Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Hebu tungalie scenario tofauti kidogo na natanguliza samahani kama mfano wangu huu utawakwaza wengine.

Tuseme jioni moja habari zikiambatana na video za mapadre ama maaskofu zionyeshwe kwenye luninga wakifanya mkutano wa siri. Hakafu taarifa ziseme walikuwa wanasuka mpango wa kukashifu uislamu na kuleta machafuko nchini. Nilicho na uhakika nacho ni kwamba mimi kama mkristo ningekuvwa wa kwanza kuungana na wananchi wengine kuwalaani hao maaskofu.

Je, wanaopinga habari iliyotolewa na Mkjj wangekuwa na subira ya kutaka hiyo habari iwekwe kwanza kwenye you tube ndio waiamini. Bila shaka maandamano yasiyo na mfano wake yangetanda kila kona ya Dar es Salaam na nchini kwa ujumla kulaani kitendo hicho na kuwasomea al badiri. Huo ndio ukweli.

Sidhani akina Mkandara na Game Theory wangejitokeza na kuwatetea maaskofu hao na kudai ushahidi zaidi kwanza, I really doubt that. Hii ndio tofauti kubwa kati yangu na mawazo mengine ninayoyasoma humu ndani.
 
To tell you the truth.. nimerudi na kusoma taarifa niliyoripoti kwanza na kuirudia mara kadhaa kuona ni kitu gani ambacho ningekisema tofauti sijakiona. Nasikitika kuwa watu wamesoma zaidi ya kile nilichosema.

a. Sijadai katika taarifa yangu kuwa ndugu hao waliokutana wamevunja sheria yoyote.
b. Sijadai katika taarifa yangu kuwa walikuwa wanakutana kwa "siri" (nilionesha tu wapi walikokuwa wanakutana)
c. Sikudai hata mahali pamoja kwamba walichokuwa wanapanga kilikuwa ni kitendo cha kihalifu. Nilichotaja na wao wenyewe wamekithibitisha ni mpango wa kueneza propaganda ya msingi wa kidini na kikabila (kitu ambacho wao wenyewe wamekikubali)
d. Hakuna mahali popote ambapo kwenye taarifa nimesema kitu chochote dhidi ya dini ya Uislamu au uenezaji dini ya kiislamu kwani ni haki ya kila muumini kueneza dini.
e. Nilichozungumzia ni muelekeo wa mpango huo na hasa zinapokuja fedha na watu wanaposhindana kuhusu fedha kutekeleza mambo hayo na zaidi hasa baadhi ya majina ya watu mbalimbali muhimu kutajwa kama Emmanuel Nchimbi.
f. Kama taarifa hiyo isingetoka tulivyoitoa jana, jana kungekuwa na mkutano wa waandishi wa habari kuhusu yale waliyoyaazimia na hivyo taarifa ile ime preempty mpango huo.


Hata hivyo, kwa vile ni mpango waliokubaliana na wao wenyewe wameuthibitisha sidhani kama wanahitaji kubadili njia. Walichoamua waende wakitekeleze tu lakini Watanzania watakaposikia tuhuma zinatolewa na watu wa kundi hili (la kina Mazinge) wasishtuke au kusema kuwa viongozi wa "Kiislamu" wanadai x,y, na z.

Kama kuna Muislamu yeyote anafikiri au anaamini kuwa taarifa yangu ni dhidi ya Uislamu au Waislamu nchini naomba radhi kabisa kawni siyo lengo langu ukizingatia kuwa baadhi ya watu waliofanya operesheni hiyo ni waumini wazuri tu wa dini ya Kiislamu ambao hawakufurahishwa na mkakati huo.

Inashanagaza watu hawakujiuliza kama mmoja au zaidi ya mmoja wa wahusika wanaotajwa ndiye aliyevujisha habari hii kwa sababu hakupenda kinachoendelea.. well I'm just saying..
 
