Mkuu BAK nakuaminia kwa mambo mengi, na kwa hili naona hujanielewa tu sina tofauti na wewe kabisa na haya ninayoandika si ya kusikia nina uhakika nayo 100%. Take it from me. Kama unavyosema Tanzania hatuna tatizo la ukabila na udini na ndio maana najitahidi kupigana kuhakikisha wanaotaka kuchoche huo udini na ukabila wanadhibitiwa.
Kwa taarifa yako sasa nimesikiliza mazungumzo yote ya hao wanaojiita mashehe na nimetizama tape zote za hao wanaojiita mashehe za huko katika vikao vyote vya Regency Hotel, Golden Tulip, Falcon Restaurant, Kinondoni Mtaa wa Kazima namba 38 na hata juzi na jana walipokuwa wakigawana pesa pale Lumumba. Najua hata nani aliyekwenda Songe, najua nani aliyekwenda Radio Kheir, najua pia ni shilingi ngapi wamepewa. Sasa ninaposema kwamba hawa jamaa wanachofanya hakina maslahi kwa nchi hii na ni hatari kwa hatima yetu kama taifa lililoshikamana.
Nimesema awali mimi ni Muislamu na sikubaliani nao hawa jamaa na hata miongoni mwao hawakubaliani na wanavyokwenda. Pamoja na kwua Muislamu, nina familia ya dini tofauti wakiwamo watoto, ndugu na marafiki wa karibu sana na tunaishi kwa amani. Hata hayo makabila ndio usisema kuna walioolewa Afrika Magharibi na katika dini nyingine. Hiyo ni kwa wengi wetu kwa hiyo si vyema kuruhusu mijadala ya ukabila hadharani ni HATARI.