Tuwe makini tunapokutana na upinzani usio na msingi katika mijadala muhimu.Hapa kuna mkundi kadhaa ya wanaojitahidi kui-discredit topic hii au kuilazimisha ibadili mwelekeo.
Kwanza kuna wale usual critics ambao nadhani kutokana na obession na useless criticism wanaweza hata ku-criticise their actual dates of birth or hawa wanajulikana.Wanachojua wao ni kupinga tu.In most cases,hawaji na topic mpya bali huvamia na kupinga tu.Hawa tumewazowea.
Kundi la pili ni wale wanaopinga kwa minajili ya kupata habari zaidi.Baadhi yao wanaweza kuwa vikaragosi wanaoshinda hapa kujua kinachoendelea.Wanatumia ujanja wa kubisha ili kupata habari zaidi.
Kundi jingine,na hili ni la hatari,ni wale wanaohusisha habari hii na "vita" dhidi ya dini flani.Hawa ni kama waumini wenye msimamo mkali.Ukitaja imani yao,hata kama ni kwa nia nzuri,basi umewachokoza.Hawapingi mada hii kwa vile wana ushahidi kuwa huu ni udaku lakini kwa vile hawataki kuona imani yao inaguswa.Jina jepesi la hawa ni WADINI,na huenda wana-wish uharamia unaozungumzwa kwenye mpango huu ungefanikiwa.
Kundi la mwisho,ambalo linashabihiana na la pili na la tatu ni hawa wenzetu wanaojifanya wanajua kila kitu.Kwa wao,kilicho sahihi ni kile wanachokifahamu wao tu.Pia akitajwa mtu ambaye ni rafiki kwao basi mada nzima ni uzushi.Pengine wanapaswa kujiuliza hivi:kama mtu anaweza kuwa cheated na mkewe without their knowledge,kwani rafiki/mtu unayemfahamu asiweze kuwa anajihusisha na mambo ambayo wewe unayamini ni rafiki yake huyajiu?Who's more closer to you,wife au rafiki?
Mwanzisha mada aliiweka habari hii kwa nia nzuri ya kuhabarishana na kupata data zaidi.Mwanakijiji akatupa data zaidi.Wenzetu huko nyumbani wameiona kwenye tv.Baadaye watuhumiwa wamekanusha kwenye gazeti (na sio kukanusha kuwa hawakukutana au hawakuzungumzia OIC,Udini na Ukabila)....lakini kuna wenzetu hawataki kuamini mpaka habari hiyo iwe kwenye youtube!!!This cant be serious.Mbona hata hotuba ya juzi ya JK kwa taifa haiko kwenye youtube na same youtube-addicted critics hawabishi?