Mag3,
Mkuu hapana tusidanganyane hapa, hakuna mtu angekubaliana na habari ambayo haina ushahidi wa maneno wala maandishi (nakala ya mkutano) ama kuhojiwa kwa m/wahusika. Mkuu hivi kweli mimi naweza kukaa nje ya kanisa nikatoa habari kuhusiana na kanisa na UDINI, watu mkaamini hata kama nimeitunga!..
Kama tungekuwa huku Majuu ningeamini wka sababu kuna sheria za utoaji habari. Ama kipindi cha Intertainment wakitumia maneno kama rumors na kadhalika nigepima pia na udaku unajulikana kuwa udaku.
Wakuu wangu, pengine watu tunatofautiana lakini mimi kufikia kuamini jambo hasa ktk maswala mazito kama dini, rangi na jinsia sii rahisi kabisa na siwezi kumshutumu mtu kwa udini, ukabila, jinsia hata kama nakisia mtu huyo anao siwezi kabisa... Ni hadi pale atakapo utumia iwe kwa kauli ama vitendo ndipo nitakapo sema, nina ushahidi mbele ya maelezo yangu.

Kumbuka mkuu wangu Nyerere kalaumiwa mara ngapi kuhusiana na UDINI lakini wachache tumeamini kwa sababu hatukuona ushahidi wowote wa habari hiyo.. mifano kibao imezungumzwa lakini binafsi hadi kesho siamini wala sintakubali kuwa Nyerere alikuwa mdini.. Na sababu kubwa sijaona ushahidi tosha wa kunifanya niamini. utunzi na usanii ndio hujengwa kwa kutumia historia na pia dini yake. Huyo huyo Nyerere angekuwa Muislaam wasingesema kitu na wangeona mabaya yote aliyoyafanya ni ktk Uongozi..
 
..this guy MTAWA ...Ndio aina ya washauri wa rais ambao wanawaharibia wale washauri wa kweli wenye elimu zao ....huyu jamaa muungwana ametoka naye mbali ...tangu anakuwa waziri .......HUYU NDIO MWENYE SIRI NYINGI ZA MUUNGWANA...na mikakati yote ya ajabu ajabu ya muungwana amekuwa akiitekeleza yeye au kufuatilia...

..kuanzia kukuwadia..,kutunza nyumba zilizotapakaa na kufanya surveillance..HADI KUWAPANGA KALUMANZILA..kimsingi ni "MSHAURI WA KAMATI YA UFUNDI NA MAMBO YASIYO RASMI YA RAIS"

...kama kuna mtu an wasifu wake kamili auweke hapa!
 
Mwanakijiji,
Unataka turudi nyuma for nothing kabisa..tusingekuwa tunazunguimzia swala hili kama vitu hivyo visingekuwepo.. usitufanye sisi sote wajinga sasa..
Haya ngoja nikuonyeshe..
1. Kuhusu kuvunja sheria na Usiri:- ulipoanza tu habari umesema
KLHN yaweza kuripoti kwa uhakika kabisa kuwa mpango wa kuanzisha uchafuzi wenye mlengo wa kidini na kikabila nchi umeundwa na sasa umefichuliwa.
Hakuna habari ama mpango unaweza kufichuliwa kama haikuwa siri..Uchafuzi wenye malengo ya kidini na Ukabila ni uvunjaji wa sheria..Habari za vijidudu na kunasa sauti na video yote hiyo inaonyesha kulikuwepo usiri mkubwa ktk mkutano huo wakati wewe mwenyewe umesema maswla ya OIC na mahakama ya kadhi hayakuzungumziwa...
2. Kitendo cha Uhalifu:-
Mkuu bado maneno yote yamejenga hoja hiyo toka mwanzo hadi mwisho.. na kama nilivyosema habari uliyoandika ina sehemu mbili. Ya kwanza ni hiyo ya Mkutano unaohusu OIC na mahakama ya kadhi kisha ukaendelea na issue ya pili ambayo umeiwekea agenda za mkutano tofauti na hizi za kwanza..Hivyo musa mwingi umeutumia kuzungumzia agenda za pili kuliko mkutano wenyewe unaohusu OIC na mahakama ya kadhi na kwa bahati mbaya watu wamedakia na kuzungumzia zaidi OIC na mahakama ya kadhi bila kujua kwamba mimi nilikuwa nazungumzia issue ya pili..
Baadaye hata mimi nikaja gundua athari hiyo kuwa hata issue ya OIC na mahakama ya kadhi imeonekana kuwa siri na kuna mambo yamejadiliwa ambayo yanajenga Udini..
Mkuu nimeshasema sana kuwa nakuaminia sana lakini mara habari kama hizi zichunguze kwanza..Field Marshall ES, huwa anaweza kaa na habari hata mwezi mzima akizipinduapindua kutafuta ukweli kisha hutafuta hata watu wa ndani kupata uhakika, na akija zitoa hapa watu tunagongana kwa sababu wahusika na yale yanayokusudiwa vinatisha na uwezekano ni mkubwa... lakini hii habari ya hawa masheikh wote uliowataja na habari yenyewe ukiitazama hawana hata Ubavu kama viongozi wa dini ila viongozi wa chombo cha kidini kilichoanzishwa, pengine hufahamu kuhusu Uislaam...Zaidi ya hapo walikuwa kweli na mkutano kama kawaida ya miaka yote...Nakama hukuwa na maana mbaya imekuwaje uzitoe hapa JF kuna habari gani nzito ya kutoa ikiwa yote uliyoyasema hapo juu hayapo!
These guys are nobody ni waumini tu kama wewe na mimi zaidi ya kuwa na elimu ya dini..Viiongozi wa Bakwata, mimi nawaona kama Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) yaani kitengo cha CCM tu..Ungenambia Mufti labda kidogo ningekubali lakini hata yeye hana ubavu wa kuwashawishi waislaam wote..isipokuwa ushawishi unaweza kutoka upande wa pili yaani wanaoupiga vita Uislaam.
Mwisho, Pengine tunasoma taarifa mbili tofauti ila nakuomba kitu kimoja rudia kusoma taarifa yako kisha pale ulipoandika waislaam weka wakristu, Masheikh weka mapadre labda utaweza kuona maanake kukaa nje ya kabati umeshindwa!..
Yawezekana kabisa wanawake wakashindwa kuelewa feelings za wanaume inabidi wote mkia kwanza ama issue walipeke kwao!
Mama huwa anasema hana wivu lakini asione kimwana mwingine akicheza slow dance na mimi (hasema wanaume hatuaminiki), lakini yeye akicheza na mwanamme haoni kosa kwa sababu yeye ni mwanamke anajiamini..yet mtu anayecheza naye ni mwanamme asiyeaminika kama mimi..
 
