Habari, Ndugu Mteja. Asante kwa kuwasiliana nasi.
Tayari tulishatoa majibu kupitia mjadala huu (thread). Endapo hukuyapata, tafadhali yapitie hapa chini:
Kukamilika kwa mradi wa Julius Nyerere imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwenye kuimalisha huduma nchini
Aidha, hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka 2025/2026 mahitaji ya juu zaidi ya umeme yalikuwa yamefikia megawati 2,188.21 huku uwezo wa mitambo ukiwa ni zaidi ya megawati 4,000.
Hadi sasa huduma ya umeme nchini ni nzuri na inapotokea changamoto yoyote wataalam wetu wanarekebisha na huduma kuendelea.
Ni vizuri kutambua siyo kila umeme unapokakati kwenye maeneo yetu sababu inakuwa TANESCO,zipo sababu nyingine za kibinadamu ikiwa ni pamoja na miundombinu kuharibiwa au kugongwa na gari. Hivyo wote tunawajibu wa kuendelea kutunza miundombinu ya umeme. Kwa zile zinahusu TANESCO zinafanyiwa kazi kwa mjibu wa utaratibu.
Kuhusu bei ya umeme,hili linamchakato wake,TANESCO ni Taasisi inayosimamiwa na EWURA na masuala yote ya bei yapo chini ya usimamizi huo.
Hivyo mamlaka hiyo inauwezo mzuri wa kulifanyia kazi kwakuzingatia taratibu zinazoongoza namna ya kupandisha au kushusha bei kwa kuangalia gharama za uendeshaji
Asante na karibu sana. ^FL