Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Wahadhiri wa Kiislamu wainyooshea kidole ITV
Godwin Myovela
Daily News; Wednesday,November 05, 2008 @21:15

Kamati ya Wahadhiri wa dini ya Kiislamu nchini, wamekanusha habari iliyotangazwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, iliyodai kuwa kuna kikundi cha dini ya Kiislamu kinachotumika kuchafua jina la mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa nchini kwa kutumia nembo ya udini na ukabila.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Chifu Hussein Msopa, alizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, na kutoa tamko la kukitaka kituo hicho cha utangazaji kuiomba kamati hiyo radhi kwa kipindi kisichopungua siku saba kuanzia jana.

“Sisi tulikuwa kwenye mkutano wetu siku hiyo, hatukualika vyombo vya habari tulikuwa tukijadili masuala matatu; OIC, Kadhi na ukabila,” alisema Msopa, na kuongeza kuwa katika ajenda hizo, walilazimika kuachana na ajenda mbili ambazo ni OIC na Kadhi kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wananchi kuiachia serikali masuala hayo.

Alisema kitu cha kushangaza ni pale televisheni hiyo ilipofuatilia kwa siri mkutano huo bila kualikwa, na kurusha mjadala na mawazo ya baadhi ya wajumbe badala ya kusubiri nini kiliamriwa au baada ya kikao, kitu kilichowatia shaka juu ya usalama wao.

Aidha, Mwenyekiti huyo alisema taarifa hiyo ilipotosha umma na kuleta uzushi na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo wanaoitakia mema dini hiyo, baada ya kueleza kuwa kikundi hicho kinachotumika kumchafua mfanyabiashara huyo, kinafadhiliwa na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Manji.

“Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho,” alisema Msopa.

Alisema kamwe Waislamu hawataacha kujadili suala la ukabila ambalo linazidi kuota mabawa nchini siku hadi siku, na kufanya baadhi ya sekta na idara za serikali kuendeshwa kikabila na bila ufanisi, sababu zinazopelekea migomo, maandamano na hata uzalishaji na huduma mbovu.

Juhudi za kumtafuta msemaji wa ITV ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile, hazikuzaa matunda, baada ya Katibu Muhtasi wake, kueleza kuwa anahudhuria mkutano, na kwamba hatazungumza na mtu ye yote. Kwa mujibu wa maelezo ya Msopa, taarifa hiyo ilitangazwa na kituo hicho Novemba 3, mwaka huu na kurudiwa siku iliyofuata, pamoja na kuonyesha picha za wahadhiri hao wakihudhuria kikao hicho.
 
mhhhh ok

2ntfv48.jpg

naona umesahau lile kundi linalolipwa kuwetha threads kwa ajili ya kuwafurahisha wanao walipa pesa....sijui hili ni la pili au lipi?

maana naona kila mtu humu ana interest na of course huwezi kuwakataza watu wasi criticise au wasikubaliane na mawazo yako
mfano tulikuwa na thread humu kuuliza watu kwa nini wanakubali kumwimba Mungu ambaye haluna aliyewahi kumwona wala kutuletea evidence kama yupo mwishowe tukaambiwa kuwa tunapenda kubisha tuuu

And then kuna lile kundi na SUPERMARKET JOURNALISTS ...kundi ambalo naona hujalizungumzia

GT,
Binafsi sina tatizo na constructive criticism.Nakubaliana nawe kwamba kwenye mkusanyiko mkubwa kama huu lazima watu watatofautiana katika hoja au interests.Lakini katika this particular mada,nadhani kuna substance kadhaa ambazo zinapaswa kuwa taken into consideration kabla ya kuipinga (japo si lazima kufanya hivyo i.e. taking those mambo kadhaa into consideration):

Habari iloyochapishwa kwenye gazeti la Habari Leo INATHIBITISHA kwamba kweli kulifanyika kikao cha aina hiyo.Wahusika wamekanusha tuhuma zilizoelekezwa dhidi yao,na kudai waombwe msamaha within 7 days,la sivyo wataanzisha jitihada dhidi ya IPP MEDIA.Stop there!Kwanini wasiende mahakamani baada ya hizo siku 7!Maana kama habari hiyo ni ya uzushi then inamaanisha wamekashifiwa.Ushahidi wa "kashfa" dhidi yao uko wazi,na kwa walikuwa na open-and-shut civil case dhidi ya huyo "aliyewakashifu"

Hadi hapo inathibitisha kuwa habari hiyo iliyowekwa hapa ina elements kadhaa za ukweli.The meeting was indeed held,some of the watajwa wamejitokeza hadharani "kukiri" kufanyika kwa mkutano huo na indirectly kuthibitisha kuwa ajenda zilikuwa OIC,KADHI na UDINI,kama ilivyoripotiwa hapa.

Kwa mtizamo wangu,ambao unaweza pia kuwa si sahihi,naona kilichofanyika hapa ni kuripotiwa kwa habari iliyoonyeshwa kwenye tv,mwanakijiji akaifafanua zaidi,na habarileo limethibitisha kuwapo kwa habari hiyo.
 
Je, kainzi kalisikia udaku? just thinking aloud...😉
 
Mkuu heshima kwako, hii habari Mwanakijiji alishaiweka kule kwenye thread yake.

Shukrani Mkuu nimeitafuta hiyo habari ili niweke hii lakini sioni labda imeshabadilishwa kichwa cha habari. Ngoja nijaribu tena. MODS please delete this thread. Thanks
 
Hii habari ndivyo ilivyoripotiwa na Habari Leo:

Habari Leo

Kamati ya Wahadhiri wa dini ya Kiislamu nchini, wamekanusha habari iliyotangazwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, iliyodai kuwa kuna kikundi cha dini ya Kiislamu kinachotumika kuchafua jina la mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa nchini kwa kutumia nembo ya udini na ukabila.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Chifu Hussein Msopa, alizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, na kutoa tamko la kukitaka kituo hicho cha utangazaji kuiomba kamati hiyo radhi kwa kipindi kisichopungua siku saba kuanzia jana.