kuna mtu yoyote anayeweza kutuambia nini sababu zilizopelekea hadi mkutano ambao haukuwa wa siri, wa dini fulani, kurikodiwa kwa SIRI?

habari ya Mwanakijiji ina lengo la kuonyesha uwepo wa mkakati wa uchochezi ( ambao ni uvunjaji sheria) wakati kimsingi, kila mtu ( licha dini) ana haki ya kujadili OIC, Mahakama ya Kadhi na Ukabila Tanzania. na sote tumekuwa tukifanya hivyo.

iweje kuwa watu wanafanya mikakati ya kazi zao (kuhubiri dini na kujadili mambo ya jamii) ichukuliwe kuwa ni jambo la kuogopwa na kupewa jina kubwa sana uchafuzi wa nchi.

na kwa yule aliyesema huyu jamaa marwa ni extrimist kwa kuwa kafungua redio station ya dini yake .........amenishangaza mnooooo!!
huu u-extrimist unakuja kama redio imefunguliwa ya kiislam tu? .....
makubwa
 
Mie nilisema toka jana,

Hii nijanja ya nyani ya watu wa CHADEMA kujitafutia umaarufu,Na huyu Mengi anatafuta balaa..Yeye badal a ya kuangalia biashara zake ameanza kusema wattu wanamtafuta.Who is he by the way?

Mwanakijiji,Ushabiki wa kushadadia mambo utakuja kukutokea puani siku moja.Zinduka na unaendelea kutumiwa bila kupima habari

Zitto,Operesheni Mwibara a.k.a operesheni Sangara mbona imesimama?au mnasubiri tarehe ya Uchaguzi?

Yeye amekuwa akimdhamili Mbunge wa Vunjo kuwachafua watu wengine watu wamekaa kimya.

Mie naona ni bora wasomewe Dua tu
 
Mie nilisema toka jana,

Hii nijanja ya nyani ya watu wa CHADEMA kujitafutia umaarufu,Na huyu Mengi anatafuta balaa..Yeye badal a ya kuangalia biashara zake ameanza kusema wattu wanamtafuta.Who is he by the way?

