Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji,
Mkuu unazungumza na mtu anayefahamu kwa undani zaidi acha hizo habari kwani tunaelewa haya maswala yamesukwa na mnaendelea kuyasuka kama mlivyoyasuka kwa Sheikh Kassim..
Mkuu unajua Ukerewe walijenga chuo cha kiislaam kinaitwa Al Jazeera, mkuu yalisemwa mengi sana na marehemu kaka yangu became a victim within his own party...isitoshe kimekuwa chini ya uchunguzi kwa miaka karibu 6 hadi leo na kinapigwa vita vibaya sana hadi kesho maneno hayaishi kila siku kinatungwa jambo..tumezoea ndio maisha yetu topka Uhuru..

Kwa hiyo sishangai na habari kama hizi hata mkusinyiko wa Waislaam itakuwa hatari..
Mkuu nilijua haya yanakuja na hakika utabiri utatimia wala sii muda!
 
Ukitaka kujua hili limepikwa, angalia tu trends, yaani Mwanakijiji alishasema kuna jambo litatokea mwisho wa wiki. Then baada ya ITV kunasa hayo matukio (Sijayaona) tayari kesha andika wahusika wote na kuwahukumu. Mipango kama hii ilikuwepo, ni waislamu tu kujihadhari, mfano:-

1. Maaskofu kuna wakati walitoa tamko kuwa kama mihadhara itaendelea basi watamwaga damu, waislamu wakajibu kuwa kama Maaskofu watamwaga damu nao watajibu. Baada ya Maimamu kujibu hilo ikatokea kamata kamata kuwa wanataka vunja amani, ndio Sheikh Kassim na wengineo wakaiwa ndani, tena Sheikh Kassim akiwa Arusha kwa matibabu.

2. Likaja suala la Mwemechai, kupitia Radio, Padri mmoja akasema amepita Mwembecha na kukuta Yesu anatukanwa. Na siku hiyo hakukuwa na hata mhadhara. Serikali kwa haraka sana ikasema italishughulikia. Basi ikaaanza kamata kamata, waislamu walipokusanyika kujiuliza kwanini hata wanaoenda polisi kuulizia waliokamatwa watawawekeaje dhamana hawarudi. Wakaletwa FFU wakatumia nguvu kubwa na damu ikamwagika.

3. Aliyekuwa Imamu wa Mwembechai , sasa marehemu (jina limenitoka), aliwahi kuletewa zawadi ya magunia ya mchele ama unga nyumbani kwake, wake zake walipouliza nani katoa hiyo zawadi wale walioleta huo mzigo wakataja msikiti mmoja wa Temeke. Wakati wake zake wanakataa hiyo zawadi, wale jamaa wakaondoka, na hapo hapo wakatokea Askari waliodai wanataka kagua nyumba. Basi ndani ya ile zawadi wakakuta mabomu. Haya matatu ni kwa uchache tu dhidi ya hujuma kwa Waislamu, lakini Mwenyezi Mungu alisema “Na kumbukeni kuhusu waumini, wanapopita katika mitihani (kuonewa, kuzushiwa nk) huzidi Imani”

Sasa hapa nadhani kuna mpango unasukwa, na nijuavyo Waislamu sasa wako katika kipindi cha hatari mno. Wanatafutiwa sababu ili ianze kamatakamata. Lakini Allah (SW) ndie mjuzi na mlinzi wetu. Yetu sasa macho na masikio baada ya hili kumepangwa nini?. Lakini wanaopanga haya hawajui tu hujenga chuki miongoni mwetu, si mimi wala anayepandikiza chuki ndio atakayepona, wote tutakuwa ndani ya tatizo.
 
Mwanakijiji,
Mkuu unazungumza na mtu anayefahamu kwa undani zaidi acha hizo habari kwani tunaelewa haya maswala yamesukwa na mnaendelea kuyasuka kama mlivyoyasuka kwa Sheikh Kassim..

eh.. umeniweka kwenye kundi la "mnayasuka" mimi na kina nani Mkuu?

Mkuu unajua Ukerewe walijenga chuo cha kiislaam kinaitwa Al Jazeera, mkuu yalisemwa mengi sana na marehemu kaka yangu became a victim within his own party...isitoshe kimekuwa chini ya uchunguzi kwa miaka karibu 6 hadi leo na kinapigwa vita vibaya sana hadi kesho maneno hayaishi kila siku kinatungwa jambo..tumezoea ndio maisha yetu topka Uhuru..

Mmezoea wewe na nani? una maana na brother wako au na kundi la watu wengine ambao wameonewa?

Kwa hiyo sishangai na habari kama hizi hata mkusinyiko wa Waislaam itakuwa hatari..
Mkuu nilijua haya yanakuja na hakika utabiri utatimia wala sii muda!

haya bwana nadhani unaliangalia hili kwa misingi ya kidini zaidi.
 
Mwanakijiji,
Wewe ndiye umelivalia njuga swala hili na habari za uzushi ukazipamba utafikiria harusi ya Nabii.. lakini ukweli ni kwamba tumegundua huu ni uhuni mtupu..na kibaya zaidi umeingia kichwa kichwa kuamini kwamba Waislaam tena masheikh wana mpango wa kummaliza Mbowe!... mkuu wangu hapo umeniumiza lazima niseme ukweli kwani naifahamu issue hii na Mbowe ni mshikaji..

Na siwezi kusema mimi mdini kwa kukataa habari hizi, labda hufahamu udini.. propaganda kama hizi ndio udini kuzikataa haiwezi kuwa udini bali ni kuondoa chuki.. wewe unajenga chuki hapa na kuna watu tayari wamekwisha kuamini.. Wakiniamini mimi watayapuuza na kutuona sisi ndugu zao lakini yako mkuu yanabomoa..
Kuna watu wataanza kujiuliza kuhusiana na Mbowe kafanya nini kwa waislaam alikuwa na mpango gani na kadhalika hivyo huwaimuzi waislaam tu bali hata Mbowe na mahusiano ya Chadema na CUF.. be careful my brother, kunguni akuumaye yuko nguoni mwako.
 
Bob

Hapa unampiga Mzee Mwanakijiji bila hoja zilizosimama. Mwanakijiji ameleta habari hapa...wewe na wengine humu forum wanaona ina uzushi sasa kwa nini hamleti hoja za kuthibitisha kwa nini hii habari haina ukweli.

Hayo maneno niliyoweka "bold" yana lengo la kubadili mjadala kwenda kusiko. Mwanakijiji ameweka majina specific ya wajumbe walikuwemo kwenye huo mkutano lakini wewe unaweka mkazo kwenye "Waislamu" kwa ujumla wao. Sioni kama ni sahihi mkuu; umeichukulia hii taarifa "personal". Ukiiangalia kwenye kona nyingine utaichukulia kama ni habari tu ambayo sio lazima uiamini 100%.
 
Yebo Yebo,

Kuna Mawaziri, Majaji, Mabalozi wamenyang'anywa nyumba baada ya kuuziwa ovyo ovyo, Bakari Mwapachu, Jaji Stephen Ihema, Balozi Adam Marwa (nyumba za Serikali za Mitaa), Balozi Ben Moses (za Serikali Kuu lakini kajinunulisha zaidi ya moja na mkewe).

Sasa huyu mtu ambae hata hakuwa mtumishi, achilia mbali Waziri, watu si wangeshamfanyia unoko kama hata Waziri ananyang'anywa ?

Na pia, nyumba zilianza kuuzwa 2001. Huyu aliuziwaje in the nineties, tena mbili, na hata sio mtumishi?

Hizo nyumba zinazoongelewa hazikuwa ni nyumba za serikali....as in GTZ...ninavyoelewa zilikuwa ni nyumba za mashirika ya umma na wakati anazinunua zilikuwa zinauzwa through public auction na kutolewa zabuni....(baada ya mtindo huo kulalamikiwa) ndiyo ukabadilishwa na sasa wafanyakazi na waliomo ndani ya nyumba wanapewa priority!
Na kama ni masuala ya yeye kutokuwa mtumishi wa serikali na amenunua hizo nyumba mbona RA amejichukulia nyumba mtaa wa Kenyatta....zamani ilikuwa nyumba ya ATC!
 
Tetesi ni kitu kisicho na ushahidi, kama wanazushiwa waende mahakamani... na huu ni mpango mmoja tu mwingine unahusisha watu wasomi zaidi na very senior na una angle ile ile.. huo utaibuka wiki ijayo Inshallah..

Asante kaka, hebu nitumie mobile yako thru PM nikupigie
 
Jamani waliokaribu na JK mwambie afukuze wale jamaa zake huko ateu hata asiowajua. Hii nchi naipenda sana na hatma yake siijui. Rais wangu Kikwete hii aibu sipendi ikukute.

I love my country, I love Tz
 
Swali ambalo nimekaa nikijiuliza bila ya kupata jibu ni je mara baada ya kufanikisha malengo yao hayo, hili suala zima litakuwa limewapa manufaa gani. Hii hali inachangiwa na Utawala wa Sasa, na mwelekeo mzima wa Nchi kutokana na viongozi waliopo.

Mimi naona kama Muungwana anategewa tu kwa kila hali. Sijui kama amestuka
 
Kichwangumu
Haya yote tunayoyaona ya vyombo vya dola na imani kukinzana na kushabihiana bila kufanana ni kwa sababu nchi haina uongozi. Wakaribu naye muungwana wamegundua JK
1. Ana low IQ hapa ndipo mataputapu yote yanapopenyea
a. Siku hizi hasomi tena hotuba kabla..anasoma anapohutubia.. hotuba ya mwisho ni mfano tosha.
b. Wamegundua haambiliki...basi na wakushauri wanaacha
c. Ana uswahiba wa ajabu na watu wa ajabu hata wanaotakiwa kuwapeleleza wanashangaa muungwana kawa na urafiki nao kwa vipi..toka lini na kwa mpango gani?
2. Wameng'amua anapenda wanawake, tena wengi sasa basi basi kila ziara wamwandalia wakutosha. Ukisikia...mzee kapumzika jua....Ndo maana ratiba za usiku ni nyingi na pia hamalizi aliyopangiwa...wapanga ratiba wanachanganyikiwa
3. Ni kweli ana wasaidizi vilaza wengine ni darasa la 7 hawa ndo wanambwembwe balaa. Pia ana wasaidizi makini ila hawajui wafanye nini...yeye huwaambia ...kwani nyie mnaonaje, andikeni mnavyoona sawa... na huyo ndie muungwana
4. Jumla ya 1-3 ni kuhujumiwa au kama si kuonekana anahujumiwa. Waliokaribu nae tafadhali wamwamshe muungwana ...grrrrrrrrrrrriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Albert Marwa ni jamaa mmoja anayetaka kumuoa mtoto wa JK lakini ni mtu anayetumia nafasi yoyote anayoipata kutengeneza pesa na moja wapo ikiwa tukio hilo!!!!!!!

Albert Marwa navyomfahamu mimi ni kuwa mpaka sasa anatembea na mtoto wa kiwket salma na ni kama keshamuoa kwa sheria za Ndoa.Na yupo karibu sana na wanafamilia wa Mhe. Rais,Kimsingi ni mtu wa karibu wa familia ya kina kikwete.al maarufu alberto.

Mwanakijiji,
Wewe ndiye umelivalia njuga swala hili na habari za uzushi ukazipamba utafikiria harusi ya Nabii.. lakini ukweli ni kwamba tumegundua huu ni uhuni mtupu..na kibaya zaidi umeingia kichwa kichwa kuamini kwamba Waislaam tena masheikh wana mpango wa kummaliza Mbowe!... mkuu wangu hapo umeniumiza lazima niseme ukweli kwani naifahamu issue hii na Mbowe ni mshikaji..

Na siwezi kusema mimi mdini kwa kukataa habari hizi, labda hufahamu udini.. propaganda kama hizi ndio udini kuzikataa haiwezi kuwa udini bali ni kuondoa chuki.. wewe unajenga chuki hapa na kuna watu tayari wamekwisha kuamini.. Wakiniamini mimi watayapuuza na kutuona sisi ndugu zao lakini yako mkuu yanabomoa..
Kuna watu wataanza kujiuliza kuhusiana na Mbowe kafanya nini kwa waislaam alikuwa na mpango gani na kadhalika hivyo huwaimuzi waislaam tu bali hata Mbowe na mahusiano ya Chadema na CUF.. be careful my brother, kunguni akuumaye yuko nguoni mwako.

he he hehe he
Mkandara bwana,umeniahc hoi sana mkulu,alafu Mengi ana Mpangowa kutuvuruga watanzania ukianzia hata ile barua ndefu ya Mtikila.Mie sidhani kuna watu wana mpangowa kumchafua Mbowe.Kwani Mbowe ni nania mpaka watu wamchafue?
 
Hii habari imekaa kiuda daku hivi. Waislam wanakaa kumkataa Kiongozi wa kichaga ilhali kuna wachaga waislamu wengi tu this doesnt add up...

Habari ina mkanganyiko na mgoloko mwingi, mara ukabila mara udini muradi kukidhi haja ya kuchochea watanzania. Huu ni mzuka wa OIC na Kadhi utatuletea habari nyingi watu wasipokuwa makini na kummeza nzima nzima kuna hatari mbeleni huko.

Same person with different faces...
 
Asante na Hongera MMKJ kwa kutuhabarisha habari nyeti, na sensitive katika usalama wa taifa letu.
Umetoa majina, sehemu, namba za magari, hadi agenda za mikutano hiyo. Kuna watu humu hata ukileta hizo sauti watakuambia umefoji. Its nothing else than udini.
Shida ya watanzania sometimes ndio hii. Badala ya kuangalia maslahi ya taifa tunaweka dini mbele hata kama tunaenda kuchinjana..
Mungu Ibariki Tanzania
 
Sounds like very bad news for our peaceful nation. Lets just pray that none of this bullshit will never happen in this country.
 
Mkuu Gembe, unapouliza Mbowe ni nani, anzia na Mtikila kufanya kampeni kwa kumchafua Mbowe Tarime.... Angalia mikakati mingi ya kumdhibiti na kummaliza kuanzia Paul Kyara wa chama cha SAU na kuendelea....

Kwa wale wanaoona hii taarifa imekaa kiudaku, wajue iko siku nchi itaingia katika matatizo kwa "staili" hii hii ya udaku.

Hapa JF kabla ya wengine kusema, tuliambiwa laptop ya Rais imeibiwa, watu wakasema udaku na hadi leo hakuna maelezo yenye mashiko, tuliambiwa msafara wa rais umepokwa mawe, ikawa ni udaku, tukaambiwa Mkapa kazomewa ikawa ni udaku lakini wanaosema ni udaku hawajaja na data zenye mashiko.

Kwa ufupi kuna tatizo, dataz ama habari ya kweli ni ile ambayo mtu anaipenda kuisikia lakini msingi wa habari ni ile usiyopenda yaani "NEWS". Kabla ya mtu kusema ni udaku, ajiridhishe kwa kufanya utafiti ili aseme, hii si kweli na ukweli ni huu........... na anayebisha aende.......

ITV walionyesha picha na Albert alionekana hadi anapotoa fedha kwa mashehe akiwa katika gari yake aina ya Benz.... na walikuwa mtaa wa Kazima, namba 38 Kinondoni,mitaa michache kutoka msikiti wa Mtambani.

Sauti ya Albert ilisikika na yeye ndiye aliyemtaja kwa jina Mtawa...... na mikakati na wapi wanapata fedha na kiasi gani na jinsi Albert anavyopanga kuwawekea fedha zaidi katika akaunti zao imesikika. Kwamba wataanzia Songea nayo imesikika katika sauti. Sasa jamani hao wanaosema ni udaku wajaribu kutafuta dataz na kuziweka na huo ndio uungwana na nitakuwa wa kwanza kumshauri Mwanakijiji aombe radhi.

Kwa ufupi ni kwamba Albert ni makini sana na kwa hili anaendelea kupanga mikakati ya kuliweka sawa, sina hakika kwa njia gani, na kama ni njia ya amani/mazungumzo ama njia mbaya na chafu zaidi.

Kwamba ni kweli ama si kweli, kwa watu waliosikiliza radio moja ambayo Albert anahusika nayo, ilianza kufanya hicho wanachotuhumiwa kukipanga katika habari ya ITV na ya Mwanakijiji na ni kumchafua Mbowe na Mengi kwa kuhusisha uchaga na udini. Jambo la ajabu wanachemsha pale walipodaiwa kumuingiza IGP kwenye uchaga na kujikuta wanaikoroga ajenda yao ya udini kwani Mwema ni Muislamu safi mwenye imani thabiti. Watachemsha kwani wanaozungumza ni viongozi wa dini, wahadhiri wanaoheshimika, sasa wanapojadili ukabila huku wakimuweka IGP musialamu wanachemsha zaidi

Sasa huo
 
cha ajabu ni kuwa mwanakijiji alianzisha thread kuuliza who is albert marwa

few minutes baadaye amemwaga hiii utadhani naye alikuwa na ofisi pale slamander

hakuna kitu humu na sana sana naona ni sign of desperation kutaka kuonyesha kuwa bado the so called flow of DATAZ bado ipo

ukweli ni kuwa hakuna kitu na sana sana naona hii inaweza ikawa ni SLANDER kwa sababu hakuna ushahidi

Halafu mnashangaa kwa nini standards zimekuwa LOW
 
Mwanakijiji,
Mkuu unazungumza na mtu anayefahamu kwa undani zaidi acha hizo habari kwani tunaelewa haya maswala yamesukwa na mnaendelea kuyasuka kama mlivyoyasuka kwa Sheikh Kassim..
Mkuu unajua Ukerewe walijenga chuo cha kiislaam kinaitwa Al Jazeera, mkuu yalisemwa mengi sana na marehemu kaka yangu became a victim within his own party...isitoshe kimekuwa chini ya uchunguzi kwa miaka karibu 6 hadi leo na kinapigwa vita vibaya sana hadi kesho maneno hayaishi kila siku kinatungwa jambo..tumezoea ndio maisha yetu topka Uhuru..

Kwa hiyo sishangai na habari kama hizi hata mkusinyiko wa Waislaam itakuwa hatari..
Mkuu nilijua haya yanakuja na hakika utabiri utatimia wala sii muda!

Watu bwana...kesho mtakuja ooh breaking news wakati upepo unaonekana kabisa.
 
Asante na Hongera MMKJ kwa kutuhabarisha habari nyeti, na sensitive katika usalama wa taifa letu.
Umetoa majina, sehemu, namba za magari, hadi agenda za mikutano hiyo. Kuna watu humu hata ukileta hizo sauti watakuambia umefoji. Its nothing else than udini.
Shida ya watanzania sometimes ndio hii. Badala ya kuangalia maslahi ya taifa tunaweka dini mbele hata kama tunaenda kuchinjana..
Mungu Ibariki Tanzania

Mwanakijiji siyo mytu wa kuaminiwa kila siku anaweza kuleta habari hapa kwa maslahi ya Chama chake,Unaweza ukaamua kujificha sana ili watu wakuone na wewe hautoki CHADEMA ila baada ya Ushindi wa kishindo wa CHADEMA tuliwajua watu kwa vyama vyao.

CHADEMA wamekuwa wakiendeleza ukabila kwa muda mrefu sana na ni dhambi inayowatafuna .Jambo baya sana ni operesheni sangara ambayo wansema inakuwaja kuwa komboa watanzani wote ila lengo lao ni jimbo la Mwibara.Kwanini hawakuiita Operesheni mwibara?
 
GT.. mimi sikumjua Marwa kabla ya jana.

Sources zangu tangu wiki iliyopita zilikuwa zinaniashiria kuna kitu kinasukwa; na jana source moja ikaleta habari na swali tu kama namfahamu "Albert Marwa". Nikasema sijawahi kumsikia wala simjui; hiyo source ikanishangaa kuwa simjui "mtoto wa mjini" nikamwambia ndio maana naitwa "mwanakijiji". Akaniambia tafuta watu wako wakuambie kuhusu Marwa.

Hiyo ndiyo sababu ya mimi kuuliza (na sikuanzisha thread unless kama nimesahau). Nilitaka kupata sources tu mtu anifeed. Bahati nzuri nilipopata kujua Marwa ni nani ndiyo wimbo ukaimbwa nikaunganisha data zangu za tangu wiki ile.

Sasa kama unahabari tofauti kuhusu mimi kumjua Marwa unaweza kuweka hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom