Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
“Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho,” alisema Msopa.

Na hawa wameishia wapi au ITV wameomba radhi, eh ? Tuendelee kusubiri.


Well, kwahiyo tusema story nzima ilikuwa bogus!! Kwa hapa JF mkosaji ni Mkjj na tunaomba atuwekee uptodates...ama sivyo akome kuleta habari zake za kizushi!!
 
Hili linaonekana kama ni muendelezo wa yale yale yaliyojadiliwa hapa....


Siku ya Ijumaa tarehe 14 Nov. 2008, TV ya TBC1 katika kipindi cha Kiislamu ilirusha kipindi hicho cha Ibada iliyofanyika katika Msikiti wa Manyema Kariakoo.

Katika mawaidha yake Shekhe wa Msikiti huo alizungumzia hali ya Kisiasa nchini na kutoa madai ya kipumbavu ambayo sijapata kusikia na ya hatari katika Nchi yetu. Labda nisemem mambo yaliyonishangaza kabla ya kutoa maoni yangu. Shekhe huyo (hastahili kuwa Shekhe kwa kauli zake) alidai yafuatayo mbele ya waumini na watanzania kupitia TV ya TBC1 (sina hakika kama wali-edit):-

Moja; ati kuna hila ya kumuhujumu Rais Kikwete kwa kuwa ni Muislamu na akathibitisha kwa kusema kuwa wakati wa vipindi vya utawala wa Marais Waislamu nchi hukumbwa na kadhia na hujuma dhidi yao. Alisema kuwa migomo na maandamano hufanyika mara kwa mara katika awamu hizo akadai kuwa hivyo ilikuwa wakati wa awamu ya 2 ya Ali Hasan Mwinyi na sasa awamu ya 4 wakati wa JK. Sheikh anashangaa (anayo haki) na kusema kuwa kwa nini maandamano na migomo hutokea wakati Marais wakiwa waislamu tu!

Sheikh, anajaribu kuwaambia Waislamu na Watanzania kuwa kuna hujuma za kidini dhidi ya Serikali ya JK; madai haya ni kutaka kusema kuwa Wasio Waislamu ndiyo wanasababisha na kuchochea haya dhidi ya Marais wa Kiislamu, ati matatizo anayokabiliana JK ni ya kidini! Ilikuwa hivyo wakati wa Ali Hasan Mwinyi pia!

Pili, Sheikh alidai kuwa Wasio Waislamu hawana haki wa kuwaamulia Waislamu nia yao ya kuifanya Tanzania kujiunga na OIC na kuanzisha Mahakama ya Kadhi na akatoa kauli ya ajabu sana kuwa kama Tanzania haitajiunga na OIC basi Tanzania haitakalika! Kauli hiyo aliitoa 'live' TBC1 na bila shaka Serikali na vyombo vya Usalama walishuhudia na kusikia kauli ya ajabu namna hiyo kutoka kwa Kiongozi huyo wa dini!
 
Well, kwahiyo tusema story nzima ilikuwa bogus!! Kwa hapa JF mkosaji ni Mkjj na tunaomba atuwekee uptodates...ama sivyo akome kuleta habari zake za kizushi!!

Eeeh! Akome tena, unataka afe njaa...!? Hujui kuna watu wanaishi kwa kuuza umbea?
 
“Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho,” alisema Msopa.

Na hawa wameishia wapi au ITV wameomba radhi, eh ? Tuendelee kusubiri.


Hmmmm! Kwa walalahoi ni guilty until proven innocent na kwa mafisadi ni vice versa!!! Ndiyo Bongo yetu!!!!
 
Yaani imejengeka kuwa Jambo likimhusishwa Mtu yeyote Mwenye jina la Kiislamu ama anayevaa kanzu/kofia ya kiislam Basi tayari jambo hilo ama lifanywe ni la kigaidi ama la kidini, lazima pajengwe taswira ya ubaya dhidi ya UISLAM hivi hizi propaganda zitaisha lini?
 
Jamani ushahidi toka ITV kuhusu kasheshe hii uko wapi? Mbona siku zinakatika tu hatusikii lolote!!! Kulikoni!!? 😕

...na walisema kwamba tungesikia mashamsham ya hilo grupu tuka Tunduma sijui wapi huko swekeni, lakini mpaka leo kimyaaaaaa!! na yule mtoa mada (mdini na baguzi nambari wani) yupo doro kaa kuku anayekufa kwa mdondo...