Mwanakijiji,Ushabiki wa kushadadia mambo utakuja kukutokea puani siku moja.Zinduka na unaendelea kutumiwa bila kupima habari

Zitto,Operesheni Mwibara a.k.a operesheni Sangara mbona imesimama?au mnasubiri tarehe ya Uchaguzi?

Yeye amekuwa akimdhamili Mbunge wa Vunjo kuwachafua watu wengine watu wamekaa kimya.

Mie naona ni bora wasomewe Dua tu


jamani kikundi cha dini walikuwa wanadiscuss ukabila hivi dini zetu zinaangalia kabila Ehee Mungu wakumbushe kwamba uliwatuma waje waaelekeze watu duniani ili waweze kufika peponi na wala si kuangalia kabila, rangi wala sura.kuna mambo mengi ambayo wangetakiwa kuongelea kama gonjwa la ukimwi kutokana na watu kukiuka maadili, ufisadi, na jinsi ya kumrudia allah,
sasa totaanza kuongelea kabila linalongoza tuangalie je wanavyeti vinavyostaili? angalieni tukimaliza kabila tutaangalia dini inayoongoza maofisini then tutafika wapi jamani..... kuonekana kwenu isijekuwa ni ishara Mungu alitaka kuwaonya kwamba huko siko..........................MUNGU UTUHURUMIE SISI WATANZANIA NA UWAADHIBU WOTE WANAOTUMIA NJIA YA DINI KUARIBU AMANI YETU KWAKUWA WEWE UNAJUWA MAWAZO YAO NA NIA ZAO
 
Waberoya said:
Mzee, kwa hiyo wengine wana mbinu za kihunihuni!!

Ok, naomba utueleze hatua utakazichukua pindi utakapoona kideo na kuhakikisha kuwa waliomo ndio hao tunaowasema! achililia mbali kuwa hujatumia nguvu hizihizi kutafuta ushahidi wa EPA,RICH.....

Waberoya,

..nimeelekeza kwamba habari hii ingewahusisha viongozi wa dini peke yao nisingejisumbua kuuliza maswali niliyouliza.

..lakini hapa ametuhumiwa mtumishi wa umma, msaidizi, na mtu wa karibu sana, wa Raisi wetu.

..ndiyo maana naomba ushahidi zaidi, na kuuliza maswali yote haya yanayoelekea kuwakera.

NB:

..nimetaja uhuni niki-relate ile sakata ya Chenge na ushirikina bungeni.

..labda ukirejea mjadala ule utaelewa kwanini nimetumia lugha niliyotumia.
 
dini zinafaa na kupaswa kujadili ukabila kwa sababu dini zinasema kuwa makabila yote sawa, hakuna lililo bora kuliko jengine.
na dini zinatakiwa kufikisha ujumbe huo kwa wafuasi wake wote.........na pia kutetea haki ya makabila yale yanayoonewa.
sidhani kama dini kujadilia ukabila na makabili ni kosa kimsingi, labda tuseme kosa linakuja njia zinazotaka kutumika kuondoa huo ukabila.
 
Yebo Yebo,
Naona watu mnazidi kupotosha hoja hapa...
Kwanza kabisa habari imezungumzia waislaam kukutana kuzungumzia maswala ya OIC, mahakama ya kadhi na Ukabilai hiyo ndio tuseme ilikuwa agenda ya mkutano.. Hilo halina taabu kabisa kwangu na wala sio jambo tunalolipigia kelele unless nyie ndicho kilichosumbua... Na nimesema itakuwa ajabu ikiwa kuwepo kwa mkutano huo unaohusu OIC na Mahakama ya kadhi ndio imebeba kichwa cha hoja hiii yaani Mkakati wa Mamluki Wafichuliwa na maswala ya Udini..kwani ni maswala haya nyote huko nyuma wakati tunazungumzia kupitia serikalini mlipinga sana na kudai yabakie ya dini inayohusika... Hivyo maswala haya hayakuwa ktk huo mkutano wa siri..

Niliposoma report ya Mwanakijiji nilijua haikuwa Udini mkusanyiko wa hao viongozi kuzungumzia maswala ya OIC na Mahakama ya kadhi kama mlivyopendekeza isipokuwa kuna jingine lililojificha ndani ya mkutano wa siri ambalo ndilo linaleta Udini..