"Sisi tulikuwa kwenye mkutano wetu siku hiyo, hatukualika vyombo vya habari tulikuwa tukijadili masuala matatu; OIC, Kadhi na ukabila," alisema Msopa, na kuongeza kuwa katika ajenda hizo, walilazimika kuachana na ajenda mbili ambazo ni OIC na Kadhi kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wananchi kuiachia serikali masuala hayo.

Alisema kitu cha kushangaza ni pale televisheni hiyo ilipofuatilia kwa siri mkutano huo bila kualikwa, na kurusha mjadala na mawazo ya baadhi ya wajumbe badala ya kusubiri nini kiliamriwa au baada ya kikao, kitu kilichowatia shaka juu ya usalama wao.

Aidha, Mwenyekiti huyo alisema taarifa hiyo ilipotosha umma na kuleta uzushi na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo wanaoitakia mema dini hiyo, baada ya kueleza kuwa kikundi hicho kinachotumika kumchafua mfanyabiashara huyo, kinafadhiliwa na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Manji.

"Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho," alisema Msopa.

Alisema kamwe Waislamu hawataacha kujadili suala la ukabila ambalo linazidi kuota mabawa nchini siku hadi siku, na kufanya baadhi ya sekta na idara za serikali kuendeshwa kikabila na bila ufanisi, sababu zinazopelekea migomo, maandamano na hata uzalishaji na huduma mbovu.

Juhudi za kumtafuta msemaji wa ITV ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile, hazikuzaa matunda, baada ya Katibu Muhtasi wake, kueleza kuwa anahudhuria mkutano, na kwamba hatazungumza na mtu ye yote. Kwa mujibu wa maelezo ya Msopa, taarifa hiyo ilitangazwa na kituo hicho Novemba 3, mwaka huu na kurudiwa siku iliyofuata, pamoja na kuonyesha picha za wahadhiri hao wakihudhuria kikao hicho.

My Take:
Angalia kile wanachotishia kukifanya baada ya siku saba na kile ambacho nilikiripoti jana kuwa kilirekodiwa kabla ya kipindi hicho kurushwa (kwamba uamuzi wa kufanya kinachotishiwa kufanywa baada ya siku saba ulifanyika kabla ya habari hii kutoka hewani- inawezekana vipi?). Je siyo kwamba baada ya siku saba watakukwa wanatekeleza hiki:

Sasa baada ya siku saba mkisikia habari ni hii itakuwa ni kwa sababu ITV wamekataa kuomba radhi au kwa vile uamuzi huo tayari ulishachukuliwa? Kwanini wasitishie kwenda mahakamani kama wanavyofanya wengine?

Hizo mahakama zetu nazo ni kichekesho kitupu, Watanzania hatuziamini na hata Jaji Mkuu alitamka kwamba Mahakama zimejaa rushwa. Hivyo hakuna uhakika wowote kwamba hao 'mamluki' watatendewa haki na mahakama. Je, kainzi kalidaka udaku? Habari nyeti zina uzuri wake lakini zile ambazo zina mambo ya udini ambayo yanatugawa Watanzania kuliko kingine chochote kile zifanyiwe kazi ili kuhakikisha ukweli wake kwa kupata ukweli toka upande mwingine wa shilingi, vinginevyo mnaweza kukuta JF inaanza kupata sifa mbaya ya kuweka udaku.
 
Mwanakijiji,

..ningeyapuuza madai haya kama jina la Bw.Mtawa lisingetajwa.

..Mtawa amekuwa msaidizi, na mtu wa karibu na Raisi, kwa zaidi ya miaka 15.
..sidhani kama ni vizuri kumhusisha na tuhuma kama hizi bila kuleta ushahidi usioweza kutiliwa mashaka.

Mkuu
mtu kufanya kazi na mkuu wa nchi kwa muda mrefu hakumuondolei tabia yake mbaya aliyonayo.

Mfano Uganda two weeks ago presidential bodyguard alihusishwa na wizi wa mamilion, Je Museven alimtumaaa?????

mfano mwingine Viongozi wetu waliofanya kazi tangu enzi ya JKN wameonekana kuiba hela za umma na sasa wanapelekwa mahakani, je pamoja kufanya kazi kwa muda mrefu wametumwa na nani. So it is a weak excuse....
 
Originally Posted by Masanja

''Hizi dini zitatumaliza. Wewe angalia hata watu ambao ungetegemea wapinge hoja kwa hoja..likija swala la dini wanachanganyikiwa kabisa
.''

Kweli ndugu yangu, itafikia hatua nikimwona mwislamu anacheza mpira nikaripoti nitalaumiwa, nikimwona mkristo anacheza dansi, nikaripoti nitalaumiwa.

Yaani kutokana na udhaifu tunaoujua sisi kuwa tunao, na kutokana na kuwa katika dini ya mashaka-mashaka, basi kila lisemwalo unaona kama unaguswa wewe, hata kama lililosemwa ni la kweli!

Siku zote inferiority complex mbaya sana! inaua, inaleta madhara ya kihoro, mwishowe unaweza hata ukaua mtu,

Taarifa hii ilikuwa ya kweli na wahusika wenyewe wamekubali! kuwa walikuwa wanajadili OIC,UKABILA NA Mahakama ya KADHI,

Fikiria kuwa maswala yanayohitaji mijadala ya kitaifa yanajadiliwa na watu wachache! wengine ni 'wakwe wa muungwana' wengine maafisa wakubwa!

Ingekuwa heri tena heri kubwa , kama katika kikao chenu hicho( sijui kama Bakwata walikuwemo) kama mngekuja na jibu kuwa, mnataka mumuombe Kikwete kuwa swala la OIC, lifuatiliwe na taasisi ya kiisalamu na sio serikali.

Lakini najiuliza katika vikao vingi sana kuna kuwa na agenda za mwaliko, na kama wastaarabu zaidi huwa mnaandikayaliyokuwa yanaelezwa katika hizo ajenda.

MNAWEZA MKAWAONYESHA WATANZANIA MLICHOANDIKA!!!! AU NYIE NI MAGENIUS KWA HIYO HAMUHITAJI KUANDIKA, for reference??

Na kwa nini muhitaji kuombwa msamaha???

Kwa nini katika kikao chenu msihusihe maaskofu, kama watanzania wenzenu??

waberoya
 
Hizo mahakama zetu nazo ni kichekesho kitupu, Watanzania hatuziamini na hata Jaji Mkuu alitamka kwamba Mahakama zimejaa rushwa. Hivyo hakuna uhakika wowote kwamba hao 'mamluki' watatendewa haki na mahakama. Je, kainzi kalidaka udaku? Habari nyeti zina uzuri wake lakini zile ambazo zina mambo ya udini ambayo yanatugawa Watanzania kuliko kingine chochote kile zifanyiwe kazi ili kuhakikisha ukweli wake kwa kupata ukweli toka upande mwingine wa shilingi, vinginevyo mnaweza kukuta JF inaanza kupata sifa mbaya ya kuweka udaku.

Mkuu siku zote ninaheshimu sana mchango wako na nitaendelea kufanya hivyo, lakini kwa hapa umekwenda kusiko, tumeanza lini kutoziamini mahakama kwa kiasi hicho? mbona ulikuwa mstari wambele kutaka mafisadi wa EPA na Richmond wapelekwe mahakamani? au ndo double standards.

Ninachofahamu mimi kazi ya media ni kutoa habari, na hii ni habari tena habari muhimu kwani inahusu mstakabari wa Taifa na watu binafsi. Hivi hatuoni kama kunawatu wanataka kutuingiza kwenye makundi ya kidini na kikabila?. Tukifikia mahali pa kususia bidhaa za mtu/watu kwa misingi ya kidini tutaliharibu taifa ni litaadhiri wafanya biashara wengi hivyo kuhujumu uchumi wa nchi.

Kwa maneno ya huyu mwenyekiti wao kwamba watawaomba Wakristo wasusie huduma za ITV kwa kuwa wametangaza kikao kilichokuwa kinajadili kwa siri mambo ya OIC, kadhi na ukabila mbona kichekesho? si ndo Wakristo watapenda zaidi huduma ITV?

Mambo haya yanahitaji umakini mkubwa, ninadhani hawa Ndg. wamekosa uvumilivu, walichopaswa ni kwenda mahakamani endapo wanahisi kutotendewa haki. otherwise, tunaelekea pabaya.
 
Nazijua mahakama zetu za Tanzania na nimeona wengi waliofungwa kwa kubambikiwa kesi au walioachiwa huru kwa kutumia pesa pamoja na kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha. Pamoja na kutaka mafisadi wapelekwe mahakamani najua chochote kinaweza kutokea, lakini kwa vile macho ya Watanzania na ya nchi za wafadhili yatakuwa yanafuatilia kesi hizo kwa karibu na shauku kubwa mahakimu wanaweza kuogopa kufanya upumbavu wao ili kuwaachia huru wahusika, lakini wanaweza kuachiwa huru.

Majaji wetu wakuu ndiyo waliosema mahakama zimejaa rushwa na ushahidi wa kauli zao ninao. Sasa kufuatia kauli zao, na mengi niliyoyaona na kuyasikia katika mahakama hizo siziamini mahakama hizo. Ushahidi wa kauli za majaji wakuu ni huu hapa chini. Swali je, Jaji Mkuu Augustino Ramadhani amechukua hatua zozote kupambana na rushwa iliyokithiri ndani ya mahakama? Mimi sijaziona hatua zozote.

Kila la kheri Jaji Mkuu katika kuutafuna mfupa wa rushwa

Tanzania Daima sauti ya watu

JAJI Mkuu mpya, Augustino Ramadhani, juzi aliupokea wadhifa wake mpya kwa kutoa ahadi nzito kwa Watanzania, ya kupambana na rushwa katika Idara ya Mahakama.

Jaji Ramadhani alitoa ahadi hiyo muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, juzi, ambako pamoja na ahadi hiyo, pia aliwaahidi Watanzania kuwa, vipaumbele vyake vingine akiwa katika ofisi hiyo, ni kupigania haki na kuhahakisha inapatikana kwa gharama nafuu.

Hizi ni ahadi nzito kwa Watanzania ambao kwa miaka mingi wamekuwa katika maumivu ya kuzikosa licha ya kuahidiwa mara nyingi na viongozi kadhaa.

Kwa jinsi tunavyomfahamu Jaji Mkuu Ramadhani, hatuna shaka kabisa kwamba anaweza kuzitekeleza ahadi zake hizi kutokana na rekodi yake nzuri ya utumishi uliotukuka katika sekta hiyo ya sheria.

Hata hivyo, tuna shaka iwapo nia nzuri aliyonayo ataweza kuitekeleza kama alivyokusudia kutokana na mfumo wa utawala wa taifa letu.

Shaka yetu, inatokana na mtiririko wa matukio mengi ya kudharauliwa kwa mahakama, yanayofanywa na baadhi ya mihimili mikuu ya dola, pamoja na baadhi ya viongozi ambao kupindisha sheria, ni sehemu ya maisha yao.

Katika Kuthibitisha shaka yetu, tunarejea maneno ya Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta, ambaye ameitumikia idara ya mahakama kwa kipindi cha miaka 40, katika hotuba yake ya kuaga kabla ya kustaafu rasmi mwishoni mwa wiki jana, alisema kuwa Bunge lina tabia ya kuingilia kazi za mahakama.

Jaji Mkuu mstaafu katika maneno yake hayo, anasema kuwa Bunge lililopita ambalo lilikuwa chini ya Spika mstaafu, Pius Msekwa lilithubutu kutengua uamuzi wa mahakama kuhusu wagombea binafsi.

Samatta, mwanasheria anayetambulika kwa umakini katika kazi yake, alitamka bayana kuwa hilo lilimkwaza na aliwataka wanasiasa watambue kuwa zama za chama na Bunge kushika hatamu zimepitwa na wakati.

Ingawa kauli hii ya Samatta inaweza kuwa msaada mkubwa kwa Jaji Mkuu Ramadhani katika kutekeleza azma yake, sisi bado tuna shaka kuhusu mafanikio hayo.

Tuna shaka kwa sababu hii si mara ya kwanza kwa viongozi wengi, wakiwamo wakuu wa nchi, tangu enzi za Benjamin Mkapa, kutoa ahadi za aina hii kwa Watanzania, lakini wanapoanza kutenda katika ofisi zao, hali inakuwa tofauti, wanashindwa kutekeleza ahadi zao.

Ieleweke kwamba, hatuna hata chembe ya kumkatisha tamaa Jaji Ramadhani katika azma yake hiyo, na wala hatuna shaka naye kuhusu kutekeleza ahadi zake.

Shaka yetu ni kwamba, Jaji Mkuu Ramadhani atakuwa tayari kupambana na vigogo, wakiwemo wanasiasa mashuhuri na maarufu, ambao wamejenga utamaduni wa kuwa juu ya mahakama.

Kwa maana nyingine, Jaji Mkuu ajiandae kunoa meno ya kuutafuna mfupa wa rushwa uliowashinda wengi, licha ya kuingia madarakani na kuahidi kwa mbwembwe kwamba watakomesha rushwa.

Kila la kheri.

Rushwa ilimnyima usingizi Jaji Samatta, Jaji Ramadhani atalala?

2007-07-22 11:13:27
Na Mhariri

Mwisho mwa wiki hii, Rais Jakaya Kikwete alimwapisha Bw. Augustino Ramadhani kuwa Jaji Mkuu mpya, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Jaji Mkuu, Barnabas Samatta ambaye amestaafu.

Viongozi hawa wawili wakizungumza kwa nyakati tofauti, suala kubwa walilogusia ni rushwa iliyokithiri katika Idara ya Mahakama hapa nchini.

Jaji Mstaafu, Samatta alikiri kuwa rushwa ni tatizo lililotawala mahakama nchini na kwamba suala hilo limekuwa likimkosesha usingizi katika kipindi chote cha uongozi wake na hadi anastaafu hali siyo nzuri.

Kwa msisitizo akasema ataendelea kusikitika kuona kuwa jaji au hakimu aliyesomea taaluma hiyo akipokea rushwa ili apindishe sheria.

Wakati Jaji huyu mstaafu akilia na rushwa hadi anastaafu, mwenzake aliyepokea kijiti, Jaji Mkuu mpya Ramadhani anasema moja ya vipaumbele vyake ni kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa katika Idara hiyo.

Akizunguma hayo mara baada ya kuapishwa juzi, akasema atahakikisha haki inapatikana bila rushwa, kwa haraka na kwa gharama nafuu, na kwamba atapangana na wenzake kuona ni jinsi gani mahakama, kama muhimili wa utawala wa nchi itajipanga kukabiliana na tatizo hilo.

``Nitahakikisha haki inapatikana kwa gharama nafuu maana haki imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa, lakini nitaweka mipango na wenzangu na kuandaa mazingira ya kupatikana haki kwa gharama nafuu`, anasisitiza Jaji Mkuu ramadhani.

Ahadi kama hii ya Jaji Mkuu mpya, siyo ajabu ilitolewa pia na Jaji Mkuu mstaafu wakati anaingia madarakani.

Na anakiri tatizo la rushwa lilikuwa linamnyima usingizi hadi anastaafu. Swali ni je, Jaji Mkuu mpya ambaye pia amepokea mkoba unaolilia rushwa atalala usingizi?

Ukiona viongozi hawa wa ngazi ya juu katika Idara ya Mahakama wanazungumzia jambo linalofanana na kusisitiza ni kero kubwa, basi ujue kazi ipo hapo.

Vilio vya wananchi kuhusu kunyimwa haki zao baada ya sheria kupindishwa ni vya muda mrefu. Na kibaya zaidi, haki ya anayestahili inapokonywa na mtu mwingine ambaye anatoa rushwa kwa Jaji au Hakimu ili apindishe sheria.

Tunaungana na Jaji Mkuu Mstaafu, Samatta kwamba inasikitisha sana kuona watendaji hao wakipokea rushwa ili kumnyima haki anayestahili.

Ni vema watendaji wote waliokabidhiwa dhamana katika ngazi zote wahakikishe wanatoa haki sawa kwa wote bila upendeleo wala ushawishi wa aina yoyote.

Yapo matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa hakimu au karani katika mahakama fulani amenaswa katika mtego wa kupokea rushwa.

Matukio haya, bila shaka yako mengi na yanayofanyika katika usiri mkubwa. Matokeo yake ni wananchi wengi wanaotafuta haki kuishia patupu na wakati mwingine kufa masikini.

Hilo ni changamoto kubwa kwa Jaji Mkuu mpya. Kama alivyoashiria mwenzake aliyestaafu kuwa tatizo la rushwa bado lipo, tunaamini kwamba uongozi huu mpya utajipanga vema kama ulivyoahidi kupata kiini cha rushwa katika mahakama zetu.

Kama ni mishahara midogo kwa watoa haki hao, hilo litizamwe. Au kama ni tamaa tu ya utajiri kupitia migongo ya wanyonge wanaopigania haki, nalo litizamwe ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Ni matumaini yetu kwamba wafanyakazi wote wa Idara ya Mahakama watatoa ushirikiano wa kutosha kwa Jaji Mkuu mpya katika kupambana na rushwa, kero ambayo imelalamikiwa na wananchi wengi kwa muda mrefu sasa bila kuonyesha dalili ya mafanikio.

SOURCE: Nipashe
 
Ninachofahamu mimi kazi ya media ni kutoa habari, na hii ni habari tena habari muhimu kwani inahusu mstakabari wa Taifa na watu binafsi. Hivi hatuoni kama kunawatu wanataka kutuingiza kwenye makundi ya kidini na kikabila?. Tukifikia mahali pa kususia bidhaa za mtu/watu kwa misingi ya kidini tutaliharibu taifa ni litaadhiri wafanya biashara wengi hivyo kuhujumu uchumi wa nchi.

Kwa maneno ya huyu mwenyekiti wao kwamba watawaomba Wakristo wasusie huduma za ITV kwa kuwa wametangaza kikao kilichokuwa kinajadili kwa siri mambo ya OIC, kadhi na ukabila mbona kichekesho? si ndo Wakristo watapenda zaidi huduma ITV?

Mambo haya yanahitaji umakini mkubwa, ninadhani hawa Ndg. wamekosa uvumilivu, walichopaswa ni kwenda mahakamani endapo wanahisi kutotendewa haki. otherwise, tunaelekea pabaya.

Heshima Mkuu

Unajua haya masuala ya kiroho na imani ni magumu sana. Tuhuma ya kufanya kikao cha siri kwa nia ya kupanga namna ya kuleta machafuko nchini ni kubwa sana. Inaweza kuwa sambasamba na Uhaini. Na hawa waliotuhumiwa na ITV kufanya vikao hivyo ni VIONGOZI sio hata waumini wa kawaida.

Nimejaribu kufikiria mantiki ya Mwenyekiti kusema watawashitaki IPP/ ITV kwa Waumini wa dini zote ili wasusie bidhaa zao nashindwa kupata jibu.

Naelewa mantiki ya kusema wataiombea dua ITV ili isifanikiwe; kwa sababu hatua hii ni ya kidini au ki-imani na huyu ni Mwenyekiti pia ni kiongozi wa dini.

Hainiingii akilini kabisa kwa nini viongozi hawa waliopewa tuhuma wasiwapeleke ITV mahakamani kwa lengo la kusafisha hadhi yao na kuifundisha adabi ITV; tena bila hata kutoa muda wa kuombwa radhi..!!
 
Yebo Yebo,
Naona watu mnazidi kupotosha hoja hapa...
Kwanza kabisa habari imezungumzia waislaam kukutana kuzungumzia maswala ya OIC, mahakama ya kadhi na Ukabilai hiyo ndio tuseme ilikuwa agenda ya mkutano.. Hilo halina taabu kabisa kwangu na wala sio jambo tunalolipigia kelele unless nyie ndicho kilichosumbua... Na nimesema itakuwa ajabu ikiwa kuwepo kwa mkutano huo unaohusu OIC na Mahakama ya kadhi ndio imebeba kichwa cha hoja hiii yaani Mkakati wa Mamluki Wafichuliwa na maswala ya Udini..kwani ni maswala haya nyote huko nyuma wakati tunazungumzia kupitia serikalini mlipinga sana na kudai yabakie ya dini inayohusika... Hivyo maswala haya hayakuwa ktk huo mkutano wa siri..

Niliposoma report ya Mwanakijiji nilijua haikuwa Udini mkusanyiko wa hao viongozi kuzungumzia maswala ya OIC na Mahakama ya kadhi kama mlivyopendekeza isipokuwa kuna jingine lililojificha ndani ya mkutano wa siri ambalo ndilo linaleta Udini..

Hapa ndipo Utata wa habari nzima umeanza na kama utasoma maelezo ya viongozi waliohudhuria mkutano ule wamesema walikutana kweli, hakuna kati yetu aliyesema hawakukutana. Kulikuwepo na Mkutano kweli Ijumaa hakuna aliyepinga isipokuwa kichombezo kilichoongezwa ambacho ndicho kimewaudhi wengi iwe kwa kuunga mkono ama kupinga Utunzi wa hizo hadithi za Mkakati wa Udini na Ukabila walengwa wakiwa Mengi na Mbowe katika maswala ambayo hata sielewi mwanzo wake.

Labda wenzangu mnafahamu vizuri swala hili tuambieni huo Ukabila unamhusu Mbowe na Mengi umeanza wapi? Kama ni Chadema hawa viongozi wa dini sio wanachama na haiwahusu ktk dini kwani hiki ni chama tu... tutajadili sisi hapa JF kwa sababu kuna nafasi ya kutazama pande mbili za shilingi..Ni mjdadala.. Iweje watu wakutane, kisha waandishi wa habari wawafuate hadi Hotelini kwa usiri ikiwa kweli nyie mwenyewe hamna matatizo na mkusanyiko huo!.. Je, ni mara ya kwanza wamekutana? hapana iweje leo iwe swala la kufukuziwa hadi video huku mkidai kwamba wao ndio wadini kufanya mikutano ya siri hotelini na mkajenga hadithi nzima wakati hamkuwepo hata karibu na mkutano huo wa siri!.

Haya naona tena kumezuka swala la Waislaam kususia IPP/ITV, sasa mlitaka wataje chombo gani ikiwa habari hii imetolewa na vyombo hivi, kisha kwa nini mnafikiria anayetakiwa kuomba radhi ni Mengi na sio mwandishi/editor, msemaji/mwandalizi wa kipindi hicho!..Yote hii inatokna ana habari iliyotanguliwa kama jina la Megji lingeandikwa ktk taarifa iliyotangulia mngesema Megji wakati hakuna sehemu hata moja jina la Mengi limetajwa..Hili jina limeibuka wapi kama sio kutokana na hadithi ya Mwanakijiji..
Na kuhusu mahakama, mbona hata Marekani na nchi za Ulaya kuna habari za Uongo hutolewa ktk TV na watu wakataka kuombwa radhi bila kwenda mahakama!..na hata siku moja hakuna mtu aliyefikiria kwamba mlengwa ni mmiliki wa kituo hicho cha habari..Hii sheria ya kwenda mahakamani inatoka wapi? hata mimi kuna watu nimeshaomba samahani ama kuwaambia waombe samahani kwa maneo waliyosema na sikufikiria kabisa kuwa mahakama ndio sheria. Hapa JF kila siku watu tunaombana samahani mbona hamsemi waende mahakamani?.. Jamani vipi akili zetu zinaanza kuganda ama! Inashangaza sana..
 
Wakuu wote

Naanza kwa kusema watanzania ndivyo tulivyo, tunabisha kila kitu

BoT scandal ilibishiwa iliitwa habari za mtandaoni leo......
tumekuwa na kawaida kama issue ikiletwa hapa watu wanaomba number za simu za watu
mathalani RPC, MP, Slaaa, Zitto na wengine ili wapige simu wazibitishe lilowekwa hapa

Mbona uhodari huo haupo kwenye hili?????? Kuna wanaomtetea MTAWA je mmempigia simu kupata opinion zake?????? Wengine wanabisha albert sijui niko nae karibu sawa mpigie simu maana utakuwa nayo tupe maoni yake???????

Ndugu wanaJF suala hili ni hatari sio kwa mbowe ama Mengi, bali kwetu sote including hao masterminder. Kikubwa sio kuiscale kwa waislamu wote bali hawa chawa wachache..

Hao viongozi wachache wa dini waliotumika haimanishi ni waislam wote na hapa ndio tatizo la GT, Mkandara, et al kuliscale kama vile mashekh wote ndio tatizo.

Watanzania tubadilike, tabia ya kujibu swali kwa kuuuliza swali???? Tuachane na mawazo mgando kwamba kila mtu hapa anakuja kuchafua mtu, ama chama fulani, ukweli upo wazi kwenye hii habari.

Swali la kujiuliza ni mashekh wangapi waliofika Dar kwa kikao chao cha kawaida???? na ni kwa nini hao 9 walijitenga????? na kwanini walikua wanahama hama maeneo??????
Na kama hilo suala lilikua ni mjadala wa kitaifa ama kikanda, Kwa nini shekh mkuu ama baraza la waislam lisitoe tamko bali watuhumiwa ndio wanatoa tamko????

Ni nini kilikua muafaka wa kikao chao ambao tunaamini wangetoa tamko laa maafikiano ya kikao chao kwa either press, baraza la uislam ama kwa waumini wao ama kwa chombo kinachohusika??? the list is long....

Lakini napenda kutoa lawama kwa upande wa tatu sasa je jeshi la polisi, na serikali imefanya juhudi gani kuclear hii vacuum????

Je wanasubiri kama EPA baada ya mwaka mmoja ndio watu wapelekwe mahakani???? Serikali inayo machinery, resources na nguvu zote za kuchunguza na kutoa tamko within 24hrs inasubiri nini????

Je ni njama walioipanga wao sasa wanaangalia jinsi ya kuifunika kombe????? note kuna watu wa ikulu wameonekana ama kusikika kwenye video ama audio

Watanzani tutafakari beyond, mipaka ya mikoa, mipaka ya dini, tutumie ubongo na sio emotions ama feelings kwenye masuala mazito ambayo yanaweza kuimaliza nchi yetu.

Challenge: Kuna mtu anajua ni watu wangapi walioanzisha vita ya ruanda na Burundi????

Think????
 
Yebo Yebo,
Naona watu mnazidi kupotosha hoja hapa...
Kwanza kabisa habari imezungumzia waislaam kukutana kuzungumzia maswala ya OIC, mahakama ya kadhi na Ukabilai hiyo ndio tuseme ilikuwa agenda ya mkutano.. Hilo halina taabu kabisa kwangu na wala sio jambo tunalolipigia kelele unless nyie ndicho kilichosumbua... Na nimesema itakuwa ajabu ikiwa kuwepo kwa mkutano huo unaohusu OIC na Mahakama ya kadhi ndio imebeba kichwa cha hoja hiii yaani Mkakati wa Mamluki Wafichuliwa na maswala ya Udini..kwani ni maswala haya nyote huko nyuma wakati tunazungumzia kupitia serikalini mlipinga sana na kudai yabakie ya dini inayohusika... Hivyo maswala haya hayakuwa ktk huo mkutano wa siri..

Niliposoma report ya Mwanakijiji nilijua haikuwa Udini mkusanyiko wa hao viongozi kuzungumzia maswala ya OIC na Mahakama ya kadhi kama mlivyopendekeza isipokuwa kuna jingine lililojificha ndani ya mkutano wa siri ambalo ndilo linaleta Udini..

Hapa ndipo Utata wa habari nzima umeanza na kama utasoma maelezo ya viongozi waliohudhuria mkutano ule wamesema walikutana kweli, hakuna kati yetu aliyesema hawakukutana. Kulikuwepo na Mkutano kweli Ijumaa hakuna aliyepinga isipokuwa kichombezo kilichoongezwa ambacho ndicho kimewaudhi wengi iwe kwa kuunga mkono ama kupinga Utunzi wa hizo hadithi za Mkakati wa Udini na Ukabila walengwa wakiwa Mengi na Mbowe katika maswala ambayo hata sielewi mwanzo wake.

Labda wenzangu mnafahamu vizuri swala hili tuambieni huo Ukabila unamhusu Mbowe na Mengi umeanza wapi? Kama ni Chadema hawa viongozi wa dini sio wanachama na haiwahusu ktk dini kwani hiki ni chama tu... tutajadili sisi hapa JF kwa sababu kuna nafasi ya kutazama pande mbili za shilingi..Ni mjdadala.. Iweje watu wakutane, kisha waandishi wa habari wawafuate hadi Hotelini kwa usiri ikiwa kweli nyie mwenyewe hamna matatizo na mkusanyiko huo!.. Je, ni mara ya kwanza wamekutana? hapana iweje leo iwe swala la kufukuziwa hadi video huku mkidai kwamba wao ndio wadini kufanya mikutano ya siri hotelini na mkajenga hadithi nzima wakati hamkuwepo hata karibu na mkutano huo wa siri!.

Haya naona tena kumezuka swala la Waislaam kususia IPP/ITV, sasa mlitaka wataje chombo gani ikiwa habari hii imetolewa na vyombo hivi, kisha kwa nini mnafikiria anayetakiwa kuomba radhi ni Mengi na sio mwandishi/editor, msemaji/mwandalizi wa kipindi hicho!..Yote hii inatokna ana habari iliyotanguliwa kama jina la Megji lingeandikwa ktk taarifa iliyotangulia mngesema Megji wakati hakuna sehemu hata moja jina la Mengi limetajwa..Hili jina limeibuka wapi kama sio kutokana na hadithi ya Mwanakijiji..
Na kuhusu mahakama, mbona hata Marekani na nchi za Ulaya kuna habari za Uongo hutolewa ktk TV na watu wakataka kuombwa radhi bila kwenda mahakama!..na hata siku moja hakuna mtu aliyefikiria kwamba mlengwa ni mmiliki wa kituo hicho cha habari..Hii sheria ya kwenda mahakamani inatoka wapi? hata mimi kuna watu nimeshaomba samahani ama kuwaambia waombe samahani kwa maneo waliyosema na sikufikiria kabisa kuwa mahakama ndio sheria. Hapa JF kila siku watu tunaombana samahani mbona hamsemi waende mahakamani?.. Jamani vipi akili zetu zinaanza kuganda ama! Inashangaza sana..

ara mimi sio mwandishi wa habari

lakini unapopata habari unafilter kile unachotaka kusema vingine unaachana navyo. So mimi na wewe hatujasikia wala kuona video, hatujui kwenye mazaungmzo yao walimtaja mengi ama mbowe mara ngapi na waliamua kufanya nini juo yao.

So mimi bado nitaamini hiyo habari ni sahihi mpaka pale tunapopata video, tape ama chochote nikasikiliza nikaridhika kwamba hawakuwa na mpango wa kuwadhuru ama kuwachafua walengwa.

Evidence ya kikao kipo na wamekiri, content ya mazungumzo wanayo watoa taarifa na participants. Je mimi na wewe tunabishana kwa lipi Mkandara????

you can do better than this
 
Mkuu Mkandara, heshma kwako, naheshimu sana michango yako kwani imejaa hoja na siyo vioja. Hata hivyo naomba kukuuliza yafuatayo;-
-Je, unaunga mkono tishio la kwamba watawashawishi Waislamu na Wakristo kususia ITV?
Sharti tukajua kwamba Wakristo hawatashawishika kutokana na sababu za mkutano huo ni OIC.
-Huoni kama kufanya vikao vya siri kujadili udini na ukabila tena vikihusisha watu wazito na
na waliokaribu na Rais, ni jambo la hatari na linatishia umoja wetu katika Taifa?
 
Bowbow,
Tunachobishana hapa ni habari ya Mwanakijiji ambaye hana tape wala hajaiona...hilo kwanza.. Pili ukisoma hoja nzingi humu zinazungumzia zaidi mkutano wa OIC na mahakama ya kadhi jambo ambalo hakuna anayebisha isipokuwa kipengele kilichoongezwa..
Nimekipinga, wahusika wamekipinga na wewe unakiunga mkono wakati hujaiona hiyo Video..wakati huo huo nyie siku zote ndo wa kwanza kuomba ushahidi kwa habari yoyote ile leo imekuwa mtuhumiwa a prove innocent hata kama hakuna ushahidi...
Tatu nashangaa mnaposema waende mahakamani wakati IPP/ITV wenyewe hawajasema lolote kuhusiana na ukweli wa habari hiyo..
Kwa nini msipate kuhakikisha kwanza kuhusiana habari hiyo kabla ya kuunga mkono wakati mnajua kabisa Udini ndio tamko zito lililobeba uzito wa mada hii..
 
Kutoa habari ambayo inaigawa nchi kuliko kitu kingine chochote kile inabidi kuchukuliwe kimakini sana. Sisi Watanzania dini inatugawa sana kuliko kingine chochote, hivyo kama waandishi wa habari watakuwa wanaandika au kusambaza habari ambazo hawajazifanyia kazi kujua ukweli wake basi kuna hatari nchi inaweza kuingia kwenye machafuko na mwisho wake ukawa na athari kubwa sana. Kwani hao ITV wangesubiri hata siku mbili au tatu kuichunguza habari hiyo kwa makini kabla ya kuitangaza kwa Watanzania kungekuwa na kosa gani? Sasa msemaji wa ITV anaingia mitini kukwepa wanahabari ili kupata more info kuhusiana na habari iliyotangazwa na kampuni yake ITV. Tumeyaona ya Wayahutu na Watutsi sasa tusipokuwa makini nasi tutaanzisha ya kwetu ya Waislamu na Wakristo, na nchi yetu itakumbwa na athari kubwa sana.
 
Bowbow,
Tunachobishana hapa ni habari ya Mwanakijiji ambaye hana tape wala hajaiona...hilo kwanza.. Pili ukisoma hoja nzingi humu zinazungumzia zaidi mkutano wa OIC na mahakama ya kadhi jambo ambalo hakuna anayebisha isipokuwa kipengele cha kilichoongezwa..
Nimekipinga, wahusika amekipinga na wewe unakiunga mkono wakati hujaiona hiyo Video..wakati huo huo bdio nyie wa kwanza kuomba ushahidi kwa habari yoyote ile leo imekuwa mtuhumiwa a prove innocent hata kama hakuna ushahidi...
Tatu nasdhangaa mnaposema waende mahakamani wakati IPP/ITV wenyewe hawajasema lolote kuhusiana na ukweli wa habari hiyo..
Kwa nini msipate kuhakikisha kwanza kuhusiana habari hiyo kuunga mkono wakati mnajua kabisa Udini ndio tamko zito lililobeba uzito wa mada hii..

Mkandara,

Watu wanataka kusambaza habari nyeti 'zenye moto' ili wawe wa kwanza bila kujali athari ya habari hizo zinazosambazwa na kama zina ukweli wowote ule. Sijui kwa nini hawaoni umuhimu wa kuifanyia uchunguzi zaidi habari hiyo na kuja na kitu chenye uhakika zaidi. Hili ni hatari sana kwa nchi yetu hasa kama habari hiyo inahusiana na udini au ukabila. Hopefully hao ITV watatoa ushahidi zaidi kuhusiana na habari waliyoisambaza vinginevyo watakuwa wamejiwekea dosari kubwa sana.
 
Nziku,
Hap mkuu umeniacha nje kabisa..kwa sababu unataka maoni yangu kuhusiana na hisia za viongozi hao..
1. Kama nakubaliana na kuomba waislaam na wakristu kususia IPP/ITV..
Mkuu sielewi mipango ya Bongo kwani huko nako kila kitu ni possible, sio huku. Huwezi kuwambia wananchi kwa kupitia dini wasiangalie TV station fulani wakakuelewa...
Swala la Wakristu kutokubaliana na maombi haya mimi binafsi kutokana na mawazo mengi hapa JF bila shaka nakubaliana nawe kuwa haliwezekani, kwani mawasiliano kati ya Waislaam na Wakristu -Tanzania imeharibika kabisa..
Kinachonishangaza ni pale tu unaposema wakristu hawatashawishika kwa sababu issue ni OIC, jambop ambalo nilitegemea wakristu wangeunga mkono kuona swala hilo linashughulikiwa na dini sio tena serikali.. Hivi nikuulize wewe ulitegemea waislaam wafanye nini baada ya OIC kuwa na Utata kupitia serikali..Hata hivyo halikujadiliwa hivyo hapakuwepo na mkakati wowote.

Kisha mkuu wangu bado unapotosha habari.. kumbuka kuna issue mbili hapa.
Ya kwanza ni hiyo ya mkutano unaohusu OIC na mahakama ya Kadhi, agenda ambazo zilikuwa zinafahamika hata kabla ya mkutano, hivyo haikuwa siri na wala sio UDINI kwani ni maswala ya dini yakijadiliwa na viongozi wa dini..Huo UDINI unakuja wapi?..si ndivyo mlikuwa mkisema toka mwanzo au dau limegeuka sasa hivi...hapa mkuu hata sikuelewi..

Maswala haya haya yalipokuwa serikalini yalisemekana kuwa ni UDINI kwa sababu serikali haiwezi kuangalia maslahi ya kundi moja la watu..sasa hilo kundi wanajadili wenyewe bila serikali bado ni Udini.. kitu gani wanahcoweza kufanya isiwe Udini!

Halafu kuna hiyo issue ya pili ambayo ni mkutano wa siri unaokwenda nje ya agenda hizo na kuzungumzia baadhi ya watu specific kwa nia mbaya..hapa ndipo mimi nimetoa hoja zangu nyingi kuhusiana napo lakini baadaye nimekuja gundua kumbe tatizo sio hili tu kumbe hata issue ya kwanza ni Nongwa vile vile..

Mwisho, Unaposema vikao vya siri inabidi unifahamishe vizuri..Kikao cha siri watu wanaalikana bila kuwepo na taarifa za mkusanyiko wao, tofauti kabisa na issue ya kwanza. Mkutano huu ulifahamika kuwepo isipokuwa issue inazidi kuwa nzito pale tunzi zilipoongezeka kuwepo kwa MKAKATI ambao hakuna hata sehemu moja umeonyesha unahusu OIC ama mahakama ya kadhi. Kwa hiyo MkAKATI wa hawa mamluki unaozungiwa ni wa pili ambao najaribu kuuangalia kuhusiana na UDINI ama UKABILA sioni hata hoja moja ya ukweli wala inayoonekana kukaribia ukweli..
Mkuu nimeuliza maswali mengi sana kuhusiana na mkutano huu wa siri hakuna mtu aliyejibu kitu zaidi ya kunitolea nje kwa sababu hamna habari yoyote zaidi ya hii iliyowekwa hapa JF..

Ni kitu gani kilizungumzwa kuhusiana na MBOWE, hamjui lakini bado mnaamini walikuwa na njama dhidi yake kwa sababu jina lake lilitajwa. NI habari gani inamhusu MENGI ilijadiliwa - hamjui, isipokuwa mnaamini ni kuna njama sio tu dhidi ya hao watu bali Taifa zima.. how? Hamfahamu lakini mnafikiria inawezekana.....
ndipo naposema hivi tuwe makini na habari kama hizi zinatugawanyisha zaidi ya kutuunganisha. Chadema leo wana uhusiano mzuri tu na CUF na kumeonekana maendeleo mazuri tu ambayo pengine ni hatari sana kwa CCM ijapo 2010. hakuna njia ya kuwagombanisha isipokuwa kwa kutumia dini. Chadema inasemekana ni wakristu na CUF inasemekana ni waislaam. Hawa hawawezi kukaa zizi moja kam UDINI utaingizwa... Adui wa Mengi anajulikana tena jina lake pia lilitajwa (kulingana habari iliyotangulia) isiwe yeye ila dini na Ukabila.. na adui wa Mbowe (Chadema) wanajulikana iweje viongozi wa kiislaam ndio watumiwe ktk hili wakati they can't do a thing kama viongozi wa dini?..Kwa hiyo watu wakajenga hoja na bahati mbaya inapokelewa..

Kumbukeni vizuri mwaka 2004 kulikua habari hapa zikitoka kwa sheikh mmoja kuhusiana na Sheikh Kassim Bin Jumaa alihusishwa na mkutano wa siri kati yake na Kighoma Malima na chama cha CUF kuleta machafuko nchini..Lilikuwa swala zito na wakristu wengi waliingia mkenge tena wengine hapa hapa kijiweni.
Nilikuwa wa kwanza kupinga hoja hiyo kwa sababu tarehe walizozitumia ktk mikutano hiyo Sheikh Kassim Bin Jumaa tayari alikuwa kesha kufa.. kuna watu humu walinibishia sana hadi siku habari hiyo ilipotoka magazetini..
Kwa hiyo wakuu tuwe makini haya maswala ya dini ni mazito sana na kutumia neno UDINI mkidhani ni msemo fulani wa kufurahisha, basi tuna wakati mgumu sana huko mbele, kwani sidhani kama tafsiri ya neno hili inatumika ipasavyo..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom