Camera za Usalama kufungwa Mlima Kitonga ili kudhibiti ajali

Watu 50 wamekufa juzi kwenye ajali ya basi la Majinjah mzee unamlisha matango pori kwa confidence kabisa. Nadhani wewe ndio haufuatilii media za bongo mkuu.

Last month kuna basi ilianguka tena ikafunga barabara luckily hakukuwa na vifo.

So huu mjadala wa Kamatu ya Ulinzi na Usalama umetokana na matukio kadhaa yaliyofululiza.
Acha uongo weka ushahidi hapa kama basi la Majinja lilipata ajali kitonga!?
 
hili ni la polisi na RC kwa suluhisho la muda mfupi na nafasi waliyopo,lakini sidhani kama ndio serikali kwa ujumla wake ifikie hitimisho hapa.

bado eneo hili linahitaji hatua kubwa zaidi ya hizi,kwa nyakati hizi tech imeshakua sana ni swala la kuweka pesa zaidi hiyo njia upunguzwe zaidi kona na barabara itanuliwe zaidi,lakini pia kingo imara zifungwe.
 

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama Barabarani ya Mkoa huo, wapo mbioni kuanza utekelezaji wa mpango kabambe wa kuweka camera za kisasa kwenye maeneo korofi kwenye barabara kuu inayounganisha Mkoa huo na Mikoa mingine na kwa kuanzia camera hizo zitafungwa eneo la Majinja Wilayani Mufindi na Mlima Kitonga Wilayani Kilolo ili kupunguza ajali za barabarani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas @salimasas amesema hayo wakati kamati yake ikiongozwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ilipotembelea maeneo kadhaa ambayo ni korofi na yanayoongoza kwa kusababisha ajali nyingi Iringa.

Asas amesema uwekwaji wa camera hizo utasaidia kupunguza ajali barabarani kwasababu zitakuwa zinafanya saa 24 na zikifungwa Polisi katika Ofisi ya RPC, RTO na OCD watakuwa wanaona LIVE kila kinachoendelea Kitonga na kote zilikofungwa, pia amesema Madereva wakijua eneo lina camera watazingatia sheria za usalama barabarani.

Katika ziara hiyo ya siku mbili Kamati hiyo imetembelea Nyang’oro, Mlima Kitonga na eneo la Majinja ambalo lilipewa jina hilo kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Kampuni ya Majinja Express lililogongana na lori la mizigo na kusababisha vifo vya Watu 50 na wengine 23 kujeruhiwa March 11, 2015.
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."
Tatizo lililopo Mlima Kitonga ni kwamba ile barabara ni nyembamba sana, lane moja tu ya kupanda na lane nyingine ya kushuka. Barabara hiyo inatakiwa kupanuliwa kwa kuongeza angalau lanes zingine mbili ili kuifanya kuwa barabara ya lanes nne(4), mbili za kupanda na nyingine mbili za kushuka mlima, kuweka sehemu za kupumzika pembeni mwa barabara, pamoja na kuweka concrete road blocks katikati ya barabara ili kutenganisha magari yanayopanda mlima na yale yanayoshuka mlima ili kuzuia ajali za kugongana uso kwa uso. Aidha, pia unatakiwa kujengwa ukuta wa zege/ukingo au kujenga strong concrete retaining wall pembezoni mwa barabara hiyo ili kuzuia au kuyakinga magari yasiweze kuacha njia na kutumbukia kwenye ngema chini na kusababisha ajali, hata kama gari litaharibika au kufeli breki bado haliacha njia na badala yake litaendelea kubaki kwenye barabara yake.
Hilo ndilo suluhisho la kudumu ili kudhibiti ajali za barabarani za mara kwa mara zinazotokea hapo Mlima Kitonga, nimewahi kuona wametumia njia hii ktk nchi mojawapo niliyowahi kutembelea hapa duniani, bado naendelea na utafiti wa kuzipata picha za barabara hiyo, nikizipata nitaziweka hapa hapa mtandaoni ili watu wa TANRODS na TARURA pamoja na Makampuni ya ujenzi wa barabara waweze kujifunza kutoka kwa wenzao walioendelea zaiddi kwenye haya masuala ya ujenzi wa barsbara
 
Back
Top Bottom