Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,478
Kuamini unaruhusiwa kuamini lolote.Mimi sio mgeni kwa huo uandishi wako, naamini kuna jambo la chini ya kapeti ambalo wadau humu jukwaani hawalifahamu.
Huwa unatumia maneno fulani yanayozidi mtazamo wa principle, yanakuwa makali sana.
Naheshimu na kutetea haki yako ya kuamini chochote unachotaka.
Lakini, facts huna kuhusu hilo.
Ukiwa na fikra za kulazimisha chuki iwepo, utaona chuki hata mtu anaposema kwa principle tu.
Ukiwa guluguja usiye na uti wa mgongo wala ubongo, nikipiga chafya kwa reflex action tu utaona nimechukia.
Mimi nimeondoka Tanzania Jiwe harufu ya mjini haijamuingia vizuri.
Hatujakutana kwenye mizunguko yetu.
Bora ungeniambia habari za George Bush au Obama, Mkapa, Mwinyi au Nyerere, labda ingeeleweka.
Hizi hapa facts.
Jiwe kaipa shavu familia yangu. Sina sababu ya kumchukia.
Jiwe Msukuma mwenzangu (angalau anajinasibisha na Wasukuma) sina sababu ya kumchukia.
Mimi naishi Marekani na sina mpango wa kurudi Bongo. Atakachofanya chochote hakinigusi binafsi. Sina sababu ya kumchukia.
These are facts.
Naandika kwa principle, sio chuki.
Ila wewe umezoea jamii yenye kuendeshwa na chuki, hivyo sishangai unaposhindwa kutofautisha principle na chuki.