Hapa ndipo Utata wa habari nzima umeanza na kama utasoma maelezo ya viongozi waliohudhuria mkutano ule wamesema walikutana kweli, hakuna kati yetu aliyesema hawakukutana. Kulikuwepo na Mkutano kweli Ijumaa hakuna aliyepinga isipokuwa kichombezo kilichoongezwa ambacho ndicho kimewaudhi wengi iwe kwa kuunga mkono ama kupinga Utunzi wa hizo hadithi za Mkakati wa Udini na Ukabila walengwa wakiwa Mengi na Mbowe katika maswala ambayo hata sielewi mwanzo wake.

Labda wenzangu mnafahamu vizuri swala hili tuambieni huo Ukabila unamhusu Mbowe na Mengi umeanza wapi? Kama ni Chadema hawa viongozi wa dini sio wanachama na haiwahusu ktk dini kwani hiki ni chama tu... tutajadili sisi hapa JF kwa sababu kuna nafasi ya kutazama pande mbili za shilingi..Ni mjdadala.. Iweje watu wakutane, kisha waandishi wa habari wawafuate hadi Hotelini kwa usiri ikiwa kweli nyie mwenyewe hamna matatizo na mkusanyiko huo!.. Je, ni mara ya kwanza wamekutana? hapana iweje leo iwe swala la kufukuziwa hadi video huku mkidai kwamba wao ndio wadini kufanya mikutano ya siri hotelini na mkajenga hadithi nzima wakati hamkuwepo hata karibu na mkutano huo wa siri!.

Haya naona tena kumezuka swala la Waislaam kususia IPP/ITV, sasa mlitaka wataje chombo gani ikiwa habari hii imetolewa na vyombo hivi, kisha kwa nini mnafikiria anayetakiwa kuomba radhi ni Mengi na sio mwandishi/editor, msemaji/mwandalizi wa kipindi hicho!..Yote hii inatokna ana habari iliyotanguliwa kama jina la Megji lingeandikwa ktk taarifa iliyotangulia mngesema Megji wakati hakuna sehemu hata moja jina la Mengi limetajwa..Hili jina limeibuka wapi kama sio kutokana na hadithi ya Mwanakijiji..
Na kuhusu mahakama, mbona hata Marekani na nchi za Ulaya kuna habari za Uongo hutolewa ktk TV na watu wakataka kuombwa radhi bila kwenda mahakama!..na hata siku moja hakuna mtu aliyefikiria kwamba mlengwa ni mmiliki wa kituo hicho cha habari..Hii sheria ya kwenda mahakamani inatoka wapi? hata mimi kuna watu nimeshaomba samahani ama kuwaambia waombe samahani kwa maneo waliyosema na sikufikiria kabisa kuwa mahakama ndio sheria. Hapa JF kila siku watu tunaombana samahani mbona hamsemi waende mahakamani?.. Jamani vipi akili zetu zinaanza kuganda ama! Inashangaza sana..

kumbe na wewe ulikuwepo??( Hapa ndipo Utata wa habari nzima umeanza na kama utasoma maelezo ya viongozi waliohudhuria mkutano ule wamesema walikutana kweli, hakuna kati yetu aliyesema hawakukutana.)tuashukuru kwa kutuhakikishia mkutano huo haukuwa na matatizo, hivi kazi ya mapaparazi ni nini? nilifikiri ni kutafuta habari na kutuhabarisha kwa hiyo yaliyosemwa kwenye habari si ya kweli inabidi washitakiwe ili next time wengine waweze kuwa na habari za kweli na sio kuomba msamaha YALE YALE YA EPA WARUDISHE FEDHA, YANI WATANZANIA BWANA TUMEFANYA NCHI YETU KAMA NYUMBA YA KUPANGA.
 
Sasa baada ya siku saba mkisikia habari ni hii itakuwa ni kwa sababu ITV wamekataa kuomba radhi au kwa vile uamuzi huo tayari ulishachukuliwa? Kwanini wasitishie kwenda mahakamani kama wanavyofanya wengine?


Kwani wamekwambia wanaitambua mahakama unayoijua wewe? Wao wanataka mahakama ya kadhi!


Waliokuwa wanaitaka mahakama ya kadhi sikuwa naelewa kwanini wanaipigia debe kwa msuli, hali kadhalika, sikuwa naelewa kwanini wengine walikuwa wanapinga. Hii ni noma washkaji!




.
 
Mkandara is a man!! amebakiza kujilipua na kwenda peponi! maana kama kila jambo linamgusa yeye na dini yake na siyo watanzania majirani zetu na ndugu zetu, kilichobaki ni nini? maana hawezi akapingana na ukweli, wakati mwingine kuna mambo ya kukaa kimya. waliosema taarifa hii ni ya uongo hatuwaoni tena......wenyewe wamekubali, walikuwa wanaongelea mambo ambayo serikali imesema wanayafanyia kazi!! hotelini siyo msikitini! wakiwa na maafisa wa ikulu!

Ili mnalo!!

waberoya
 
HEBU tuweke kumbukumbu sahihi, na waliotizama ama kusikiliza ile habari ya ITV usiku wa Jumatatu saa 2.05 na saa 4.40 pamoja na Jumanne asubuhi watakubaliana nami pasi shaka kwamba haikuwa na hata chembe ya neno "waislamu" wala "Mashehe" wala haikumtaja MEngi wala Mbowe ila ilitumia kikundi hicho, kuchafua watu. Hata aliyepost hii thread hakuwa anaelewa mantiki ya habari husika ndio maana akaweka maswali kibao kabla ya Mzee Mwanakijiji hajaweka habari yake ya KLHNews.

Naona hawa mashehe hawakusikiliza habari yenyewe wamesimuliwa na kama walisikiliza hawakuwa makini na hivyo walisikia wanachofikiri na si wanachoona na kusikia ama wamesoma JF na habari ya KLHNEWS wakaitumia.

Pia naona humu JF wameingia kwa nguvu na wanapambana kujitetea na kupotosha. Inawezekana ama Albert, Mtawa ama wafuasi wao wako busy humu JF kubadili mwelekeo na kupotosha na bahati mbaya sana HAbari Leo wameandika habari bila kusikiliza tape/habari ya ITV its soo sad, gazeti la serikali kutumika kama lilivyotumika jana kumlinda Makamba.

Ni aibu na serikali kama Taasisi kutumika kama ambavyo lEO TBC1 itatumika kutoa taarifa ya Press Conf hiyo ya huyo anayejiita Mwenyekiti ni hatari sana kama serikali kama taasisi ya Watanzania wote bila kujal dini, itikadi wala kabila haitajitenga na uovu huo. ITV haikumtuhumu mtu wala dini ilisema kuna njama za kuchafua watu kwa msingi ya dini na ukabila jambo ambalo wahusika wamekiri na kazi wameianza katika radio ya Kiislamu iitwayo Radio Kheir FM tokea Jumanne usiku.
 
HEBU tuweke kumbukumbu sahihi, na waliotizama ama kusikiliza ile habari ya ITV usiku wa Jumatatu saa 2.05 na saa 4.40 pamoja na Jumanne asubuhi watakubaliana nami pasi shaka kwamba haikuwa na hata chembe ya neno "waislamu" wala "Mashehe" wala haikumtaja MEngi wala Mbowe ila ilitumia kikundi hicho, kuchafua watu. Hata aliyepost hii thread hakuwa anaelewa mantiki ya habari husika ndio maana akaweka maswali kibao kabla ya Mzee Mwanakijiji hajaweka habari yake ya KLHNews.

Naona hawa mashehe hawakusikiliza habari yenyewe wamesimuliwa na kama walisikiliza hawakuwa makini na hivyo walisikia wanachofikiri na si wanachoona na kusikia ama wamesoma JF na habari ya KLHNEWS wakaitumia.

Pia naona humu JF wameingia kwa nguvu na wanapambana kujitetea na kupotosha. Inawezekana ama Albert, Mtawa ama wafuasi wao wako busy humu JF kubadili mwelekeo na kupotosha na bahati mbaya sana HAbari Leo wameandika habari bila kusikiliza tape/habari ya ITV its soo sad, gazeti la serikali kutumika kama lilivyotumika jana kumlinda Makamba.

Ni aibu na serikali kama Taasisi kutumika kama ambavyo lEO TBC1 itatumika kutoa taarifa ya Press Conf hiyo ya huyo anayejiita Mwenyekiti ni hatari sana kama serikali kama taasisi ya Watanzania wote bila kujal dini, itikadi wala kabila haitajitenga na uovu huo. ITV haikumtuhumu mtu wala dini ilisema kuna njama za kuchafua watu kwa msingi ya dini na ukabila jambo ambalo wahusika wamekiri na kazi wameianza katika radio ya Kiislamu iitwayo Radio Kheir FM tokea Jumanne usiku.

Currently Active Users Viewing This Thread: 58 (16 members and 42 guests)
Halisi, amagoma, Baba Watatu, gaijin, Kwayu, LazyDog, Masatu, Mbalamwezi, Mkandara, Mr. Zero, mutua12, Mwita Maranya, Phillemon Mikael, Shedafa, Tuandamane, Verily Verily
 
unaweza kuwa mchochezi ila usijue kama unafanya uchochezi at the expense of dataz
 
unaweza kuwa mchochezi ila usijue kama unafanya uchochezi at the expense of dataz

Na unaweza kuwa unajua unafanya uchochezi ila usijali kwa sababu nia yako sio positivity, responsibility ama objectivity.

Hakuna mtu hatari duniani kama yule ambae hajali kitu, hususan ambae anasema yuko kwenye "mission."

Kuhani...I'm on a mission, and my mission is very clear. Believe me it is not news.

Mwandishi wa habari, mleta taarifa tena mwenye rep ya juu katika social commentary and news reporting Tanzania anakwambia yuko kwenye mission nyingine!!!

Kwa hiyo, Mama, tunarudi kule kule: Tanzania hakuna viable news media. I wish ingekuwepo, sio kwamba nawapakazia ukilaza bure, I really really wish ingekuwepo. Haipo.
 
Kutoa habari ambayo inaigawa nchi kuliko kitu kingine chochote kile inabidi kuchukuliwe kimakini sana. Sisi Watanzania dini inatugawa sana kuliko kingine chochote, hivyo kama waandishi wa habari watakuwa wanaandika au kusambaza habari ambazo hawajazifanyia kazi kujua ukweli wake basi kuna hatari nchi inaweza kuingia kwenye machafuko na mwisho wake ukawa na athari kubwa sana. Kwani hao ITV wangesubiri hata siku mbili au tatu kuichunguza habari hiyo kwa makini kabla ya kuitangaza kwa Watanzania kungekuwa na kosa gani? Sasa msemaji wa ITV anaingia mitini kukwepa wanahabari ili kupata more info kuhusiana na habari iliyotangazwa na kampuni yake ITV. Tumeyaona ya Wayahutu na Watutsi sasa tusipokuwa makini nasi tutaanzisha ya kwetu ya Waislamu na Wakristo, na nchi yetu itakumbwa na athari kubwa sana.
Walivyoripoti kwenye taarifa ya habari ni kwamba waliwanasa ijumaa na hiyo habari waliiripoti jumatatu.so labda waliichunguza na wakagundua kitu ndio mana wakailete kwetu.
 
  1. Huu mkutano wa viongozi wa waislamu (kuna uwezekano waislam wanawakilishwa na viongozi wa vikundi zaidi ya kimoja), ulikuwa halali?

    .
  2. Makundi mengine yanayowakilisha waislam Tanzania, mpaka sasa, wametoa maoni yoyote? Je, wako upande upi?



    "Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho," alisema Msopa.
  3. Kundi hili dogo la viongozi wa waislam, wanawezaje kujihalalishia kuyafanya haya kwa niaba ya waislam wote? Je, hivi ndivyo shughuli zinavyoendeshwa kwenye uislam?




.
 
Na unaweza kuwa unajua unafanya uchochezi ila usijali kwa sababu nia yako sio positivity, responsibility ama objectivity.

Hakuna mtu hatari duniani kama yule ambae hajali kitu, hususan ambae anasema yuko kwenye "mission."



Mwandishi wa habari, mleta taarifa tena mwenye rep ya juu katika social commentary and news reporting Tanzania anakwambia yuko kwenye mission nyingine!!!

Chukua tahadhari.

Kwa hiyo, Mama, tunarudi kule kule: Tanzania hakuna viable news media. I wish ingekuwepo, sio kwamba nawapakazia ukilaza bure, I really really wish ingekuwepo. Haipo.

Mzee Mwanakijiji bandwagon imedandiwa kumbe mwenzetu uko kwenye mission? ni mission gani? ina/mewalenga kina nani na nia yako ni nini hasaa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom