Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Hivi karibuni nilibahatika kupita katika nchi ya wadachi baada ya kutoka Tanzania. Katika safari hii huko Udachini jijini Amsterdam, nilijiuliza mara nyingi kama kweli watanzania tuko tayari kuwa na demokrasia na uhuru tunaoutaka. Pengine hatuelewi tunachokitaka na pale tunapoonjeshwa hali halisi, tunakurupuka na kulalamika; tusijue la kufanya kwani hatukujiandaa.

Fikiria hivi, kila mtaa kuwe na mgahawa wa kuvutia bangi na madawa ya kulevya, kuwepo na mtaa ambao ni mahsusi kwa malaya kufanya kazi zao huku wakilindwa na polisi na serikali kuwatoza kodi (achilia mbali kipato kitokanacho na utalii wa kuja kuona malaya hao). Hizi shughuli zote, kwa wenzetu, ni haki za binadamu na demokrasia ya kuchagua hali ya maisha mtu atakayofuata.

Mahali paliponifurahisha zaidi, ni makumbusho ya nyumba ya Anne Frank. Anne Frank alikuwa ni mtoto wa kiyahudi aliyekuwa akiandika kuhusu maisha yalivyokuwa wakati wayahudi wanaangamizwa na sera za Hitler na wafuasi wake. Katika jumba hili la makumbusho, pamoja na kuruhusu kuonesha sehemu Anne Frank na familia yake walipojificha na mbinu walizotumia kuishi mpaka wakakamatwa, kuna sehemu ya mwisho yenye ukumbi wenye onesho liitwalo "Freedom2choose". Katika onesho hili, projekta inaonyesha habari teule zilizotokea duniani na kuuliza watazamaji kama wanafikiri habari/jambo waliloona kuwa ni haki au si haki. Kuna mifano mingi inayogusa issue muhimu kama vile uhuru wa kuabudu [swali lake ilikuwa kuvaa nguo zenye kuonyesha dini ya mtu kazini (kama vile hijabu kwa waislamu, kilemba kwa singasinga na yamulke kwa wayahudi) ni vizuri au inakiuka uhuru wa kuabudu]; nyimbo zenye chuki dhidi ya mashoga na wasagaji; uchomaji wa bendera n.k. Watazamaji wanapewa takriban nusu dakika kubonyeza kitufe cha ndio au hapana halafu projekta inaonyesha maoni ya watazamaji hao.

Sikusudii kuwachosha na habari za safari yangu bali nakusudia kutoa changamoto ya kufikiri kabla ya kulipuka na kuanza kushutumu watu au ukweli. Kutokana na mtiririko wa threads niliouna, nimegundua kuwa wengi wetu tunataka mambo ambayo hatuyajui kwa kina na wala hatuelewi maana yake. Zaidi ya hapo, hatukubali kutokukubaliana. Kwa mfano, kuna ubaya gani kwa watu wa dini moja kukutanika kwa lolote lile? Hakuna. Tena, kuna ubaya gani kwa chombo cha habari au mtu mmoja kutafuta habari kiupelelezi na kisha kuutangazia umma? Hakuna! Je, sio sisi ndio tulilalamika kufungiwa kwa Mwanahalisi na uonevu wote wa vyombo vya habari? Inakuwaje tena habari ikiandikwa yenye kutugusa (iwe ni dini, itikadi, kabila au jinsia) basi tunageuka kuwa mbogo?

Kama tunataka demokrasia na uhuru wa kweli, basi, tuwaache wenye kutafuta habari na watafute. Tusijiulize kuwa wanatafuta habari kwa minajili gani. Kama hatukubaliani nazo basi na tukanushe kistaarabu na kibinadamu. Kama tunaona ni udaku, basi hatuna ulazima wa kuzisoma. Na kama tunaona tumedhalilishwa, haki haikutumika na tunanyanyasika, basi, mahakama itatoa haki (hopefully). Lakini, tusianze kusomeana dua au kuhamasisha serikali ifungie gazeti/chombo cha habari au kuhamasisha watu wasusie watu au bidhaa.

Kumbuka, leo huyo anayeondoa uhuru wa habari leo, unampa nafasi ya kukuamulia uwe na dini gani kesho, kabila gani liongoze nchi keshokutwa na kabla hujang'amua, tunakuwa na chuki kama majirani zetu wa Rwanda na Burundi miaka michache iliyopita au vifo vya Wayahudi katika vita kuu ya pili.

Rabuka Mtukuka atupe hekima na kutuepushia balaa hili tunalolitafuta kwa kasi na ari mpya!
 
sasa watu watajuaje kuwa wewe si mmoja wa hao viongozi wa CCM au Chadema au mfuasi mmojawapo ambaye naye amenunuliwa na Wamarekani?

Watanitambua kwa matendo yangu na ninayosema .Nasema huu ni mpango wala si wa dini fulani bali ni mkakati wa chama Mfilisi.

Waswahili wanasema:what u speak is what u think and eventually the same become part of ur life.

Mimi nasema wazi na huu ndio ufuasi wangu CCM imeshindwa kuongonza nchi hii ni kwa sababu imetekwa vivyo hivyo CHADEMA kimetekwa na viongozi wajuu kabisa ambao ni mafisadi fulani wameiga staili ile ile ya MAFISADI wa CCM.

Angalia Mtikila alivyo washutumu nawao wakamshutumu vilevile kijinga kijinga maana shetani huwa hataki deal ulifanye kiakili ili watu wasitambue.

Kama mnasubiri watanzania wezangu mabadiriko kutoka CCM ya leo na CHADEMA ya leo mmeliwa mmelamba kusiko.

Na waswahili wanasema: U Time time before time times u.
 
Tatizo letu wa Tanzania
1.Mnaamini mapinduzi yanaletwa na vyama
2.Wakuu wenu wa vyama wameshajuwa kuwachezesha KASINGAAAAA KASINDAGAAAA KAB'OKA
Vyama vyenu mfilisi vimewapendezesha kiasi cha kuwafanya vipofu .
Mimi ni mkristu lakini nawaambia OLE WETU.
Hii ISUE ni 90% ya kupikwa viongozi wa chache wa CHADEMA wanatafuta support ya wakristu kwa kumanipulate hisia zenu ,Jamani kuweni na wenye akili kama NYOKA.
Naomba kuuliza kwani viongozi wachache kabisa wajuu wa chadema hawawezi kuufadhili mpango huo kwa kuwanunua hao masheikh wenye njaa nakujidai kurecord??
CCM nao viongozi wa juu kabisa ni MAFISADI na Wamelanguliwa na Waarabu .Sasa mnakoelekea kwa ushabiki wenu wa CCM na CHADEMA umefika pabaya.Hivi vyama viongozi wao wajuu ndio wanaiua hii nchi.Badala ya kuuza sera wamekuwa mainjinia wa kupika stori na maskendo na kutoana uhai ili wawatenganishe mpate kuwasapoti.

We stupid Tanzanians who be witched us??

MkamaP, if the above post is anything to go by, you portray a typical and obviously the best example, how sad.
 
... whistling... peke yako ndio utajulikana hivyo wengine hadi tuone video!

Hiyo video hakuna kitu chochote

Kwani leo nikishuka hapo bongo na milioni kadhaa siwezi amrisha hapo baadhi ya mashekieh wakiwa wamevaa kanzu na maaskofu waki act shekieh anapanga kitu fulani ama askofu anapanga kitu fulani na kuwachukuwa video nini kinashindikana??

Hilo tukio zima lina series za KIHUNI hata nikiona picha sitokubali.
1. Waislamuu wachukie media za mengi ili iwe je? Na kwanini wasichukie mfano Radio Maria ama tumaini?
2. ina maana chadema kwa mbowe hakuna waislaamu??
Na hao mafisadi walikuwa wanaandaa huo mkakati ili iwe je? baada ya kutengenisha waislamu na wakristu kwamba hapo OIC ndio itakuja?? Huo ni uhuni tu wa vyama mflisi.
 
ndiyo maana umesema vyema ni matendo na kile mtu anasema ndicho kinatujulisha mtu huyo ni nani. Very good.
 
Hiyo video hakuna kitu chochote

Kwani leo nikishuka hapo bongo na milioni kadhaa siwezi amrisha hapo baadhi ya mashekieh wakiwa wamevaa kanzu na maaskofu waki act shekieh anapanga kitu fulani ama askofu anapanga kitu fulani na kuwachukuwa video nini kinashindikana??
.

Mkamap unanichekesha sana, yaani ukiwa na hela tu utaamrisha maaskofu wavae kanzu, ili waonekane waislamu!! yaani una confirm is possible kwa waislamu au wakristo kununuliwa na wenye hela na wakafanya lolote lile!

1. Kwa hiyo katika hili unasema hawa jamaa wamenunuliwa? na hawakuwa maaskofu, maana majina yao yanajulikana
2. Sijaona mantiki ya kuzungumzia udini, maana katika kundi hili wako wakristo pia na majin yao yapo, kama watakuwa walibadili dini basi ni kwa muda tu ili wapate hizo hela unazozisema!
3. Na kwa nini ufikirie kuwa Tz hiki kitu cha kununua kundi fulani inawezekana? wazo hilo unalipata wapi na kwa vigezo gani??
4. Jibu lolote utakalojibu swali la 3, je unafikiri haiwezi ku apply katika kundi hili? na kwa nini?

waberoya
 
Mpanda merikebu,
Waholanzi wanaruhusiwa kuwa HIGH ila si madawa makali ya kulevya. Wanachoruhusiwa ni Soft Drug na humo ndani ya soft drug ni au Marijuana aka bangi aka Nzyemu. Ila wana masharti kuwa ukishalivuta na kuanza sumbua watu mtaani basi cha moto utakiona.
Juu ya UMALAYA kwa kweli laiti ningelikuwa Rais wa Tanzania basi ningeliruhusu hata Tanzania kuwe na Kibali na kulipa kodi kwa malaya. Hata mashoga nao ukakutwa unauza na hulipi kodi ni ndani tu kwa kutokulipa kodi. Sasa tunajifanya Tz umalaya haupo na watu wanafaidika sana tu. Hii biashara ina umri kumzidi Yesu.
Mjadala wa dini kweli mkali sana. Watu wanajisahau na kujibu mashambulizi ya ujumbe alioandika kwa kutumia jina la jingine. Nimegundua kuwa watu wako busy kuingia na kutoka JF kwa majina tofauti. Mtu A anamwambia mtu B maneno xxx, B anajibu maneno YYY na ghafla unaona mtu C anakuja na kumwambia B kuwa "ujumbe wako YYY naona hukunielewa". Hapo unajua kumbe A ni C. Jiangalieni kwa hili watu wa majina x2.
Waarabu na Waizrael wanauwana kwa ardhi. Kenya nao ni ardhi na siasa na sasa hata kazi hawataki maana wana Obama. Congo wanauwana kwa madini. Columbia wanauwana kwa Unga. Mafia wanauwa kwa Mali. Dini zetu zote zimetoka kwa Waarabu (Kumbuka Izrael ni Palestine). Ila ilipofika Tanzania ndiyo ikawa kama kwamba ilizaliwa hapo. Nakumbuka maneno ya Obama kuwa watu NJAA ikizidi, hukimbilia BIBLIA (dini) na Bunduki. Naona Obama uchagzi ujao wa atakuja kusema "si mnaona Tanzania, niliwaambia mkabisha na sasa mfano mwingine ule."
Kweli tunahitaji Zuma hapa Tanzania. Tunahitaji Bush ambaye akija anasema "au uko na sisi au uko kinyume na sisi". Napendekeza ile Lindi yote iwe ni GUANTANAMO ya wazushi wote bila ya kujali Dini zao na makabila yao. Hapo KOKORO lianze kubeba wahusika na wasiohusika. Ukinaswa basi ujue "Utatumbukiamo". MkamaP nenda kalale.
 
Hii ISUE ni 90% ya kupikwa viongozi wa chache wa CHADEMA wanatafuta support ya wakristu kwa kumanipulate hisia zenu ,Jamani kuweni na wenye akili kama NYOKA.

Naomba kuuliza kwani viongozi wachache kabisa wajuu wa chadema hawawezi kuufadhili mpango huo kwa kuwanunua hao masheikh wenye njaa nakujidai kurecord??

Hili suala la kuwa ni mpango wa kutungwa kama sinema haupo, na ushahidi wa hili ni kusoma habari zilizoandikwa katika HAbari Leo na msuguano mkali humu JF. Kama walipanga wasingeanza kuishambulia ITV na utasikia zaidi maana mkakati wao unaendelea kwa kasi kubwa zaidi. Ila nafurahi kwamba element ya fedha imeanza kueleweka.

Nawatakia mjadala mwema.
 
Tatizo letu wa Tanzania
1.Mnaamini mapinduzi yanaletwa na vyama
2.Wakuu wenu wa vyama wameshajuwa kuwachezesha KASINGAAAAA KASINDAGAAAA KAB'OKA

Vyama vyenu mfilisi vimewapendezesha kiasi cha kuwafanya vipofu .

Mimi ni mkristu lakini nawaambia OLE WETU.

Hii ISUE ni 90% ya kupikwa viongozi wa chache wa CHADEMA wanatafuta support ya wakristu kwa kumanipulate hisia zenu ,Jamani kuweni na wenye akili kama NYOKA.

Naomba kuuliza kwani viongozi wachache kabisa wajuu wa chadema hawawezi kuufadhili mpango huo kwa kuwanunua hao masheikh wenye njaa nakujidai kurecord??

CCM nao viongozi wa juu kabisa ni MAFISADI na Wamelanguliwa na Waarabu .Sasa mnakoelekea kwa ushabiki wenu wa CCM na CHADEMA umefika pabaya.Hivi vyama viongozi wao wajuu ndio wanaiua hii nchi.Badala ya kuuza sera wamekuwa mainjinia wa kupika stori na maskendo na kutoana uhai ili wawatenganishe mpate kuwasapoti.

We stupid Tanzanians who be witched us??

I want to smoke whatever you have been smoking.
 
Mkamap unanichekesha sana, yaani ukiwa na hela tu utaamrisha maaskofu wavae kanzu, ili waonekane waislamu!! yaani una confirm is possible kwa waislamu au wakristo kununuliwa na wenye hela na wakafanya lolote lile!

1. Kwa hiyo katika hili unasema hawa jamaa wamenunuliwa? na hawakuwa maaskofu, maana majina yao yanajulikana
2. Sijaona mantiki ya kuzungumzia udini, maana katika kundi hili wako wakristo pia na majin yao yapo, kama watakuwa walibadili dini basi ni kwa muda tu ili wapate hizo hela unazozisema!
3. Na kwa nini ufikirie kuwa Tz hiki kitu cha kununua kundi fulani inawezekana? wazo hilo unalipata wapi na kwa vigezo gani??
4. Jibu lolote utakalojibu swali la 3, je unafikiri haiwezi ku apply katika kundi hili? na kwa nini?

waberoya

Mkuu
Fedha inaongea wacha mchezo sio kwa TZ tu ni duniani kote ila sema kiwango chake kinatofautiana kutoka na hali ya wananchi.

Kwa TZ ni rahisi zaidi ukiwa na vimilioni kadhaa tu kwa sababu maisha ya wananchi yanasikitisha.

Kwa hiyo kucheza kitu kama hicho ni kawaida kabisa.
 
Yes hata mimi nalijua hilo, ndiyo maana inawezekana kwa hawa jamaa pia!
 
Hivi karibuni nilibahatika kupita katika nchi ya wadachi baada ya kutoka Tanzania. Katika safari hii huko Udachini jijini Amsterdam, nilijiuliza mara nyingi kama kweli watanzania tuko tayari kuwa na demokrasia na uhuru tunaoutaka. Pengine hatuelewi tunachokitaka na pale tunapoonjeshwa hali halisi, tunakurupuka na kulalamika; tusijue la kufanya kwani hatukujiandaa.

Fikiria hivi, kila mtaa kuwe na mgahawa wa kuvutia bangi na madawa ya kulevya, kuwepo na mtaa ambao ni mahsusi kwa malaya kufanya kazi zao huku wakilindwa na polisi na serikali kuwatoza kodi (achilia mbali kipato kitokanacho na utalii wa kuja kuona malaya hao). Hizi shughuli zote, kwa wenzetu, ni haki za binadamu na demokrasia ya kuchagua hali ya maisha mtu atakayofuata.

Mahali paliponifurahisha zaidi, ni makumbusho ya nyumba ya Anne Frank. Anne Frank alikuwa ni mtoto wa kiyahudi aliyekuwa akiandika kuhusu maisha yalivyokuwa wakati wayahudi wanaangamizwa na sera za Hitler na wafuasi wake. Katika jumba hili la makumbusho, pamoja na kuruhusu kuonesha sehemu Anne Frank na familia yake walipojificha na mbinu walizotumia kuishi mpaka wakakamatwa, kuna sehemu ya mwisho yenye ukumbi wenye onesho liitwalo "Freedom2choose". Katika onesho hili, projekta inaonyesha habari teule zilizotokea duniani na kuuliza watazamaji kama wanafikiri habari/jambo waliloona kuwa ni haki au si haki. Kuna mifano mingi inayogusa issue muhimu kama vile uhuru wa kuabudu [swali lake ilikuwa kuvaa nguo zenye kuonyesha dini ya mtu kazini (kama vile hijabu kwa waislamu, kilemba kwa singasinga na yamulke kwa wayahudi) ni vizuri au inakiuka uhuru wa kuabudu]; nyimbo zenye chuki dhidi ya mashoga na wasagaji; uchomaji wa bendera n.k. Watazamaji wanapewa takriban nusu dakika kubonyeza kitufe cha ndio au hapana halafu projekta inaonyesha maoni ya watazamaji hao.

Sikusudii kuwachosha na habari za safari yangu bali nakusudia kutoa changamoto ya kufikiri kabla ya kulipuka na kuanza kushutumu watu au ukweli. Kutokana na mtiririko wa threads niliouna, nimegundua kuwa wengi wetu tunataka mambo ambayo hatuyajui kwa kina na wala hatuelewi maana yake. Zaidi ya hapo, hatukubali kutokukubaliana. Kwa mfano, kuna ubaya gani kwa watu wa dini moja kukutanika kwa lolote lile? Hakuna. Tena, kuna ubaya gani kwa chombo cha habari au mtu mmoja kutafuta habari kiupelelezi na kisha kuutangazia umma? Hakuna! Je, sio sisi ndio tulilalamika kufungiwa kwa Mwanahalisi na uonevu wote wa vyombo vya habari? Inakuwaje tena habari ikiandikwa yenye kutugusa (iwe ni dini, itikadi, kabila au jinsia) basi tunageuka kuwa mbogo?

Kama tunataka demokrasia na uhuru wa kweli, basi, tuwaache wenye kutafuta habari na watafute. Tusijiulize kuwa wanatafuta habari kwa minajili gani. Kama hatukubaliani nazo basi na tukanushe kistaarabu na kibinadamu. Kama tunaona ni udaku, basi hatuna ulazima wa kuzisoma. Na kama tunaona tumedhalilishwa, haki haikutumika na tunanyanyasika, basi, mahakama itatoa haki (hopefully). Lakini, tusianze kusomeana dua au kuhamasisha serikali ifungie gazeti/chombo cha habari au kuhamasisha watu wasusie watu au bidhaa.

Kumbuka, leo huyo anayeondoa uhuru wa habari leo, unampa nafasi ya kukuamulia uwe na dini gani kesho, kabila gani liongoze nchi keshokutwa na kabla hujang'amua, tunakuwa na chuki kama majirani zetu wa Rwanda na Burundi miaka michache iliyopita au vifo vya Wayahudi katika vita kuu ya pili.

Rabuka Mtukuka atupe hekima na kutuepushia balaa hili tunalolitafuta kwa kasi na ari mpya!

Mpanda Merikebu long time not see you here my friend. Maneno safi sana hapo juu....Tunaomba usipotee sana bana ama kama merikebu ikikumbwa na dhoruba tunakuombea uzima na safari zako.
 
Nadhani sasa hivi tumefikia mahala swala hili tunaweza kuliweka ktk kipimo.. nashukuru sana kusoma maelezo ya ndugu yetu Mfumwa ambaye kasema kwa ufupi sana kuelezea kile nilichopinga mimi..
Huwezi kabisa kutumia jina la dini, rangi, jinsia kwa mawazo ya kundi la watu wachache...Hii lugha nimeiona humu siku nyingi na mara zote nimejaribu kukemea lakini badala ya watu kutazama substance kujibu hoja zangu, wao huja na hoja zinazohusiana na chupa...
Mara nyingi Mtikila amekuja na maswala mengi yanayotatanisha lakini hata siku moja sijawahi kufikiria kwamba mawazo yake yana represent waumini wake..Acha huyo Mtikila tumeona viongozi wetu wengi wa kidini wakitumia nafasi zao kutangaza maswala ya kisiasa baada ya kupewa mshiko kidogo lakini bado hatuwezi kuhukumu dini ama dhehebu zima...Siwezi kufikiria hata mara moja kwamba Nyerere au Mkapa walifanya waliyoyafanya kama viongozi wanao represent mawazo ya wakristu..

Swala hili linatisha zaidi pale waandishi wetu wanapotumia jina la mtu toka Ikulu kuhusika hivyo kwa mtu yeyote mwenye akili ya kutambua.. Hoja nzima ilikuwa kuonyesha kwamba Kikwete ana mtu wake ndani ya njama hizi za Waislaam. Na vile yeye ni Muislaam, dhahiri malengo ya mikutano hii sio nzuri kwa waumini wa dini nyinginezo..
Kwa hiyo wale wote wanaofikiria kwamba mimi huwa nashikwa na jazba pale jina la Waislaam wanapohusishwa nawaomba waelewe kwamba kila wanaposema Waislaam hivi ama vile wana maana hata mimi ni mmoja wa njama hizo.. mara nyingi zungumzia wahusika, majina yao na pengine kuepuka kutumia maumbile yao, dini zao, makabila yao kujenga hoja ya maamuzi ya watu hao..
Ni ktk hali kama hii watu wengi wamevitazama vyama kama Chadema na CUF kwa rangi zake na hawajali tena kusoma dira ya vyama hivyo kulingana na sera wanazojaribu kuziuza..Na kwa bahati mbaya mawazo kama haya chama CCM wanafahamu wapi pa kuwamaliza Chadema na CUF na hakika uchaguzi 2010, kwa kutumia issue kama hizi watarudi Jukwaani..
Maswala ya dini, kabila, rangi na jinsia ni mazito sana kuliko maswala yote ya Ufisadi...nawaomba sana tuwe makini na hata siku moja msije fikiria kwamba tatizo langu ni mimi kuwa Muislaam kwani hoja sio mimi hata kidogo isipokuwa natazama kilichomo ndani ya chupa hiyo kama kinajenga ama kubomoa jamii yetu...
 
Tatizo mkuu ni hicho chama chenu mbadala
Niliwaambia siasa za chama chenu kupandilia migongo ya mifisadi kuna siku itawapandilia wenyewe.

FISADI dawa yake ni kumpeleka mahakamani full stop.Lakini kuutumia mgongo wa fisadi kujipatia umaarufu ni UHUNI MKUBWA na likikosekana li mgongo la fisadi unatafuta mbinu zingine ili ujipatie umaarufu kama hizo unazoziona.

