HEBU tuweke kumbukumbu sahihi, na waliotizama ama kusikiliza ile habari ya ITV usiku wa Jumatatu saa 2.05 na saa 4.40 pamoja na Jumanne asubuhi watakubaliana nami pasi shaka kwamba haikuwa na hata chembe ya neno "waislamu" wala "Mashehe" wala haikumtaja MEngi wala Mbowe ila ilitumia kikundi hicho, kuchafua watu. Hata aliyepost hii thread hakuwa anaelewa mantiki ya habari husika ndio maana akaweka maswali kibao kabla ya Mzee Mwanakijiji hajaweka habari yake ya KLHNews.
Naona hawa mashehe hawakusikiliza habari yenyewe wamesimuliwa na kama walisikiliza hawakuwa makini na hivyo walisikia wanachofikiri na si wanachoona na kusikia ama wamesoma JF na habari ya KLHNEWS wakaitumia.
Pia naona humu JF wameingia kwa nguvu na wanapambana kujitetea na kupotosha. Inawezekana ama Albert, Mtawa ama wafuasi wao wako busy humu JF kubadili mwelekeo na kupotosha na bahati mbaya sana HAbari Leo wameandika habari bila kusikiliza tape/habari ya ITV its soo sad, gazeti la serikali kutumika kama lilivyotumika jana kumlinda Makamba.
Ni aibu na serikali kama Taasisi kutumika kama ambavyo lEO TBC1 itatumika kutoa taarifa ya Press Conf hiyo ya huyo anayejiita Mwenyekiti ni hatari sana kama serikali kama taasisi ya Watanzania wote bila kujal dini, itikadi wala kabila haitajitenga na uovu huo. ITV haikumtuhumu mtu wala dini ilisema kuna njama za kuchafua watu kwa msingi ya dini na ukabila jambo ambalo wahusika wamekiri na kazi wameianza katika radio ya Kiislamu iitwayo Radio Kheir FM tokea Jumanne usiku.
Mwanakijiji anasema:-
KLHN yaweza kuripoti kwa uhakika kabisa kuwa mpango wa kuanzisha uchafuzi wenye mlengo wa kidini na kikabila nchi umeundwa na sasa umefichuliwa. Mpango huo ambao unawahusisha watu mbalimbali wenye majina makubwa umedhihirika kuanzia siku ya Ijumaa iliyopita.
Mpango huo ulianza kusukwa wiki chache zilizopita na hatimaye kuanza kutekelezwa siku ya Ijumaa iliyopita. Kwa wanaokumbuka siku ile (ya Ijumaa) kulikuwa na mkutano wa Waislamu kuelezea masuala mbalimbali ya maslahi yao na hasa suala la OIC. Baadhi ya viongozi wa Waislamu toka mikoani walikuwa jijini pia.
Ilikuwa ni katika nafasi hii timu iliyokuwa imeanza kukusanywa iliweza kuwakutanisha viongozi mbalimbali hao wa Waislamu kwa kuandaa mkakati kamambe ambao kwa madai yao mipango yake inatoka ndani na juu kwenye serikali. Katika kufanya hivyo viongozi kama 9 hivi wa Kiislamu waliweza kupatikana na kukutanishwa katika hoteli ya Regency siku ya Ijumaa.
Miongoni mwao ni mashehe na viongozi wengine wa kidini; baadhi yao ni pamoja na Shekhe Mazinge, Mwaipopo, Said Liko, Chifu Msokwa, Ustaadh Twaha, Dr. Salehe, Abubakar Bonde, Sheikh Amour Jongo, Rajabu Jazba, na Ustaadh Ramadhani. Waliokuwemo kwenye mkutano huo pia ni pamoja na Albert Marwa (inadaiwa ni mtoto wa kulelewa wa Generali Marwa) pamoja na mtu mmoja aitwaye Mtawa (huyu yasemekana ni mtumishi wa ngazi ya Juu ikulu). Walikuwepo baadhi ya watu wengine ambao wanadaiwa kuwa ni maafisa wa Usalama wa Taifa ambao kutokana na sheria hatuwezi kuwataja majina yao.
Kumbe kwa mujibu wa HALISI, ITV hawakusema huo mpango ni wa Waislamu, kwa maana hawakutaja "waislamu" wala "Mashehe" bali walitumia kikundi hicho. Na pia haikuwataja Mengi wala Mbowe. Sasa hizi habari za KLHN ya kwamba walikuwa wanataka kuwaonesha waislamu kuwa Bw. Reginald Mengi na Freeman Mbowe ndio maadui wakubwa wa maslahi ya Waislamu nchini, zimepatikana wapi?.
Hapa kwa mawazo yangu kuna jambo linapikwa, kwanini?, kufanya kikao TZ haikatazwi, si kila kikao ama mkutano unaomba kibali, mfano kuna vikao vya kuchangia harusi, vikao vya kusherehekea kipaimara, vikao vya kamati za ushindi (Friends of Simba, Yanga Family n.k), vikao vya vijiweni, hivi vyote huombi ruhusa hata siku moja. Na kuvifanya hivi vikao sio lazima vitangazwe watu wote wajue kuwa kuna kikao kitakaa sehemu fulani, na kutotangazwa kwake hakuvifanyi kuwa vya siri, na hata kama vitakuwa vya siri haviwi haramu. Sasa swali linakuja, hivi vilikuwa vikao vya siri (kama kweli), then mtu aweze kunasa matukio yote mpaka sauti, hapa kuna kitu kikubwa kimefichwa. Kuna WATU WANATUMIWA KWA MASLAHI MADOGO YA KWAO, LAKINI HAWALIANGALII TAIFA. Kulikuwa na msuguano kati ya Mengi na Manji, isijeikawa kuna kutaka kusukumiwa bomu hapa, ili kuondoka katika mada muhimu.
Nikisema kweli, kama alivyoandika Halisi (Maandiko yake juu), kuwa ITV walisema ni kikundi hicho hapa ningeona kuna fare, lakini hili la Mwanakijiji na KLHN kusema moja kwa moja ni mpango wa Waislamu sikubaliani nalo, kwa kuwa tu anadai na siku ile kulikuwa na Mkutano wa Waislamu. Nimefuatilia hili, hawa jamaa hawakuhudhuria huo mkutano (uliofanyika Kidongo Chekundu) wa Waislamu, na kama walihudhuria walikuwa sio wazungumzaji. Hivyo kama walikuwa wanazungumzia hayo hayahusiani na mkutano ule wa Kidongo Chekundu ambao Mwanakijiji anataka kuonesha kuwa matukio hayo yalitokea siku moja. Na kwa ushahidi Mkutano wa Kidongo Chekundu uliripotiwa na Gazeti la Mengi la The Guardian (
Muslim clerics warn govt on OIC stance). Ndani ya mkutano huo viongozi maarufu wa waislamu kama Shehe Baswalehe, Amir wa shura ya maimamu, Shehe Kundecha nk walikuwepo
Turudi kwa kunasibishwa suala ama masuala ya Waislamu wachache kuwa ni ya Waislamu wote. Wakitoka watu wenye imani ya kiislamu, wakaenda wakamwibia Baba Askofu. Mwandishi wa kwanza akaripoti hivi, Kundi la majambazi limevunja nyumba ya Baba Askofu na kuiba kila kitu, pia limefanya kitendo haramu cha kumnajisi shemeji wa Baba Askofu, then ikajulikana wote ni waislamu. Na mwandishi wa pili akaripoti, Waislamu wavunja nyumba ya Baba Askofu na kuiba kila kitu, oia wamefanya kitendo haramu cha kumnajisi Baba Askofu. Hapa katika hawa waandishi wawili wote wanafikisha ujumbe wa kuibiwa Baba Askofu na kufanyiwa tendo baya kwa shemeji yake, lakini kuna tofauti kubwa kati ujumbe utolewao kwa hao waandishi wawili. Hivyo siku zote hata kama Waislamu ama muislamu akifanya kosa, sio kuwajumuisha wote. SISEMI KUWA WALIOTAJWA WAMEFANYA KOSA, mpaka uletwe ushahidi bayana hapa.