Ni vigumu sana kwa watu wanaoamini kwamba Unity inaweza kuwa ni Udhaifu..Kwanza ni Imani kisha unafuata kuelewa au kuelimika.labda tuna uwezo mdogo wa kukuelewa mkuu maana mawazo yako yamepita uwezo wetu wa kufahamu au kukuelewa; ila usikate tamaa kujaribu kuendelea kutufahamisha.
Ni vigumu sana kwa watu wanaoamini kwamba Unity inaweza kuwa ni Udhaifu..Kwanza ni Imani kisha unafuata kuelewa au kuelimika.
Kwa kuongezea tu nitakupa ukweli ambao wengi hatupendi kuuweka maanani leo hii. Waislaam waliutaka Uhuru wa Tanzania mapema lakini wasingeweza kufanikiwa pasipo support ya Wakristu. Ndipo walipokuja na plan ya kuwavuta Wakristu na mwalimu akapewa Uenyekiti.
"Kwa ujumla chama hiki (TAA) kilitokana na vyama vingine vidogo vidogo vya awali kama vile vyama vya kikabila. Buhaya Union huko Bukoba kwa mfano ndicho kilichobadilishwa na kuwa African Association. Mahali pengine kama Dodoma chama hiki kilitokana na kikundi kidogo cha wafanyakazi serikalini. Huko Zanzibar kilitokana na juhudi za wasomi waliotaka kuunganisha Wakristu na Waislamu"(Labda huu ndio ‘ukweli' unaozungumziwa). "Hadi kufikia mwaka 1940 Chama hiki (TAA) kilikuwa kimeanza kushughulikia mambo muhimu ya kisiasa kama vile kutaka Waafrika wapate sauti katika serikali. Baada ya vita vya Pili vya Mabeberu madai ya Chama hiki yalilenga zaidi katika kupata wanachama wengi kutoka kila sehemu ya nchi, wanaume kwa wanawake. Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Dodoma tarehe 29 Machi, 1945 iliamuliwa kuwa juhudi zifanywe kuhakikisha kuwa katika kila mji mkuu wa jimbo kunakuwa na tawi la African Association lenye nguvu. Jukumu hili liliendelea hadi 1948 wakati Chama hiki kilipogawanyika katika matawi mawili – la Tanganyika na la Zanzibar. Tawi la Tanganyika liliitwa Tanganyika African Association (TAA) na la Zanzibar likaitwa African Association – Zanzibar…….
Baada ya vita Tanganyika iliendelea kuwekwa chini ya Baraza la Udhamini ikiangaliwa na Uingereza. Waingereza walijaribu kuleta mabadiliko kadhaa katika mambo ya uchumi na siasa ili waonekane kuwa wanaiendeleza Tanganyika. Kisiasa, kwa mfano, walijaribu kuwaingiza machifu ambao hawakuwa wawakilishi halisi wa wananchi…… Katika uchumi pia Waingereza walianzisha miradi mingi bila kufanya utafiti kamili hivyo kuwakera sana wananchi. Upinzani kama ulivyotokea huko Upare wakati wa Mbiru, au ule wa Wahehe kukataa kuogesha ng'ombe zao, au umoja wa Waluguru katika kupinga juhudi za kuhifadhi mapori na kulima matuta inadhihirisha kwamba ilipokaribia miaka ya 1950 wananchi walikuwa imara kukabiliana na wakoloni….
Chama cha TAA kilitumia mambo haya yote katika kuwaunganisha watu na kuwaelekeza pamoja katika kutafuta haki zao. Juhudi hizi ziliendelea katika kila jimbo hadi mwaka 1953 ambapo kulifanyika mkutano mjini Dar es Salaam na Mwalimu Julius K. Nyerere akachaguliwa kuwa kiongozi wa TAA. Kwa wakati huu TAA likuwa bado haijaweka madhumuni yake wazi ya kupigania uhuru hivyo Mwalimu Nyerere alipopendekeza umuhimu wa kuandaa chombo cha kupigana na mkoloni wajumbe waliafiki na kumpa kazi ya kuandaa katika ya Chama, Mkutano wa mwaka ulifanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 7 hadi 9 Julai, 1954 na kuhudhuriwa na wajumbe kumi na saba. Wajumbe hao ni:
1. Julius K. Nyerere – Rais wa Chama
2. Germano H. Pacha – Jimbo la Magharibi
3. Joseph Limalando – Jimbo la Kaskazini
4. Abubakari Ilanga – Jimbo la Ziwa
5. Said Kitwana – Jimbo la Ziwa
6. Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
7. C. Millinga – Jimbo la Mashariki
8. L. Makaranga – Jimbo la Ziwa
9. Saadani Kandoro – Jimbo la Ziwa
10. Kisung'uta Gabara – Jimbo la Ziwa
11. Saidi Tewa Saidi – Jimbo la Mashariki
12. Dossa Azizi – Jimbo la Mashariki
13. Ally W. Sykes – Jimbo la Mashariki
14. Patrick P. Kunambi – Jimbo la Mashariki
15. Joseph Kassela-Bantu – Jimbo la Mashariki
16. Abdul K. Sykes – Jimbo la Mashariki
17. John Rupia – Jimbo la Mashariki
Wajumbe wa Chama hiki cha TAA walikubali kukibadilisha jina lake na kuitwa Tanganyika African National Union (TANU)".
Kwa kuongezea tu nitakupa ukweli ambao wengi hatupendi kuuweka maanani leo hii. Waislaam waliutaka Uhuru wa Tanzania mapema lakini wasingeweza kufanikiwa pasipo support ya Wakristu. Ndipo walipokuja na plan ya kuwavuta Wakristu na mwalimu akapewa Uenyekiti.
Turudi kwenye mada yetu...Hakuna zaidi ya kuwaondoa CCM madarakani..Kama lengo lenu CCJ sio kuwaondoa CCM madarakani why form a party 18 years after demokrasia imetangazwa?. Again utasema pengine hiyo ITIKADI yenu, hapa mkuu nataka kujua hiyo itikadi itafanya kitu gani tofauti ikiwa CCM wataendelea kuongoza nchi?Ni lazima kuwe na mambo fulani ya kuunganisha. Zaidi ya kuondoa CCM madarakani ni vitu gani vinapaswa viwe msingi wa muungano wa upinzani Tanzania?
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu maneno yako ni pamoja ya kudhihirisha kwamba Ukweli huo hupendi kuiwekea maanani kama nilivyotanguliza usemi wangu.. Ni kitu gani kinachokufanya ufikirie kwamba Wakristu walikuwa hawataki Uhuru?.. Mkuu wangu naanza kufikiria kwamba wewe unavuta fikra za Udini mbele ya ukweli.
ehe!Kipengele cha B hadi mwisho ni uzushi wako mwenyewe... Ni fikra zako duni tu (Inferiority complex) mkuu wangu ktk udini kwa sababu hapa tunazungumzia Uhuru wa nchi nzima ambapo kulitakiwa uchaguzi wa nchi nzima na kulikuwa na masharti yake kama haya ya leo mnayojiandikisha ambayo ushindi usingewezekana kwa TAA pasipo kuwaunganisha nguvu za Wakristu hasa kutoka bara ili kupata kura za wananchi za kutosha.
This is very interesting; wewe ukizungumzia mambo ya dini (kwa jina la ukweli excluding all others) ni kuwa uko objective. Mimi nikigusa mada hiyo hiyo na kudai ukweli ninakuwa mdini! Unataka tuamini kuwa wewe katika kuzungumzia kile unachokiita "ukweli" basi ur the only undisputed authority katika mambo haya ya "historia" na mtu mwingine akijaribu kuyapinga basi ni "mdini".Pengine rudia kusoma ile mada tulowahi kuizungumza sana humu - WATU MUHIMU KTK HISTORIA YETU. Utagundua ukweli na kwamba mimi sina fikra za kidini ila kuutafiti ukweli wa historia ya harakati za Uhuru wetu..
Mzee Mwanakijiji,
Katika maelezo yangu, I can back up na fact na ndio maana nimekuomba usome mada ile ya Watu muhimu ktk Historia yetu. Sikuandika mimi habari hizi wala kutunga historia. Unaweza kwenda library, kukutana na historian kutafuta ukweli. Na kama utapata majibu tofauti njoo hapa tuzungumze na sio kuandika hisia zako kwa kufikiria Mkandara alikuwa na maana hii. Nimekwambia sikuwa na maana hata moja ya maandishi yako uloandika bado unasema oooh mimi ndiye undisputed authority... nimesema wapi hivyo. Yote uloandika hapo juu toka kifungu B hadi mwisho ni maneno yako mwenyewe ambayo wewe pekee ndio unaamini hivyo na hata umefikia kusema Bibie Ntilie alikuwa na maana hiyo. Wee nani kusoma vichwani mwa watu? Labda unataka kunambia Bibie Ntilie ni wewe mwenyewe.. Nitarudia niliyoandika mwanzoni sikuwa na maana uloandika wewe hata chembe ni unyonge wako mwenyewe wa kutojiamini.
Mkandara, kwanini vyama vilivyoop vya upinzani visiungane au kwanini vimeshindwa kuungana? na kwanini bila ya CCJ haviwezi kuungana bado?
Mkandara, nafuatilia majadiliano haya kwa makini sana, ila pia huyu Bibi Ntilie anazama deep in very interesting way haswa anapokuja kuwa backed.Mzee Mwanakijiji, yote uloandika hapo juu toka kifungu B hadi mwisho ni maneno yako mwenyewe ambayo wewe pekee ndio unaamini hivyo na hata umefikia kusema Bibie Ntilie alikuwa na maana hiyo. Wee nani kusoma vichwani mwa watu? Labda unataka kunambia Bibie Ntilie ni wewe mwenyewe.. ni unyonge wako mwenyewe wa kutojiamini.
Mkandara, nafuatilia majadiliano haya kwa makini sana, ila pia huyu Bibi Ntilie anazama deep in very interesting way haswa anapokuja kuwa backed.
Kufuatia interest zangu kwake, (Bibi Ntilie), nikamsoma kidogo baadhi ya post zake za nyuma nikazikuta very interesting. Nothing is imposible under the sun!.
Huu ubishi na upinzani wa kukataa general premise ya 'Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu", unanipa posibility ya baadhi ya wapinzani hawana lengo la dhati la ukombozi, bali ama wako 'kazini' kutimiza wajibu wao, ama wanapigania nafsi zao katika mwelekeo wa kutapata kujizuia wasizame, hivyo wako tayari hata kukumbatia chelewa (CCJ) na kuyaepuka mabua (Chadema, CUF, etc ) ambayo tayari yanaelea (Vimeshasajiliwa).
Ukitapatapa kwenye maji na kujifariji kwa kukumbatia chelewa, ni hakika utazama!.
Tuendelee na mjadala.
Itikadi ni ya mlengo wa kulia, nitafafanua zaidi wiki ijayo: Kwa ufupi:
- Limited but responsible government
- Minimal gvt spending
- promotion of free enterprise
- Self - Reliance
- African Socialism as corrected by the new understanding in economics, social justice
- Rule of law
- Restoration and promotion of founding principles of our nation(among them equality of status, accessibility to wealth and of opportunity, african unity - we are not afraid of Kenyas or Ugandans!, etc)
- Defense of the traditional family
- Absolutely and categorical opposition of all forms of exploitation of man by man!
- Fighting for the rights of workers and peasants of our country to give them opportunity to prosper in the globalized economy.
.. na mengine mengi..
kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!
Huu ubishi na upinzani wa kukataa general premise ya 'Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu", unanipa posibility ya baadhi ya wapinzani hawana lengo la dhati la ukombozi, bali ama wako 'kazini' kutimiza wajibu wao, ama wanapigania nafsi zao katika mwelekeo wa kutapata kujizuia wasizame, hivyo wako tayari hata kukumbatia chelewa (CCJ) na kuyaepuka mabua (Chadema, CUF, etc ) ambayo tayari yanaelea (Vimeshasajiliwa).
Ukitapatapa kwenye maji na kujifariji kwa kukumbatia chelewa, ni hakika utazama!.
Tuendelee na mjadala.
Kwa huu mchanyato wa ki-ideolojia hapo juu ninacoclude kuwa CCJ is just another mediocry, bigoted, populist, oppurtunistic gang to ensure UFISADI ENDELEVU....
Omarilyas
Msingi wa muungano uwe ni kuwaweka watu hawa pamoja, kujenga mazingira ya watu hawa kujiunga na chama na kujisikia ni sehemu na wadau wa movement hiyo katika kuleta mabadiliko wanayoyahitaji ndani ya nchi yao, lakini hili kufanyika SIO LAZIMA kuunganisha vyama bali kujenga imani na matumaini ya watu hawa kwa chama, na kwa viongozi wa chama chao.
Wakati mwingine gharama za kuunganisha vyama ni kubwa sana kuliko kuanzisha harakati mpya.