CCM mbofu mbofu mbofu lakini CHADEMA mhhhhhhhh
 
HIvi sasa kina Mazinge wamewasili Songea kwa ajili ya shughuli hizi za kutekeleza maazimio yao. Tusubiri kusikia kitu kutoka huko labda leo au siku chache zijazo.
 
Waache waendelee na shughuli zao zenye malengo wa kuwaumbua Mungu watu na Media zao ambazo zina operate kwa mazingira ya kukadamiza wengine na ku promote Ukabila (ajenda)
Hii inamanisha kikao walicho kaa ni halali na ni-right yao ya kikatiba na agenda za vikao tutazipima sisi wananchi tusio wadini, bila kujali Majina, Machifu, Makabila, Dini nk
Unapo ona dini yako inachafuliwa, unayo right ya kuilinda hatakama unafanya kazi ikulu
Sisi wananchi ndio tutajaji watakapo present kesi yao, sasa tuache kupotosha na kutishia amani waTZ (MENGI NA MBOWE SI MIUNGU WALA MANABII LAZIMA TUWAJADILI)
 
Waache waendelee na shughuli zao zenye malengo wa kuwaumbua Mungu watu na Media zao ambazo zina operate kwa mazingira ya kukadamiza wengine na ku promote Ukabila (ajenda)

ila na wao wenyewe wasijekujikuta wanafanya kila wanachowatuhumu wengine.
Hii inamanisha kikao walicho kaa ni halali na ni-right yao ya kikatiba na agenda za vikao tutazipima sisi wananchi tusio wadini,

Umejuaje kuwa "nyie" wananchi siyo wadini?

bila kujali Majina, Machifu, Makabila, Dini nk
Unapo ona dini yako inachafuliwa, unayo right ya kuilinda hatakama unafanya kazi ikulu

That seems to be the train of thoughts in operation here..

Sisi wananchi ndio tutajaji watakapo present kesi yao, sasa tuache kupotosha na kutishia amani waTZ (MENGI NA MBOWE SI MIUNGU WALA MANABII LAZIMA TUWAJADILI)

Yeah isipokuwa miungu kina Mazinge, Mtawa na wenzao wasijadiliwe. Very good reasoning.
 
Mkuu
Fedha inaongea wacha mchezo sio kwa TZ tu ni duniani kote ila sema kiwango chake kinatofautiana kutoka na hali ya wananchi.

Kwa TZ ni rahisi zaidi ukiwa na vimilioni kadhaa tu kwa sababu maisha ya wananchi yanasikitisha.

Kwa hiyo kucheza kitu kama hicho ni kawaida kabisa.

MkamaP!
Wale wachezaji wa mpira wa miguu uliokuwa unatafuta watu hapa JF wa kukutafutia umeshawapata?
 
ila na wao wenyewe wasijekujikuta wanafanya kila wanachowatuhumu wengine.

Umejuaje kuwa "nyie" wananchi siyo wadini?

That seems to be the train of thoughts in operation here..

Yeah isipokuwa miungu kina Mazinge, Mtawa na wenzao wasijadiliwe. Very good reasoning.

Mjadala ndio democracy tunayopigania, mbaya ni anaeficha, tutawaumbua kutumia uwazi
Naamini wa TZ wengi hawana Udini kama walivyoweza kuwachaguwa wakina JK na MKapa bila kujali dini zao

Wakristo wangapi toka ikulu wanahudhuria vikao vya makanisa na kupanga mikakati chungu tele mingine ikiwa ya siri hatuja ona Vinzi vya ITV kuiripoti, ni hivi karibuni tu makanisa walikaa vikao na kutoa tamko kuusu OIC kwa nini ITV haikurecord haya?
Wakina Mazinge pia lazima wajadiliwe bila kupotosha jamii kama vile pia hatutopenda Mungu watu kupotoshwa, (Treat every one with respect regardless,,)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom