jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,395
- 25,520
Wakuu Wote; Pongezi sana kwa kuleta Dataz.
Nina mawili matatu ya kuongeza kuhusu wasifu wa kijana Albert Marwa (ingawa sidhani kama bado ni kijana.!!!).
Yeye ni mtoto wa kufikia wa Meja Gen Marwa RIP. Inasemekana Albert ni mzaliwa wa Uganda ambaye aliochukuliwa na Meja Gen wakati wa vita vya kumfukuza Iddi Amin mwaka 1979. Ni kijana mpole anayejificha kiasi kulinganisha na rafiki zake kama kina Kinje. Ni mtu makini sana kwenye mambo yake mengi (ananikumbusha msemo wa " mwenda pole, ndiye mla nyama").
Nilimfahamu kwa karibu mwanzoni mwa miaka ya 90 akiwa anafanya biashara tofauti tofauti ili mradi anaingiza hela la maana (na hela ya maana aliingiza). Katika mojawapo ya biashara zake aliwahi kuwa na kampuni ya Clearing and Forwarding kipindi kile Serikali ya Mzee Ruksa haikusanyi kodi..!! Katika kipindi hicho aliwahi kuwa mmoja wa wafanyabiashara walioingiza bia za makopo za Heiken Tanzania. Akiwa na kampuni ya Clearing and Forwading alipata hela nyingi kwa kuuza Mafuta/Petrol yaliyoandikishwa kwenda nchi jirani (ambayo hayajalipiwa kodi) nchini Tanzania.
Niseme wazi kuwa pamoja na yote niliyojua kuhusu Albert miaka ya 90 ilikuwa dhahiri kuwa ana biashara "ya pembeni" ambayo inamuingizia hela zaidi ya zile nilizokuwa nazijua. Hili lilidhihirika kati ya mwaka 1997 - 1998 aliponunua nyumba 2 (za serikali) Oysterbay akazifanyia ukarabati mkubwa kabla ya kuzipangisha. Kipindi hicho alikuwa anaishi Upanga opposite na Califonia Dreamer/ Jolies Club.
Mabinti: Albert ni mtu mwenda pole, anajipanga vizuri. Katika moja ya strategy zake naona ana ka-historia ka kujipatia "influence" kupitia mabinti wa vigogo wa serikali. Mwaka 1997 alikuwa anatoka na mtoto wa Zakhia Meghji, Salama. Nikawahi kusikia tetesi kuwa anataka kumuoa ila sijui kama ni mahari ilikataliwa au nini kilichotokea. Wadau hapa wametoa dataz kuwa alibadili dini na kumuoa mtoto wa Balozi wetu UN na siku za karibuni alitaka kumuoa mtoto wa JK...ni dhahiri kuna ka-record fulani hapo.
Tetesi ya biashara zake: Mtakumbuka kuwa miaka ile ya 1990, enzi za Mzee Ruksa Jijini Dsm kulikuwa na mtu aliyefahamika kama Abdul Msomali, walikuwa karibu na Albert. Hii ilileta tetesi kuwa na yeye aliwa ni mtu wa Unga. Pia, miaka ya mwanzoni 2000 nilisikia tetesi tena kuwa ana kundi lake la majambazi au wazee wa kazi kama walivyojulikana mitaani. Hili lilitokana na Fact kuwa mdogo wake ambaye ni mtoto wa Meja Gen akiwa na wenzake walikamatwa na bastola wakipanga kufanya uhalifu (sijui kesi iliishia wapi). Tetesi nyingine ni kuwa kutokana Baba yake kuwa Meja Gen alikuwa anafanya biashara ya Silaha kwenye vita vinavyoendelea nchi jirani. Sikuwahi kuhisi wala kuhakikisha lolote kuhusiana na tetesi hizi.
My Take: Ni karibu miaka 20 sasa tangu nilipomfahamu Albert. Ni mtu makini sana, mwenye connections zenye nguvu ya ajabu Tanzania (alinunua nyumba za serikali Oysterbay kabla hata ya kifo cha JKN..!!). Ni mtu anayejua kutumia nafasi vizuri, yuko tayari kujipanga hata ikibidi kubadili dini ili mradi mambo yake yanakwenda vizuri. Kwa yeye kujiingiza kwenye masuala ya imani kali, kunamuweka kwenye spot light sidhani kama strategy hii mpya itampa mafanikio anayoyategemea.
Naomba Kuwasilisha
Yebo Yebo hapo juu data zimetulia kiaIna na kwa kweli umezIchambuwa kutokana na uzoefu wako..Ila una memory duh! Kama kijana anataka kuuza silaha kwa kuanzisha vurugu basi mahesabu hayo si mazuri kabisa..Ila kama mambo ya usalama wa Taifa yako lege lege kiasi hiki basi hali si nzuri kabisa na kusema kweli tunataka mabadiliko....Haya mambo ya nchi kuongozwa kihivi sasa yatatufikisha pabaya.