Meet tour is a good idea but it should not only last while the party is in the process of getting registration. One mistake that our opposition make and I don't know why since it's basic politics is that you should constantly sell yourself to the people and not only during campaign season. Another thing I don't like about most opposition party is that they are easy to mention what CCM has not done or failed to do rather than saying what they plan to do and how they are going to do it.
 
duh.. sorry.. unajua tena wakati mwingine mawazo yanafikiria kinyume nyume.. .. masahihisho yamefanyika. Shukrani. Niwaache mjisomee hayo wakati naenda kuwaunga mkono wazawa hapa..

Nimesoma hotuba zote mbili ila ile ya kwanza inanipa wasi wasi kwani ina makosa madogo madogo ambayo ama yanaonesha kuwa waandisha hawakuwa makini au ni mwendelezo wa yale yale ya CCM. Hotuba ya pili ni nzuri pia ila imeishia hewani. Sikuona hitimisho lenye uzito ule ule kama ilivyoanza kwenye utangulizi.
 

Too emotional brother "sentamental"!
And the problem of this is you react instead of responding
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…