MKJJ tuletee updates za hawa mamluki!! ebo!!






OIC +MAHAKAMA YA KADHI

subject
*Assalaam Aleykum.
Enyi wailsamu wa Tanzania, mpo tayari kuondoa udhalimu wa Maaskofu? Tushiriki maandamano Ijumaa, ni haki yetu jumuiya ya kiislam (OIC), ni haki yetu kuwa na mahakama ya kadhi, kwa nini tupangiwe maisha ya kuishi? Kwa nini tuongozwe na Maaskofu?' Huu ni ujumbe unaosambwazwa kwa kasi sana miongoni mwao. Nawe sambaza ujumbe huu kwa kadiri uwezavyo, huu sio ujumbe wa kunyamaza nao!
​





There you go!



.
 
​






OIC +MAHAKAMA YA KADHI

subject
*Assalaam Aleykum.
Enyi wailsamu wa Tanzania, mpo tayari kuondoa udhalimu wa Maaskofu? Tushiriki maandamano Ijumaa, ni haki yetu jumuiya ya kiislam (OIC), ni haki yetu kuwa na mahakama ya kadhi, kwa nini tupangiwe maisha ya kuishi? Kwa nini tuongozwe na Maaskofu?' Huu ni ujumbe unaosambwazwa kwa kasi sana miongoni mwao. Nawe sambaza ujumbe huu kwa kadiri uwezavyo, huu sio ujumbe wa kunyamaza nao!
​





There you go!

.



tupendane tu jamani wakristo waislam and wapagani.... mkiangalia nini maana ya dini zote ni kuifanya dunia the better place to live wala sio mengine hivi kuna aliyeenda huko juu na kurudi kuwaeleza ni nani anayetawala?????? Mh itakuwa vipi ukiwadharau waislam then ukakuta mtume ndo anapokea wageni, na je ukikuta Yesu ndo anayepokea wageni...............
kama hili swala la OIC linaelemea dini moja zaidi na tunataka liwe la kitaifa haiwezekani Period! sasa hivi mtang'ang'ania lakini at the end hata hiyo misaada haitawafikia itaishia kwa mafisadi tu tutabaki kuambiwa zile hela zilitolewa na jumuia ya kiisilamu haziwahusu wakristo, tunamambo mengi ya kurekebisha sasa kabla hatujaanzi biashara yetu ya kuomba omba tutengeneze maghala yakuwekea hicho tunachokiomba kwanza tusije chubuka migoti kwa kuomba halafu tuweke kwenye ghala linalovuja.....Mwishowe wakristo nao watasema zikowapi .....................
 
Lazydog huna kitu hapo. Kampeni yako chafu hii haipo kwenye misahafu (Kurani). Acha kuchochea mambo yasiokuwa na tija kwa Watanzania. Pamoja na kwamba una uhuru wa maoni hayo yametoka nje ya mwelekeo na maadili ya Watanzania.
 
Lazydog huna kitu hapo. Kampeni yako chafu hii haipo kwenye misahafu (Kurani). Acha kuchochea mambo yasiokuwa na tija kwa Watanzania. Pamoja na kwamba una uhuru wa maoni hayo yametoka nje ya mwelekeo na maadili ya Watanzania.



Watu wamehoji mbona hawasikii lolote!!
Nimepokea huo ujumbe unaosambazwa kwenye email. Sifanyi kampeni mie!




.
 
Kuna watu hawana kumbukumbu: Naomba niwakumbushe (unaweza kuangalia ukurasa wa pili wa thread hii tulipoposti hii habari kwa mara ya kwanza). Hapa ninairudia nikiweka majina katika bold ili kuwafanya watu waunganishe habari zinazoendelea na hii na kuelewa ni nini kinaendelea.

Na Mwandishi Maalum

KLHN yaweza kuripoti kwa uhakika kabisa kuwa mpango wa kuanzisha uchafuzi wenye mlengo wa kidini na kikabila nchi umeundwa na sasa umefichuliwa. Mpango huo ambao unawahusisha watu mbalimbali wenye majina makubwa umedhihirika kuanzia siku ya Ijumaa iliyopita.

Mpango huo ulianza kusukwa wiki chache zilizopita na hatimaye kuanza kutekelezwa siku ya Ijumaa iliyopita. Kwa wanaokumbuka siku ile (ya Ijumaa) kulikuwa na mkutano wa Waislamu kuelezea masuala mbalimbali ya maslahi yao na hasa suala la OIC. Baadhi ya viongozi wa Waislamu toka mikoani walikuwa jijini pia.

Ilikuwa ni katika nafasi hii timu iliyokuwa imeanza kukusanywa iliweza kuwakutanisha viongozi mbalimbali hao wa Waislamu kwa kuandaa mkakati kamambe ambao kwa madai yao mipango yake inatoka ndani na juu kwenye serikali. Katika kufanya hivyo viongozi kama 9 hivi wa Kiislamu waliweza kupatikana na kukutanishwa katika hoteli ya Regency siku ya Ijumaa.

Miongoni mwao ni mashehe na viongozi wengine wa kidini; baadhi yao ni pamoja na Shekhe Mazinge, Mwaipopo, Said Liko, Chifu Msokwa, Ustaadh Twaha, Dr. Salehe, Abubakar Bonde, Sheikh Amour Jongo, Rajabu Jazba, na Ustaadh Ramadhani. Waliokuwemo kwenye mkutano huo pia ni pamoja na Albert Marwa (inadaiwa ni mtoto wa kulelewa wa Generali Marwa) pamoja na mtu mmoja aitwaye Mtawa (huyu yasemekana ni mtumishi wa ngazi ya Juu ikulu). Walikuwepo baadhi ya watu wengine ambao wanadaiwa kuwa ni maafisa wa Usalama wa Taifa ambao kutokana na sheria hatuwezi kuwataja majina yao.

Mpango huo ambao “vijidudu” vya uchunguzi viliweza kuunasa kwa picha na kwa sauti kimsingi una malengo yafuatayo.

a. Kuwaonesha waislamu kuwa Bw. Reginald Mengi na Freeman Mbowe ndio maadui wakubwa wa maslahi ya Waislamu nchini.
b. Kwamba Mengi na Mbowe wana mkakati wa kuhakikisha kiongozi anayekuja ni kutoka kabila la Wachagga. Katika hili la dhidi ya “Uchagga” wanamkakati walikuwa wana uhakika wa kutobughudhiwa na polisi kwenye mikutano ambayo waliipanga kuifanya hasa wakiamini kuwa IGP Said Mwema yuko upande wao. Hata hivyo mmoja wao aliapa kuwa aliwahi kuambiwa na Dr. Nchimbi kuwa Mwema ni Mchagga (sijui kwa upande wa mama) na hivyo wasitarajie sana.
c. Walioleta mpango huo wamemhusisha kiongozi wa juu serikalini kuwa ndiye aliyewatuma kutekeleza mpango huo hasa kuonesha kuwa vyombo vya IPP vinatumika kueneza Ukristu, kukandamiza Waislamu, na kuinua Wachagga. Hili litaelezwa ili Waislamu waanze kuvisusisa vyombo vya habari vya IPP.
d. Kuendelea kuwahusisha Mengi na Mbowe katika vifo vya Chacha Wangwe na Gavana Ballali.

Katika kutekeleza mpango huo timu hiyo ilikuwa ijipange na kuandaa bajeti ya kiasi kisichopungua shilingi milioni 100 ambazo zitagawanywa kati yao na kwa wale ambao watakuwa tayari kutekeleza mpango huo. Kiasi ambacho cha awali ambacho kila mmoja alikuwa agawiwe ni kama milioni tatu tatu huko mmoja wa wanamkakati huo akiahidi uwezekano wa kupata fedha zaidi kutoka kwa Bakhresa. Kiasi cha awali kinadaiwa kutolewa na mfanyabiashara Yusuph Manji wa Quality Group.

Siku ya Jumamosi kundi hilo la wanamkakati lilikutana kwenye hoteli ya Golden Tulip kuendelea na mipango yao ambayo ka nzi ka KLHN kalikuwa kanafuatilia kila hatua tena kwa ukaribu kabisa.

Wakiwa na magari yenye namba za usajili za T267 ABT na T87 ABG wanamkakati wakiongozwa na Mazinge, Mwipopo (spelling yaweza isiwe sahihi) na Chifu Msokwa walihamisha kikao chao kingine kutoka Golden Tulip kuelekea Msikiti wa Mtambani ambapo waliamua kubadilisha na kuelekea Msikiti wa kwa Mtoro. Ka nzi kaliweza kunasa habari za kutosha.

Siku ya Jumapili kikao chao kiliendelea huko Kinondoni mtaa wa Kazina nyumba (censored) ambapo kuanzia saa tisa hadi majira ya Magharibi waliendelea na mipango yao na maazimio yao ikiwemo la kuhakikisha kuwa viongozi watakaoshiriki katika mkakati huo wa kuitisha mikutano mbalimbali mikoani wahakikishe na wao wanapata watu angalau 20 chini yao.

Kutoka kwenye vikao hivyo iliazimiwa uitishwe mkutano wa waandishi wa habari ili kuweza kufafanua madai yao dhidi ya Mengi na Mbowe na hivyo kuanzisha mchakato huo wa kueneza propaganda hii ya udini na ukabila. Baadhi ya wajumbe walikuwa wameshaondoka siku ya Jumatatu kuelekea mikoani kuanza kazi hiyo na hilo ndilo lililosababisha vyombo vya ITV kurusha hivyo walivyonavyo.

KLHN imepata nafasi ya kusikiliza masaa ya kutosha ya mazungumzo ya kundi hili na jambo moja ambalo tunaweza kusema kwa uhakika ni kuwa linatia hofu na kuuliza tumefikaje hapa.

Hata hivyo mpango huo haujaenda vizuri kama ulivyotarajiwa hasa baada ya kutokea mabishano ya kiasi cha fedha huko baadhi ya wajumbe wakiamini kuwa Bw. Albert Marwa amepewa fedha zaidi kuliko alizowapatia wajumbe hao. Wengine wameanza kudai kuwa Bw. Marwa ndiye aliyeinjinia mpango wa wao kunaswa na vyombo vya kielectroniki.

Jioni ya leo (jumanne) ka nzi ketu kanaruka ruka mikoani kamethibitisha pasipo shaka kuwa baadhi ya simu za wahusika wakuu zimekuwa ‘tapped’ ili kuweza kujua jinsi operesheni hii ilivyoendesha kikamilifu ikihusisha utaalamu na ujasiri wa hali ya juu kuliko uwezo wowote wa TISS kuwanyemelea mafisadi.

Msimamizi wa Operesheni hii ardhini ambaye alizungumza na KLHN kwa masharti yale yale mliyoyazoea amesema kuwa hawakuwa na mpango wa kuhusisha vyombo vya usalama kwani kwenye suala zima vyombo hivyo baadhi ya wahusika wake wa kuu wamo ndani mpango huu na hivyo njia pekee ilikuwa ni kuwadokeza tu watu kuwa mpango huo upo, unajulikana, na utakapoanza kutekelezwa Watanzania “wasishtuke”.

Hata hivyo wameahidi kuwa endapo Mwendesha Mashtaka Mkuu ataamua kuunda "Special Tribunal" ya kufuatilia suala hili ili kuona mashtaka yoyote kuletwa au uchunguzi ushirikiano unaweza kutolewa kwa kadiri ya kwamba vyanzo vyote vya habari hii vitabakia kuwa siri na havitalazimishwa kujitaja isipokuwa kuleta ushahidi kama ulivyo (raw evidence). Nje ya hapo amesema kuwa hawana "imani na Polisi wala Usalama wa taifa kwenye suala hili".

KLHN inaendelea kufuatilia kwa karibu mpango huu na kufichua njama yoyote ile ya kifadi yenye lengo la kuleta mgongano wa kidini au kikabila nchini. Baadhi ya habari zitasahihishwa kwa kadiri wingu linavyozidi kusafishika zaidi.
 
Mwanakijiji,

..umeandika Chief Msokwa, lakini mimi niliposikiliza BBC nimesikia Chief Hussein Msopa.

..nadhani huyo ni mtu mmoja na ndiye aliyetoa tamko la BAHAKITA.

..labda tusubiri watakapoanza kampeni zao za kuibomoa CHADEMA.

..CHADEMA watakabiliana vipi na kampeni hizo? wananchi watazipokea vipi kampeni za BAHAKITA?
 
Mwanakijiji,

..umeandika Chief Msokwa, lakini mimi niliposikiliza BBC nimesikia Chief Hussein Msopa.

..nadhani huyo ni mtu mmoja na ndiye aliyetoa tamko la BAHAKITA.

..labda tusubiri watakapoanza kampeni zao za kuibomoa CHADEMA.

..CHADEMA watakabiliana vipi na kampeni hizo? wananchi watazipokea vipi kampeni za BAHAKITA?


JK.. .taarifa hiyo niliandika a while ago, na jina sikulipata vizuri, ni Msopa.

Jambo hili sasa nalielewa zaidi kuliko wakati mwingine wowote; hili suala wala halihusiani na dini bali na siasa zaidi katika kufikia malengo fulani fulani. Naamini maneno ya hawa jamaa yamekuja katika jitihada za kukifanya CCM kuwasikiliza. Endapo serikali ya CCM ikisema kuwa hakuna OIC wala Mahakama ya Kadha timu ya watu hawa hawa watageuka na kusema CCM ni chama kisichajli maslahi ya "Waislamu" kana kwamba ndani ya CCM wamejaa wakristu watupu!

Nadhani sasa watanzania wanaweza kuamua vizuri mambo na kutambua ni wakati gani wanachuuzwa na ni wakati gani kweli kuna mtu anawatetea. Naamini hadi pale watakapoona kuwa kile wanachokitetea ni kwa Watanzania wote itakuwa vigumu sana kwa wao kushinda mbele za hoja. Utetezi wa jambo lolote ni lazima hatimaye uoneshe kuwa ni kwa ajili ya Taifa na Wananchi wote watanufaika pale matatizo x,y,na z yatakaposhughulikiwa.


lakini cha kusikitisha zaidi ni kuwa hawa jamaa wanafikiri Waislamu wote ni kundi moja ambalo linafanana kwa kila hali. Ni sawa sawa na wale hapa US ambapo wanapozungumzia "African-Americans" wanamaanisha watu wote wenye sifa na vitu vinavyofanana. Kiasi kwamba kuna watu wanafikiri watu wote weusi wanamuunga mkono Barack Obama au wanakubaliana na sera zake!. Mawazo ya kina Msopa na wenzao yaweza kuwa ni mawazo ya baadhi ya waislamu, lakini kuyatoa kana kwamba ni mawazo ya Waislamu wote ni kuchezea akili zetu.
 
Mzeee Mwanakijiji,
Mkuu wangu habari kamili za hawa jamaa nimezipata na zimetokana na Siasa baada ya mfarakano wa Upinzani ktk kukubaliana.. Sielewi Chadema imewajibu vipi wapinzani wenzake na kumetokea nini baina ya vyama hivi vya Upinzani.. Hivyo mbinu zimekwisha undwa kuibomoa Chadema..Na sielewi kama mbinu hii imetoka CCM isipokuwa ktk strategies ambazo zimepangwa kutumika ni kutumia vitu ambavyo Chadema kama chama haikubaliani navyo..
1. OIC na 2. Mahakama ya Kadhi ni hoja nzito sana ambazo nyie mnazichukulia very light lakini msichofahamu ni kwamba wapo Waislaam kibao wanaweza kujiunga na upandew wa pili hivyo kupunguza kabisa nafasi ya Chadema mwaka 2010..

Kumbukeni CUF mwka 2000 ilifanya vizuri sana bara toka kata, madiwani na hata Wabunge lakini lilipoingia tu swala La Udini.. mwaka 2005 walitoka watupu na kura zao zote zilirudi. Ukirudi nyuma na NCCR- Mageuzi mwaka 1995 walifanya vizuri sana lakini within 5 yrs walitafuta dawa yake wakaipandikiza na watu wakaamini NCCR -Mageuzi ikafa...
Hili sio swala la Waislaam, Wakristu, Mengi wala Manji mkuu wangu isipokuwa ni nyenzo za kupandikiza chuki..Na trust me ikiwa leo tunaweza kupinga/kuunga tofauti za Israel na Gaza kwa kutumia dini, itakuwa kazi ndogo sana kuimaliza Chadema...
 
Jamani ni lazima tuwe makini sana,Rwanda,na Burundi mambo yalianza kama hivi.kuna picha kubwa hapa inaendelea bila watu wengi kujua,Mwanakijiji kuwa makini sana na unachoandika kwani watu wengi sana tunakutegemea katika mambo mengi sana,pengine unaweza kuwa kiongozi wetu wa baadaye kwani mambo mengi unayoyaandika ni kweli na ni muhimu sana kwetu haswa sisi tulioko mamtoni.
Kuna gogoro kubwa sana ndani ya TZ na hii inatokana na tangu mambo ya ufisadi yaanze,wanasiasa,wafanyabiashara nk wanamalizana,wenyewe kwa wenyewe,kuna wanaotafuta kulipiza visasi.Kihistoria kipindi hiki ni kizuri sana kwani sasa tunakwenda kwenye maendeleo ya kweli,kwani viongozi wote na watu wachafu wataumbuana na waTanzania watawaona kwa macho na wengi wao kuishia jela,kuna changa la macho,na kiini cha macho hapa kwani tusikiaribu kipindi hiki kwa kukifanya kiwe cha udini,tunakosa picha kubwa sana hapa,change hazitatokea,usinielewe vibaya mwanakijiji kazi yetu na yako ni kuyaweka kwa wananchi lakini tuwe makini sana,mfano mashehe wenge uliowataja hapo juu siku nyingi sana wako majukwwani kupinga mambo mbalimbali yanayohusu waislamu,viongozi wafanyabiashara nk kama sikosei kuna wakati kama miaka 14 iliyopita hivi mashehe haohao uliwataja hapo juu walikuwa wanasema wanataka kulipua mabomu ya mengi jinsi gani na kiasi gani alikopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali na bila kulipa mpaka wakati wakati ule na mabenki hayo sasa yamekufa au kuuzwa .kuhusu Marwa kuna mambo mengi sana nayajua kuhusu huyu jamaa going back 1990s.hivyo tusiwe majaji kazi yetu ni kuziweka stori hizi kwa watu wazisome,na siyo uislamu,Mambo makubwa yanaendelea bongo naomba Tuangalie BIG SCREEN na kuona kila kitu
 
Mzeee Mwanakijiji,
Mkuu wangu habari kamili za hawa jamaa nimezip[ata na zimetokana na Siasa baada ya mfarakano wa Upinzani ktk kukubaliana.. Sielewi Chadema imewajibu vipi wapinzani wenzake na kumetokea nini baina ya vyama hivi vya Upinzani.. Hivyo mbinu zimekwisha undwa kuibomoa Chadema..Na sielewi kama mbinu hii imetoka CCM isipokuwa ktk strategies ambazo zimepangwa kutumika ni kutumia vitu ambavyo Chadema kama chama haikubaliani navyo.

Hili kwangu lina mantiki zaidi na jinsi nilivyolipata tangu mwanzo, sasa naelewa zaidi kuwa it is more about politics than anything else. Lakini la pili ni kuhusu "ulaji". Nilichogundua ni kuwa baadhi ya hawa jamaa ni fotocopy ya Rev. Mtikila na kilio chake cha "Tanganyika" na "Saa ya Ukombozi". NI yeye aliyejitaja kuwa ni mtetezi wa "walalahoi". There is a striking similarities kati ya hawa viongozi wa dini wanapojivisha uanasiasa.

1. OIC na 2. Mahakama ya Kadhi ni hoja nzito sana ambazo nyie mnazichukulia very light lakini msichofahamu ni kwamba wapo Waislaam kibao wanaweza kujiunga na upandew wa pili hivyo kupunguza kabisa nafasi ya Chadema mwaka 2010..

Sielewi unaposema "nyie" unaniweka na kundi la kina nani. Nikizungumzia nafsi yangu naamini waliyoyakoroga mambo hayo mawili siyo Chadema, siyo CUF, siyo NCCR Mageuzi, na siyo Wakristu au Waislamu. Walioyakoroga ni CCM kwa kuahidi kuwa wakichaguliwa basi "watalitafutia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi" na pili wao wenyewe wakasema (Membe mwaka jana) kuwa "Hakuna tatizo lolote kwa Tanzania kujiunga na OIC".

Hivyo utaona kuwa hakuna mtu mwingine yeyote anayebeba lawama kwa kukosekana mahakama ya kadhi au Tanzania kutokuwa mwanachama wa OIC isipokuwa CCM. Tatizo la CCM hata hivyo ni kuwa hoja zake ni dhaifu katika hili hawajaweza kushawishi jamii kubwa ya wananchi, na katika nchi ya kidemokrasia serikali inafanya kazi kwa kuwashawishi raia wake na si kwa vitisho au matumizi ya nguvu. So far, Chama cha Mapinduzi has failed miserably to argue for the two causes.


Kumbukeni CUF mwka 2000 ilifanya vizuri sana bara toka kata, madiwani na hata Wabunge lakini lilipoingia tu swala La Udini.. mwaka 2005 walitoka watupu na kura zao zote zilirudi. Ukirudi nyuma na NCCR- Mageuzi mwaka 1995 walifanya vizuri sana lakini within 5 yrs walitafuta dawa yake wakaipandikiza na watu wakaamini NCCR -Mageuzi ikafa...
Hili sio swala la Waislaam, Wakristu, Mengi wala Manji mkuu wangu isipokuwa ni nyenzo za kupandikiza chuki..Na trust me ikiwa leo tunaweza kupinga/kuunga tofauti za Israel na Gaza kwa kutumia dini, itakuwa kazi ndogo sana kuimaliza Chadema...

mzee mimi Chadema ikifa sitasumbuka, CCM ikifa sitasumbuka, CUF ikifa wala sitajali. NInachojali zaidi ni Tanzania na hatima yake. Kama Chadema ni kikwazo kwa mafaa ya Taifa letu basi haistahili kuwepo. Kama CCM ni kikwazo nayo haistahili kuwepo.
 
Jamani hiyo chadema yenyewe inayobomolewa ikowapi. This is rubbish. Naombeni kujua.. hii vita ni yanani dhidi ya nani.. CCM na CHADEMA? Is it that CCM inataka kupunguza makali ya chadema by rallying Muslims against them ama ni nini?

About Albert Marwa alibadili dini kwasababu zakibiashara na waarabu fulani.. Ndio akaanzisha radio station n.k

Nyumba alizonunua sio za serikali nadhani ni za mashirika ambayo yalibinafsishwa au kitu kama hicho. Moja ninayo ijua iko baada ya kushuka kilima nyege to the right baada ya residence ya balozi wa Rwanda. Hii kwa zaidi ya miaka kumi sasa maana nimekaa mtaa ule tangu 1998 mpaka 2009 na mpaka kesho hajaipangisha. Aliwaachia washkaji zake wakae.. tuseme ni wafanyakazi wake katika biashara zake mbali mbali ikiwemo ya Unga. Ni kweli anauza unga, silaha siju. Kuna jamaa alikua anakaa pale ambae anaitwa Salum he was for about 10yrs, one of Albert's henchmen.
 
1.Jamani hiyo chadema yenyewe inayobomolewa ikowapi. This is rubbish.

2. Naombeni kujua.. hii vita ni yanani dhidi ya nani.. CCM na CHADEMA?

3. Is it that CCM inataka kupunguza makali ya chadema by rallying Muslims against them ama ni nini?

- Saafi sana tupo ukurasa mmoja hapa mkuuu!
 
Mwanakijiji,

..umeandika Chief Msokwa, lakini mimi niliposikiliza BBC nimesikia Chief Hussein Msopa.

..nadhani huyo ni mtu mmoja na ndiye aliyetoa tamko la BAHAKITA.

..labda tusubiri watakapoanza kampeni zao za kuibomoa CHADEMA.

..CHADEMA watakabiliana vipi na kampeni hizo? wananchi watazipokea vipi kampeni za BAHAKITA?


Kuna mtu amegundua uhusiano kati ya kundi hili na lile lililotangaza karibuni kupitia BBC na kwenye magazeti mbalimbali kupinga operesheni Sangara na kusema kwamba CHADEMA ina nia mbaya na waislamu?

PM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom