mfumwa,
Hakuna tatizo kuomba nawe uone. Ila hakuna kipya sana utakachojifunza tofauti na vilivyowasilishwa humu - hata ukionyeshwa footage yote (badala ya ile fupi wengi tuliyoiona kwenye TV). Ndiyo maana wale tuliyoiona hiyo fupi, hujasikia tukimwomba Mwanakijiji aturushie hiyo aliyoiona yeye.
Kama anavyosema Waberoya kilichobaki baada ya kuhabarishwa, ni kukaa macho kuona hali ya mambo itakavyojidhihirisha muda unavyokwenda.
Pamoja na kuona hiyo video footage, bado nina maswali yasiyo na majibu. Kuna mambo kadhaa nategemea yatafuata. Yasipotokea, hiyo itajenga taswira fulani kuhusu suala hili. Ni swala la muda tu, tutapata kufahamu kwa uzuri, nini kinaendelea.
Usikonde mfumwa!
Unajua hapa LazyDog unanishangaza, manake unakimbia kivuli. Unasema "Ila hakuna kipya sana utakachojifunza tofauti na vilivyowasilishwa humu - hata ukionyeshwa footage yote (badala ya ile fupi wengi tuliyoiona kwenye TV)". Kuna tukio lililooneshwa kwa ufupi, ndio hilo la ITV, lakini kuna pia yasiyooneshwa, unaniambia kuwa hata nikioneshwa kila kitu hakuna jipya nitakalojifunza. Sasa wewe umesema umeona na walio wengi hicho kidogo cha ITV, umejuaje hayo yasiyooneshwa mpaka uniambia hata nikioneshawa yote hakuna kipya nitakachojifunza?. Kazi ipo hapa, umeona kwa uchache, ila unatoa majibu ya yote na usiyoona (kuna walakini!!!!!!!!!!).
Pili kujifunza na kuelewa kuna tofautiana, uelewa wako sio uelewa wa Mfumwa, na ulewa wa Mfumwa sio wako, na vivo hivyo kwa wengineo. Nilikuwa naangalia kipindi kimoja, watoto wa miaka 5 walikuwa wanaulizwa mnataka kufanya nini mkikua, mmoja akasema anataka kuwa Daktari wa binadamu sababu Mama yake ni hivyo, mwingine akasema anataka kuwa Rais, mwingine akasema anataka kuwa Obama, aliyenifurahisha alisema kuwa anataka kuwa Ngo'ombe, nilishtuka, hata mwendesha kipindi akamuuliza tena, akarudia jibu, akaulizwa kwa nini, akasema anataka asihangaike anakaa ndani tu na kuletewa kila kitu, ila huyu alikuwa anawaza wale wa "zero grazing". Sasa narudi kwako, kuelewa kwako si kuwa kila mtu ataelewa kama wewe, ama tafsiri si lazima tuwe sawa.
Unapomnukuu Waberoya, eti kilichobaki tukae macho, hiyo sio haki. Wote tukisikiliza ndio tutaimba wimbo mmoja, manake ukisema unaona limetokea hili, si tulisikia ama kuona kile kitu, ndio maana, sasa likitokea jambo, ukasema lilizungumziwa na hao jamaa ama lilioneshwa, mimi na wasioona tutaamini vipi. Leteni tuoe na tusikie tucheze ngoma moja.
Sasa unatakiwa kuwa wazi, ulichoona, sio kusema "Pamoja na kuona hiyo video footage, bado nina maswali yasiyo na majibu. Kuna mambo kadhaa nategemea yatafuata. Yasipotokea, hiyo itajenga taswira fulani kuhusu suala hili", sasa wote tungeona, wote tukatoa maono (taswira) yetu, halafu wote tukawa tumeshaweka maswali huon mtiririko ungekuwa mzuri. Kuliko sasa kikitokea kitu, utaanza ndio maana tuliona hiki na kile, ama tulisikia hili na lile, bila wengine kuona wala kusikia. NJOO NA MASWALI NA MAELEZO YENYE MSHIKO, usirukie............