Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sekenke, Nov 4, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #1
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanabodi

  Naomba kwa mwenye habari zaidi atufahamishe kuhusu hili.

  Katika taarifa ya habari ya jana (3 Novemba 2008) saa mbili usiku, na leo asubuhi (04 Novemba 2008), kituo cha ITV kilionyesha habari ambayo ilionekana kuwanasa jamaa kadhaa bila wao kujua. Maelezo (ambayo hadi sasa sijayaelewa vizuri) ni kwamba hao jamaa wameonekana katika hoteli kubwakubwa jijini (bila kuzitaja), na kwamba walikuwa wakipanga kuwachonganisha na kuwachafua mfanyabiashara-mwanasiasa mmoja na mfanyabiashara flani, kitu kama hicho.

  Ilionekana kwamba mpiga picha wa ITV alikuwa kajificha kwenye moja ya vyumba vya juu vya hiyo hoteli akiwachukua bila wao kujua, na akawafuatilia hadi mitaani mabako aliweza kunasa hadi sauti zao. Walionekana wakibishana kuhus kiwango cha pesa walizopewa ili kutimiza kibarua chao, jina la Manji lilisikika mara kadhaa, na kwamba baada ya mikakati hiyo watatawanyika ili kuanza kazi yao ya uchafuzi wa hali ya hewa kisiasa. Baadhi wataanzia Ruvuma (hapo sijui mlengwa), mmoja atabaki jijini kumshughulikia Kawawa.

  Samahani kama nashindwa kuielezea vizuri habari yenyewe kwani ilikuwa haijakaa sawa, ndio maana nakuja kwenu na kuomba yeyote aliyefuatilia na kuelewa na mwenye taarifa zaidi atumwagie tuweze kujua nini kinaendelea.

  Natanguliza shukrani
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Its simple Manji Vs Mengi Volume 2
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Someone please elaborate this further, so Manji recovered from the alledgedly severe malaria, aka suicide attempt aka drug overdose aka juju effect aka staged sudden illness. And what exactly was on itv?
   
 4. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #4
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kilichoonekana kwenye luninga ni hao mamluki kadhaa, kama sita hivi. Mmoja alionekana kavaa kanzu. Kwa pamoja walionekana hapa na pale, mandhari ya watu wanaopanga mikakati... pia wasio makini. Hata hivyo, muhabarishaji alionekana kuwa na uhakika na anachokisema kuhusu mipango waliyokuwa nayo. Kwa bahati mbaya muhabarishaji/msomaji hakuwa wazi sana na aliacha maswali mengi zaidi, ni bora hata asingeirusha ile habari.

  Mengi was not there, in person, but from the audio dub he was all over, as the alleged first party. The second party is this unknown businessman as referred to by the news anchor... it would appear that there was a third party... there are lot of loose ends...

  Knowing JF and its tentacles, I am sure someone out there has info on the conundrum, if at all.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hii habari imeanza kuvuja jana mchana na inahusiana na masuala ya OIC...
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mzee Mkjj

  najua wewe kainzi kako kapo fast hebu mwaga mambo hapa naona huyu Sekenke anashindwa panda mlima. Mwaga mambo jamvini
   
 7. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ngoja nivue viatu na kuvaa sandals, nichukue kinywaji baridi toka katika friji na nikae mkao mzuri maana ndiyo kwanza picha imeanza.

  Haya mzee wetu wa bush mwaga utamu.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu anaitwa Albert Marwa... I need more info..
   
 9. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wewe kidatu,hujatulia,vipi maji yamejaa lakini ?maana nasikia tnataka kununua ile mitumba ya dawson
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Albert Marwa ni jamaa mmoja anayetaka kumuoa mtoto wa JK lakini ni mtu anayetumia nafasi yoyote anayoipata kutengeneza pesa na moja wapo ikiwa tukio hilo!!!!!!!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  wiki iliyopita nilidokeza kuhusu "mgongano" utakaotokea mwishoni mwa juma. Namalizia kuandika ripoti yangu na nitawawekea hapa muda si mrefu ujao kama "Exclusive News".. majina yatatajwa... stay tuned..
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  ...nadhani sasa mengi na ITV yake wanaweza kuandaa kile kipindi maarufu cha kufuatilia nyendo CHEATERS.....

  ...KIMSINGI mimi sio fun wa manji wala mengi...but in this nadhani mengi atakuwa amepiga below the belt jeb......ukitaka kuwarekodi watu wana sema nini dar kwa siri kwenye pubs hata iwe ya level 8 au movenpick....hutapata tabu kuwanasa watu wakipanga chochote ...hata ukitafuta wa kuwapa kesi ya uhaini utawakosa...........watanzania ni hodari kwa siasa na kufanya mipango vijiweni...!

  katika hali kama hiyo ITV wamefanya papara kuirusha hiyo habari hewani..na tena itaonekana ni muendelezo wa ugomvi binafsi na manji.....!..ambao hatusaidii na sanasana ,....manji anaweza kumpeleka mahakamani kwa hili.......na itahalalisha ,matumizi mabaya ya media...

  ....kwa taarifa sensitive kama hiyo kabla ya ITV kuamua kuitangaza ..ingebidi waihalalishe kwa kupeleka huo mkanda kwenye vyombo vya usalama........na defianately ingeweza kuwekwa wazi na KAMANDA WA POLISI wa mkoa ....na hata kama asingetangaza wangekuwa na uwezo wa kumuuliza swali ....na kuli back na information waliyo nayo....

  kama wana mkakati wa mengi walikuwa smart ..wakasubiri hao culprits wakakamatwa ndo wairushe hiyo habari....wangekuwa wamemmaliza kabisa manji ..maana ingeweza kuwa award winning news...like"..polisi mkoa wa dar es salaam inawashikilia watu 8...kwa kosa la kupanga ......."..unaonaje habari kama hiyo then ikawa backed na picha walizopiga kwa siri...si umemaliza!!!.....its all about wrong strategies........lets wait for manji"s heat back...who knows anaweza naye kurekodi watu..ie wafanyakazi wake watakaokuwa wanakiri kupewa pesa na mengi .......na kumuwekea sumu kwenye chai hadi akaumwa......si tunaongelea tuhuma nzito bila kushirikisha vyombo vya dola..?
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  wiki iliyopita nilidokeza kuhusu "mgongano" utakaotokea mwishoni mwa juma. Namalizia kuandika ripoti yangu na nitawawekea hapa muda si mrefu ujao kama "Exclusive News".. majina yatatajwa... stay tuned..
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Ndio maana tukio lilikuwa limefanyika Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na habari ikarushwa Jumatatu usiku. Leo Albert amehojiwa na polisi, Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi.

  Kwa ufupi ukiangalia taarifa yenyewe inasema kazi imeanza jana kwa maana wamekwishaondoka watu kwenda Songea na watapata mapokezi ya ma-RPC na Ma-OCD pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya pamoja na wabunge wanaofungamana nao katika mikoa husika.

  Kwa hiyo kuchelewa kuitoa ingekuwa kutoa nafasi ya kosa kufanyika. Nadhani wamejifunza ya Mtikila Tarime maana mbinu ni zile zile ambazo Mtikila alikabidhiwa kule Tarime na hakukamatwa na polisi wala wana usalama kabla ya kupokwa mawe. Tukae tukijua hata huyo Albert hatafanywa lolote na si kwa sababu ya JK bali kwa nguvu ya pesa unless JK atoe amri jambo ambalo hawezi kusema akamatwe, huku akiwa anaambiwa na wasaidizi wake kwamba "mambo yanakwenda vizuri mheshimiwa".
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Hii habari nilipenyezewa toka jana, lakini kama ilivyo ni ya moto mno ndio maana nikatunza maktaba kusubiri upepo, ingawa bado ni ya moto sana nitajaribu kuigusa kidogo tu,

  kuna mkakati wa kikundi flani cha imani kuwachafua wale wote kwenye jamii yetu wanaopingana nao katika ishu yao ya imani nzito, hapo kwenye luninga ilikuwa inapagwa mkakati ya kutaka kutekeleza azma yao, lakini wakanaswa, anayehusika sana na huu mkakati ni kijana mmoja mdogo sana, anayeitwa Marwa, ambaye alibadili dini siku za nyuma ili kumuoa mtoto wa Mang'enya RIP, aliyewahi kuwa balozi wetu UN, na kiongozi wa zamani wa taifa, ni rafiki wa karibu sana na Kinje, maana na yeye ni mtoto wa Meja General Marwa RIP,

  According to the dataz, huyu kijana ambaye amem-divorce tayari mke wake, amekua akijaribu sana kumuoa mtoto wa Muungwana, lakini Muungwana ameweka mguu chini kwamba labda over his dead body. Huyu kijana ambaye ninamfahamu kwa karibu sana, recently amekua akijishughulisha sana na imani za dini yake za ki-extremist, na hata kufikia kufungua Radio ya dini yake, na amekuwa akijihusisha na huu mkakati akidai anatumwa na Muungwana,

  According to the dataz, Mengi ndiye aliyekuwa amewekwa on the top of the lists na hiki kikundi kuchafuliwa kwanza, now this is very alarming! Nimeamua kutoka jana nilipopata hizi dataz, kwamba nitatumia muda wangu mwingi sana in the next four days kabla ya kufikia mkutano wa NEC, kushughulikia kwa karibu sana ishu ya OIC.

  Respect!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Maalum

  KLHN yaweza kuripoti kwa uhakika kabisa kuwa mpango wa kuanzisha uchafuzi wenye mlengo wa kidini na kikabila nchi umeundwa na sasa umefichuliwa. Mpango huo ambao unawahusisha watu mbalimbali wenye majina makubwa umedhihirika kuanzia siku ya Ijumaa iliyopita.

  Mpango huo ulianza kusukwa wiki chache zilizopita na hatimaye kuanza kutekelezwa siku ya Ijumaa iliyopita. Kwa wanaokumbuka siku ile (ya Ijumaa) kulikuwa na mkutano wa Waislamu kuelezea masuala mbalimbali ya maslahi yao na hasa suala la OIC. Baadhi ya viongozi wa Waislamu toka mikoani walikuwa jijini pia.

  Ilikuwa ni katika nafasi hii timu iliyokuwa imeanza kukusanywa iliweza kuwakutanisha viongozi mbalimbali hao wa Waislamu kwa kuandaa mkakati kamambe ambao kwa madai yao mipango yake inatoka ndani na juu kwenye serikali. Katika kufanya hivyo viongozi kama 9 hivi wa Kiislamu waliweza kupatikana na kukutanishwa katika hoteli ya Regency siku ya Ijumaa.

  Miongoni mwao ni mashehe na viongozi wengine wa kidini; baadhi yao ni pamoja na Shekhe Mazinge, Mwaipopo, Said Liko, Chifu Msokwa, Ustaadh Twaha, Dr. Salehe, Abubakar Bonde, Sheikh Amour Jongo, Rajabu Jazba, na Ustaadh Ramadhani. Waliokuwemo kwenye mkutano huo pia ni pamoja na Albert Marwa (inadaiwa ni mtoto wa kulelewa wa Generali Marwa) pamoja na mtu mmoja aitwaye Mtawa (huyu yasemekana ni mtumishi wa ngazi ya Juu ikulu). Walikuwepo baadhi ya watu wengine ambao wanadaiwa kuwa ni maafisa wa Usalama wa Taifa ambao kutokana na sheria hatuwezi kuwataja majina yao.

  Mpango huo ambao “vijidudu” vya uchunguzi viliweza kuunasa kwa picha na kwa sauti kimsingi una malengo yafuatayo.

  a. Kuwaonesha waislamu kuwa Bw. Reginald Mengi na Freeman Mbowe ndio maadui wakubwa wa maslahi ya Waislamu nchini.
  b. Kwamba Mengi na Mbowe wana mkakati wa kuhakikisha kiongozi anayekuja ni kutoka kabila la Wachagga. Katika hili la dhidi ya “Uchagga” wanamkakati walikuwa wana uhakika wa kutobughudhiwa na polisi kwenye mikutano ambayo waliipanga kuifanya hasa wakiamini kuwa IGP Said Mwema yuko upande wao. Hata hivyo mmoja wao aliapa kuwa aliwahi kuambiwa na Dr. Nchimbi kuwa Mwema ni Mchagga (sijui kwa upande wa mama) na hivyo wasitarajie sana.
  c. Walioleta mpango huo wamemhusisha kiongozi wa juu serikalini kuwa ndiye aliyewatuma kutekeleza mpango huo hasa kuonesha kuwa vyombo vya IPP vinatumika kueneza Ukristu, kukandamiza Waislamu, na kuinua Wachagga. Hili litaelezwa ili Waislamu waanze kuvisusisa vyombo vya habari vya IPP.
  d. Kuendelea kuwahusisha Mengi na Mbowe katika vifo vya Chacha Wangwe na Gavana Ballali.

  Katika kutekeleza mpango huo timu hiyo ilikuwa ijipange na kuandaa bajeti ya kiasi kisichopungua shilingi milioni 100 ambazo zitagawanywa kati yao na kwa wale ambao watakuwa tayari kutekeleza mpango huo. Kiasi ambacho cha awali ambacho kila mmoja alikuwa agawiwe ni kama milioni tatu tatu huko mmoja wa wanamkakati huo akiahidi uwezekano wa kupata fedha zaidi kutoka kwa Bakhresa. Kiasi cha awali kinadaiwa kutolewa na mfanyabiashara Yusuph Manji wa Quality Group.

  Siku ya Jumamosi kundi hilo la wanamkakati lilikutana kwenye hoteli ya Golden Tulip kuendelea na mipango yao ambayo ka nzi ka KLHN kalikuwa kanafuatilia kila hatua tena kwa ukaribu kabisa.

  Wakiwa na magari yenye namba za usajili za T267 ABT na T87 ABG wanamkakati wakiongozwa na Mazinge Mwipopo (spelling yaweza isiwe sahihi) na Chifu Msokwa walihamisha kikao chao kingine kutoka Golden Tulip kuelekea Msikiti wa Mtambani ambapo waliamua kubadilisha na kuelekea Msikiti wa kwa Mtoro. Ka nzi kaliweza kunasa habari za kutosha.

  Siku ya Jumapili kikao chao kiliendelea huko Kinondoni mtaa wa Kazina nyumba (censored) ambapo kuanzia saa tisa hadi majira ya Magharibi waliendelea na mipango yao na maazimio yao ikiwemo la kuhakikisha kuwa viongozi watakaoshiriki katika mkakati huo wa kuitisha mikutano mbalimbali mikoani wahakikishe na wao wanapata watu angalau 20 chini yao.

  Kutoka kwenye vikao hivyo iliazimiwa uitishwe mkutano wa waandishi wa habari ili kuweza kufafanua madai yao dhidi ya Mengi na Mbowe na hivyo kuanzisha mchakato huo wa kueneza propaganda hii ya udini na ukabila. Baadhi ya wajumbe walikuwa wameshaondoka siku ya Jumatatu kuelekea mikoani kuanza kazi hiyo na hilo ndilo lililosababisha vyombo vya ITV kurusha hivyo walivyonavyo.

  KLHN imepata nafasi ya kusikiliza masaa ya kutosha ya mazungumzo ya kundi hili na jambo moja ambalo tunaweza kusema kwa uhakika ni kuwa linatia hofu na kuuliza tumefikaje hapa.

  Hata hivyo mpango huo haujaenda vizuri kama ulivyotarajiwa hasa baada ya kutokea mabishano ya kiasi cha fedha huko baadhi ya wajumbe wakiamini kuwa Bw. Albert Marwa amepewa fedha zaidi kuliko alizowapatia wajumbe hao. Wengine wameanza kudai kuwa Bw. Marwa ndiye aliyeinjinia mpango wa wao kunaswa na vyombo vya kielectroniki.

  Jioni ya leo (jumanne) ka nzi ketu kanaruka ruka mikoani kamethibitisha pasipo shaka kuwa baadhi ya simu za wahusika wakuu zimekuwa ‘tapped’ ili kuweza kujua jinsi operesheni hii ilivyoendesha kikamilifu ikihusisha utaalamu na ujasiri wa hali ya juu kuliko uwezo wowote wa TISS kuwanyemelea mafisadi.

  Msimamizi wa Operesheni hii ardhini ambaye alizungumza na KLHN kwa masharti yale yale mliyoyazoea amesema kuwa hawakuwa na mpango wa kuhusisha vyombo vya usalama kwani kwenye suala zima vyombo hivyo baadhi ya wahusika wake wa kuu wamo ndani mpango huu na hivyo njia pekee ilikuwa ni kuwadokeza tu watu kuwa mpango huo upo, unajulikana, na utakapoanza kutekelezwa Watanzania “wasishtuke”.

  Hata hivyo wameahidi kuwa endapo Mwendesha Mashtaka Mkuu ataamua kuunda "Special Tribunal" ya kufuatilia suala hili ili kuona mashtaka yoyote kuletwa au uchunguzi ushirikiano unaweza kutolewa kwa kadiri ya kwamba vyanzo vyote vya habari hii vitabakia kuwa siri na havitalazimishwa kujitaja isipokuwa kuleta ushahidi kama ulivyo (raw evidence). Nje ya hapo amesema kuwa hawana "imani na Polisi wala Usalama wa taifa kwenye suala hili".

  KLHN inaendelea kufuatilia kwa karibu mpango huu na kufichua njama yoyote ile ya kifadi yenye lengo la kuleta mgongano wa kidini au kikabila nchini. Baadhi ya habari zitasahihishwa kwa kadiri wingu linavyozidi kusafishika zaidi.
   
 17. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nilisema miezi mingi nyuma kwamba mafisadi kutumia mtandao wa waislamu. Kuna watu wakiniona muongo na mzushi. Laiti kama mngenielewa toka wakati huo

  PM
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Wakati tunasubiri wingu kusafishika hii ingewekwa kama ni tetesi.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Nov 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tetesi ni kitu kisicho na ushahidi, kama wanazushiwa waende mahakamani... na huu ni mpango mmoja tu mwingine unahusisha watu wasomi zaidi na very senior na una angle ile ile.. huo utaibuka wiki ijayo Inshallah..
   
 20. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #20
  Nov 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  ......this is really terrific.............lakini daima MUNGU atawaadhibu wanafiki.,..wanaotaka kuharibu UMOJA wa nchi yetu...

  ..MUNGU Atawaadhibu wanasiasa ambao baada ya kushindwa kazi wanataka kudandia religion or tribal affiliation....

  MUNGU atunusuru na vugu vugu kama hizi ambazo tulishazisahau kwenye nchi yetu tamu na nzuri...AMANI YETU NI JAMBO LA MSINGI...si dini waala rangi au kabila...wote tukiumia tunavuja damu....

  kwa hakika nimeelewa kwa nini hii taarifa ilitolewa pasipo kuhusisha security organs..lakini pia imedhibitisha kuwa kuna watu wana uwezo mkubwa sana katika medani ya upelelezi......

  nadhani MUNGU anawatumia ili kulinda UMOJA wa nchi yetu......na daima hata kama hawana vifaa wala pesa za kuingia field ..watapata taarifa na wataendelea kuzipata kwa umakini huu.....huu...
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...